Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Wadau wa Demokrasia Barani Afrika unawahusisha Viongozi Wakuu Wastaafu wa Nchi mbalimbali Africa katika Ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia jijini Arusha.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Sierra Leone Mhe. Ernest Bai Koroma (kushoto) pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Desalegn wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Gran Meliá kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali kutoka Ndani na Nje ya Nchi kabla ya kufungua Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Viongozi Wastaafu kutoka Ndani na Nje ya Nchi mara baada ya kufungua Mkutano wa Jukwaa la Demokrasia Afrika uliofanyika katika Hoteli ya Gran Meliá Jijini Arusha tarehe 17 Julai, 2023.