Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,252
Serikali yetu kupitia wizara ya Afya naona ipo busy na kampeni za chanjo za Uviko19 huku ikijisahaulisha huduma muhimu huko kwenye Hospital za serikali.
Jana nilienda kutembelea mama mmoja jirani yangu Alieenda kujifungulia Mt Meru hosp,na mtoto kuwekwa chumba cha joto kwa muda wa wiki mbili maana mtoto alizaliwa kabla ya Umri.
Nikiwa pale wodini naona wakina mama wamelala kwenye kitanda kimoja wengine wawili vitanda vingine hadi watatu pamoja na watoto wao wachanga ikabidi nimuulize yule mama jirani yangu nilienda kumsalimia, hapa mnalala Vipi wanawake wawili na watoto wenu ilhali vitanda ni vidogo? Akasema ndo hivyo hivyo hamna namna.
Basi nikiwa pale akaletewa Bill ya Hospital ambayo ilikuwa Tsh. Laki 300,000.
Nilivofika nilimkuta yupo na mumewe Na walikuwa tayari kuondoka ila baada ya bili kuja ikabidi waghairi kuondoka ili kesho aje amtoroshe mke wake maana hana namna kabisa ya kupata hiyo pesa.
Baada ya bili kuja alienda kuomba apunguziwe maana yeye ni kibarua tu mjini hapa hana Kazi na. Mkewe ni mama wa nyumbani.
Ombi hilo lilivogoma mwamba uamuzi aliouchukua ni kutoroka kukimbia bili.
Wizara ya afya tunaomba mfuatilie huko kwenye Hospital zenu boresheni huduma zenu na pia muweke viwango rafiki vya gharama kwa ajili ya wananchi wenu tafadhali