Hotuba ya Rais Magufuli Vs Freeman A. Mbowe

Hotuba ya Rais Magufuli Vs Freeman A. Mbowe

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,950
Reaction score
12,549
Nimezitazama na kusikiliza hotuba zote za viongozi hawa wawili kupitia YouTube.

Ya Mbowe nimeisikiliza na kuitazama kupitia MwanaHalisi Youtube Channel na takwimu zinaonesha kuwa imesikilizwa na kutazamwa na watu 1,300,000+ hadi kufikia leo tarehe 17/5/2020 saa 5:50 usiku.

Ya Rais Magufuli, nimeitazama na kuisikiliza kupitia East Africa Radio YouTube Channel na mpaka kufikia saa 5:50 usiku leo tarehe 17/5/2020 hotuba yake ilikuwa imesikilizwa na kutazamwa (views) na watu 230,000+

Yet, bado kuna watu wanasema CHADEMA chini ya Mbowe imekufa. Je, mtu akisema wasioitakia mema Chadema wanajilisha upepo nitakuwa ninakosea kweli?

Hii ni dhahiri shayiri kuwa, takwimu hizi zinatoa taswira ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu 2020 iwapo uchaguzi utakuwa FREE and FAIR kama ilivyo kwa watazamaji wa YouTube channels hizi ambazo hakuna wizi wala uchakachuaji wa matokeo.

Reference: Kila mwenye computer ama simu yake aingie Youtube channels hizo ku-verify hiki nilichokiposti hapa.
 
Sasa unashindwa kutumia japo maji kwenye hicho kichwa chako kufikir...ya Rais ilikuwa live TBC ,star TV na kwingine sasa hiyo ya Mbowe ilikuwa live wapi
Sio kweli.

Vigezo vya takwimu hizi vinafanana.

Hotuba zote zinekuwa posted almost 6 past hours baada ya kuwa zimerushwa live hewani.

Kwa hiyo kilichotumika sio hotuba kuwa live.
 
Watu wameangalia TBC&Star TV ...kuna haja gani ya kucheki YouTube tena?

Utafiti wangu hauwahesabu hao...

So, don't even mention that....

BTW, hata kama ungeweka TV mbili hapo...

Moja ikimuonesha Mzee wa anga Mh Mbowe na nyingine Mzee Magufuli, nakuhakikishia polisi watakuja na maji washa na mabomu ya machozi kusambaratisha wanaomsikiliza na kumtazama Freeman Mbowe...!!

Pole sana...
 
Hili la "kwani wote ni CHADEMA", sijasema wala kuandika mimi. Hilo ni la kwako....

Mimi nimeandikwa " number of views" bila kujali aliyetazama ni CHADEMA au wewe CCM ama asiyekuwa na chama.....just views!!
Rudia kuusoma uzi wako ndio utajua nimemaanisha nini!
 
Unadhani na mbowe angepata nafasi ya kuangaliwa kwenye TV pangekuwa tofauti na mh Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa Rais ndo anaongelea crisis inayoendelea nchini halafu watu wakamsikilize kiongozi wa chama!!! Kwan nyuzi zote mbili si zilikuwa hapa jf? Wa Rais na wa huyo kiongozi upi ulitembea zaidi... Watu sio wajinga wajinga hivyo kama unavyofikir...Si wote wamefungiwa kwenye mavyama kama wewe.
 
Utafiti wangu hauwahesabu hao...

So, don't even mention that....

BTW, hata kama ungeweka TV mbili hapo...

Moja ikimuonesha Mzee wa anga Mh Mbowe na nyingine Mzee Magufuli, nakuhakikishia polisi watakuja na maji washa na mabomu ya machozi kusambaratisha wanaomsikiliza na kumtazama Freeman Mbowe...!!

Pole sana...
Sasa kama hutaki kuhesabu hao ni shida zako hizo...Mimi na wote tuliopo nao hapa tumetazama Star TV live,..Shida yetu hotuba ya Mheshimiwa na tumeicheki...huko utube haina haja.. Ndo uhalisia huo,uukubali uukatae kivyako...halafu sijui unanipa pole ya nn;umevurugwa😅
 
Hotuba ya Mbowe kuangaliwa na watu Milioni na kitu tena sio live ila wametumia vifurushi vyao kuangalia maana yake ni kuwa watu wana mapenzi nae ingekuwa watu hawampendi au hawaipendi Chadema hata views laki 1 asingefika binti .

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbowe anapendwa sana ndio mana amerudisha hela alizoiba bungeni na ame bow 🙇 kwa speaker 🔊
 
Kamalizie na takwimu za kwenye runinga, sa we unakuja kumuelezea mtu aliepo tv online za youtube aise umlinganishe na yule ambae watu wanamtazama kwenye runinga bila bundle uwalinganishe,wewe mwenyyewe ulikuwa unamtazama kwenye simu au computer ukiwa mwenyewe lakini wenzako walikuwa wanamtazama Magufuli wakiwa wamestay home na familia zao wakichukua tahadharu,wewe kuhangaika na mavocha,kijana stay home, chukua tahadhari, nawa mikono kwa sabauni na maji yanayotiririka.
 
Yet, bado kuna watu wanasema CHADEMA chini ya Mbowe imekufa. Je, mtu akisema wasioitakia mema Chadema wanajilisha upepo nitakuwa ninakosea kweli?
Ya magufuli ilikwenda live kwenye vituo vyote vya televisheni na redio,pia ilirudiwa tena saa moja usiku,pia utafiti wako haukugusa channel.ya ikulu mawasiliano.

Ya mbowe ilipatikana vichochoroni,ndio mana ukaona hao 1.3 wamejazana,ukute hao ni wote wa ughaibuni
Yaani katika watanzania milioni 55,unajivunia kutazamwa na watu milioni 1.3!
 
Back
Top Bottom