Elimu kwa Umma: Tumia Wakala kwenye Safari za Ndege au Huduma za Hoteli kuepuka hasara na kuharibu ratiba zako

Bonheur Travels Tanzania

JF-Expert Member
Dec 29, 2020
252
499
Ndugu WanaJF,

Kwa mara nyingine tena tunakuja na uzi mahsusi kwa wote wanaofanya safari kwa njia ya anga. Huu ukiwa ni mwendelezo wa mtiririko wa threads zetu za Elimu kwa Umma ambapo tunakusudia kuelimisha wasafiri na wanaotarajia kusafiri kuhusu mambo mbalimbali ili safari zao ziwe salama na zenye mafanikio bila kupata hasara wala kuharibu ratiba zao.

Leo tungependa kushauri juu ya umuhimu wa kutumia Wakala (Travel Agency) pale unapopanga safari yako iwe ni mapumziko, kutalii au kujifunza. Tutaambatanisha na huduma ya booking kwa ajili ya hoteli au sehemu za kupumzikia hasa ugenini.

Swali ambalo mara nyingi watu huuliza ni; kwanini nitumie Wakala badala ya kwenda "direct" mtandaoni au kwenye kampuni husika (mfano shirika la ndege) kukata tiketi au ku-book hoteli?

Ni kweli. Kufanya huduma moja kwa moja kwenye kampuni au shirika husika inaaminika kuwa ni njia salama na yenye mantiki kwa kila anayetumia huduma. Pia kuhusu gharama, inaaminika kuwa kukata tiketi moja kwa moja na kukata tiketi kupitia kwa wakala huenda kukawa na tofauti za bei na kadhalika, jambo ambalo sio kweli.

Hata hivyo, kuna faida kubwa zaidi kwa mteja kutumia Wakala badala ya kwenda kufanya huduma moja kwa moja kwenye wavuti au ofisi za shirika la ndege / hoteli husika. Kwa uchache, faida atazozipata ni pamoja na:

1. Wakala humsaidia mteja kuhusu mchakato mzima wa ukataji tiketi au ku-book hoteli kabla, wakati na baada ya safari/likizo husika. Hapa ni pamoja na kumsaidia kuahirisha safari wakati wa dharura, kumshauri na kumsisitiza kuhusu muda wa safari, ratiba za safari na taratibu nyingine zote ambazo mara nyingi abiria hujisahau na kujikuta wanapata hasara au wanaharibu ratiba zao.

2. Wakala humsaidia mteja kuchagua ndege au hoteli bora kulingana na bajeti yake. Mara nyingi hutokea abiria kulazimika kulipa gharama za ziada tofauti na bajeti yake ya awali pale anapofanya booking moja kwa moja bila kujua kama kuna options nyingine. Faida hii anaipata kwa wakala pekee.

3. Wakala humpa ushauri wa kweli (honest) mteja kuhusu sehemu ambazo anaweza kwenda kufurahia huduma kwa gharama rafiki kupitia machaguo ambayo wakala anayo kwenye orodha yake.

4. Uhusiano baina ya Wakala na Mashirika au Hoteli mbalimbali hurahisisha kupewa kipaumbele anapofanya booking. Hii ni kutokana na kufanya nayo kazi mara kwa mara. Ni rahisi zaidi kwa wakala kuwasiliana moja kwa moja na watoa huduma kama kuna mapendekezo anayotaka kufanyiwa kwa niaba ya mteja.

5. Wakala humpatia namba ya simu mteja ambayo watakuwa wakipigiana simu muda wowote ikiwa kuna kitu mteja anahitaji. Hilo mteja hawezi kulipata kutoka kwenye tovuti za booking au kampuni husika.

Na mengine mengi tu.

Kuhusu hofu ya gharama; mara nyingi kama sio zote mteja hulipia gharama ile ile ambayo angechajiwa na shirika la ndege/hoteli au pengine chini yake kutokana na mapendekezo ya Wakala au "ofa" ambazo wakala anapatiwa na mashirika/hoteli hayo.

