Hotuba ya rais Kikwete Bungeni Julai 16 - Full Text | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya rais Kikwete Bungeni Julai 16 - Full Text

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Jul 16, 2010.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Nimeiambatanisha hotuba ya JK kwenye attachment hapa chini, ipo kama word document, naamini ni rahisi kwa wengi kuipata na kuipitia.
   

  Attached Files:

 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Namnukuu:

  Mheshimiwa Spika,
  Kwa upande wa wasanii hasa wa muziki, katika miaka mitano hii tumeshuhudia kukua na kustawi kwa muziki wa kizazi kipya na uigizaji wa filamu. Nasikitishwa sana na hali ya wasanii kutokupata malipo ya haki kwa kazi zao. Niliamua nijaribu kusaidia. Nilipokutana na baadhi ya wana muziki wa kizazi kipya wakanieleza haja ya wao kuwa na mastering studio yao ili waweze kumiliki kazi zao. Nimeshawanunulia mtambo huo uliogharimu shilingi 50 milioni. Hivi sasa tumelipia mtaalamu mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam asaidie kutengeneza njia bora ya kusambaza kazi za wasanii wa muziki na filamu ili wapate malipo halali kwa jasho lao. Mafanikio ya zoezi hili yatatufundisha namna ya kuwasaidia wasanii wa fani nyingine pia.
  Mheshimiwa kweli kafanya kazi kubwa sana, ni mfano wa kuigwa :smash:
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa ni muongeaji mzuri. Utekelezaji mh! Pia bunge lingekuwa linajaa hivi mwaka mzima ingekuwa kheri
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]Michezo, Burudani na Utamaduni[/FONT]
  [FONT=&quot]Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&quot]Tuliahidi kuendeleza shughuli za michezo na utamaduni. Tumerudisha michezo mashuleni ili tujipe fursa ya kubaini vipaji vya watoto wetu na kuviendeleza. Nimetimiza ahadi yangu ya kumgharimia mwalimu wa mpira wa miguu wa Timu ya Taifa Stars kutoka nje. Kocha Marcio Maximo kutoka Brazil aliajiriwa na amesaidia sana kuinua kiwango cha soka hapa nchini. Tanzania imepanda kutoka nafasi ya 172 Desemba 2005 hadi nafasi ya 108 Aprili 2010. Mimi naamini kama tutaongeza juhudi tupo karibu kufanikiwa zaidi.[/FONT]

  [FONT=&quot] Tumeshapata makocha wa riadha na ngumi. Nimekubali ombi la CHANETA kumlipia kocha wa mchezo wa netiboli. Hivi karibuni nilisaidia kugharimia kambi ya mazoezi na posho za wachezaji wa Twiga Stars ili waweze kushiriki vizuri katika mashindano ya soka la wanawake Afrika. Ushindi wao ni fahari ya nchi yetu. Tutaendelea kuwasaidia ili waendelee kupeperusha Bendera yetu kwa mafanikio makubwa zaidi. [/FONT]
  [FONT=&quot]Nafurahi kwamba kupitia Taifa Stars moyo wa uzalendo umezidi kuongezeka miongoni mwa Watanzania. Tofauti na ilivyokuwa zamani, ni jambo la kawaida kuwaona Watanzania wakivaa jezi za timu yetu ya taifa au wakienda uwanjani wakiwa wanapeperusha bendera yetu ya taifa. [/FONT]

  [FONT=&quot]Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa upande wa wasanii hasa wa muziki, katika miaka mitano hii tumeshuhudia kukua na kustawi kwa muziki wa kizazi kipya na uigizaji wa filamu. Nasikitishwa sana na hali ya wasanii kutokupata malipo ya haki kwa kazi zao. Niliamua nijaribu kusaidia. Nilipokutana na baadhi ya wana muziki wa kizazi kipya wakanieleza haja ya wao kuwa na mastering studio Nimeshawanunulia mtambo huo uliogharimu shilingi 50 milioni. Hivi sasa tumelipia mtaalamu mshauri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam asaidie kutengeneza njia bora ya kusambaza kazi za wasanii wa muziki na filamu ili wapate malipo halali kwa jasho lao. yao ili waweze kumiliki kazi zao. Mafanikio ya zoezi hili yatatufundisha namna ya kuwasaidia wasanii wa fani nyingine pia.[/FONT]
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ahsante mhe rais kwa kuendelea kusimamia nchi yetu vizuri mpaka kuendelea kudumisha amani, utulivu na upendo wetu pamoja na kudumisha muungano wetu.

  Ahsante kwa kuendeleza yale mazuri yaliyoachwa na viongozi waliotangulia na kuweza kuhimili vishindo vyote kutoka kwa watu na makundi mbalimbali na ahsante tena kwa kusamehe wale wote waliokukosea kwa namna moja au nyingine katika utendaji wako

  Nakuombea mazuri huko mbeleni uzidi kuwa na nguvu zaidi kama ukifanikiwa kuchaguliwa tena na wananchi wa Tanzania uweze kutuwekea viongozi mahiri, shupavu na wazalendo ambao wataweza kuwa msaada kwako na kwa taifa hili siku za mbeleni.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,382
  Trophy Points: 280
  Nimerekodi sehemu kubwa ya hotuba ya Rais na utaweza kuiona kwenye channel yangu ya youtube/mwanakijiji
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Jamani, kuna baadhi ambayo ameyaongea anadai yametekelezwa, na anavyosema mengine yapo njiani kutekelezwa (mpeni kura!) hivyo tuwe watu wa subira, itapendeza mtu akasoma juu ya mafanikio ya awamu ya nne kwenye attachment na kisha akachangia, naamini hapo ndipo tutakuja na hotuba mbadala ya hii ya mheshimiwa rais.

