Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hatutaki Rais mto porojo tunataka Rais Mtendaji, hata kusema kawafukuza kazi tu hawezi, anaweza nini sasa. bla bla bla bla kila kitu bla bla bla utafikiri mtoto anajifunza kuongea

Ulitaka aandamane ndio ujuwe kuwa anatenda. Hizo kauli tu zinakuonesha kuwa ni mtendaji na anafatilia kila kitu kwa kina.

Sasa hapo kazi ni kwa madaktari amma wafanye kazi, amma waache, amma waendelee na kugoma wafukuzwe. Nini zaidi?
 
Yuko yule Dr. mtetezi wa wanyonge? Ni mtanzania yupi anayemtetea? Mgomo huu una mshiko mkubwa wa viongozi wa kisiasa kutimiza malengo yao huku watanzania wa kawaida ndio wanaothirika, kumbukeni maiti haiti hazipigi kura.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Yuko yule Dr. mtetezi wa wanyonge? Ni mtanzania yupi anayemtetea? Mgomo huu una mshiko mkubwa wa viongozi wa kisiasa kutimiza malengo yao huku watanzania wa kawaida ndio wanaothirika, kumbukeni maiti haiti hazipigi kura.

Chama
Gongo la Mboto DSM
Si umemuona Mnyika kule kwenye thread nyingine.
 
Idiot! Hata mimi huwezi niita kazini unilipe 10,000 na nimesomea kwa miaka mi5.
 
Halafu mbona PM alisema kuwa hili suala liko mahakamani na haliwezi kuzungumzwa mpaka mihimili iheshimiane sasa huu mhimili wa Rais hauhitaji kuheshimu mingine in other way kesi iliyoko mahakamani haina mashiko kwani Rahis amekwishawaamuru waondoke au wafanye kazi. Au mie sijaelewa??????
 
nilimsikiliza jk jana jioni star tv star moja na nusu. hotuba iliyoandikwa hapa ndiyo ni sahihi. ndiyo yaleyale aliyoyasema.


nimejifunza yafuatayo:-
1- madai makubwa ya madaktari yanawahusu wao wenyewe. sijaona msisitizo mkubwa kuhusu vifaa kama t scan nk......
hii inaonesha kuwa tuliwatetea sn bila kujua undani wa madai yao.

2- pana uwezekano wa madaktari kurudi kazini na vile serikali imepata ujumbe, inaweza kuwatatulia mambo yao taratibu.


milioni 3 na nusu kabla ya marupurupu mengine ni hela nyingi kwa kuanzia. ukijumlisha marupurupu unaweza pata hadi milioni 10. madaktari bingwa watafikia hadi milioni 17 kwa mwezi. hizi ni pesa nyingi! madaktari wajue kuwa hawajasoma peke yao. hata wataalamu wa sekta nyengine nao wamesoma lkn mbona hawalipwi kiasi hicho. wakumbuke kuwa serikali husimamia gharama za mafunzo yao kwa 100%
 
Ulitaka aandamane ndio ujuwe kuwa anatenda. Hizo kauli tu zinakuonesha kuwa ni mtendaji na anafatilia kila kitu kwa kina.

Sasa hapo kazi ni kwa madaktari amma wafanye kazi, amma waache, amma waendelee na kugoma wafukuzwe. Nini zaidi?

Kama kusoma na kupata hekima za kufikiri imekuwa tabu basi jaribu maombi, hakuna sehemu yoyote kwenye hii hotuba ambapo Diwani Kikwete anaonekana kufanya maamuzi ya aina yoyote, hicho inachokifanyia reference ni kwamba kawarudishia mpira madaktari na huyo anayejiita muajiri ikionekana wazi kabisa amekwisha sahau kwamba aliwahi kujigamba kwamba yeye ndio muajiri mkuu, mbona haonyeshi huo uajiri mkuu.

Nionyeshe hapa, ni sehemu gani Diwani Kikwete katoa authoritative statement ya kuwafukuza kazi madaktari
Ndugu Wananchi;
Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa. Kwa sasa hatuwezi kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/= na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari.

Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.


Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun'guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.


bla bla bla bla bla
 
Jamani kama unaona mshahara ni mdogo si uhame, hao madaktari wana maslai yao hapo ndo maana wanangangania, yote ya kugoma ya nn, si waende uko Aga khan ambapo kuna vitendea kazi vizuri?
 
