Hotuba ya rais Kikwete Bungeni Julai 16 - Full Text

Nyepesi nyepesi zilizonifikia ni kwamba JK ameamua kutoa USD 50,000,000 (za serikali, si zake) ili kununua MASTERING STUDI baada ya kushauriwa kwamba eti wanamuziki wa Bongo Flava wamekosa studio ya aina hiyo??.

NI KWLEI SERIKALI IMETOA DOLLAR MILIONI HAMSINI KUNUNUA STUDIO HIYO??

Tumeliwa au tumelamba dume?
 
Alikuwa amesimama au amekaa? Saa zote alikuwa amekumbatia ile podium, kama vile alikuwa anashindwa kusimama on his own!
 
Nyepesi nyepesi zilizonifikia ni kwamba JK ameamua kutoa USD 50,000,000 (za serikali, si zake) ili kununua MASTERING STUDI baada ya kushauriwa kwamba eti wanamuziki wa Bongo Flava wamekosa studio ya aina hiyo??.

NI KWLEI SERIKALI IMETOA DOLLAR MILIONI HAMSINI KUNUNUA STUDIO HIYO??

Tumeliwa au tumelamba dume?

Mkuu kwa kadiri ninavyoona kwenye document ambayo ndiyo alikuwa anaisoma ni kuwa ni TSHS 50,000,000 na si USD 50,000,000.

Nadhani mkandarasi ni mchina :twitch:
 
Mkuu kwa kadiri ninavyoona kwenye document ambayo ndiyo alikuwa anaisoma ni kuwa ni TSHS 50,000,000 na si USD 50,000,000.

Nadhani mkandarasi ni mchina :twitch:

MKuu invisible nime PM. mwaka huu ni lazima JF iandaye debate kwa tzs 8M haziwezi kutushinda. Utamu wa haya mambo huwa ni pale anapokuwa mtu anayeweza kujibu au kuja na data mbadara.
 
Jamani, kuna baadhi ambayo ameyaongea anadai yametekelezwa, na anavyosema mengine yapo njiani kutekelezwa (mpeni kura!) hivyo tuwe watu wa subira, itapendeza mtu akasoma juu ya mafanikio ya awamu ya nne kwenye attachment na kisha akachangia, naamini hapo ndipo tutakuja na hotuba mbadala ya hii ya mheshimiwa rais.

Nasubiri kwa hamu sana comments za comrade Malaria Sugu (MS)

Kwa uelewa wangu wa aina ya hotuba, hii naiweka ktk persuasive class. Hapo kajitahidi ku-iproove utoaji wa speech kwa kubaki ktk maandiko. Inaonekana njia ya bora ni kumulazimisha kusoma alichoandikiwa.

Naona akiacha tu kusoma, anatoa upupu! Nimeona akijaribu na nikaona wasiwasi wa wafuasi wake, nyuma yake.

Ubora wa speech pia siyo sana ktk level ya Taifa. Lazima speech ya aina hii iwe ya kukumbukwa, itofautiane na ile ya mbunge anayetafuta kura. Hii ya leo sivyo maana ilikuwa ni muhtasari wa matukio mema yaliyopita na kuna sehemu nyingi sana imefanana na yale ambayo yameshasomwa na mawaziri Bungeni mengine yalisomwa juzi (na waziri wa fedha, siku mbili zilizopita). Tena neno kwa neno.

Wasiwasi wangu juu yake ni kwa nini ameshindwa kutaja tukio kubwa la kujiuzuru kwa Lowassa kama Waziri mkuu ktk serikali yake? Nadhani anajaribu kutusahaulisha ili baadaye Lowassa aonekane mwema.
 
Wasiwasi wangu juu yake ni kwa nini ameshindwa kutaja tukio kubwa la kujiuzuru kwa Lowassa kama Waziri mkuu ktk serikali yake? Nadhani anajaribu kutusahaulisha ili baadaye Lowassa aonekane mwema.
Kinachofurahisha wengi mmeishtukia sehemu hii!
Kama mnavyojua tulianza kazi, nchi ikiwa katikati ya ukame mkubwa wa aina yake kutokea tangu uhuru. Kukawa na upungufu mkubwa wa chakula, takriban watu wapatao 3,776,000 walipatiwa chakula na Serikali. Ukame huo pia ulikausha maji katika mabwawa yetu ya kuzalisha umeme hivyo kukawa na upungufu mkubwa wa umeme na tukalazimika kukodi vinu vya kufua umeme kutoka nje.
Sasa hapa ndipo nilitarajia angeligusia suala la kina Lowassa, maanake bado anamhitaji Lowassa serikalini? Tetesi za siku nyingi zinaweza kuwa kweli kuwa Lowassa will strike back?
 
