Hotuba za Rais kila mwezi

Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Nani msamaria mwema amshike Kikwete sikio kuwa michezo yake hiyo ya kutufanya sie walugaluga hailipi tena? we are sitting on time bomb kwenye mambo mengi hapa. we dont want to loose another roho juu ya maslahi ya watu. Wakenya waliuana wakaona hailipi sasa wamechuku break. ' wenye akili hawahitaji kuwa rocket scientists kuona kuwa nchi hii ni noma tupu, poor us". Balali kimya kabisa. Mafisadi jisalimisheni, coming with plan
B soon.
 
Hilo ni "chaguo la Mungu" hivyo tuendelee "kuvumilia" na kumuombea tu!
 
MegaPyne umetudanganya,

Hii haiwezi kuwa hotuba ya mtukufu rais kwa Taifa. Rais hawezi kulihutubia taifa kwa kupiga projo tu kuhusu za safari zake za nje na kumalizia na porojo nyingine za kutoa rambirambi kwa mara nyingine tena baada ya alizokwisha toa oafficially kuhusu msiba huo huo.

Rais huwa anatumia muda huu kutoa summary ya hali ya nchi (State of the Nation) na utendaji wa ya serikali yake.
ni kweli ndugu yangu kichuguu, nimeangalia mwenyewe nikaona yote aliyobandika megapayne ndo hayo aliyozungumza jana kwenye tv. Inasikitisha lakini ndio hali halisi.
 
Mtemi wao kwenye hotuba alikuwa ni Nyerere tu ambaye kila hotuba yake ilikuwa na elements za philosphy kiasi kuwa alikuwa hakosi kuacha quotable quotes.

Kweli Kichu, hebu cheki kwotabo kwoti ya Mzee Kifimbo kuhusu hii hali:

"In his Oath to Office, the President of the United Republic swears to uphold and to defend the Union itself and its Constitution - it is his first duty" - Our Leadership and the Destiny of Tanzania page 2
 
Tusimlaumu Bure, hayo ndiyo anayoyasimamia. Amefanikiwa kuonyesha jinsi ambavyo anatofautiana na wengi. lakini, hiyo ndiyo maana ya kuwa rais?
 
Tukubali au tukatae, Rais hatuna may be mpaka 2015. Na kumlinganisha JK na Mkapa ni kama kulinganisha maji na mafuta. Hivi keli rais nahutubia taifa ananza kuelezea safari zake za nje halafu watu wanamsifia. Kama hana cha kuongea si bora akae kimya tu. Kwani ni nani alimlazimisha kulihutubia taifa kila mwezi? Yeye mwnyewe ndiyo alisema atazungumza na taifa kila mwezi. Kama mambo yenyewe ndiyo haya ni bora tu akae kimya asubiri sikukuu za kitaifa kuliko kuongea utumbo na kupotezea watu muda kwa kufuatilia hotuba isiyo na kitu.
 
Tukubali au tukatae, Rais hatuna may be mpaka 2015. Na kumlinganisha JK na Mkapa ni kama kulinganisha maji na mafuta. Hivi keli rais nahutubia taifa ananza kuelezea safari zake za nje halafu watu wanamsifia. Kama hana cha kuongea si bora akae kimya tu. Kwani ni nani alimlazimisha kulihutubia taifa kila mwezi? Yeye mwnyewe ndiyo alisema atazungumza na taifa kila mwezi. Kama mambo yenyewe ndiyo haya ni bora tu akae kimya asubiri sikukuu za kitaifa kuliko kuongea utumbo na kupotezea watu muda kwa kufuatilia hotuba isiyo na kitu.

I thought i was the only one who really was suprised. Yaani i was so much pissed off hadi nikadhani mimi ndio siko rational. Hivi kweli rais mzima na yote haya yanayoendelea nchini anatumia muda kulihutubia taifa kwa kutueleza asafari zake za nje na misaada aliyoomba miezi hiyo? Hivi mmeshanotice hotuba zake zilivyoja uombaomba? japan wamesema watatusaidia hapa....usa tumeomba wafanye hivi.........china walitujengea kile etc etc, jamaa yuko very confortable na kuombaomba hata wala harushi challengi kwa wananchi wake, anazidi kucreate mind zetu na za vijana wetu wa vizazi vijavyo kwamba tanzania/africa can only succeed kwa kuombaomba. Kwa aina hii ya rais tumeliwa tena kwa muda mrefu.
 
hivi Kwa Nini hawafanyanyi " Proof Reading" Kabla Ya Hizi Hotuba Kusomwa Na Rais , Ili Ni Jambo La Aibu Sana Na Kuhuzunisha ....whoever Is Writing These Speeches Should Be Fired.

