Mimi msimamo wangu utakuwa ni kama ulivyo. Sigeuki nyuma nikawa jiwe. Hawa watu wanaubaguzi wa hali juu tena kibaya zaidi wanaufanya kwetu dhidi ya wazawa, lakini watu hawataki kuuona huo wala kuuzungumzia wanataka kuzungumzia ubaguzi aliofanyiwa yeye tu!
Ubaguzi kivipi Bro?
Hatutibiwi kwenye hospitali "zao", i.e Aga Khan, Hindu Mandal, Burhani, TMJ etc?
Walituzuia kwenye majumba "yao" ya sinema? Empire, Odeon, Empress, Drive inn etc?
au kwenye mahoteli "yao" Seacliff, White sands, The courtyard etc?
Tataizo "letu", kujieleza ndio shughuli, kubaguliwa kivipi?
Sidhani kama tunaweza kuwaita Azim Dewji & Mohammed Dewji-Simba, Mar Abbas Gulamali-Yanga, Shaffi & Moh'd Bora-Majimaji, Naushad Moh'd -Malindi (tena huyu ana mke Mswahili), etc kuwa hawa jamaa walikuwa wabaguzi...
Kuna watanzania wenye asili ya kihindi-wagoa wanaojihusisha na mambo ya dini, si wabaguzi, kuna wagoa wanaojihusisha na muziki mf; INAFRIKA Band, si wabaguzi...
Kuna watanzania wenye asili ya kihindi-masinga singa wanaojishughulisha na ufundi pale gerezani, si wabaguzi...
Ubaya wa wachache wetu (watanzania wazawa-wabantu) ni tabia za utoro kazini & uvivu, udokozi, fitna & majungu , na kukubali Rushwa (tena za kipuuzi i.e fulana, kofia, na wale vibosile kwenda kwenye maduka "yao" kuomba tv, mafriji etc) ndio maana hawa jamaa wanatudharau, sio kutubagua.
Hapa nilipo, kuna wahindi nane kutoka East africa, wana heshima na adabu, tena wanasema "wewe ndugu yetu, tumetoka wote nyumbani!", na kiingereza hawataki kukizungumza, kiswahili tu!.
nyinyi wote mnazungumzia "hawa watu" sijui "wahindi vile au hivi" huo ni mjadala mwingine, hamjajieleza vya kutosha kwanini binti huyu specifically, asiwe miss Tanzania? Msianze kusema makosa ya jamii nzima mumwadhibu yeye? Je, binti huyu amewahi kuwabagua watu weusi, je binti huyo alikuwa anajitenga kwenye mashindano n.k mtaendelea kupiga kelele "wahindi hivi au vile" haifanyi kuwa hoja yenu ya kumbagua huyu binti iwe na nguvu!
Mnaweza kusema "wahindi walitunyima mihogo" au "wahindi hawakutupa maji ya kunywa" kuwa ni wabaguzi wakubwa hilo lote sawa na mimi naelewa na ninafahamu kuna wahindi ambao wana tabia hizo za kibaguzi tena si kidogo! Hilo wala siyo mjadala, mjadala ni Richa Adhia amefanya nini cha kibaguzi ambacho kinamfanya asistahili kuwa Miss Tanzania? Hadi hivi sasa hakuna aliyethubutu kutuonesha japo kitu kimoja isipokuwa porojo za "wahindi wako hivi ohh wahindi wako vile"
Give me some undisputable facts kwamba Richa Adhia hastahili kuwa Miss Tanzania kwa vile amefanya hivi au vile au hakufanya hivi au vile!! haya ya 'wahindi wabaguzi' I have had enough.. stick to the topic..
Kwa nini Richa Adhia, aliyekuzaliwa na kukulia Tanzania anayezungumza Kiswahili, Kiingereza, Na Kisukuma (sijui alijifunza shule gani Kisukuma!!) ambaye hakuna hata mahali pamoja ametoa kauli za kibaguzi (at least not in public) au amefanya kitendo chochote cha kuwadhalilisha watu weusi, asiwe Miss Tanzania? Can i make this question more pointed than that?
Unathubutu kuwaita hata dada zetu maimuna pamoja na kujua wazi mfumo wetu wa elimu unavyolegalega kwenye ufundishaji wa Kiingereza. Huoni walakini wowote wa dada zetu kukosa ushindi wa Miss Tanzania kwa kuwa 'walijikanyaga' katika kujibu swali kwa kiingereza. Wakati huo huo huoni mapungufu aliyokuwa nayo huyo mdosi ambayo hayakustahili yeye kupewa ubingwa huo!