Mimi tatizo langu ni kutokuwa na hali au hotuba za kuonyesha kuwajibika

Utaona ameongea wazi kuhusu mkataba wa TRL ulioingiwa na Serikali ya Mzee mkapa. Hii ina maana ni serikali ya mwaka 2015 do itakuja kututajia makosa au kurekebisha makosa ya awamu ya JK.

Ameeleza mafanikio na changamoto. Katika baadhi kweli kidogo serikali ya JK inatakiwa kupewa credit. Lakini kuonyesha uwajibikaji ilitakiwa atuambie wapi walikwenda mrama wakagundua wakarekebisha.

  • Kwa nini JK hasemi Kujiuzulu kwa Lowasa kama moja ya credibility za kuonyesha na kujenga dhana ya utawala bora na uwajibikaji.No matter lowasa awe na kosa au hana lakini alitakiwa ataje hili. Otherwise na yeye ni kama anaona alimtoa kafara mshikaji au anahisi bado anamuhitaji.
Nadhani hapa ndo JK nina wasi wasi hataki kuonekana mbaya hata kwa watu wabaya . Alitakiwa aseme serikali imewashtaki Viongozi wa ngazi ya Juu kama mawaziri XYZ, watendaji ABC na GHJ . hata kama ni usanii alitakiwa azitaje wazi wazi .
 
Hebu msikilizeni Rais anachosema kuhusu suala la TRL ... "
......... Kwa ajili hiyo, Serikali ya Awamu ya Tatu iliamua kutafuta kampuni ya uendeshaji wa reli ije isaidie kuendesha Reli yetu ya Kati. Hivyo ikapatikana kampuni ya RITES ya kutoka India. Wakati ule iliaminika kuwa kampuni hiyo ingesaidia kupata jawabu kwa tatizo linaloisibu reli yetu. Bahati mbaya matarajio yetu hayakuwa, ndiyo maana tumelazimika kufanya uamuzi tulioufanya wa kuanza mazungumzo na wabia hao ili Serikali ichukue tena reli hiyo na kutafuta namna nyingine iliyo bora ya kuiendesha reli yetu. "
Mheshimiwa anaposema Bahati mbaya ana maana gani ? ........Huku ni kulea uzembe tuu, watu waliohusika walitakiwa kupelekwa Jela.

Nina wasiwasi pia JK anaposema serikali ya awamu ya tatu pale penye -VE outcome na kuacha kutumia serikali ya awamu ya tatu kwenye +ve outcome.

Bora angetumia neno serikali ya CCM. Mbona hausishi neno serikali ya awamu ya tatu na mradi kama wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Kahama ?
 
Ingekuwa matumizi ni maendeleo basi asilimia 99% ya watanzania wangekuwa na maendeleo, lakini viongozi hususani wa Tanzania wanatakiwa waelewe matumizi ya pesa sio maendeleo bali ni majumuisho ya mambo mbalimbali ikiwemo nidhamu, utekelezaji, tija, mipango mizuri na matokeo ya hayo matumizi.

Kuhusu reli watu walipiga kelele saana, lakini wenye kula wakaweka pamba, sasa wameishakula vya kutosha na kupata mtaji wao ndio wanatuambia oh ilikuwa bahati mbaya, kweli wanasiasa/ au serikali yetu hii haina mapendo kabisa na sisi.
 
Mbona hakuzungumzia kuhusu shirika la ndege ?
Wakuu yani mnazidi kunifanya nicheke sana! Sasa nimeweza kujua watu wako smarter kuliko mtu anavyoweza kudhania. Nimeona mkuu mtazamaji naye kagundua kwenye reli kaamua kumsukumia zigo Mkapa naye kujineemesha kwa sifa, sasa mkuu Rufiji ukaishtukia hii ya ATCL, safi kabisa!
 
Wizi mtupu,

Hotuba imejaa ujanja ujanja wa kupika maneno na blah blah kama kawa.

Najua wanafiki wamepiga makofi na kupongeza, ila anachokisema sijapata kukiona mpaka leo.

Ameacha waziri wake akiimaliza COSOTA akidhani itajiendesha automatically. Halafu anasema wasanii wanataka studio ya mastering ilhali deal inasimamiwa na akina Ruge!!!!!???? wizi mtupu.