Nilisema na nitaendelea kusema Madaktari hususani wa Tanzania ni watu wa ajabu sana,wabinafsi wa kupindukia....huwezi kuamini katika madai yote 12 ni dai 1 tu(dai namba 11-Huduma za afya ziboreshwe nchini) ndo linaweza kuwa na manufaa kwa Wananchi kwa ujumla,madai mengine yote ni ya kunenepesha matumbo yao yafikie kule mpaka wawe wanashindwa kuhudumia wananchi...inachefua sana,ningekuwa ni mwenye mamlaka nchi hii ningeweka uaratibu maalum,kifo chochote kitakachotokea kwenye Hospital fulani kwasababu ya kukosa huduma za madaktari,au utolewaji wa huduma haba kwa makusudi ningekamata Madaktari wote wa zamu according to rosta zao na kuwahukumu kunyongwa mara 1,us***e mtupu,huwezi kudai Mill 8 kasoro kwa mwezi wakati watumishi wengine wa serikali wanachukua Laki 5,kwa maoni yangu hata hiyo option aliyowapa ni ya ajabu sana,na sasa ndo nakubaliana na Lowasa kuwa ni kweli Serikali ya J.K imekosa uwezo wa kufanya maamuzi magumu,huku ni kubembelezana pasipo sababu zozote za msingi.
 
kwa mujibu ya hotuba hii kiwete anahusika sana na kilichomtokea Dr. ulimboka...anajifnya kuongea kwa machungu na kuguswa lakinih hovyo ...''Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.''

I also wanted to say the same thing kutokana na hicho kipengele cha Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.''


Hapo mkulu anausika ni kwamba walishaona doctor ulimboka ndio kikwazo tangu mwanzo
 
Jamani hivi ni kwanini Serikali haitaki kusema kuwa "MADAKTARI WANADAI MAZINGIRA BORA YA KAZI NA SIO MISHAHARA NA POSHO" NIFEDHEHA KWA MKUU WA NCHI KUONGEA UONGO. Hii ni kupandikisha chuki kwa Wananchi dhidi ya Madaktari kuwa hawawajali wanajijali wenyewe hili jambo ni baya sana ukiliiangalia kwa undani ama kwa kina madhara yake ni makubwa.

JK na Serikali yako "DHAIFU" muache mara moja kupotosha UMMA kuhusu suala la MGOMO WA MADAKTARI

Hivi unajua kusoma vizuri kweli au wewe ni mmoja kati ya wale wanaofaulu kila mwaka kwenda Form I wakati hata kuandika majina yao vizuri hawajui?,wewe unasoma kabisa katika madai 12 yote ni moja tu la kuboresha mazingira bora ya kazi,11 yote ni posho na mishahara ya kunenepesha matumbo yao tu,bado unasema JK ameupotosha Uma,hii ni akili timamu kweli?
 
hivi lini mara ya mwisho JK kutembelea hospitali za serikali. siku moja akiwa hana safari za nje atembelee hospital za temeke muhimbili aone wagonjwa wanavyolala chini sakafuni ndio aone hali halisi ilivyo sio akae ikulu asubiri report kutoka kwa wasaidizi wake ambao mara nyingi hawampi hali halisi ya nchi ilivyo

