Mtazamaji
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 5,937
- 1,437
Kwa takwimu zangu nilizonzo ni nchi moja tu Afrika ambayo haichukui hata senti tano toka mataifa ya nje katika bajeti yake ya Serikali. Nayo ni nchi ndogo iitwayo Eritrea. Ulaya hawaipendi kabisa kwasababu imetafsiri uhuru katika vitendo, na kwa maana hiyo wanashindwa kuibana kwa kutumia mbinu yao ya misaada.
Wakati Tanzania ikipata 44% ya pesa ya bajeti toka wafadhili, hii inamaanisha kuwa ukiwaudhi wafadhili basi hata mishahara ya watanzania haitakuwepo. Sasa utawaambia nini wanajeshi wakati hawajapata mshahara wao!
Usipoliona hilo kama ni hatua kubwa sana sijui nini kwako kitakuwa kikubwa. Wasalaam!
Zawadi je serikali imekopa shilingi ngapi kufidia nakisi ya bajeti yake. Tusije tukadanganywa kuwa tumepunguza utegemezi wa wafadhali wakati huo huo fuko la deni la taifa linapanda exponetialy. Denmark wakitataa kukupa msaada ukaenda kukopa kwa Libya kufidia ule msaada uliotegemea hakuna cha kufurahisha hapo.Hata hao Eritrea unaowasifu sio kuwa bajeti yao inajitosheleza.kiasi kikubwa chanakisi ni mikopo ambayo nadhani unajua masharti yake. Na sababu ya eritriea kukataliwa misaada ni bajeti yao kubwa ku fund jeshi.
Nitaungana na wewe kupongeza hili la kupunguza utegemezi wa misaada kwenye bajeti kama hakuna mikopo nyuma yake.