how to get the ring.


kweli, hata wanaume wanaokuja kwa gia za ndoa huwa wanaogopwa kama njaa.
 

Sasa hapa kitakachokuwa kinakusumbua ni mazoea tu!
 

Missed you too gfsonwin dearest, ni majukumu tu yalinibana ila sasa na mimi nimewamiss vyakutosha kwahiyo ntajaa humu.

BTT. . .
Mwambie Husninyo ndoa tu kama ndoa bila vionjo vingine haiwezi kuleta furaha. Unaweza ukaipata na ukaishia kujutia kumfahamu mume wako.

mimi bana nathamini furaha yangu na sipendi kero

Hahahha. . . Unaona sasa. Mtu anaweza akakupa ndoa alafu ukaigharamia kwa furaha yako binafsi.

Filipo . .asante bana.
 
Last edited by a moderator:
kweli, hata wanaume wanaokuja kwa gia za ndoa huwa wanaogopwa kama njaa.

Kumbeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!

Ndio maanaaaaa!!!!!!!!

Kuna kitu nimekumbuka hapa,huenda kilisababishwa na hii makitu aiseee!!!!
 
Husninyo suala ndo hilo la ndoa na kuvalishwa pete ya ndoa. naweza kukuvalisha pete hata leo kwa mapenzi yako kuwa unataka uvalishwe pete ila kama sina mpango na wewe utavaa hiyo pete ya uchumba miaka kibao
Na huwezi ukanilazimisha kuwa nikuoe hata kama nimeshakuvalisha pete ya uchumba
Sasa inapotokea kuwa umelazimisha nikuvalishe pete ya uchumba wakati mimi bado nipo nipo sana utakaa nayo mpaka itaota kutu maana bado sina mpango na wewe
Na naweza kukuvalisha tuu ili kutimiza lengo lako kuwa na wewe uonekane upo na mtu au committed wakati huo huo mimi naendelea kula good time na watu wangu kutafuta perfect couple na utashangaa siku ya siku unatoswa vile vile licha ya pete yako
Suala hapa ni maelewano ya pamoja na utayari wa pande zote mbili kuingia kwenye ndoa na sio kulazimisha muda wangu ukifika sitakuwa na msalie mtume nitajitosa tuu na utaifurahia ndoa ila ukifanya kulazimisha utakuwa unabaki home kulea na kuzaa watoto wakati mimi niko mtaani nakula starehe
 
Last edited by a moderator:

huo ni kwa upande wako, kwa upande wa mwanamke inabidi afanye maamuzi sasa.
 
Last edited by a moderator:
Huwa najiuliza tu

Kila binadamu ana njaa ya kuthaminiwa,kupendwa n.k.wakati binadamu huyohuyo hayuko tayari kuyafanya hayo kwa binadamu mwingine

Ni yupi atampenda nani na yupi atamthamini nani?

hapo chacha maana mara nyingi watu wanaangukia pua, unapenda usipopendwa na ulipopendwa huna habari napo.
 

mmh sawa kwa mda wako namimi naenda kimachale huwezi kunitumia miaka mitatu huku target yako ipo kwengine nikiona hueleweki nachapa lapa. na wanaume mmezidi kama unaona uliyenae huna future nae si umuache mapema yann kupotezeana muda
 
Last edited by a moderator:
Kumbeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!

Ndio maanaaaaa!!!!!!!!

Kuna kitu nimekumbuka hapa,huenda kilisababishwa na hii makitu aiseee!!!!
mbona una dalili za kuchakachua hii yuziful thread!
 
mmh sawa kwa mda wako namimi naenda kimachale huwezi kunitumia miaka mitatu huku target yako ipo kwengine nikiona hueleweki nachapa lapa. na wanaume mmezidi kama unaona uliyenae huna future nae si umuache mapema yann kupotezeana muda

shansarie ya nini kumuamsha aliyelala bana wakati mimi napata huduma zote kwake sasa ya nini nikuambie kuwa sina muda na wewe. Kuna mambo ambayo wewe mwenyewe wapaswa uyaangalie na uchape mwendo kama unaona giza mbele na sio usubiri mpaka upigiwe kengele ya hatari bana
 
