Black Butterfly
Member
- Aug 31, 2022
- 54
- 99
Oktoba 9, 2023 nilikwenda kumpeleka Ndugu yangu pale MOI kwaajili ya kupata vipimo kutokana na hali yake kiafya kusumbua kwa muda mrefu. Kufika pale Daktari akamwandikia kipimo cha Magnetic Resonance Imaging (MRI) ili kubaini tatizo lake. Balaa likaanza kufika Lab, kuna foleni ndefu kuzidi mwendokasi za Kimara.
Ikabidi tuchague siku za mbele ambazo zinakuwa hazina watu wengi. Tukachagua Alhamisi Oktoba 12, 2023, Ndugu yangu alikuwa kama mtu wa 10 katika list ya watakaofanyiwa uchunguzi siku hiyo, sasa licha ya kufika mapema kwenye muda tuliopangiwa tumekuja kupata Kipimo masaa 10 baadaye. Na tulipohoji kwanini inakuwa hivyo majibu yao ni mashine ilikuwa mbovu kwa siku 2 hivyo Wagonjwa wa siku hizo mbili wameingizwa kwenye siku hii.
Hilo sio tatizo sana, issue ni kwanini Hospitali kubwa kama Moi inayohudumia Wagonjwa wa karibu Nchi nzima kwenye masuala ya Mifupa iwe na Mashine moja tu ya kufanya Vipimo? Yaani pamoja na Kodi na Tozo zote tunazopigwa na Serikali inashindwa kununua mashine hata 5 kuzifunga pale MOI kweli? au ni kupuuza Afya za wananchi kwasababu hawana la kuwafanya?
Hebu fikiria Mashine moja ihudumie Wagonjwa wa Ndani (Waliolazwa, na wengine wanatoka ICU kila muda na kusababisha Wagonjwa kusubirishwa au kuondolewa kwenye mashine ili mgonjwa wa ICU aingia, what a shame), bado hiyo hiyo ihudumie Wagonjwa wa nje na wengine wenye Rufaa zao. Ni aibu kwa Nchi inayotumia mabilioni ya Fdha kutangaza vitu vya ajabu ikiwemo Royal Tour wakati Mahospitali hakuna Vifaa Tiba na Wahudumu Wachache.
Ni hayo. Badilikeni