Taasisi ya MOI yawafanyia upasuaji wa kurekebisha Kibiongo Watoto 10 baada ya mafunzo ya madaktari wa nje

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imewafanyia upasuaji wa kurekebisha kibiongo watoto 10 kwa mafanikio makubwa katika kambi maalum iliyoendeshwa na madaktari bingwa wa MOI kwa kushirikiana na Madaktari bingwa kutoka Marekani , Italia, Palestina na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kambi hii ilianza Februari 5 hadi 9, 2024 ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mpango mkakati wa MOI wa kuwajengea uwezo wataalam wa ndani ili wawe mahiri katika kurebisha migongo iliyopinda (Scolliosis) iliyoanza mwaka 2017.

Akizungumza wakati wa kufunga kambi hiyo katika vyumba vya upasuaji MOI, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Lemeri Mchome amesema kuanza kwa huduma hii hapa nchini kumesaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi.

Amebainisha kuwa zaidi ya wagonjwa 50 wenye changamoto ya vibiongo wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji kwa kuwa wapo kwenye orodha ya kusubiri.

“Gharama za upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda (Kibiongo) kwa mtoto mmoja ni kati ya Shilingi Milioni 15 hadi 17 lakini nje ya nchi gharama zinafika hadi Shilingi Milioni 60,” amesema Dkt. Mchome.

Ameongeza kuwa Wagonjwa wa vibiongo wanaendelea kuongezeka nchini hadi kufika wagonjwa watatu kwa mwezi huku takwimu za Dunia ikiwa ni Asilimia 1 hadi 5 wana tatizo hilo, jumla ya Wagonjwa 10 watafanyiwa upasuaji.

Ameongeza kuwa kutokana na mafunzo hayo wanayoyapata wanaweza kuwasaidia kubaini wenye changamoto hiyo katika hatua za awali kabla ya kufikia hatua ya upasuaji na kuwa hiyo itsaidia kupunguza gharama kwa Serikali kupeleka wagonjwa nje ya nchi.
Snapinsta.app_426679297_18085756411419322_784583669033969827_n_1080.jpg

Snapinsta.app_426252868_18085756366419322_2785297174554107682_n_1080.jpg

Snapinsta.app_426636280_18085756429419322_5260164872936625694_n_1080.jpg

Snapinsta.app_426619212_18085756438419322_5874464149747660078_n_1080.jpg

Upande wake mkufunzi kutoka nchini Palestina, Prof. Alaa Ahmad amesema mafunzo hayo yamelenga kuiwezesha MOI kuwa kituo cha umahiri katika matibabu ya kurekebisha mgongo Afrika Mashariki, Kati na Kusini.

“Mafunzo haya ya umahiri katika kufanya upasuaji wa kurekebisha kibiongo yataiwezesha MOI kuwa kituo cha umahiri cha kutibu na mafunzo Afrika Mashari na Kati na kusini ambapo wataalam wao hujifunzia hapa MOI,” amesema Prof. Alaa.

Kambi hiyo imeanza tangu Mwaka 2019 ambapo imekuwa ikifanyika kwa kuangalia matibabu mbalimbali husuasani yale ya kibingwa ili kuongeza uwezo wa madaktari wa Kitanzania.
 
Back
Top Bottom