Angefanya suprise visit kimya kimya akiwashtua watatandika mashuka mapya
 
SIKU chache baada ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Ahmed Msangi, kudaiwa kuhusika kwenye sakata la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, imeelezwa kuwa ofisa huyo amewekewa ulinzi mkali.
Habari za ndani ya jeshi hilo zinasema kuwa ofisa huyo anaishi kwa mashaka kutokana na tuhuma nzito aliyotupiwa, hatua iliyowafanya wakuu wake kumpa walinzi wawili wa kulinda usalama wake wakati huu ambapo uchunguzi unaendelea chini ya tume maalumu iliyoundwa.
“Issue ya Dk. Ulimboka imemweka pabaya afande Msangi, anaishi kwa hofu sana hadi kufikia hatua ya kupewa walinzi wawili,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Hata hivyo, pamoja na kukiri kusikia tuhuma hizo ambazo amezikana, Msangi ameliambia Tanzania Daima kuwa, yeye hana hofu kwa kuwa anajua hajafanya wala kuhusika kwa namna moja ama nyingine na tukio la Ulimboka.
Alikanusha kupewa ulinzi, ingawa Tanzania Daima lilishuhudia kwa siku mbili akiwa ameambatana na watu wengine wawili kila alipokwenda, ingawa alikiri kuwa ni askari wake na kwamba hilo ni jambo la kawaida.
Kwa mujibu wa kanuni za kazi za polisi, Kamanda wa Polisi wa mkoa ama wa Kanda Maalumu ndiye tu anayepewa ulinzi binafsi, lakini si mkuu wa upelelezi wa mkoa.
JK, serikali imtese Ulimboka kwa lipi?
Rais Jakaya Kikwete, ameeleza kushangazwa kwake na tuhuma zilizotolewa na baadhi ya madaktari na wana harakati kwamba serikali inahusika kumteka na kumpiga kikatili mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari, Steven Ulimboka.
Katika hotuba yake jana kwa Watanzania, Kikwete pamoja na kuelezea masikitiko yake makubwa na kuhuzunishwa na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dk. Steven Ulimboka usiku wa Juni, 26, 2012, alidai kushangazwa na tuhuma kwamba serikali inahusika na ukatili huo, akisema haoni sababu ya msingi ya kufanya hivyo, ikizingatiwa kuwa ndiye aliyekuwa kiungo muhimu baina ya serikali na madaktari.
Kikwete alisema ingawa ni ukweli kwamba Dk. Ulimboka hakuwa mtumishi wa serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano hayo na pia kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, bado ndiye aliyeamuru aachwe aendelee kuwapo maadam madaktari wenzake wamemuamini na anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na serikali.
Aliongeza kuwa kutokana na mwenendo wa mazungumzo ulivyokuwa ukiendelea, hakukuwa na sababu za serikali kufikia hatua ya kumdhuru Dk. Ulimboka.
“Kwa nini serikali imdhuru Dk. Ulimboka? Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa,” alisema.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Dk. Ulimboka aitesa serikali


na Hellen Ngoromera


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
 
Hapa ndipo ninapo amini serikali kuhusika katika sakta ala Mwakingwe.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"] [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 02 July 2012 08:08

Jakaya-Kikwete2.jpg

Mh Rais Kikwete[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]



ASEMA MADAKTARI WASIOKUBALI MSHAHARA WA SERIKALI
WAFUNGASHE VIRAGO


Boniface Meena
WAKATI Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka akiendelea na matibabu Afrika Kusini, Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali haihusiki na kilichomtokea daktari huyo kwa kuwa alikuwa kiungo muhimu katika majadiliano baina ya pande hizo mbili.

Rais Kikwete alisema hayo jana katika hotuba yake ya kila mwezi, ambapo mbali na suala hilo, pia alizungumzia sababu za mgomo wa madaktari na usafirishaji wa wahamiaji haramu.

Dk Ulimboka ambaye alikuwa anaratibu mgomo wa madaktari unaoendelea nchi nzima kutokana na Serikali kushindwa kutimiza madai yao mbalimbali, anatibiwa figo na majereha aliyoyapata katika sehemu mbalimbali za mwili, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana, kisha kupigwa, kung'olewa kucha, meno mawili na kutupwa katika Msitu wa Pande, usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.

Tangu kutokea kwa unyama huo uliofanywa na watu wasiojulikana, baadhi ya wananchi na wanaharakati wamekuwa wakiilaumu Serikali kuwa inahusika na utekaji huo na wengine wakienda mbali zaidi, kuwa watekaji walikuwa wanamlazimisha kueleza nani yuko nyuma ya mgomo wa madaktari.

Rais Kikwete, kama awali alivyosema Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, walisema wanatambua kuwa, Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka kuhusu kilichomtokea Dk Ulimboka, lakini yeye ameshangazwa na hisia hizo, kwani haoni sababu ya Serikali kufanya hivyo.

"Dk Ulimboka alikuwa kiungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali," alisema Rais Kikwete.

Alisema Serikali haina sababu ya kumdhuru Dk Ulimboka kwa sababu suala la mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kuusitisha, hivyo anayekaidi amri hiyo atakuwa ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola, ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu.

"Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dk Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru?" alihoji na kuongeza:

"Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali," alisema Rais Kikwete.

Alisema alichofanyiwa Dk Ulimboka kimemsikitisha na kumhuzunisha kwa kuwa ni kitendo cha kinyama na kinyume kabisa na mila na desturi za Tanzania.

Alisema Watanzania hawajazoea mambo hayo na kwamba ameelekeza vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane.

"Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa," alisema.