Last edited by a moderator:
mmh sawa kwa mda wako namimi naenda kimachale huwezi kunitumia miaka mitatu huku target yako ipo kwengine nikiona hueleweki nachapa lapa. na wanaume mmezidi kama unaona uliyenae huna future nae si umuache mapema yann kupotezeana muda

hapo tumeenda sawa, yaani sio kuganda hapo wakati unajua kabisa matarajio hayapo.
 
good time hapo jua kwamba wewe haupo katika list yangu ya kukuoa bado nipo nipo sana na natafuta wa kunifaa na kuwa mke na so wewe upo na wengine wapo na bado hakuna wa kumvika pete ya ndoa hapo

Hahahaha. . .hapo nimekusoma. Ukipata mbuzi mnono ndio unanunua.




Pengine anaogopa akihallisha mbele ya watu itabadilika for the worst (wanawake wengi tu wanaangukia humo) Akishavaa pete na kusign cheti mahusiano yanageuka mashindano. Ku-avoid hilo jamaa anaamua mbaki tu hivyo hivyo. Mwingine labda anaogopa gharama za harusi n.k

Wakati mwingine sisi wanawake tunawapa wanaume sababu nyingi sana za wao kuogopa kuhalalisha na ku-formalise mahusiano na sisi maana hatuchelewi kubadilika na kuonyesha makucha. Sasa wanaona ya kazi gani.

Sana sana unachoweza kufanya ni kumshawishi kwa matendo (sio maneno) mmilikiane kihalali.


Huwa najiuliza tu

Kila binadamu ana njaa ya kuthaminiwa,kupendwa n.k.wakati binadamu huyohuyo hayuko tayari kuyafanya hayo kwa binadamu mwingine

Ni yupi atampenda nani na yupi atamthamini nani?

Eiyer hapo ndipo mtihani ulipo. Tatizo lipo kwenye ubinafsi na kutokujua wapi ndio na wapi sio bila kusahau kwamba hatuzingatii yale ambayo ni muhimu. Tunadanganyika kwa sura na pesa, mengine yanabaki kusindikiza tu.

Ila ubinafsi ni zaidi . . . Wanaopenda na kuwathamini wenzao wanakutana na majanga, wanaotaka kupendwa na kithaminiwa hawako tayari kupenda na kuthamini, wanaotaka wenzao wawe waaminifu unakuta wao sio waaminifu. Mwisho wa siku tunaishia kupata "MIS MATCH" kwenye mahusiano.
 
Last edited by a moderator:
hapo chacha maana mara nyingi watu wanaangukia pua, unapenda usipopendwa na ulipopendwa huna habari napo.

My dear,

Ndoa ni jambo gumu sana kwa kizazi hiki
Kuna mavurugu sana!

Tunadhani ni jambo la maonesho au la mzaha hivi
Hakuna tena ule umuhimu na heshima
Unakuta mtu anasema eti anataka aolewe ili aondoe nuksi
Sijui ni kuondoa nuksi au kuongeza mi sijui!
 
sijui kwanini sipendi kuolewa! naona sipo tayari...hata nikidate mtu nadate yule ambae naona hataki kuoa!... kuolewa kupo jamani msijilazimishe! kama ipo ipo tu! maisha ni haya haya ..usiache kuishi kisa huna pete mkononi!maisha yaendelee siku ya kuolewa ikifika utaolewa tu!
mi sihamii kwa mtu kamwe,wala sizai na mtu inadvance kamwe! ujue swala la ndoa ni mungu mwenyewe u know!Mungu alimuumba adamu baada ya muda akaona adamu yupo lonely so akaona amtafutie msaidizi ! Mungu anajua maisha yetu so tumuachie yeye wakati wake ukifika atakupa tu! just relax!
 

alafu ukishamvalisha pete kumridhisha na wewe kula goodtime mtaani unafaidika nn roho yako itakuwa na amani zaidi endapo utamwambia ukweli kuwa hauko tayari kumuoa yeye ili ajaribu pande nyingine kuliko kujitengenezea dhambi bure
 
Last edited by a moderator:
Mie sikubaliani na dhana ya kuwa kwenye mahusiano mwanamke anataka ring tu.

Kuna wanamme na wanamme bana. Kama wanamme wafanyavyo kwa wanawake, na wanawake tunafanya hayo hayo kwa wanamme.

