How GOD is smart

How GOD is smart

Naomba ya video yako uliyompinga huyo sheikh..... kwasababu kama hicho kitu hakipo ina maana sheikh amepotosha na anapaswa apingwe.... naomba inayompinga huyo huyo sheikh.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muulize huyo sheikh akupe ushahidi hayo maneno ameyapata wapi. Maana hajatoa ushahidi ameongea tu,na sisi ushahidi ni Qur'aan na sunnah.

Ukileta huo ushahidi na mimi nitakueletea mapokezi ambayo ni sahihi juu ya suala la Al Hoor Ain.

Nipo ....
 
Naomba ya video yako uliyompinga huyo sheikh..... kwasababu kama hicho kitu hakipo ina maana sheikh amepotosha na anapaswa apingwe.... naomba inayompinga huyo huyo sheikh.

Sent using Jamii Forums mobile app

Naomba umuulize huyo sheikh hayo maneno ameyapata wapi. Sababu sisi katika uislamu tunasema amesema Allah (Qur'aan) aliye juu na amesema mtume wa Allah (Sunnah).

Kisha nikuletee mapokezi sahihi juu ya Al Hoor Ain.

Nipo ....
 
Nilikuwekea hii sehemu fulani, haukurudi tena...... do u remember????View attachment 1071536View attachment 1071537

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa hapa unaweka ushahidi wa kuhusu nini au hoja yako ni nini ?

Ushahidi kwa waislamu ni Qur'aan na maneno ya mtume amani ya Allah iwe juu yake.

Sasa pakuanzia unachotakiwa kuniletea mimi na kukijadili ni aya au hadithi,sio maneno makavu sampuli hiyo.

Nimekupa kazi hiyo,na subiri aya na hadithi.

Nipo ....
 
Sasa hapa unaweka ushahidi wa kuhusu nini au hoja yako ni nini ?

Ushahidi kwa waislamu ni Qur'aan na maneno ya mtume amani ya Allah iwe juu yake.

Sasa pakuanzia unachotakiwa kuniletea mimi na kukijadili ni aya au hadithi,sio maneno makavu sampuli hiyo.

Nimekupa kazi hiyo,na subiri aya na hadithi.

Nipo ....
Case closed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwezi ukasema Mungu ni Smart..yaani hapo ni kumkufuru Mungu kabisa.....Mungu yuko above all kinds or even thingink of human smartness.....yaani Mungu hayuko katika hata level ya kuwa judged kama ni smart au hapana.....au hata kumfikiria kama ni smart...

GOD is GOD....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Well, vyote ulivyoandika hapo juu ni very illogical, since natumia logic nichangiapo mijadala(bila shaka kila mtu anapaswa kutumia pia), kipingele hiki pekee ndicho angalau kinaweza fanyiwa majadiliano, ili niweze kuendelea kuchangia, naomba unijibu swali nitakalo kuuliza ili niweze kuchanganua kama kipengele hiki nacho kina at least chembe za logic ama nachenywe ni pumba tu. Swali langu ni, tangua niwe na akili zangu timamu, sijawahi kumuomba mungu anisaidie kitu chochote kile, lakini nina mafanikio makubwa kuliko wakeshao wakimuomba(moja wapo ni bado napumua{natumia point yenu kuu ya kuwa mungu ndio mgawaji wa pumzi}), kwanini mungu ni mnafiki kiasi kwamba anawanyima wafuasi wake waaminifu na watiifu pumzi na mafanikio mengine, ila ananipa mimi nisiye hata na muda nae?
Kwa jinsi unavyoongea...unamuweka Mungu katika hali na hulka za kibinadamu...yaan uomba ndo upewe huombi haupewi.Hizi ni akili za kibinadamu kabisa.....Mawazo ya Mungu si mawazo yetu....Nani alikuambia mpaka umuombe Mungu ndo anakupa au pia unajuaje kama hicho ulichonacho ni kidogo sana kuliko ambacho Mungu angekupa kama ungemuomba??Unaojiona umekamilika lkn kumbe ungeweza kukamilika mara elfu zaidi kama ungemuomba Mungu wako..
Je...
1.Ulimuomba Mungu uzaliwe na uwepo katika dunia hii?
2.Ulimuomba Mungu akupatie wazazi hao aliokupatia?
3.Ulimuomba Mungu akupatie jinsia uliyonayo?
4.Ulimuomba Mungu akupatie hiyo rangi ulionayo?
5.Ulimuomba Mungu uzaliwe kwenye hilo kabila lako.?
6Etc...
Sasa kama hukumuomba Mungu hata akupe uhai kitu ambacho ndo cha msingi..sembuse kukupa huto tu mali twako ambako unahisi unawazidi sana wengine??
7.JE UMEJILINGANISHA NA WATU WENGINE WOTE WACHA MUNGU NA WANAOMUOMBA MUNGU NA UKAGUNDUA KUWA UNAWAZIDI KIPATO NA MAENDELEO?
8.JE HAMNA WATU AMBAO HATA HAWAJUI MAMBO YA MUNGU ZAIDI YAKO LKN STILL NI MATAJIRI ZAIDI YAKO NA HUTAKUJA KUWAFIKIA DAIMA WEWE NA UKOO WAKO WOTE??

