Hotuba hii haina msaada wowote kwa mwananchi aliyekuwa anatarajia kumsikiliza Rais wake leo! Na kwa sasa suala hili la hotuba linaonekana kama ni mzigo kwa Rais kwani ameamua kupiga porojo.
Hotuba yake yote ina vipengele 37:
Vipengele 31 ameomba radhi na kuzungumzia sababu za kushindwa kutoa hotuba kwa miezi mitatu mfululizo. Mambo yote aliyozungumza hapa wananchi wanayajua maana Wizara ya Mambo ya Nje imekuwa ikiripoti matokeo ya vikao vyake vyote awapo nje ya nchi. Kwa hiyo kwa hili si jipya la mwananchi kusubiri kusikia kutoka kwa Rais ambaye hajazungumza kwa miezi mitatu!!!!
Vipengele 3 anakiri kuwepo na matukio mengi katika kipindi cha miezi mitatu! Na nukuu yeye mwenyewe
Kumekuwepo na matukio kadhaa hapa nchini yaliyogusa maisha, nyoyo na hisia za watu kwa namna mbalimbali.
then
Kwa vile mambo ni mengi kiasi sitapata nafasi ya kuyazungumzia yote moja baada ya jingine.
sasa Wananchi wanajiandaa kusikia hayo machache ambayo Rais anaweza kuzungumza ... mara
Nawaomba tuwe watulivu kwani utulivu wetu ni sehemu ya jawabu. Ni imani yangu kuwa kila anayeitakia mema nchi yetu atafanya hivyo.
Ina maana yale matukio yote ya miezi mitatu ndio hivyo Rais ameshayazungumzia!!
Vipengele 2 anatoa pole kwa msiba wa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe. Rais anasema kifo chake cha ghafla kimetushtua na kutusikitisha wengi. Kama Rais aliamua kuweka kipengele cha msiba kwanini ameshindwa kutoa pole kwa msiba wa Bhoke Munanka, huyu alikuwa mtumishi wa Serikali tena kwa kipindi kirefu!!!
Kipengele 1 Hitimisho Rais anamalizia kwa kusema
Kwa mara nyingine tena nawashukuru tena kwa msaada wenu na ushirikiano wenu. Mimi na wenzangu mliotupa dhamana ya kuliongoza taifa letu tutaendelea kuwatumikia kwa nguvu na uwezo wetu wote ili tufikie kwenye dhamira yetu ya kuharakisha maendeleo ya nchi yetu.
Hii ndio hotuba ya Rais kwa wananchi wake, baada ya miezi 3 mfululizo!! Nadhani hotuba nyingine itakuwa Oktoba!