Mkuu heshima kwako, nashukuru kwa majibu yako mazuri lakini kuna haya machache hujaweka sawa au uajaribu kukwepa kwa makusudi, au yenye lengo la kujinufaisha binafsi kwa mrengo wa chama unachokishabikia... 1. Nianzie kwenye red. Kwa hiyo ikitokea kwenye Engish dictionary neno hilo limegeuzwa maana mtarudisha tena bungeni kufanya marekebisho? Na Dictionarymnayotumia ni ipi? sheria za wapi hizo zisizotoa maana halisi ya neno kwa neno? 2. Sheria iatoa hukumu ya not less than, hivyo inategemea hakimu ana amkaje au Watawala wanataka uhukumiwe vipi... unaweza fungwa miaka 50 kwa makosa yasiyo na kichwa wala miguu. 3. Whistle blower si lazima awe mwandishi wa habari au mwenye connection kokote, hizo sheria za kumlinda embu tuwekee hapa. 4. Suala la kukupa Password za BoT ni next to impossible na hakuna police wa kufanya huo uchunguzi narudia tena hakuna, embu niambie Singa singa wa IPTL alipewa password za BOT na nani? Hivi hii sheria ilikuwa tayari au bado? Wataendelea kuiba au wataacha? Vipi EPA? Mkuu tukubaliane kuwa hii ni sheria ya kujiandaa na uchguzi, ni ya kulinda watawala waje na porojo za kuwahadaa wananchi, lakini tambua kuwa hakuna kisicho na mwisho!