Usiwaze kuhusu Mungu kwa mawazi ya kibinadamu......Mungu haeleweki ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alimpa option achague awe upande wake au wa shetan hakutaka kutumia nguvu ya kumlazimisha kumfuata Mungu, ili adamu asiseme Mungu amenilazimisha kumtumikia
Kabla ya kumpa option inamaana mungu hakuweza kujua mambo yajayo kua adamu atafata upande wa shetani?

Kama alijua inamaana alishindwa kulirekeshisha swala hilo liende sawa na mapenzi yake?

Kama mungu alijua hilo swala kua adamu hatomtii ilikuaje ampe tena option ya kuchagua?? Je inamaana mungu hakuwa na hakika ya vision aliyoiona kabla ya tukio mpaka akaamua kumpa option ili ahakiki???

Kama mungu alijua jambo la mbeleni halafu akaliacha litokee pasipo kulirekebisha inamaana hayo ni mapenzi yake na sio kosa la adam wala shetani kwasababu wote wako chini ya uwezo wake, sasa kivipi awaahidi moto wa milele viumbe wake kwa makosa ambayo aliwaumbia yeye na alikua na uwezo wa kuyaondoa yasiwepo?

Sent using unknown device
 
Thanks for your post. Nimewahi kusikiliza mahubiri ya Dr. Myles Munroe kuhusiana na maombi. Kiukweli alinifungua mambo mengi sana. Kumba kuna baadhi ya vutu Mungu hawezi vifanya duaniani mpaka sisi wanadamu (tunaemwamini) tumruhusu afanye. GOD IS GOOD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanadamu alivyomkataa Mungu means ana Uhuru wa kuchagua maisha anayotakz yeye bila hata kumtegemea Mungu, na still ukapata mafanikio ikiwepo utajiri, na ndo maana nikasema hawez kukulazimisha umtegemee Kwa jambo lolote lile, na ndo ile point ya u-smart inapokuja

Kwa hy swala LA wewe kumtegemea Kwa jambo lolote lile ni swala LA hiari yako

Na hao wanamtegemea Mungu na bado hawafanikiwa, ni simple unapotaka kumtegemea Mungu lazima ujiandae na vita kutoka Kwa shetani. Na pili watu waliokoka hawafanikiwa Kwa sababu wengi wanategemea miujiza na sio akili, ili ufanikiwe lazima utumie akili, kumbuka Mungu alivyosema watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa.