Hata Richa ni dada yetu!! Kama alikuwa na mapungufu ya sifa zilizokuwa zinahitajika basi tujadili na tupinge ushindi wake katika parameters hizo. Mnapotoka nje na kuanza kuingiza asili yake na kuanza kumuita majina kama "mdosi"n.k., huo ni ubaguzi na mimi naupinga kwa nguvu zangu zote. Two wrongs don't make a right. Wahindi ambao ni wabaguzi na wao nawapinga kama ninavyowapinga Waafrika weusi walio wabaguzi na mtu/ watu wengine wote walio wabaguzi. Ubaguzi ni ubaguzi tu. Mimi kubaguliwa na Mhindi hakuhalalishi mimi kumbagua Mhindi mwingine asiye na makosa na ambaye hajanibagua na hakuhalalishi mimi kuchukia jamii nzima ya Kihindi. Ndugu zangu humu mnanitisha na hizo feelings zenu za kibaguzi. Nilidhania Tanzania hatuna mambo haya but I guess I was wrong!!!!!!
Wako wadosi wengi tu wenyewe wanajiita wadosi wala hawaoni noma, iweje wewe uone noma zaidi yao? Dada zetu kuitwa maimuna hukuona ubaya wowote! Mimi wahindi sio dada zangu wala kaka zangu hata siku moja, siwaoni sehemu za starehe zilizojaa waswahili, siwaoni kwenye sherehe zetu kama vile harusi n.k. mpaka zile za vingunge wa chama na serikali. Siwaoni kwenye vilio vya watu weusi, hata kwenye misiba ya Kitaifa kama ajali ya meli ziwa victoria na ajali ya treni pale TRC wadosi sikuwaona hivyo kwangu mimi siwaoni kama kaka au dada zangu.
Juzi juzi tu tulikuwa na msiba wa dada yetu Amina Chifupa, pamoja na kuwa alikuwa na umaarufu mkubwa lakini hao 'dada zako na kaka zako' hatukuwaona kwenye msiba huo hilo wewe hulioni. Angalieni vizuri mjue ni nani mbaguzi!
Five queens picked for world contests
2006-08-21 07:53:45
By Majuto Omary
Five queens won chances to represent Tanzania in various miss world beauty contests over the weekend.
The beauties are Jamillah Munisi, who will represent Tanzania in Miss Globe International, Upendo Mpanda (Miss Intercontinental) and Angella Kileo (Miss International).
Others are Edna Audax (Miss Top Model of the World) and Richa Adhia (Miss Earth).
The queens won the local titles at the Beauty Queen of Tanzania Contest held at the Dar es Salaam Holiday Inn last Saturday.
The contestants competed wearing clothes designed by three local designers - Farouque Abdelah from Zanzibar, Angelo-Elly Mlaki of Neith Fashions and up and coming designer Loveness Mpanda of Dar es Salaam.
Other awards went to Siah Lyimo, who won Miss Talent, Aziza Mbogga (Miss Punctuality), Nora Alex (Miss Personality) and Sarah Martin (Miss Photogenic).
Other queens who contested at the event organized by Maria Sarungi but did not win any award are Anna Mshana, Halima Mandari, Kaneza Kapfunsi, Neema Chembe and Sherehe Abdallah.
The contest was sponsored by Holiday Inn Hotel, Golden Tough Salon and Valley Springs.
Rehema Sudi last year represented Tanzania at the Miss Earth, Magreth Wilson Chacha (National Costumes in Miss International), Joan Cassian (Miss Intercontinental) and Tetemaria Mallya (Miss Top Model).
ndugu yangu kada tafadhali punguza munkari! baba wataifa alisha sema tusibaguane kwa dini,rangi, kabila, jinsia eneo unalotoka au nanmna nyingine yeyote ile.
Wazawa ni nani?
During my lifetime I have dedicated myself to this struggle of the African people. I have fought against white domination, and I have fought against black domination. I have cherished the ideal of a democratic and free society in which all persons live together in harmony and with equal opportunities. It is an ideal which I hope to live for and to achieve. But if needs be, it is an ideal for which I am prepared to die.