  Nasubiri kwa hamu sana comments za comrade Malaria Sugu (MS)
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Jul 16, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,968
  Trophy Points: 280
  ..hapa ametoa pesa yake mfukoni kununua huo mtambo, au ni pesa ya serikali yetu?

  ..linganishe pesa hizo na mabilioni yaliyotumika kuileta timu ya mpira ya brazil.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh,Invisible na wewe unamkampenia Rais Kikwete,duu,kumbeee sasa nimepata nimekuelewa.
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Ni maneno tu hata kwenye kanga yapo!
   
 11. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Hebu msikilizeni Rais anachosema kuhusu suala la TRL ... "

  Nyote ni mashahidi kwamba tumehangaika sana na Reli zetu mbili za TAZARA na Reli ya Kati katika kipindi hiki cha miaka mitano. Kwa miaka kadhaa Reli reli zetu hizi zilikuwa na matatizo mengi na kusababisha huduma za uchukuzi wa abiria na mizigo kuathirika. Kiini cha tatizo ni uendeshaji usioridhisha. Kwa ajili hiyo, Serikali ya Awamu ya Tatu iliamua kutafuta kampuni ya uendeshaji wa reli ije isaidie kuendesha Reli yetu ya Kati. Hivyo ikapatikana kampuni ya RITES ya kutoka India. Wakati ule iliaminika kuwa kampuni hiyo ingesaidia kupata jawabu kwa tatizo linaloisibu reli yetu. Bahati mbaya matarajio yetu hayakuwa, ndiyo maana tumelazimika kufanya uamuzi tulioufanya wa kuanza mazungumzo na wabia hao ili Serikali ichukue tena reli hiyo na kutafuta namna nyingine iliyo bora ya kuiendesha reli yetu. "
  Mheshimiwa anaposema Bahati mbaya ana maana gani ? ........Huku ni kulea uzembe tuu, watu waliohusika walitakiwa kupelekwa Jela.
   
 12. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #12
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Read between the lines GS!
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu, mimi hapo niliposikia BAHATI MBAYA nikajua huyu alomwandalia amedhani kawa smart sana; na eti wabunge wakafurahi na kupiga makofi kisa kasema "Tulichukua maamuzi mazito sana kusitisha ubia na mwekezaji huyu (RITES)"
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mhe. anasema hivi:
  Mheshimiwa Spika,
  Wakati Mfuko wa Akina Mama umekopesha zaidi ya wanawake 300,000, hadi Mei 2010 Mfuko wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ulikuwa umekopesha shilingi 45.2 bilioni na wajasiriamali 67,000 wamenufaika. Halmashauri za Wilaya 128 zimekopesha vijana jumla ya shilingi 1.16 bilioni kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Vijana.

  Mipango ya Serikali ya uendelezaji wa sekta binafsi, uwekezaji na uwezeshaji wananchi kiuchumi imewezesha shughuli za kiuchumi kupanuka na hivyo kuchochea ongezeko la ajira nchini. Hivyo, utekelezaji wa ahadi ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM kuhusu kuzalisha ajira milioni moja umeenda vizuri, kwani hadi kufikia mwezi Juni 2010, ajira 1,313,121 zilikuwa zimezalishwa nchini kote.
  Kina mama gani hao wamenufaika hivyo? Hizi ajira pia nina wasiwasi sana, huenda kuna mtu anaweza kunifungua macho wakuu?

  Nahisi hapa ndipo kwenye MABILIONI YA KIKWETE! Nachoka kabisa, maanake kuna watu wamenufaika na fedha hizi lakini mamilioni ya watanzania wakiendelea kuishi katika hali mbaya sana mijini na vijijini.
   
 15. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ....read between the lines GS.....!
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Jul 16, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kauli hii ni matunda ya safari ya jana bungeni?
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mkuu unaweza kufikiria zaidi ya hivi; achana na hoja zilizoshafungwa kabisa... Kama huwezi kusoma between the lines basi kumradhi tu
   
 18. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wala si waziri aliyeyatamka maneno hayo bali ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Kikwete ndiye aliyetamka hivyo wakati akifunga Bunge la Muungano tar 16/07/10.

  Nanukuu sehemu ya hotuba
  ;"Katika kipindi hiki pia tumepandisha kima cha chini cha mshahara ya watumishi wa umma kutoka shilingi 65,000 mpaka shilingi 135,000 sawa na ongezeko la asilimia 107".......Mwisho wa kunukuu.

  Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi kima cha chini cha mshahara kilikuwa sh. 104,000 kwa mwaka wa fedha wa 2009/2010. Hivyo basi serikali wameongeza mshahara kwa takribani sh. 31,000 (30%). Hiki natumai ndicho kiwango ambacho serikali iliwaahidi TUCTA kuwa itakitangaza kutokana na mashauriano waliyoyafanya.

  Wafanyakazi sijui wachekelee au wanune kwa kuwa kima cha chini kilichotangazwa na serikali hakijafikia kile cha TUCTA hata kwa nusu yake?
   
 19. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  mbona anaongelea mambo madogo madogo, ambayo hastahili kuyataja katika hotuba. kazi kweli kweli
   
 20. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #20
  Jul 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Dah,

  Shy bana... Ama kweli ukipenda kitu huwezi kuona ubaya wake. Hayo mekundu mkuu ni ya kumpongeza JK seriously?
  Mkuu, wapo wanaoona kuwa ni MAKUBWA SANA haya na kuona kuwa RAIS kajitahidi kama unavyomwona mkuu Shy hapo juu!
   
Loading...