Hoteli ya Mgonja? Parrot Hotel

Hoteli ya Mgonja? Parrot Hotel

Hiyo hotel inapigwa nyundo balaa yani walikua wanavunja kila mara humo ndani,pia finishing yake sio nzuri kama imelipuliwa tu
Hakukabidhiwa engineer mmoja, kuna maengineer walikula pesa na kusepa pale, ndio maana Mzee haelewani na vijana wake, ni wasomi Ila Mzee hawashirikishi kwny mambo ya msingi analeta watu wake wanampiga pesa halafu wanasepa zao

Kwenye finishing keshaita kampuni kama 4 za wahandisi

Labda kama humjui Shana Boy ndio unaweza kushangaa
 
Ka Magu kana wivu kwa wezi wenzie! Hakataki kapitwe wakati kenyewe ndio kanamilki fuko la hela!
 
Mkuu Lifer good analysis.Hili jengo karibu wakaazi wote wa mji wa Arusha wanajua linamilikiwa na G Mgonja tatizo linakuwa jinsi ya kumlink na umiliki.Hassan Hussein Mshana hana ubavu wala wazo la kuwa na jengo kama hili anatumikia wakubwa.

Hii issue kwa kiasi kikubwa inafanana sana na umiliki wa Kibo Hotel ambayo mheshimiwa B P Mramba anaimiliki kwa siri.Baada ya kustukiwa nasikia ameamua kumuuzia Uhuru kenyatta.

Serekali ikitumia vyombo vyake vyema kama UWT na TRA bwana Hassan Hussein Mshana hatakuwa na ujanja wa kuendelea kutudanganya.

Mkuu Lifer tunasubiri nondo zako kwa hamu.
UWT!?! Huu sasa utani.
 
Hii Tanzania tamu sana jamani kha! Nilikuwa nihamie Zimbabwe sihami tena kwani nitakosa hizi songombingo za kaboka mchizi 🤣 😀
 
Daaah hiyo nyumba kweli finishing yake ni hovyo,mradi umetumia pesa nyingi ila haikamiliki,bado bank walikua na mzozo nae kipindi cha 2018
Mgogoro ni kuwa hiyo bajeti hapo aliwekewa na kampuni moja ya uhandisi, yeye alikuwa na pungufu ya hela hiyo...akaenda bank kukopa ili amalizie vitanda, makabati, secretary stuffs na vitu vidogovidogo, akashindwa kurejesha pesa kwa wakati na wale wahandisi wakaondoka

Nahisi sasahv pesa itakuwa imejidouble kwa penalties kwasababu uchumi wake si mzuri na hata angemaliza mwaka huu hakuna wageni

Yaani kifupi tatizo kubwa la pale ni Management, yule Mzee ni Mbishi na mjuaji haswaa na hapendi Outsourcing

The situation is terrible
 
Kibao mbele ya jengo kinasema:

Proposed Building of Parrot Hotel...
Client: Hassan Hussein Mshana...

Jengo la katikati linaitwa "Arusha Consultants House" limefunguliwa hivi karibuni. Jengo la rangi ya Pink ni "Arusha Golden Rose" la Mama Maeda.

Mmiliki wa hili jengo la Parrot Hotel according to nyaraka za Arusha Municipal Council, ni jamaa mmoja anayefahamika kwa jina la Hassan Hussein Mshana, maarufu mjini Arusha kwa jina la "Shanna Boyz". Huyu bwana Mshana, anajihusisha na biashara ya wholesale ya mafuta ya kupikia na vitu vya matumizi ya kila siku kama Viberiti, Sukari etc. Pia inasemekana kuwa, ana migodi ya Tanzanite huko Mererani, wilaya ya Simanjiro, mkoa wa Manyara. Ujenzi wa hii hoteli ulianza mwanamo mwaka 2005. Kabla ujenzi haujaanza, kiwanja inapojengwa, kilikuwa kikitumika kuuzia mbao wakati wa mchana na kuegeshea Mabasi ya "Air Msae" wakati wa usiku. Inasemekana kwamba, aliyekuwa akiuzia mbao kwenye hiki kiwanja ndiye aliyekuwa amewakodishia wamiliki wa "Air Msae" sehemu ya kuegesha mabasi yao usiku.Kwa jina anaitwa "Kampa" na kabila lake ni Mhaya kutokea Bukoba. Hata hivyo, kiwanja hakikuwa cha kwake (Kampa) bali yeye pia alikuwa amekodisha kutoka kwa wamiliki halali ambao according to nyaraka za office ya registry of lands, northern zone, iliyopo Moshi, ni shirika moja la umma linalofahamika kwa jina la "NEDCO" (National Estates and Design Company)

Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema, huyu bwana Kampa, alimtapeli bwana Hassan Hussein Mshana kwa kumuuzia hicho kiwanja wakati akijua fika yeye siyo mmiliki halali wa Kiwanja. Inasemekana kwamba, bwana Mshana aliingia mkenge baada ya Kampa kumpa title feki ya kiwanja iliyokuwa ikionyesha kuwa Kampa ndiye mmiliki, wakati sio(Wamiliki halali ni NEDCO).Baada ya Mshana kununua kiwanja kutoka kwa Kampa, alianza mara moja ujenzi wa Hoteli yake ya "Parrot". NEDCO wenye offiici zao Mkoa wa Dar es Salaam, ndipo wakapata habari kwamba kiwanja chao kimevamiwa na kuna ujenzi kabambe wa hoteli unaendelea.NEDCO walijaribu kumtafuta bwana Kampa wamuulize nini kinaendelea bila mafanikio. Wliposhindwa kumpata Kampa, NEDCO walikimbilia mahakamani na kufanikiwa kupata injunction ya kumsimamisha bwana Mshana asiendelee na ujenzi.Pia walimfungulia Mshana shitaka la "Tresspassing" on their property.Mshana alipokuwa served na injunction ndipo akashtukia kuwa alikuwa kaingizwa mjini na Kampa. Mshana aka retain legal counsel, legal counsel wakamshauri aombe "out of court settlement" na NEDCO.Inasamekana hii settlement ili invlove NEDCO kumuuzia Mshana kiwanja hicho hicho for an "undisclosed" sum of money.Suggesting that Mshana paid for the same plot twice!!

Mpaka leo hii haifahamiki Kampa yupo wapi. Kuna an "outstanding" warrant for his arrest at the Arusha Central Police Station, to face charges of Fraud & Forgery.Anyways, baada ya settlement na NEDCO, Mshana thought his problems were over, kumbe infact they had just began. Manispaa ya Arusha ambao ndio wahusika wa kutoa vibali vya ujenzi, wakamsimamisha asiendelee na ujenzi kwa kuwa ailkuwa akijenga bila "building permit" Habari zisizothibitishwa zinasema kuwa, manispaaa ya Arusha wakati huo ikiwa chini ya Mkurugenzi (Noah Mwaikuka) pamoja na mwanasheria wa manispa "Solicitor general" (Anderson Msumba) pamoja na Engineer (S. Ngagani) walipata amri kutoka the highest levels of government, wampe mara moja kibali cha ujenzi bwana Mshana. Bwana Mshana hatimaye alipata kibali cha ujenzi ndani ya wiki moja(bila kupigwa fine yoyote) akaendelea na ujenzi wake.


.......Story continues later, where I will talk about the connection between Hassan Hussein Mshana and former Permanent secretary - Paymaster General, Ministry of Finance, Tanzania (Gray.S. Mgonja). I will also talk about how Initially, The Contractors Registration Board of Tanzania (CRB) and later the Engineers Registration Board (ERB) of Tanzania tried to stop the construction of this "Parrot Hotel" bila mafanikio, due to powerful forces within government always intervening on behalf of Mshana........ stay tuned...
Hassan Hussein Mshana, maarufu mjini Arusha kwa jina la "Shanna Boyz"......Hatunaye tena. Mazishi yake ni leo tarehe 17.2.2021. tatizo la kupumua.
 
Mtoa mada labda aliminywa kabla hajamalizia story yake, Kwa Arusha, jengo hili linahisiwa ni la Mgonja. nyuma ya hili jengo kuna nyumba za NSSF na kwa taarifa nilizonazo, mmiliki wa jengo hili amezinunua ili kuongeza eneo la car park na tayari wapangaji wa nyumba hizo walipewa notice ya kuhama.
Sio nyumba za NSSF, ni nyumba za benki
 
Duh hili tatizo la kupumua limekuwa zito kweli kweli hasa kanda yetu ya kambo.
 
Back
Top Bottom