No Comment
 
Kama hotuba ndio kama ile ya jana JK hahitaji kuendelea kutoa hotuba. Aachene nazo endelee na uvascodagama wake.
 
Jamaa ni mwenyekiti wa AU sasa pale alikuwa anahutubia waafrica kama mwenyekiti wa african union...wishoni akatoa rambirambi kwa familia ya chacha ambalo ni jambo la kiungwana tuu,....kwani mwenyekiti wa AU hatakiwa kutoa rambi rambi kwa familia ya mwafrica mwenzake......NA BADO
 
Mapinduzi ya haraka yanatakiwa, kwa khali hii hatutafika popote
 
Sijawahi kuwa dissapointed kama jana!!!

Nimeuonea aibu Utanzania wangu kama kiongozi wa sisi anaweza akakaa mbele ya TV na kuongea yale aliyoyasema!!! Ni aibu!
 
Nilikuwa nina wasiwasi kwanini hapakuwa na hotuba lakini ukweli wa itinerary yake unaonyesha tarehe za mwisho za April, May na June ndizo alizokuwa safarini mh. Rais wetu... Na kwa kuwa anasema amesita kutoa recorded hotuba akiwa nje ya nchi... basi mimi mwananchi wa kuangalia mambo kwa upana zaidi nimemuelewa rais wetu.

Of course mkuu wewe lazima umuelewa, na sisi tumekuelewa kwa kumuelewa Rais wetu!
 
Sijawahi kuwa dissapointed kama jana!!!

Nimeuonea aibu Utanzania wangu kama kiongozi wa sisi anaweza akakaa mbele ya TV na kuongea yale aliyoyasema!!! Ni aibu!

Ina maana wewe mahojiano yake na Shaka Ssali mwaka jana hukuyaona?
 
Kuna mtu mmoja kauliza kama hiyo hotuba mkuu kajiandikia mwenyewe..
 
JK hana mpya Mzee wa kucheka cheka

na lulanga, bombay, - 1.08.08 @ 08:30 | #26790

INASIKITISHA KUONA MKUU WA NCHI AMBAYE HAJAONGEA NA TAIFA KWA MIEZI MITATU AKITUMIA MUDA WAKE WOTE KUZUNGUMZIA SAFARI ZAKE ZA NJE. JK MISSED A GOLDEN OPPORTUNITY KWA MAANA HUO ULIKUWA NI MUDA MUAFAKA WA KUTOA MSIMAMO WA SERIKALI YAKE KUHUSU MASUALA NYETI KAMA ZANZIBAR NI NCHI AU SI NCHI, PESA ZA EPA NI ZA UMMA AU ZA WATU BINAFSI, MEREMETA INA UHUSIANO NA USALAMA WA TAIFA AU NI WIZI MTUPU. INASIKITISHA KUONA MKUU WA NCHI ANAKIMBIA MASUALA HAYO NA ANAZUNGUMZIA MAMBO YA SAFARI ZA NJE.

na Roman kaluta, Morogoro/Tanzania, - 1.08.08 @ 08:55 | #26811


JK ni robot

na lulanga, bombay, - 1.08.08 @ 09:37 | #26835

Inashangaza sana kuona mkuu wa nchi anakwenda kutatua migogoro ya nchi mbali mbali eti yeye ni mkuu wa umoja wa africa.
una nini raisi mbona migogoro ya nchini mwako huyatatui

wazanzibari tunataka kauli yako na sio ya mizengo pita bangi kua zanzibar nchi ema si nchi.
ukishatoa ufafanuzi tutajua kua tunaendelea na muungano au la.

znz tumechoka hatuoni hiyo faida ya kuungana nanyi ila hasara

na KIDANGA , NUNGWI, - 1.08.08 @ 09:42 | #26841

Jk bwana! mie nadhani umeomba radhi kwa kutuambia tuvumilie shida kana kwamba ulitereza kumbe, unaomba radhi kwa kutokutusimulia tenzi zako za safari za ughaibuni...ndio hujazungumza nasi kwa miezi miwili je, kipindi chote hicho hakukuwa na cha kuzungumzia zaidi ya mambo ya afrika? habari za ndani mi nimesikia rambirambi zako juu ya kifo cha chacha na mzee munanka.

