Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Zanta kama akitekeleza hayo ni faida kwa nchi sio madr peke yao!
Imagine gvt inamiliki fleet worth 5trillion sasa kama watayauza na kuwa na gari za kawaida si watasave zaidi ya 2 trillion leave alone maintanance cost ya hayo magari ie wese na service.
Sasa madai ya madr sidhani kama yanafika 2trillion which means akifanya smart spending nchi itakuwa na ela za kufanya mambo ya msingi on afya,elimu,kilimo nk
 
point. angeita press conference ili wamuhoji kama kweli serkali haikuhusika kumshughulikia dr. Ulimboka kwa kmung'oa meno, na kucha kwa koleo (unyama unyama - mafiosso wakubwa hawa) . JK. kama hamkuhusika alkubra mujaraba!!!!!!!!!!!!!! mtashughulikiwa na mola mwenyewe kadri alivyopanga
 
“Kwa nini serikali imdhuru Dk. Ulimboka? Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa,” alisema.

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Dk. Ulimboka aitesa serikali


na Hellen Ngoromera
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]

MUUAJI MKUBWA WEWE! ulimfunga babu sea na familia yake kwa lipi? UMEMUUA PROF MWAKYUSA KWA LIPI?
 
Binafsi hotuba ya raisi haikunifurahisha haikugusa maswala nyeti kama vile maisha magumu ajira hakuna hotuba yake ilikuwa zaidi kutetea serikali yake ya magamba. Kwakeli likikuelemea lazima uteleze huu ndio mtazamo wangu kwa hotuba ya kiongozi mkuu kama huyu
 
Nini kisichoeleweka kwako kama Rais amesema "kama kuna mtu wa serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake bnafsi na si Serikali au kutumwa na seikali." Hii imeeleweka wazi.

it is only a retard and the one who can not read between the lines, ndio anaweza kuelewa. Lakini mwenye akili timamu hawezi kuamini kuwa mahakama yetu huwa inaua watu wanaokaidi amri yake, au mtu anaye operate peke yake anapewa silaha, gari, radio call, maagizo na analindwa na serikali nzima na kupelekwa nje ya nchi.
 
Inlation isikutishe, wenye ujanja wa biashara wanaitumia hii chance ku export kwa wingi na wanawekeza kwenye uzalishaji wa kuuza bidhaa nje. Mbaya kukiwa na inflation halafu hatuwezi ku afford, mpaka sasa Bar zinajaa kila siku.

Kumbuka Tanzania kuna mzunguko mkubwa wa fedha zisizolipiwa kodi, hiyo inasababisha sana kukuwa kwa inflation. Measures zipo jikoni, usiwe na shaka.


wee vipi? unazungumzia suala la inflation halafu unafananisha na uongezekaji wa Bar?. Inflation ina direct effect katika maisha ya kila siku ya kila mwananchi, hizo Bar zako unadhani zinamgusa kila mwananchi hata yule asiyekunywa?. Una uhakika kuwa wananchi wana-afford huu mfumuko wa bei unaosababishwa na serikali dhaifu?
 
Ni wale aliosema kuwa walipinga tangu mwanzo uwepo wa Dr. Ulimboka kwenye mazungumzo ilihali yeye si mwajiriwa wa Serikali. Mh. Rais tutajie ili 'Tume ya Uchunguzi' ianze nao. Tafadhali Mheshimiwa...
 
huyu kiketwe hata hao wake zake hawamshauri. Kuli zake ni za utu uliokufa
 
Nadhani Stella Manyanya atamsaidia kuwataja maana inaelekea na yeye anawajua ila ameona bora avurumishe kwanza bomu kusiko ili wananchi watoe mawazo yao huko,lakini nadhani amechelewa sana,angemuuliza Chagonja na Msangi.
 
huyu kiketwe hata hao wake zake hawamshauri. Kuli zake ni za utu uliokufa

Mkuu, umekusudia kulikosea jina au bahati mbaya?
Makosa kama haya yanaufanya hata ujumbe wako
usieleweke wala kupewa uzito. Kuwa makini...
 
Kama Amiri Jeshi Mkuu wetu anaweza akapiga hatua moja mbele na kutangazia taifa kwamba KUNA UWEZEKANO WASHUKIWA WA JARIBIO LA MUAJI WA DR ULIMBOKA wakawa sehemu ya serikali yake lakini eti yeye hakuwatuma kufanya hilo sasa hadi hapo ni kwamba anachotafuta kutufahamisha hapa ni kwamba siku zote hizi madarakani ARMED FORCES zetu mbalimbali zimekua zikienenda tu bila UDHIBITI KUTOKA KWAKE kumbe???????????????????

