kweli kabisa mwanaume wa kuoa anajulikana kabisa! na ambao sio waoaji wanajulikana live liveDaaahhh mtoa mada umenifanya nikumbuke historia 2 nyuma za kweli kabisa
Kila la kheri kwa wanaotarajia kuolewa/kuoa.
- Incident ya kwanza jamaa alikuwa na girlfriend one day was friday akaenda mchukua alimpigia demu ashuke chuni kabisa, demu akawa ready ila bado room ili jamaa akifika tuu ashuke waondoke. Hee!! ile jamaa kafika kapata parking akampigia demu uko wapi akamwambia nakuja hapo niko kwenye ngazi nashuka simu ikakatwa demu kushuka chini jamaa kumbe alishawasha gari na kuondoka hee demu kufika chini anampigia simu jamaa jamaa kamwambia nimeshaondoka ukitaka kuja kwangu panda basi uje. Looh demu akasema yaani hapa sijaolewa anashindwa kunisubiri dakika 3 jee nikiolewa nae si ndo atakataa kuongozana na mie barabarani isiwe tabu demu akaamua kujitoa kwenye mahusiano ila kabla ya kuondoka akamfata jamaa ili mpashe na kumpa vidonge vyake. Alipofika akamwambia ulichokifanya ni kibaya na sikupendezewa nacho bora uhusiano wetu uishie hapa kwa sababu unaonesha huwezi kunisubiri hata dakika 2 ukinioa si ndo kabisaa. Kwa taarifa yako usifikiri nina shida ya kuolewa na wewe, si lazima nikiachana na wewe ntaolewa na wengine jamaa akaona demu kastukia dili kumbe hakuwa na mpango nae akaomba msamaha ila demu akammwaga. So hapo ni bora kusoma alama za nyakati.
- Issue ya pili ilitokea kwamba demu alikuwa na boyfriend wake ambae ndo wanaanza chuo wote wako chuo mwaka wa kwanza. Kama kawa katika maongezi demu akawa anamchombeza huu uhusiano wetu lini utafika kwa wazazi? Jamaa alikuwa anasomea udaktari ila ndo kwanza anaanza level ya medical assistant ndo aende Muhimbili kupata degree. Jamaa alikuwa mkweli hakumdanganya demu akamwambia mie kuoa hadi nipate dregree na niwe na kazi inilipe mshahara mzuri au niwe na hospitali yangu kama si dispensary au pharmacy yangu. LOOOH demu akapiga mahesabu hapo yuko chuo mwaka wa kwanza, hadi jamaa amalize medical assistant bila kufeli au kurudia mwaka ni miaka 3 na akimaliza aende Muhimbili udaktari akifaulu bila kurudia mwaka ni miaka mingine saba na hadi aajiriwe mshahara mzuri au awe na hospitali, dispensary au pharmacy yake ni miaka mingine 3 kwa kukadiria jumla miaka 13 tangu hapo looh wakati huo demu alikuwa na miaka 21 ukijumlisha hiyo miaka 13 atakuwa na miaka 34 hapo ujue hakujaytokea tatizo lolote na iwapo jamaa ni kipanga yaani hatarudia mwaka au kukwama kufungua hosp au disp. yake demu akamwambia asante sana kuniambia ukweli, kweli nakupenda tutakuwa tunabanjuana tukimisiana ila naanza mapema maana sitaweza kukuvumilia hadi umalize. So ni vema kuwekana wazi kuliko kuzeeshana halafu mtu anakuja kuoa mwingine baada ya miaka yote hiyo. Jamaa hadi leo hajaoa ila amezaa watoto 2 na wadada tofauti, alishamaliza udaktari na kaajiriwa na haeleweki ataoa lini. Hivyo wadada ukingijea mkaka akuambie tuoane kesho utadoda na kuchina better ask mapema ujue mchakato.
Ni habari iliyowakumba wadada wawili tofauti ninaowafahamu.
kipoozeo utabaki kupoza tu lakini kuna wale ambao unajua kabisa yupo njema na mmeridhiana lakini hakuna anegusia ndoa.nahisi kuna hofu anakuwa nayo mwanaume na ndio maana anaweza asigusie kabisa hilo swala, pengine kumuuliza ungeweza kumtoa hofu na kujua lililopo kichwani kwake badala ya kuendelea kusubiri gizani huku bidada una mijihamu na peteHusyn, mwanamme anayetaka kukuoa hata kama hajasema unakuwa unamjua tu. Hat kama hajawahi sema, na mwanamme anayekuchukulia poa unamjua tu.
Sema wanawake sometimes hatukubali matokeo, unajua kabisa huyu mwanamme kwake wewe ni kipozeo, unataka umfosi akutoe kutoka kwenye kipozeo hadi uwa mke. Wapo wanaofanikiwa, wapo ambao hawafanikiwi kuwalazimisha.
hata mapadri wanapenda ati. lol
, safi sana Eiyer nimeona mabadiliko. ukitendwa mahusiano yaliyopita ni challenge ya kukufanya uwe imara katika mahusiano yajayo na si sababu ya kukupa hofu.
tuimbe mapambio sasa.