na pandu, Kwerekwe, - 1.08.08 @ 10:30 | #26868

We Kidangi, we ni mgeni wa siasa! Mie sikutemea aongee zaidi ya hivyo alivyoongea.
Kuhusu status ya zenji kwani we hufahamu kuwa ni mkoa mkubwa ambao unavijimikoa vingi! Majibu unayo wewe mwenyewe! Wala usijibu kwa jasba. Ulimsikia kasema tuvute subira kwani hakuna tatizo linalimzidi kimo, na akawataka wanaoitakia mema Tz wawe na uvumilivu na utulivu!
Maanake ukileta 'unrest' au vujo wewe utakuwa huitakii mema nchi yetu! Swala la kuwepo muungano halina mjadala, wala haliamliwi na wewe. Ni sawa na wazazi wako waliokuzaa, huwezi ukawaambia unataka uamue kama waendelee kuwa wazazi au la. Wao watabaki wazazi. Mipango kwa sasa ni kuunda united republics of African states (united states of Africa). Hatupigi hatua moja mbele harafu turudi mbili nyuma hatuwezifika.
Cha msingi ni kuuboresha muungano ili tuwe na serikali moja na zanzibar igawanye ijulikane kama kanda yenye mikoa mitano kama kanda ya ziwa nk!
Heee, hayo ni maoni yangu, na naamini ni maoni ya wanaoitakia heri Tanzania bila kuwa na ubinafisi!
Utasubiri sana, kama bado untegemea rais aseme vinginevyo. Nchi ni Tz, zenji ni kanda.
Mungu ibariki Tz, mungu ibariki Africa.

na Hero, Tz, - 1.08.08 @ 10:45 | #26876

Kwa kweli rais hatuna! Inasikitisha sana eti rais anazungumzia mambo yake ya hovyo hovyo ktk safari ambazo tumezichoka siku nyingi kuzisikia badala ya kuzungumzia mambo ya msingi yanayofukuta ndani ya nchi yake?!

Ni dhahiri JK alifaa aendelee kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa si kuwa rais.

na Msugu Pe-igwite, Dar, Tz, - 1.08.08 @ 11:19 | #26889

Jk, wewe ni jamii ya matapeli tu , na endelea kuwatali wananchi wako kwa hadithi zako za alinacha . maendeleo hakuna, maelewano bungeni hakuna, baraza la wawakilishi pia vurugu tupu, wewe unasema ulikuwa nje,sasa wewe umechaguliwa ili ushuhulikie mambo ya nje ya Tanzania tu? au bado unakipenda kilecheo chako cha waziri wa nje? usidanganye watu ilenafasi ya uwaziri ndio mwisho wa uwezo wako na wala sio kuwa rais wa nchi. jiuzulu tu kama umeshindwa. nani asiejuwa kama hao uliokwenda kuwapigia magoti huwa hawatimizi ahadi zao? wewe si mbunge wa bagamoyo tena Jk, wewe ni rais wa nchi sasa oneshavitendo na wala sio hizo hadithi zako za kila mwisho wa mwezi ,ondowa shida za watu kwavitendo nasio kwa domo tu , hebu jaribu kumwambia mkeo avumilie shida uone kama hajadai talaka, nyinyi ccm vipi kila kiongozi anaetoka kwenu analazimisha waku kuvumilia shida tu mbona nyinyi hamvumilii kazi kuwaibia wananchi tuuuu... watanzania tunatapeliwa huyu jamaa ni tapeli.

na Bigfather, PBA, - 1.08.08 @ 11:22 | #26892

hebu watanzania wenzangu nendeni hapa msome hiyo hotuma yake yote ni aibu
http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/

na kipekecho, Tanzania, - 1.08.08 @ 11:23 | #26893

pole jk mimi kwa maoni yangu unatupiga changa la macho tu safari yako haina chochote kikubwa hayo mataifa makubwa yapo taaban kwa kupanda hali ya maisha na wananchi wao wanalalamika kila siku maisha kuwa juu iweje leo mafuta yanapanda kila siku katika mataifa makubwa leo mataifa hayo yasaidie kushuka bei ya mafuta kwa nchi za africa tafuta jingine hapo umechemsha