Hizo ni faida na ushauri wa kitaalamu ambao tumeona tuwapatie kutokana na uzoefu tulionao kwenye industry hii. Sio shurti kufanya hivyo. Mwisho wa siku muamuzi wa mwisho ni mtu mwenyewe.

Karibuni kwa maoni na maswali kama yapo turahisishe maisha!
 
Website za airlines na booking.com zipo nimlipe Agent Commission fee ya 70USD kwa kazi gani? Baadhi tuna-accummulate points kila tulisafiri tunapata discount/upgrade Sasa ya nini nipate stress Tena?
 
Website za airlines na booking.com zipo nimlipe Agent Commission fee ya 70USD kwa kazi gani? Baadhi tuna-accummulate points kila tulisafir tunapata discount/upgrade Sasa ya nn nipate stress Tena?

Chagua Agent ambaye hatozi hizo fee.

Wapo Mawakala ambao wanalipwa na shirika au hoteli husika hivyo hawamchaji mteja chochote na bado wanampa hiyo personal assistance ambayo hawezi kuipata kwa mtoa huduma wake.

Mfano sisi Bonheur Travels Tanzania hatuchaji gharama za ziada wala tozo yoyote ile kutoka kwa mteja.

Asante.
 
Nakubaliana na wewe sometime kufanya bookings na Wakala inaweza kuwa rahisi zaidi kuliko kufanya wewe binafsi. Hasa kipindi cha high season.
 
Kwa kuongezea:

Travel Agent anamsaidia mteja kujaza fomu mbalimbali au kumtafisiria mantiki ya kila kipengele pale ambapo mteja atapata tabu kuelewa.

Inatokea mara nyingi, abiria wa ndege hushindwa kusoma maelekezo ya tiketi na matokeo yake kuachwa na ndege au kuharibu ratiba zake.

Faida hii ni muhimu sana kwani mteja anakuwa na access ya kuwasiliana "kirafiki" na Agent muda wowote hata usiku wa manane
 
Kwa kuongezea:

Kila Travel Agency ina taratibu zake na namna inavyofanya biashara na wateja wake. Kwa asilimia kubwa, hazitakiwi kutoza tozo yoyote kwa abiri kwa kisingizio cha service charge, zinazofanya hivyo ni aidha hazina muda mrefu kwenye kazi hizo au hazina 'connection' ya kutosha.

Ni vyema kuchagua Agency ambayo haitozi gharama zozote za ziada bali zile za huduma tu kama zinavyoainishwa kwenye mashirika ya ndege au mahoteli husika.

Asante.
 
Kwa kuongezea:

Epuka kumlipa Agent pesa yoyote moja kwa moja. Agent anatakiwa kukusanya taarifa zako tu za malipo kisha malipo hayo unayafanya moja kwa moja kwenye shirika au hoteli husika.

Zipo Agency zinachukua pesa kwa mteja kwa kisingizio cha kusaidia mchakato wa malipo, japo sio kwa nia mbaya lakini inapotokea dharura na agency husika ikashindwa kuendelea na biashara, migogoro huibuka na wateja wengi kuanza kufuatilia mchakato wa malipo yao huku wengine wakipoteza muda na fedha.

Epuka.

Asante.
 
Hapana sina. Umenipa elimu. Mimi nilikuwa nawaogopa sana travel agencies kwa kigezo cha surchages.

Asanye kwa elimu.

Karibu sana mkuu. Tunafurahi kusikia umepata elimu.

Ni matumaini yetu utafanya maamuzi makini wakati unapotaka kufanya safari au kutafuta sehemu za mapumziko.

Tunakutakia kila kheri.
 
Kwa kuongezea:

Hakikisha Travel Agent unayemtumia amesajiliwa na ana uzoefu na ujuzi wa huduma hiyo. Hii itakusaidia kunufaika na mahusiano yake ambayo ameshayajenga na mashirika ya ndege, kampuni za utalii na mahoteli mbalimbali kwa muda mrefu. Pia kwa uharaka wa kufanikisha mipango yako.

Asante.
 
Mbona hata website kampuni yenu haina? Hii day and age mnategemea mtu anaishi arusha aje kwa ofisi yenu dar kwa mahitaji ya usafiri?
 
Back
Top Bottom