Acha ujinga wamevunja sheria hawawezi kuachwa...
Kumbuka, kuna good laws na bad laws.
Suala sio ujinga. Na pia nachelea kusema sina uhakika kama kuna mahakama zimeshatolea ufafanuzi juu ya ukiukwaji wa sheria katika maeneo husiak, ukiachilia Jangwani na maeneo ya Mto Msimbazi. Hivyo sisi kama Taifa, tuna haja ya kutafakari kwa kina athari zitakazojitokeza. Kwa wale ndugu zetu wa Jangwani waliopewa mpaka viwanja na mifuko ya saruji, hao sina cha kuwatetea. Ila kwa Hotel kama Double Tree & Slipway hapa endapo kama zikivunjwa, hiyo itakuwa imekula kwetu kama Taifa. Kwanza, hizo hotels zinatoa ajira kwa watanzania wengi....japo kuna mtakaokuja kusema ajira zenyewe hazitoshei kimapato lakini wafanyakazi wanaishi. Serikali inapozibomoa, hata hicho kidogo kilichokuwa kikipatikana na kupelekwa nyumbani hakitakuwepo. Pili, serikali nayo itakosa mapato katika kodi...kuanzia kodi ya jengo, vat, paye, na sdl. Pengine ili kuondokana na kadhia iliyopo, na endapo kweli hotel hizo ziko kwenye njia ya mkondo wa maji, ni vyema kuzitaka zigharamie ujenzi wa mfereji kulingana na mainjinia wa manispaa watakavyoshauri.
Vivyo hivyo natoa rai kwa Serikali ya JPM kuhakikisha kwamba busara inatumika zaidi katika maamuzi. Ni dhahiri Dar kuna maeneo mengi 'yamevamiwa' na watu kujenga pasipo ramani ya mipango miji. Badala ya kutupiana lawama, kati ya jiji na wananchi, Wizara ya Ardhi chini ya Mh. Lukuvi wanahitaji kutumia weledi wao zaidi katika kuangalia wepi kuna majengo hatarishi na kuhakikisha wanayaondoa. Pia, serikali ihakikishe kwamba nakala ya ramani ya mipango miji, katika eneo husika inapatikana katika ofisi za Serikali ya Mtaa na sio wao kuikumbatia katika ofisi za Manispaa na huko Wizarani. Nashauri ramani ziwekwe Serikali Mtaa kwa sababu huko ndiko viwanja vingi vya maeneo ambayo hayajapimwa hupata baraka zake wakati wa manunuzi....ile tozo ya 10%.
Mwisho, tusisahau kwamba kwa jiji kama Dar majengo mengi yamejengwa kiholela, na serikali hii hii imekuwepo muda wote ikiachia hali iendelee kufikia mahali hapa. Maadam nia na uthubutu wa kuboresha makazi yetu ni mzuri, lakini bado kuna haja ya suala hili kushughulikiwa kwa busara na hekima zaidi kuliko kutumia nguvu. Tusipoangalia, tutajikuta tunavunja jengo la Tanesco Ubungo kwa kusimamia tafsiri ya sheria (good or bad?) na huku kodi zetu zikiendelea kupotea pasipo na tija.
Nawasilisha.