na king, tz, - 1.08.08 @ 11:26 | #26896

tuwe pole watanzania, haya ni matokeo ya jasho letu wenyewe, mana mkuu wa nchi tunamtengeneza wenyewe.
tugange lijalo la jk limekwisha, tusitegemee maajabu mana yeye na ma shosti wake wana shahada za usanii sasa wanashindwa kutofautisha kati ya uongozi wa nchi na sanaa za maonyesho. nadhani kwa kuwa sheria zinaruhusu basi tukubali kuweka mtu mwengine badala ya jk. hii ndiyo suluhisho na tukifanya masihara kuanzia 2010 kuelekea 2015 tutalia na kusaga meno mana jk na wenzake watageuka mbogo. kwa sasa wanajifanya ********* na tunasema tutakalo na kufanya tutakavyo kwa kisingizio cha uhuru na haki za binaadamu. ila tujiandae kama hatutaamua kufanya mageuzi makubwa ndani ya ccm na ndani ya mfumo wa seriakali.

na mamy, dsm, - 1.08.08 @ 11:58 | #26910

JK hana haja ya kutuomba radhi. Nani anataka hotuba zake zilizojaa porojo badala ya vitendo? Tunataka vitendo siyo ngonjera na sanaa za hovyo.
Afadhali angetuomba msamaha kwa kuuza nchi yetu na kushindwa kukidhi matakwa yetu.

na Mpayukaji, Sirini, - 1.08.08 @ 12:53 | #26923

wewe hero unajua chochote kuhusu zanzibar ? unajua tulivyoipata nchi yetu .
nakubali mzee wako atabaki kua mzee wako lakini una haki ya kumpinga ikiwa anavyokupeleka sivyo .
znz sio mkoa ni nchi tena yenye raisi.na kama unasema ni mkoa basi niambie kikwete ni raisi wa mkoa gani ? pinda ni raisi wa mkoa gani ? na hero ni raisi wa mkoa gani?

kama huwezi **** u and your mother
and hold your self

inavyoonesha hii computer umeazima na ndio mana ukawa uko haraka kukosoa wazanzibari eti nchi yao ni mkoa
je ushawahi kwenda zenji au unasikia tu?

na KIDANGA , NUNGWI, - 1.08.08 @ 13:57 | #26941
 
Sijawahi kuwa dissapointed kama jana!!!

Nimeuonea aibu Utanzania wangu kama kiongozi wa sisi anaweza akakaa mbele ya TV na kuongea yale aliyoyasema!!! Ni aibu!
Alitekeleza wajibu aliojifunga nao mwenyewe, kukaa mbele ya wananchi na kuongea pumba zisizohaririwa ama zilizohaririwa na viazi wenzake. Namuunga mkono member mwingine aliyesema aendelee na ufirauni wake lakini hotuba aachane nazo maana anatuonyesha yeye ni narrow minded kiasi gani. Pili namuunga mkono member mwingine aliyesema yanatakiwa mapunduzi/mageuzi ya haraka, na hilo ndio litatutoa hapo vinginevyo ndege ya Tanzania inaelekea kugonga mlima wakati wowote kwa kuwa haina rubani ama rubani anashinda chooni.
 
JK, kama huwezi kuyazungumza mambo ambayo Watanzania wengi wanataka uyazungumze ni bora kuachana na hizo blah blah zako za kila mwisho wa mwezi zisizo na kichwa wala miguu.

Baada ya kimya kirefu, Rais asema…

Ba Mdogo
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

NIMESHANGAZWA na utetezi alioutoa Rais Jakaya Kikwete kwamba alishindwa kuzungumza (au kuwaambia) wananchi wake kwa muda wa miezi mitatu kutokana na kubanwa na muda.

Mwenyewe amesema katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita kuwa alishindwa kuzungumza na wananchi kwa sababu kila ilipofika mwisho wa mwezi, wakati alip[opaswa kutoa hotuba hizo, alikuwa nje ya nchi.

Lakini huko nyuma, tulishazoeshwa na mtangulizi wake, ambaye ndiye aliyeasisi mpango wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi, anapojiona kuwa hatokuwapo nchini, alirekodi hotuba yake na kuiacha ili itangazwe siku muafaka.

Rais Kikwete anasema ameshindwa kufanya hivyo kwa sababu amepata maoni kutoka kwa baadhi ya watu kuwa hawaufurahii utaratibu huo.

Hawaufurahii kwa sababu wanamuona leo akizungumza nao, lakini wakati huo huo wanamsikia akizungumza akiwa nje ya nchi katika shughuli nyingine.

Hili linaleta maana yoyote? Najiuliza hivi kwa sababu katika hayo mazungumzo yake, sidhani kama watu wanamuangalia yeye zaidi ya ujumbe anaoutoa.

