Hotuba ya rais Kikwete Bungeni Julai 16 - Full Text

[FONT=AHIFFO+Tahoma]Pimeni wenyewe ilani ilichosema na utekelezaji anaojisifia nao![/FONT]

Kilimo ni sifuri. Hakuna kilichofanyika, kwani hata mbolea tunategemea nje. Na tukipapata hapa ndio uchumi wa taifa utakua.

Ni kweli viwanda ndio vinavyokuza uchumi kwa kasi, lakini leo wakati 65% ya waTZ wanaishi vijijini na kutegemea kilimo kama ajira, ni dhahiri kuwa ukiimarisha huko utajumuisha 65% ya waTZ katika uchumi.

Isitoshe hata kilimo kinahitaji viwanda katika kupata Pembejeo, usindikaji n.k.
 
Mkuu, mimi hapo niliposikia BAHATI MBAYA nikajua huyu alomwandalia amedhani kawa smart sana; na eti wabunge wakafurahi na kupiga makofi kisa kasema "Tulichukua maamuzi mazito sana kusitisha ubia na mwekezaji huyu (RITES)"

January.....na sasa atampa uwaziri
 
Idadi hii ni kubwa kuliko kesi zote za rushwa zilizopata kupelekwa Mahakamani katika kipindi cha miaka 20 kabla ya hapo, ambazo zilikuwa 543. Kati ya kesi hizo 780 Serikali imeshinda kesi 160. Katika kipindi cha miaka 20 kabl a ya hapo (yaani kuanzia 1985 – 2005) Serikali ilishinda kesi 58 tu. Mapambano bado yanaendelea.

Hizi takwimu zantia shaka.....je vipindi vilivyolinganishwa suala la rushwa lilikuwa la kiwango sawa?Huu usshindi wa serikali ni 20.5% ina maana 79.5% ilipoteza?...kama ni hivo basi mkuu hajafanikiwa
 
Kwanza nasikitika sana, Watanzania tumejadili hotuba hii hapa kwa siku sizizofikia 3, kwa masuala yatakayosimamiwa na huyu jamaa kwa MIAKA MITANO!. Muungwana hasifu aliyofanikiwa, bali huelezea alipokwama, na nini kilichosababisha - sio 'bahati mbaya', 'nje ya uwezo' 'hali ya kimataifa' nk. Mbona hakusema:

Hizo kompyuta kwa kila mwanafunzi ifikapo 2013 itatumia umeme gani, wanafunzi watakalia madawati yepi, wakifundishwa na waalimu gani, kwa lugha ipi, wakilishwa na nani, maji yao wanaogea wapi, wanakunywa lini, wazazi wao wanafanya nini, vita dhidi ya ufisadi, madawa ya kulevya, uonevu kwa mafukara, vitaondolewa lini kwenye vyombo vya habari na kupelekwa kwenye UTENDAJI na UFANISI!!! Mchagueni, laana ya wazazi wenu mliialika wenyewe!
 
NISHATI NISHATI NISHATI
Miaka mitano hii ilijawa na changamoto tele kwa upande wa sekta nzima ya nishati. Tulikabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa umeme kwa sababu ya ukame lililotufundisha kupunguza utegemezi kupita kiasi kwa umeme wa maji. Tumeongeza uzalishaji wa umeme kutokana na gesi asilia kwa megawati 145 pale Ubungo na Tegeta.
Hii sio changamoto sababu imekuwepo miaka nenda rudi. Aliingia Mwinyi akasema Changamoto, kaja Mkapa kasema changamoto na JK anasema ni Changamoto. Huu ni mtihani ulioishinda CCM. Chagamoto inakuja mara moja mara ya pili haitakiwi kuwa changamoto

Hivi sasa mchakato unaendelea wa kujenga kituo kingine cha MW 100 Ubungo kitakachotumia gesi asilia na cha MW 60 Mwanza kitakachotumia mafuta ya dizeli. Bahati mbaya mipango ya kuzalisha MW 300 Mtwara kwa kutumia gesi ya Mnazi Bay haukuweza kutekelezwa kwa sababu wabia wetu walijitoa kutokana na msukosuko wa uchumi wa dunia. Umeme wa MW 200 kutokana na makaa ya mawe ya Kiwira umecheleweshwa na taratibu za milki ambazo karibuni zitamalizika...............
Ningependa kwenye hotuba JK atuhakikishie watanzania wachache tunaotumia umeme suala la mgao sasa litwakuwa hadithi mwaka gani.? Tatizo la bei za umeme Tanzani kuwa kubwa ukilinganisha na nchi za SADC ??? Kuleta makampuni binafsi ni serikali kukwepa majukumu yake tena katika mazingira ya hali ya NISHATI ilivyo mhhh.Hapa kwenye Nishati kuna failures nyingi na sio changamoto.

Kuna mtaalam alisema standby power generators zinazotumiwa Twin Tower ya BOT zinaweza ku supply umemme mikoa ya Dodoma na Singida kwa pamoja. Sasa kwa mfano huu mdogo unaweza kuona Jinsi NISHATI ya kutoamika ya tanzania inazidi kutukamua watanzania.
 
Hii ndio kampeni ya kwanza ya Mheshimiwa Rais kwa wanachi wa Tanzania. Amejilemba na kujipamba kwa watanzania wote.

Nilitegemea wana JF wangeijadili kwa kina na marefu hotuba hii kwa siku nyingi. Katika mazingira nisiyoyaelewa nasikitika kusema kuwa wana JF wamekuwa kama wamemwagiwa maji ya baridi saa 12 asubuhi, na kusinyaa na kuzibwa midomo kana kwamba wamekubali kuwa JK kafanya kazi kubwa na aendelee na kipindi kingine cha Miaka mitano.

Msidhani kuwa mnaweza kuwapigia debe CHADEMA au CUF bila ya kuipangua hotuba hiyo. Safari ya kuelekea katika uchaguzi ndio imeanza na wapinzani wasitoe nafasi toka day 1. Miezi mitatu ni muda mfupi sana, hatuwezi kusubiri, na hii si kwa wapinzani tu bali hata wana CCM wanaotaka maendeleo ni lazima kuijadili kwa kina hotuba hiyo na kueleza mapungufu ili wahusika waweze kujirekebisha.

Kwa hotuba kama hiyo kujadiliwa hapa JF kwa siku nne tu, ni dhahiri kuwa JK kashinda.
 
Back
Top Bottom