Kwa sasa Hospitali ya KCMC ina huduma mbovu sana kuliko hospitali zote za rufaa za zamani(Muhimbili, Mbeya, Bugando)
Japokuwa ni taasisi bora sana kwa mafunzo kwa wataalamu mbalimbali wa afya lakini kwenye kutoa huduma huwezi kuamini kama hii ni Hospitali inayomilikiwa na Kanisa tena wanaiita taasisi ya Msamaria mwema!!
*Mambo kama haya ni ya kawaida kabisa kwa sasa pale KCMC
1/RUSHWA
(Kuanzia getini kwa walinzi, wafagiaji, Nesi, Wanafunzi, Madaktari mpaka chumba cha operation)
2/LUGHA CHAFU
(Ni jambo la kawaida kabisa mtumishi kumtukana mgonjwa au ndugu wa mgonjwa, Staff wa utawala wana lugha ya nyodo kama miungu wadogo)
3/USUMBUFU
(utaambiwa faili halionekani, Urudi kesho, fomu za bima hazipo, Muhusika hayupo kn)
4/UKABILA
(Pale ni uchaga kwenda mbele, kama wewe sio mchaga huna chako, wachaga wamefanya kama hospitali yao)
5/NGONO
(Ipo wazi wazi kuanzia kwa watumishi wao kwa wao au watumishi na wanafunzi lakini pia watumishi na wagonjwa au ndugu wa wagonjwa, sijui hali ya maambukizi ya Ukimwi upoje pale?)