Kama imebainika kuwa watu wanavutwa zaidi na mzungumzaji kuliko ujumbe wake, hiyo ni dalili ya wazi kuwa hakuna ujumbe wa nguvu unaotolewa na hicho kinachozungumzwa na mzungumzaji.

Je, tuliishiwa na habari muhimu kiasi hicho katika kipindi hiki chote? Aliyoyazungumza Rais ni muhimu, lakini hivi umuhimu wake unalingana na aliyoacha/kukwepa kuyazungumza?

Nilitarajia kuwa baada ya kimya cha muda mrefu, Rais angeibuka na mambo ambayo kwa hakika yamelitikisa taifa kama yeye mwenye alivyoeleza kwenye hotuba yake. Inashangaza kwamba wakati anajua kuwa kuna mambo yaliyolitikisa taifa, anaamua kuzungumza mambo mengine ambayo umuhimu wake hauwezi kulinganishwa na kutikisika kwa taifa.

Lakini labda ninaweza kuwa ninalaumu kitu nisichokifahamu kwa undani kwa sababu inawezekana kwa vipimo vyake, aliyoyazungumza ndiyo ambayo Rais anayoyaona kuwa mambo mazito kwa taifa kwa kipindi chote ambacho alikaa bila kuzungumza na wananchi.

Kama ndivyo, mimi naomba nitofautiane naye. Hii ni kwa sababu mengi ya aliyoyasema, yanayohusisha zaidi ziara zake nje ya nchi (ambayo ndiyo sababu iliyomfanya ashindwe kuzungumza na wananchi wake), yaliripotiwa kwa mapana na vyombo vya habari. Nakumbuka katika baadhi ya ziara hizi, ujumbe wa Rais ulihusisha pia waandishi wa habari.

Pia, huko alikokwenda, kutokana na wadhifa wake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), alivutia waandishi wa habari wa kimataifa na ambao walisaidia kupeperusha ujumbe wa kilichojiri kila alipo.

Mengi ya mambo hayo, hayakuwa na utata wowote, hasa yanapohusishwa na Tanzania na mustakabali wa wananchi wa Tanzania kulingana na matatizo yanayowakabili hivi sasa.

Kwa upande mwingine, yapo masuala kadhaa hapa nyumbani, ambayo yana utata na yanahitaji ufafanuzi wa kina na wengi waliposikia kuwa Rais hatimaye amepata nafasi ya kuzungumza na wananchi wake, atatoa ufafanuzi kuhusiana na masuala hayo.

Kuna suala zima la mgogoro wa kisiasa Zanzibar. Hadi dakika za mwisho, hatua iliyokuwa imefikiwa kwenye mazungumzo hayo, ilionyesha kuwa yamekwama na ilielekea kuwa mtu mwenye nafasi kubwa ya kuyakwamua ni yeye, ambaye ndiye aliyeyaanzisha. Lakini kwake hili halikuonekana kuwa muhimu.

Kuna suala la uchunguzi wa wizi wa mabilioni ya fedha za umma kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ya Benki Kuu (BoT). Nalo hakuliona kuwa lina umuhimu wa kuzungumzwa? Miezi sita aliyopitoa kwa timu ya kuchunguza wizi huo imeshapita.

Kwa kuwa wanaofanya uchunguzi huo wanaonekana kuamua kutowaeleza wenye fedha wamefikia wapi katika uchunguzi wao, ilikuwa vema kwa mtumishi huyu wa Watanzania awaeleze mabosi wake kuhusiana na hilo.

Alipotoa hadidu za rejea kwa timu hiyo, alisisitiza kuwa kurejeshwa kwa fedha ni suala muhimu na lipewe kipaumbele. Tuliambiwa kuwa takriban sh bilini 60 zimerudi lakini BoT wanasema fedha hizo hazijapelekwa kwao. Hakuna taarifa zozote fedha hizi zimekwenda wapi. Au zimewekwa kwenye akaunti ya mtu binafsi? (Tulishaambiwa kuwa si fedha za serikali.).

Kuna suala zima la kupanda kwa gharama za maisha kunakotokana na kupanda kwa bei za mafuta na nafaka duniani. Tanzania imeathirika kama zilivyoathirika nchi nyingine. Si ajabu iwapo suala la kupanda kwa bei za bidhaa hizi, likaathiri bajeti zinazoendelea kupitishwa.