Wasanii wanahitaji shule hawataki hizo studio zake mkuu. Tunataka shule za maana ziwepo nchini au skolaship za sanaa. Punguza kodi kwa vitu vya sanaa. Tunahitaji Art museum na si cultural house mzee.
Irudishe Nyumba ya sanaa kwa wasanii maana imeshapotelea mikononi mwa matapeli na unajua hilo.

Kuhusu sanaa nakupa ziro na ahadi zako ni ziro tupu.

Sana sana achievement ni kwa wasanii kushiriki kupiga picha nawe kwa ajili ya matangazo ya kampeni za kitaifa na si zaidi ya hapo.

NIMEKEREKA KWELI KWELI
 
Nimerekodi sehemu kubwa ya hotuba ya Rais na utaweza kuiona kwenye channel yangu ya youtube/mwanakijiji
Kaka mwanakijiji
hiyo sehemu kubwa ya hotuba mbona siipati huko kwenye tube? Kuna hizi tu

Wizi mtupu,

Hotuba imejaa ujanja ujanja wa kupika maneno na blah blah kama kawa.

Najua wanafiki wamepiga makofi na kupongeza, ila anachokisema sijapata kukiona mpaka leo.

Ameacha waziri wake akiimaliza COSOTA akidhani itajiendesha automatically. Halafu anasema wasanii wanataka studio ya mastering ilhali deal inasimamiwa na akina Ruge!!!!!???? wizi mtupu.

Wasanii wanahitaji shule hawataki hizo studio zake mkuu. Tunataka shule za maana ziwepo nchini au skolaship za sanaa. Punguza kodi kwa vitu vya sanaa. Tunahitaji Art museum na si cultural house mzee.
Irudishe Nyumba ya sanaa kwa wasanii maana imeshapotelea mikononi mwa matapeli na unajua hilo.

Kuhusu sanaa nakupa ziro na ahadi zako ni ziro tupu.

Sana sana achievement ni kwa wasanii kushiriki kupiga picha nawe kwa ajili ya matangazo ya kampeni za kitaifa na si zaidi ya hapo.

NIMEKEREKA KWELI KWELI

Wewe na wewe nae
Wsaaani wa nch gani uliona wanatafutiwa shule na serikali. The only real msanii anayeweza kupata scholarship hata akienda ubalozi wowote ni Mjomba. Mjomba ni product ya Bagamoyo. je nyie wasanii mnahudhuria hata semina za chuo cha bagamoyo.? wasanii wengi wanadhani bagamoyo ni chuo ya wacheza ngoma.

Kwanza wasanii wa muziki washukuru imetokea kuna rais(JK) wa dunia ya sasa amejaribu kuchungulia na kuonyesha concern za matatizo yao.Kuna real National critical issues ambazo serikali ya JK haijafanya hata huo unaosema usanii aliojaribu kuwafanyia wasanii . Kila kijiji kinahitaji trekta la kilimo.

Ruge au mtu yeyote kusimamia kitu amabcho sio mali yake sioni tatizo. Kama kutakuwa na pricniple na guidelines atakazopewa na atasimamiwa na utendaji wake wa kazi kutathminiwa kila baada ya muda fulani nadhni hakuna kitakachoharibika.
 
Last edited by a moderator:
Mbona hakuzungumzia kuhusu shirika la ndege ?

Binafsi namsifu kwa kutoongelea ATCL. Ukweli ATCL haina tija na manufaa kwa Taifa. JK alikurupka kutoa ruzuku alivyonigia madarakani kufadhili shirika la ATC lililokufa. Shirika ambalo sijui linasafisrsiha wananchi % ngapi. Linasafirisha mizgo ton ngapi?Limeajiri watanzania wangapi?.Shirika ambalo mshindani wake ni precission.

Effort za kiakili na kifedha zote za serikali ya JK next term inatakiwa ziwe kwenye TRL/TAZARA Through TRL/TAZARA tutazishika rwanda , rwanda,malawi na zambia mpaka DRC.

Tuachane na mambo ya poltical national Pride wakati hakun real feasible banefit kwanye ATC. Nashangaa kwa nini hawajawapa wachina hili shirika 80 %. Our real Nationa pride should be RAILWAY
 
Nimetulia na kuisoma hutuba yake yote, na mara tu baada ya kumaliza nilichofanya ni kumpa 'THANKS' mletaji wa hoja hiyo ndugu Invisible.

Juu ya hotuba kwa leo nina mawili tu ya ksema, maana nilitumia muda mwingi kuisoma hivyo nimechoka kuandika mengi.