Alisema anatoa mkono wa pole kwa Dk Ulimboka na kumwombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania wenzake katika ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete pia alimpongeza Juma Mgaza ambaye alimsaidia Dk Ulimboka kumtoa katika pori alikotupwa na kumpeleka kituo cha polisi kwa moyo wake wa huruma.

Kuhusu mgomo
Kuhusu mgomo unaoendelea Rais Kikwete alisema, kiwango cha mshahara cha Sh3.5 milioni wanachokitaka madaktari Serikali haina uwezo wa kukitoa, hivyo daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara huo, awe huru kuacha kazi na kwenda kwa mwajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho.

Rais Kikwete alisema, kwa sasa Serikali haiwezi kuwaahidi kuwa inao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa Sh3.5 milioni na posho zote zile, kwani ikifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa Sh7.7 milioni kwa mwezi, kitu ambacho haitakiweza.

"Si vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama walivyo madaktari. Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha. Nasi tutamtakia kila la heri,"alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alisema, madaktari hawana sababu ya kugoma ili washinikize kulipwa mshahara huo kwani uwezo haupo.

"Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe," alisema.

Alisema mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo kwa wale wanaokwenda kinyume na sheria za kazi na wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma.

Alisema anajua baada ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa yatajitokeza, lakini ni bora kufanya hivyo ili ijulikane Serikali haina daktari.

"Mlitegemea mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya utaratibu wa kuziba hilo pengo na huyo anayekuja awe na mahali pa kuishi."

Kutokana na hali hiyo amewasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini, kwani Watanzania wanateseka na kupoteza maisha.

Sababu za mgomo
Rais Kikwete alisema kwamba, kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na mwafaka kwa kiasi fulani na kutoafikiana kwa baadhi ya mambo kati ya madaktari na Serikali.

Alisema suala la kwanza ni suala la kufanya kazi katika mazingira hatarishi ambalo Serikali imekubali hoja ya kuchukua hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi.

Pia alisema Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili na utekelezaji wake utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni yapi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike.

Rais Kikwete alisema kuwa, madaktari wamekataa suala hilo la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.

Alisema suala la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi ambalo Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia nyumba za kuishi.

Rais Kikwete aliongeza kwamba, kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango, Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba.

Alisema jambo hilo limekataliwa na madaktari na kutaka lazima walipwe asilimia 30 ya mshahara kama posho ya nyumba.

Rais Kikwete alisisitiza kwamba, Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali wanayotendewa kama wafanyakazi wengine wote wa umma.

Alisema suala lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu na pande zote mbili ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa watumishi wa umma, hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao.

Kuhusu posho, alisema Serikali imekubali kuwapo posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.

Alisema madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali ilipe posho hiyo sasa.

"Tofauti hapa si posho hiyo kuwapo, bali ni rai ya Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo. Madaktari hawaoni haja ya kufanya hayo," alisema.

Alisema kuna mambo mawili ambayo hayakuwa na mwafaka kabisa kati ya pande hizo mbili na la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance).

Rais Kikwete alisema, Serikali ilishaongeza posho hizo tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka Sh10,000 hadi Sh25,000 kwa daktari bingwa, Sh20,000 kwa dakari mwenye usajili wa kudumu na Sh15,000 kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo kazini (Interns).

Alisema hata hivyo, madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara.

Rais Kikwete alisema ugumu wa kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa kazini na kwamba ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea aendelee kulipwa.

Alisema jambo la pili ambalo mwafaka haukufikiwa baina ya Serikali na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari ambao madaktari wanataka uwe Sh3.5 milioni wakati Serikali inasema kiasi hicho hatukiwezi.

Alisema Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati ya asilimia 15 mpaka 20 kama ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha.

Rais Kikwete alisema, kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya Sh1.1 milioni na Sh1.2 milioni kutegemea kiwango kipi hatimaye kitaamuliwa.

"Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania Sh3.5 milioni," alisema.

Alisema ni muhimu madaktari wakatambua kuwa wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwapo hata kwa mujibu wa maadili ya udaktari.

Alisema viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza madaktari katika mgogoro na mahakama na waajiri wao isivyostahili.

Rais Kikwete alisema ni vyema viongozi wa madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana mahakamani kuwa hahusiki nao.

Rais Kikwete alisema madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka hatarini kwani mfanyakazi hana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa kushiriki mgomo unaokubalika kisheria.

"Huu siyo. Watapoteza ajira, hawana pa kukimbilia, hawana cha kuwalinda. Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao, kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali. Lazima watafakari kwa hayo wafanyayo," alisema.