Kwa nini Rais hakuona umuhimu wa kulizungumzia hili? Au hana cha kuzungumza kuhusu hilo? Tunaamini kuwa kama nchi tunapaswa kuwa na mikakati yetu ya kukabiliana na hali hiyo. Hatuwezi kuwaambia wananchi waongeze uzalishaji tu ikawa ndio dawa ya tatizo hilo.

Hata wananchi wakilima na kuongeza uzalishaji, serikali nayo inafanya nini kukabiliana na hali hiyo? Ina mchango gani katika harakati za wakulima kuongeza uzalishaji?

Rais alishapokea ripoti ya tume aliyoituma kuchunguza mikataba ya sheria za madini. Nilitarajia kuwa huu ulikuwa wakati muafaka wa kutoa ufafanuzi kuhusu kilichoelezwa kwenye ripoti hiyo na kueleza serikali imeyachukuliaje mapndekezo yaliyotolewa.

Hata kama kazi hiyo haijakamilika, ingetosha tu kubainisha msimamo wa jumla wa serikali kuhusiana na ripoti hiyo. Je, imekidhi haja? Ina msaada wowote wa kuikomboa nchi kutoka kwenye matatizo ambayo yalisababisha timu hiyo iundwe? Lakini hatujaambiwa hayo.

Rais amekiri katika hotuba yake kuwa kumetokea mambo ambayo yameitikisa nchi. Lakini hayo aliyoyazungumza ndiyo yaliyoitikisa nchi kweli?

Kwa upande mwingine, hivi ni lazima aongee kila mwisho wa mwezi? Katika utaratibu wa kukabiliana na matatizo, mikakati inatakiwa kulikabili tatizo pale linapojitokeza.

Ni vema kuwa amejiwekea utaratibu wa kuzungumza kila mwisho wa mwezi. Lakini ingekuwa vema akafahamu kuwa utaratibu huu si msahafu kwamba hauwezi kubadilika. Ingekuwa vema na msaada mkubwa kwa Watanzania kila linapotolea jambo kubwa, rais akachukua muda kuzungumza na wananchi wake.

Ingekuwa busara kila linapotokea jambo linalolitikisa taifa, Mkuu wa Nchi akajipa muda kuzungumza na watu wake. Haisadii kuliacha taifa linatikisika, lipo kwenye majonzi, halafu mkuu wa nchi anakwenda nje.

Kwa kuwa utaratibu wa kuzungumza na wananchi umewekwa naye, ni dhahiri kuwa anaweza kuubadilisha. Na mimi napendekeza aubadilishe ili kumwezesha kuzungumza na wananchi wakati wowote inapolazimu kufanya hivyo.

Anaweza kuendelea na utaratibu wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi. Lakini pale anapoona kuwa kuna jambo muhimu la kulizungumza, na ratiba zake zinambana kiasi kwamba hatopata muda mwishoni mwa mwezi kuzungumzia hilo, ni vema akatafuta wakati mwingine wowote kuzungumza na wananchi kuhusu jambo hilo, si lazima iwe mwisho wa mwezi.

Ikumbukwe kuwa mawasiliano ni moja na nyenzo muhimu ya maendeleo. Kusikokuwa na mawasiliano inakuwa vigumu sana kuwaunganisha watu katika jambo lolote linalofanyika. Iwapo Rais atakatiza mawasiliano na wananchi wake kama hivi, asishangae wananchi watakapomuona kuwa amebadilika.

Hata kwa utaratibu wa kurekodi hotuba zake, iwapo jambo litakalokuwa linazungumza ni la muhimu, hao wanaolaumu kuwa hawapendi kumsikia katika hotuba za kurekodiwa, watafuta usemi wao.

Wananchi hivi sasa wanalazimika kuishi katika dunia ya uvumi. Kuna uvumi mwingi kuhusiana na mambo makubwa yanayolikabili taifa na ndhani haya ndiyo yanayosababisha mtikisiko ambao hata rais ameuona.

Ukweli huondoa uvumi. Ni wakati sasa rais akajenga mazoea ya kutoa ufafanuzi wa masuala haya kabla uvumi haujaanza kusambaa.

Kuna haja gani ya kuendelea kuficha mambo ambayo nusu yake yanajulikana na wananchi hata wa kawaida? Kwa kuwa hakuna anayejitokeza kusema ukweli ulivyo, wananchi wanaanza kutunga yao ili kujazia maswali ambayo hayana majibu katika taarifa wanazozipata.

Katika mazingira kama haya, mchawi ni yule anayeficha taarifa.
 
Back
Top Bottom