1. Katika hotuba zote za marais waliopita, sijawahi kuisoma hotuba iliyotulia kwa TAKWIMU kama hii hasa katika eneo la uchumi. Hotuba za maraisi wote waliopita utasikia maneno kama, tumefanya vuzuri sana, imepanda, imeongezeka n.k hutaziona Namba. Hutuba hii inampa mdadi msomaji kutoachia njiani na akipenda kupinga aje na takwimu zake.

Nimeshaanza kusoma hoja zikieleza kuwa hotuba imekaa kijanja janja, sasa ndugu zanguni elezeni ni wapi na takwimu zako halisi ni zipi?

2. Yote kumi lililonipendeza katika hotuba yote ni upunguzaji wa tegemezi katika bajeti toka (2005,) 44% hadi (2010), 28%. Hapa ndipo aliponifikisha.
Kwa sababu hili lilikuwa linaniuma sana tena sana, tena sana. Maana kwa upande wangu ilikuwa kama kujidanganya ukaeleza eti uchumi unapanda kwa asilimia 7, lakini bajeti yako kila mwaka inaongezeka kwa kutegemea misaada toka nje.

Nategemea hali hii ya kupungua itaendelea kila mwaka wa bajeti mpaka ifikie 10% ndio moyo wangu utatulia.
 
Nina wasiwasi pia JK anaposema serikali ya awamu ya tatu pale penye -VE outcome na kuacha kutumia serikali ya awamu ya tatu kwenye +ve outcome.

Bora angetumia neno serikali ya CCM. Mbona hausishi neno serikali ya awamu ya tatu na mradi kama wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Kahama ?
Pengine kumbukumbu zangu sii nzuri lakini nakumbuka RITES waliingia nchini JK akiwa rais... Ebu nitafute data zaidi lakini nina hakika Rites wameingia na kuweka mkataba na serikali wakati wa JK..
 
2. Yote kumi lililonipendeza katika hotuba yote ni upunguzaji wa tegemezi katika bajeti toka (2005,) 44% hadi (2010), 28%. Hapa ndipo aliponifikisha.

Huu lazima utakuwa ni ulevi au kupenda kupindukia unawezaje kusifia kitu kisichokuwa na consistency???????????? By the look of things kweli umekunwa na kufikishwa - left, right and centre.
 
Huu lazima utakuwa ni ulevi au kupenda kupindukia unawezaje kusifia kitu kisichokuwa na consistency???????????? By the look of things kweli umekunwa na kufikishwa - left, right and centre.

Sielewi ndoto ya mtanzania ilikuwa wapi, lakini ndoto yangu ilikuwa pale ambapo nchi yangu Tanzania itaondokana na bajeti inayotegemea wafadhili. Sikujua kwanini viongozi walikuwa wakilalama eti tusiingiliwe na mataifa ya nje wakati hayo mataifa ndiyo yalikuwa yakilipa mishahara ya watanzania mpaka mawaziri na Rais. Ukweli sikuelewa kabisa kwanini tulidai UHURU!!

Kwa takwimu zangu nilizonzo ni nchi moja tu Afrika ambayo haichukui hata senti tano toka mataifa ya nje katika bajeti yake ya Serikali. Nayo ni nchi ndogo iitwayo Eritrea. Ulaya hawaipendi kabisa kwasababu imetafsiri uhuru katika vitendo, na kwa maana hiyo wanashindwa kuibana kwa kutumia mbinu yao ya misaada.

Wakati Tanzania ikipata 44% ya pesa ya bajeti toka wafadhili, hii inamaanisha kuwa ukiwaudhi wafadhili basi hata mishahara ya watanzania haitakuwepo. Sasa utawaambia nini wanajeshi wakati hawajapata mshahara wao!

Usipoliona hilo kama ni hatua kubwa sana sijui nini kwako kitakuwa kikubwa. Wasalaam!
 
  • Kwa nini JK hasemi Kujiuzulu kwa Lowasa kama moja ya credibility za kuonyesha na kujenga dhana ya utawala bora na uwajibikaji.No matter lowasa awe na kosa au hana lakini alitakiwa ataje hili. Otherwise na yeye ni kama anaona alimtoa kafara mshikaji au anahisi bado anamuhitaji.

.

Amesamarise hotuba, vinginevyo ingechukua masaa 10 na wabunge wangesinzia.

La msingi ni kutaja mafanikio ya kiutendaji na ukuaji wa uchumi.
 
Back
Top Bottom