Daaahhh mtoa mada umenifanya nikumbuke historia 2 nyuma za kweli kabisa
Kila la kheri kwa wanaotarajia kuolewa/kuoa.
- Incident ya kwanza jamaa alikuwa na girlfriend one day was friday akaenda mchukua alimpigia demu ashuke chuni kabisa, demu akawa ready ila bado room ili jamaa akifika tuu ashuke waondoke. Hee!! ile jamaa kafika kapata parking akampigia demu uko wapi akamwambia nakuja hapo niko kwenye ngazi nashuka simu ikakatwa demu kushuka chini jamaa kumbe alishawasha gari na kuondoka hee demu kufika chini anampigia simu jamaa jamaa kamwambia nimeshaondoka ukitaka kuja kwangu panda basi uje. Looh demu akasema yaani hapa sijaolewa anashindwa kunisubiri dakika 3 jee nikiolewa nae si ndo atakataa kuongozana na mie barabarani isiwe tabu demu akaamua kujitoa kwenye mahusiano ila kabla ya kuondoka akamfata jamaa ili mpashe na kumpa vidonge vyake. Alipofika akamwambia ulichokifanya ni kibaya na sikupendezewa nacho bora uhusiano wetu uishie hapa kwa sababu unaonesha huwezi kunisubiri hata dakika 2 ukinioa si ndo kabisaa. Kwa taarifa yako usifikiri nina shida ya kuolewa na wewe, si lazima nikiachana na wewe ntaolewa na wengine jamaa akaona demu kastukia dili kumbe hakuwa na mpango nae akaomba msamaha ila demu akammwaga. So hapo ni bora kusoma alama za nyakati.
- Issue ya pili ilitokea kwamba demu alikuwa na boyfriend wake ambae ndo wanaanza chuo wote wako chuo mwaka wa kwanza. Kama kawa katika maongezi demu akawa anamchombeza huu uhusiano wetu lini utafika kwa wazazi? Jamaa alikuwa anasomea udaktari ila ndo kwanza anaanza level ya medical assistant ndo aende Muhimbili kupata degree. Jamaa alikuwa mkweli hakumdanganya demu akamwambia mie kuoa hadi nipate dregree na niwe na kazi inilipe mshahara mzuri au niwe na hospitali yangu kama si dispensary au pharmacy yangu. LOOOH demu akapiga mahesabu hapo yuko chuo mwaka wa kwanza, hadi jamaa amalize medical assistant bila kufeli au kurudia mwaka ni miaka 3 na akimaliza aende Muhimbili udaktari akifaulu bila kurudia mwaka ni miaka mingine saba na hadi aajiriwe mshahara mzuri au awe na hospitali, dispensary au pharmacy yake ni miaka mingine 3 kwa kukadiria jumla miaka 13 tangu hapo looh wakati huo demu alikuwa na miaka 21 ukijumlisha hiyo miaka 13 atakuwa na miaka 34 hapo ujue hakujaytokea tatizo lolote na iwapo jamaa ni kipanga yaani hatarudia mwaka au kukwama kufungua hosp au disp. yake demu akamwambia asante sana kuniambia ukweli, kweli nakupenda tutakuwa tunabanjuana tukimisiana ila naanza mapema maana sitaweza kukuvumilia hadi umalize. So ni vema kuwekana wazi kuliko kuzeeshana halafu mtu anakuja kuoa mwingine baada ya miaka yote hiyo. Jamaa hadi leo hajaoa ila amezaa watoto 2 na wadada tofauti, alishamaliza udaktari na kaajiriwa na haeleweki ataoa lini. Hivyo wadada ukingijea mkaka akuambie tuoane kesho utadoda na kuchina better ask mapema ujue mchakato.
Ni habari iliyowakumba wadada wawili tofauti ninaowafahamu.
................. jana nilikuwa nachungulia kitabu cha steve harvey cha ACT LIKE A LADY THINK LIKE A MAN.ni kitabu kizuri sana ila sie wengine uvivu wa kusoma vitabu tunakosa mengi.
steve anasema wanaume wanajua kabisa kuwa wanawake wanataka ndoa. wanawake wanatakiwa kujiondoa katika mentality ya kizamani ya kusubiri mpaka mwanaume atangaze ndoa. tunatakiwa kuset timeline for the ring, mwambie mpenzi wako unachotaka na matarajio yako. haina maana kuwa katika mahusiano ambayo hayakupeleki kule unataka kwenda, kwa case hiyo tafuta mtu ambaye mna direction moja. wanawake wengi huwa wanashindwa kufunguka kwa wapenzi wao kuhusu ndoa vile wanaogopa au wanahisi ni vigumu lakini ni ngumu zaidi kudate na mtu mpaka mnazaa watoto na hana mpango wa ndoa (wakati wewe intention yako ni kuwin pete).
muoneshe mwanaume thamani yako na asikutumie kama vile amekodi nyumba mwisho wa siku akipata sehemu nzuri anahamia huko. set standards zako na angalia kama anafit huko.
