Suala la madaktari naona Mkuu ameendeleza propanganda zilezile za kwamba kulikuwa na makubaliano. Makubaliano gani wakati mazungumzo yalikuwa hayajakamilika, hebu tuwekeeni haya makubaliano yakiwa na sahihi za pande zote mbili tuone.
Na JK ameendelea kuudanganya umma na kuufitinisha na madaktari kwa kuonyesha kuwa madaktari tatizo kubwa waling'ang'ania mshahari wa mil 3.5 wakati walikuwa wanajadiliana na kabla ya makubaliano serikali ikatangaza hizo 15% na labda sasa wanafikiri kuongeza mpaka 20% maana hii haikuwepo mwanzo. JK bila aibu anautangazia umma nyongeza ya posho ya kuchunguza maiti, dai ambalo halikuwepo kati ya yale waliyokuwa wanajadili.
JK acha kutishia nyau, hamuwezi kufukuza madaktari wote walioko kwenye mgomo, mnajidanganya, wasikilizeni madaktari na mfikie muafaka warudi kazini, kuendeleza vitisho na kuwakamata na kutesa viongozi wao haitawasidia.
Huduma gani zimeboreshwa kwenye hospitali za mikoa eti na sasa wanageukia wilayani, hii sio era ya kusema uongo na ukafikiri utapata watu. Ukifika mahospitalini sasa hivi hakuna dawa, hakuna vifaa tiba, hakuna watumishi. Hospitali eti zimepandishwa hadhi ya kuwa za rufaa zikiwa hazina madaktari bingwa, sasa nashangaa kama rufaa inatoka kwa MD inakwenda Kwa MD sijui itakuwa rufaa ya namna gani hiyo. Hospitali kuzitaja kwa uchache ni mfano hospitali ya mkoa wa rukwa ambayo ina bingwa mmoja tu ambaye ni surgeon nae yuko kwenye administration. JK usitupige changa la macho hakuna maboresho yoyote yalofanywe. Nchi imekushinda step down.
mkuu sio kwamba utashindwa kwenda Jamaica kubembea.Mnafiki Mkubwa dhaifu, TISS na mwanao ndio ulowatuma kumfanyia unyama Ulimboka, utalipa hapahapa duniani.