Golden Rose ninavyofahamu siyo hotel ya Mama Maeda.
Ilijengwa kwa hela hela za mtoto wake aliyekuwa akisoma Urusi na anaitwa Rose.
Wakati wa Ukoministi, alikuwa akifanya biashara kubwa sana kati ya Urusi na West Europe, na wakati huohuo Tanzania na Urusi. Pale uwanja wa ndege walikuwa wakifikiri anafanya kazi ubalozini maana alikuwa anajaza ndege vifaa kibao kutoka Russia. Kumbuka kuwa miaka hiyo, Warusi hawakuangalia sana faida ya abiria na mizigo. Ndege zao mara nyingi zilikuwa zimejaza silaha na hivyo wakati wa likizo, wanakuwa kama vile wanawaachia na wengine wafaidi kidogo. Ndiyo maana wanafunzi wa Urusi walikuwa wakirudirudi sana nyumbani miaka ya 80 kwani bei ilikuwa rahisi sana.
Anyway, turudi kwenye hoteli yetu. Ila hizo nguzo zinaonekana nyembama sana kwa jengo la ghorofa 15. Ndiyo haya majengo ikitokea kituko cha Haiti, hakuna atakayepona humo ndani maana lina-crush utafikiri kipande cha Zege kwenye crushing test.