Tatu kuna uhabu wa Mafundisho ya jinsi ya kufanikiwa ki-Mungu, tunajua kuna namna ya kufanikiwa ki-shetani (Freemason na Kwa njia za kichawi), na kibinadamu, lakin ki-Mungu hayo Mafundisho yamekua adimu mengi yaliyoko ni ya uongo
Safi sana. Nimependa majibu yako. Pia nami niongeze point. Unaweza ona mtu hamtumikii Mungu na anamafanikio makubwa na pia unaweza ona mtu ni mtiifu sana ibadani lakini hafanikiwi. Ndugu yangu kuna tofauti kubwa sana ya kuzitii sheria za dini na kumtii Mungu. Hapa ndipo waumini wengi wanapofeli. Nawasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maada nzuri na mimi kukikazia kazia kidogo ni hivi
1.Asili ya Mungu ni nini? Asili (Nature) ya Mungu ni Roho (YOHANA 4:24).Sasa kama Mungu asili yake ni Roho na kuna roho aina mbali mbali Roho ya mungu ni ya aina gani??,Roho ya Mungu ni TAKATIFU (HOLY).sasa kwa asili ya Mungu kuwa Roho inamaana anapatikana kila mahali,Duniani,chini ya dunia,angani,mbinguni na ulimwenguni koote kwa wakati mmoja!

2.Mungu Hakumtuma Yesu aje na mwili wa Binadamu,kilichofanyika nikwamba Mungu mwenyewe aliumba mwili then akaingia ndani yake,yaani Mungu alijificha kwenye ule mwili ambao ulizaliwa na Mariam,Mungu Mwenyewe alikuwa ndani ya YESU Kristo! angalia maajabu ya Mungu,Muda huo huo alikuwa ndani ya Yesu,Muda huo huo alikuwa Mbinguni kwenye kiti cha enzi,Muda huo huo alikuwa ndani ya Yohana mbatizaji kwakuwa yohana mbatizaji alizaliwa tayari amejaa roho mtakatifu(roho wa Mungu)!,hukusoma andiko lilikuwa linatabiri kuja kwa Yesu na likasema ataitwa Emmanuel maana yake MUNGU PAMOJA NASI?,(ISAYA 7:14),Na pia kuna andiko linasema Mungu alijidhihirisha katika mwili akakaa kwetu? (1Timotheo 3:16) maana yake Mungu alitengeneza mwili then akaingia ndani yake then akaja kwa binadamu,alijidhihirisha katika mwili,kama vile wewe unavyoweza kujidhihirisha kwenye mavazi mbalimbali,ukavaa suti,au jens,au ukajidhihirisha na nguo za cadet nk..zile ni nguo tu ila wewe uko ndani ya zile nguo,na kwakuwa Mungu alikuwa anakuja kukomboa wanadamu ilimbidi aje kwa sura ya kibinadamu aishi na binadamu,awaonyeshe binadamu namna ya kuishi bila kutenda dhambi sasa Mungu ni roho ilimpasa aende kwenye nyumba ya daudi atengeneze MWILI halafu auvae huo mwili azaliwe kwa njia ya mwanamke kama binadamu wengine then atufundishe namna ya kuishi maisha matakatifu na hatimaye kafara ifanyike msalabani kuukomboa ulimwengu woote


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mungu huyuhuyu wa Vatican? yesu wenu huyo hajulikani anataka nini anabadilika km kinyonga, mara muarabu mara mgiriki, mara Blondish, sasa tuwaeleweje? tena yesu wako huyu katili sana aliuza watu km pipi!!! akishirikiana na watoto wake, mpaka leo ana wapa watoto wake silaha za kuua waafrica! ALSHAABAB, Boko, msumbiji.nk,

kama Adamu na hawa walikuwa ni wenyeji wa Ulaya, walizikwa ulaya, wewe mwafrica anakuhusu nini? kiherehere tu cha kujua miungu ya watu!

Nakwambia mleta mada yesu mzungu haji ng'ooo! mtasubiri sana, na kweli yuko smart sana,
 
Back
Top Bottom