"the
number one cause of failure in this country is the fear of failure.
Fear paralyzes you from taking action. Dont be afraid to lose
him, because if a man truly loves you, hes not going
anywhere"
tujadilini jamani, tuanze kuset timeline au twende na zama zetu za mwaka 47 za kusubiri kuambiwa.lol.
nawasilisha.
Ha ha ha, mnaweza kuulizana mwanzoni na kuwekana sawa kabisa.
Ila moyo wa binadamu msaliti, mnaweza fika njiani mioyo ikawasaliti aidha wote wawili au mmoja wao. Kama kuna mawasiliano ya kutosha ni bora kuongea na kuwekana sawa mkajua nini cha kuamua kuanzia hapo. Kama mnabadili uelekeo wa mahusiano yenu wote wawili? Au kama mnaahirisha ili msijeumizana zaidi kwa mmoja wenu?
Ndio maana nasema ni kompliketedi kuja na formula.
Nikupe story na mtu wangu wa karibu, japo yeye hajui chimbuko la ndoa yake. Kijana alitongoza msichana mahali, akakuta msichana ana mwanamme wake,. Yule kijana kwa hasira akaenda tongoza mpwa ya yule mwanamme wa msichana aliyekuwa anampenda kama kumkomoa huyo mwanamme aliyemnyang'anya tonge mdomoni. Kweli akampata mpwa, akamlamba kama mara kadhaa. Ile anataka kumtema mpwa, na alikuwa ndio ana miaka 17 tayari ana mimba na mpwa ni wife material. Hadi leo wana watoto watatu.
Hawakuwa na mawasiliano, hakukuwa na nia njema to start with, but wameishia kuvishana pete kanisani.
Lakini hii ya kumwekea CCM timeline ni kujichubua kifua kwa kokoto.
hayo mazoea ni sababu tosha, tena ya kueleweka sana tukweli ni mazoea tu, hatuna sababu ya kueleweka katika hilo na hatupendi mabadiliko.
nadhani hapo kwenye red ndo haswa binadamu tunapokosea, tunadhani kwa sababu miaka inabadilika basi hata life style zetu zinatakiwa zibadilike....Ukinipa timeline nita kuogopa. Ni either nita kukimbia au nitakupa
pete then nianze kukaa mguu ndani mguu nje niki kuchunguza kwanini uko
so desperate hivo!!!
Nadhani Old is gold,sio lazima kila kitu kibadilike hata kama hiki ni kizazi kipya.
ni kweli
kuogopa jana ni ujinga
jana inatakiwa ikufanye uwe imara
Smile ukigonga 35 bila bila, utayakumbuka haya unayosema, i promise u.yaani wadada wa siku hizi mtu yoyote akipropose ndoa kwao jibu ni yes! kisa ndoa ndoa! aonekane ameolewa! aya bwana! mi napita tu
Ndo maana hapo juu niliweka kwenye mabano kuwa mimi siyo mfano mzuri sana....
ni kwa sababu niliulizwa kabla hata sija-settle kwenye mahusiano, yaani mimi naona nayaanza mahusiano tu naulizwa kuolewa, na juzi tu nimeulizwa kuolewa naye tena.....
siamini kwenye kum-push mwanaume akuoe (labda sababu sijawahi kuwa desperate kuolewa) kama kuolewa kunakuja tu. na kweli naamini kama mwanaume anakuhitaji wewe kuwa mwenzi wake wala hasubiri wewe umwulize, atakuuliza tu.
ila ni kama bado unakuwa unaogopa kumake the moves
yaani wadada wa siku hizi mtu yoyote akipropose ndoa kwao jibu ni yes! kisa ndoa ndoa! aonekane ameolewa! aya bwana! mi napita tu
kugawa papuchi ili uolewe ni kujishusha heshima, na hapo kweli lazma vidume vitake advantage. "sio wote wamepangiwa ndoa" nukuu ya ankal Kaizer.mie panaponichosha ni wadada tu wapo desperate na ndoa, wakaka walaaa, nina mdada hapa ofisini natamani hata dk hii ajibiwe ombi lake la kupata mume jamani, mana tukimaliza huu mwaka bila-bila atachizika, na wakaka wameshajua shida yake ni ndoa wanamtumiaje sasa? yeye anabaki labda nimeandikiwa huyu, kesho hamuoni na ameshafanya nae yote, then wanakuja kulalamika "wanachezewa" hawachezewi wanajichezea wenyewe, ndoa si kamari jamani useme "ngoja nijaribu" labda nitafanikiwa.
ha haaaa, chezeya life partner wewe......So sweet Fixed Point