Hoja za madaktari
Rais Kikwete alisema katika mambo 12 ambayo madaktari waliyawasilisha pande zote mbili zilifikia mwafaka na kukubaliana kwa pamoja kwa mambo saba.

Alitaja la kwanza ni kuhusu usafiri wa kwenda na kurudi kazini ambalo limeshashughulikiwa.

Alisema jambo la pili, ni madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya Afya ambalo Serikali na Wizara ya Afya zimechukua hatua za utekelezaji wake.

Jambo la tatu, alilitaja Rais Kikwete kuwa ni hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya ambalo tayari Serikali imechukua hatua.

"Uongozi wa juu wa wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya. Lakini, jambo la kustaajabisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona. Kwanza walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na kamati yake kwa miezi mitatu bila ya mafanikio," alisema.

Rais Kikwete alisema kuwa, jambo la nne walilokubaliana ni viongozi kuwalazimisha kupewa rufaa ya kutibiwa nje suala ambalo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amewaeleza madaktari wazingatie maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au asiwe kiongozi.

Alisema jambo la tano ambalo pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari waliofukuzwa.

"Hawa ni wale Interns waliokuwa wamerudishwa wizarani kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na Lugalo. Hili ni jambo ambalo lilikuwa limemalizika kitambo na wote walikuwa wamerudi Muhimbili," alisema.

Rais Kikwete alisema jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya ambalo Serikali imeliafiki.

Rais Kikwete alisema jambo la saba, ambalo pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza posho ya uchunguzi wa maiti.

Alisema jambo hilo jipya halikuwepo mwazoni, hata hivyo, Serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka Sh 10,000 hadi kufikia Sh100,000 kwa daktari na Sh50,000 kwa wasaidizi wake,” alisema.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Idadi kubwa ya wakazi wa nchi hii wanajua jinsi Mh Jakaya Mrisho Kikwete alivyo na visasi na anavyooua wale anaoona wanamzuia njia yake ya kufilisi nchi hii
Mwandosya alimzuia asinunue IPTL
Mwakyembe alikuwa against na mtandao haramu wa wafirisi wa mali za umma uliomuweka madarakani Kikwete
Dr Ulimboka- amesimama wima kuhakikisha sekta ya afya inaboreshwa
huyu Jakaya hawezi kutushawishi kwamba hajatoa amri kama amri jeshi mkuu kuamlisha kuwauua watu hao jambo la kumuuliza ni kwamba amenufaika na nini baada ya kuwajeruhi hao
 
Kwani tangia lini hasa kwa hawa wanasiasa wamekubali jambo japo uchunguzi unafanyika na mambo yanaishia juu kwa ju. Kwanini jk usikubali tu nchi imekushinda ukaachia madaraka wakaendelea wanao weza? Ukifanya hivyo tutakuona shujaa
 
nyinyi ndio umewashuka kwa uongo wenu. Kikwete kaweka wazi asiyetaka aache kazi kwanini ahangaike kugoma? Si aende atakapoyapata hayo?

Kumbe kikwete ndiye aliyewazidishia mishahara ya kuanzia kutoka chini ya laki mbili mpaka zaidi ya millioni, leo yeye ndiye mbaya? Amma kweli hamna zaidi ya ufataani tu.

"usiku na mchana wanafanya kazi kwann wasiongezewe kula? Mbunge analipwa sh. Ngapi? Anafanya kazi mda gani? Elimu yake unaijua? Tunagoma hamwez kufukuza hata! Utani tu huo!
 
Mbona Madaktari walikua wanaendelea na mgomo wakati swala lipo mahakamani????
Its high time waemde wakaajiriwe huko wanakoona watalipwa zaidi.
Mwajiri binafsi atawapa Key Performance Indicator na review za kila mwezi.
Most of them (sio wote)wamezoea kuzuga zuga hospitali za serikali na kuwaelekeza wagonjwa hospitali zao/walizoajiriwa binafsi.Roho ya mtu haina Price TAGS.Mamia ya wananchi wasio na hatia wameumia,wamekubaliwa mambo 7 out of 12 atlist wangepunguza ukali wa mgomo basi.Au wangegoma kuwatibia viongozi.Tunawaheshimu sana Madaktari ni kweli kazi wanayoifanya ni ngumu na ina risk but naona walikua selfish na wali exagerate the situation.Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Africa.
 
Back
Top Bottom