Kuna aina ya mwanamme wa kula naye good time, labda mnashare interest nyingi na vitu vidogo vidogo. Wa aina hii sidhani kama mwanamke atataka ring yake.

Kuna mwanamme mwingine ni husband material, kuna mwanamme once unapoingia naye kwenye mahusiano, hata kama hujawahi fikiri kuolewa, unaanza kujihisi kutamani ndoa, unaanza kujihisi kuwa mama, unaanza kujihisi unataka kuwa mke. Wakati huo huo si lazima mwanamme huyo anajisikia vile akiwa na wewe, inawezekana wewe kwake ni wa kupita tu.

Na kuna wakati unakuwa na mwanamme kwa ajili ya kupitisha muda tu, yeye anaanza kukuona mke, anajiona mme kwako, anaanza tamani kuwa baba wakati wewe mwanamke uko pale very strategic unasubiri right candidate aje usepe fasta.

Sasa hii kuset timeline ya ring sio kitu automatic kwa kila mahusiano, ni pale wote mnaoana na kuhisi mwaweza ishi pamoja. Utamsetiaje mtu timeline wakati wewe kwake hukwolifai kabisa kuwa mke? Si atakupiga kibuti kesho yake tu? Na ukisema uondoke kwake ukatafute wa kukuoa wala haumii, inakuwa sawa na mzee mstaafu wa Afrika mashariki kuiziria mafao yake serikali kisa madogo? Si bora uchukue kwanza hicho kidogo afu udai kikukbwa?

Mie naona kinachodetermine kuweka timeline ya kuoana kwa tabia/mitazamo/mapenzi kwenu wote wawili na nature ya mahusiano.

Utadaije ndoa kwa mtu mliyekubaliana kuanzia awali mnapitisha muda? Labda wote mmejifanya nyumba ndogoz wakati mna waume/wake zenu? Utadaije ndoa kwa mtu aliyekuambia ana mpenzi permanent ila labda hayupo kwa wakati huo ana atarudi? Utadaije ndoa kwa mtu ambaye labda ni irresponsible lakini tu mzuri kitandani?

It's complicated, kwa mtizamo wangu.
 

ujue rocky, wanaume huona kuwa wanaweza kupata mwanamke wa kuoa muda wowote wakihitaji, ila ukweli ni kuwa wanaweza wasipate mke mwema vile vile. wakati wewe unaonja onja huku muda wako ukiwa bado ujue hata huyo mpenzi wako anaweza anakawa anatafta pa kwenda kutua, ukija sema urudi kwake mpige hatua mbele mwenzio kashabadili maamuzi. kuna thread moja humu jamaa analalamika karibu ataachika maana alikuwa na mpenzi wake kamuwekea mapozi sahvi yamemtokea puani hizo swaga.
 
Last edited by a moderator:


Kimsingi kwanza binadamu ni lazima tuheshimiane

Tukijua heshima ni kitu gani itatusaidia sana,siku hizi tunaishi kama ng'ombe hivi,tunataka tulishwe tuhudumiwe lakini wakati wa kutoa maziwa ni lazima tufungwe kamba miguuni kwa kuwa hatutaki kutoa maziwa kwa hiyari yetu!

Hebu fikiria tu kwamba mtu unakutana na mwenzako halafu unampa uhuru wa kuwa YEYE,anaona kama wewe unamuogopa hivi au anadhani unamtega halafu utakuja kumfanyia jambo baya,anajitengenezea hofu halafu anakuja kukuambia eti unamtisha kwa wema wako wakati yeye anajitisha mwenyewe kwa hofu zake mwenyewe

Tunaishi kihisia hisia zaidi bila kufikiri na kutumia akili zetu

Tatizo lingine ni watu kuruhusu jana iwaamulie leo
Yaani kwakuwa mtu alitendwa jana anakuwa nahofu mpaka kwenye mahusiano ya leo kitendo kinachopelekea kuharibu mahusiano yake mapya
Sikatai watu kuchukua tahadhari lakini kuchukua tahadhari ni kujifunza zaidi na sio kuwa na hofu,ukijifunza kutokana na matukio ya kale au zamani utaweza kuyatumia kuimarisha mahusiano yako ya leo,lakini siku hizi watu wanayatumia mahusiano yaliyopita kuvunja mahusiano ya leo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…