Hakika kama huo ndio ukweli wa mambo basi kuna tatizo kubwa ajabu ki-utawala humo.Kimsingi ni lazima Rais Kikwete atueleze kwamba ndani ya nchi hii kumbe kuna Amiri Jeshi wangapi wanaohusika na kuongoza, kudhibiti, kutuma na kuadhibu vyombo vyetu mbalimbali vya usalama nchini????

Na kama hilo halitoshi, Rais vile vile akatueleze kwamba Alhaji Ahmed Msangi pamoja na Abeid waIkulu wote wako wapi hadi dakika hii?????????????? Kama hilo nalo atakua hajui kwamba sehemu ya wana-usalama anaowaongoza wako wapi kwa wakati gani na kwa dhumuni gani ... basi hadi hapo mie sisemiiiiiiii!!!!!!!!!!!
 
Kakiri kuwa huenda na watu wa state na wamefanya kwa sababu zao.....tumemzoea kukana,hata DOWANS alisema hawajui
 
Nimeamka ck nyingi ndo maana nina ufahamu juu ya jambo hili, Mkuu njia ndo hiyo, hizo zingine unazosema zimeshindikana. Mgomo wa kada yoyote una athari, walimu wakigoma kunakuwa hakuna elimu, madereva wa mabasi nao kunakuwa hakuna safari, Daktari naye wagonjwa wanakufa hiyo ndo kada yake, we unataka agome kula? nani atamsikiliza.

Na hayo ndo malengo ya mgomo wowote ili haki husika inayodaiwa ipatikane. Huwezi kuwazuia kudai haki zao kwa kisingizio cha watu kufa halafu madai yao yanashughulikiwa kisiasa, eti tunaendelea na mazungumzo,mpaka lini? hadi kufikia watu wakaamua kugoma ni kwamba haya madai ni ya muda mrefu. Mliolala amkeni sasa msikubali kuwa foolled kila siku kuwa serk haina uwezo ili hali fedha zinalundikwa kwe akaunt za viongozi huko uswisi na kujinunulia makasri hapa nchini na nje ya nchi, vijana wetu wanasoma kwa shida vyuoni ili hali tuna rasilimali nyingi ambazo iwapo mikataba isingalifungwa ktk misingi ya rushwa na ubadhirifu yasingalitokea hayo.

Wakati umefika sasa Kila mmoja asimame pale alipo adai stahili yake(wakulima, wanafunzi,wafanyakazi) M/mungu atalipa juhudi InshaAllah. mamayeyo usiogope kufa, wacha siye tufie wodini, lakini watoto na wajukuu zetu wanufaike hapo baadae na mgao sawa wa raslimali za Taifa letu.Hakuna anaye sapoti mauaji lakini fahamu kwamba hakuna kudai haki kwa lelemama, ikifikia hatua hii ni lazima watu wafe ili kupata mapinduzi ya kweli na ufumbuzi wa kudumu wa suala husika(watu wangapi walikufa South Afrika wakati wa kupinga ubaguzi wa rangi? lakini leo ni historia na kamwe ubaguzi ule haurudi tena mpaka kiama I swear, lakini kwa kuwa watu waliamua kukataa bila kujali watu wangapi watakufa) .

Kwa kuwa watawala tulionao wamekwisha fahamu watu wlionao ni wa aina ya mamayeyo ndo maana wanatuburuza. Tubadilike sasa tuache uoga usio na msingi ambao ndo umetufikisha hapa tulipo, Wanasiasa wanatuona waTZ kuwa ni watu mabongolala tusiojuwa haki zetu, tuziondoe hizi mindset kwenye vichwa vyao.

Zingatia hapo nilipoweka red. Ni kweli kabisa wanasiasa wanawaona ninyi ni mabongolala ndo wanawadanganya ili mgome, ndugu zenu wafe, na wao wakiugua wanapelekwa nje. Kama kweli mna uzalendo na mnagoma ili haki itendeke, basi mngehamasisha mgomo kwa wafanyakazi wa sekta zoote nchi, hapo ujumbe ungefika kwa sababu serikali isingeweza kureplace wafanyakazi wa sekta zote nchini. Lakini kwa sababu ya ulafi wa wachache wanaodai haki yao wenyewe hamtafanikiwa ng'o! Take my word.
 
Back
Top Bottom