Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

Imebadilika pale serikali iliamua kuchangia huduma, na ukwel ni kwamba serikal inachelewa sana kutoa inachoahidi na pengine kutokutoa kabisa
 
Imebadilika pale serikal iliamua kuchangia huduma, na ukwel n kwamba serikal inachelewa sana kutoa inachoahid na pengine kutokutoa kabisa

2002 kuna ndugu yangu alilazwa hapo kcmc, on that time kulikuwa poa kidogo
 
Tatizo la KCMC siyo madaktari bali huduma ya wagonjwa kulala haswa vyumba vya kulaza wagonjwa na sometime vitanda. Kwa ufupi KCMC imezidiwa na wagonjwa baada ya hospital ya Mkoa ya Mawenzi kufa na hivyo wagonjwa wengi kuamini kuwa watapata huduma nzuri KCMC kuliko Mawenzi. Ili kuinusuru KCMC serikali inatakiwa iiifufue hospitali ya Mawezi iwe fully functionally na kuipatia vifaa vyote vinavyohitjika pamoja na madaktari la sivyo lawama zaidi kwa KCMC ziko njiani kwani lazima tukubali kuwa ufanisi wa KCMC miaka 10 iliyopita ulikuwa bora kwa 60% ya ufanisi uliopo sasa
 
Umeona eh?!

Anyway,pole kwa yaliyokukuta ndugu yangu.

Asante sana mkuu! pia namshukuru mungu kwa mgonjwa tulimpeleka mount meru hospital na pale kuna daktari alitusaidia kweli! mungu am'bariki sana.
 
Kweli kcmc imechoka kuanzia majengo hadi huduma imeshuka sana. kcmc bila kushikwa mkono na kukabidhiwa kwa daktari fulani ujue huna chako. hata muasisi wake Askofu Stephano Ruben Moshi (R.I.P.) angerudi leo angelia machozi.
 
Mungu ainusuru!! mpaka uwe na refa ndiyo upate huduma yakueleweka!! afu ma chaplain kibao pale, haya kama vile hawayaoni, au kazi yao ni kuombea tu wagonjwa na kuwatia moyo?
 
Imebadilika pale serikali iliamua kuchangia huduma, na ukwel ni kwamba serikal inachelewa sana kutoa inachoahidi na pengine kutokutoa kabisa

kwa hiyo na serikali inahusika? bad government if they are concerned...
 
suala si madaktari, bali system nzima ya afya tz, serekali haijali kabisa afya za watanzania, serekali hii imeanzisha system ya uchangiaji huduma, huku yenyewe ikiwa haichangii kabisa au inachelewesha mchango wake na muda mwingine inaleta kiasi kidogo tofauti na inavyotakiwa, sasa hapo ndo unapokuta hakuna vifaa, madawa, congestion ya wagonjwa nk. serekali imekuwa ikiwadharau na kuwanyima haki zao madaktari( rejea mgomo wao uliopita) huku wakipigania uboreshwaji wa hali ya afya na sisi wananchi kuendelea kulala chini hospitali (mfano muhimbili), na kuwalaumu madaktari badala ya serikali, hakika huku ni kupoteza muda. serikali inatakiwa kuboresha hali ya afya nchini na sio kutwa kucha wananchi kuwapigia kelele madaktari kama kwamba wao ndo wanatakiwa kununua vifaa, madawa nk
 
Mimi pia nimeitembelea hospitali hii mara kadhaa huwezi linganisha na hospitali kama bugando, mambo ya kcmc hayaeleweki,pamoja na serikali kuchelewesha ruzuku, lakini wao wenyewe hawaoneshi jitihada zozote za kuboresha huduma. Ni kweli wamezidiwa na wingi wa watu na hapa inabidi serikali iangalie hizi zonal hospitals kwa kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kutoa fweza according to the budget, mfano hosp ya muhimbili mahitaji yake kwa mwaka ni billioni 3 then serikali inawapa millioni mia tatu na wanasema kasungura ni kadogo!!!!!! Hapo unategemea nini.
Ni lazima tukubali sekta ya afya hapa nchini sio kipaumbele cha serikali.
 
kweli kabisa mkuu mganga wa jadi na mkuu konar, mmesema kitu! ila mwisho wa siku tusisahau kuwa serikali hii hii iliyopo madarakani ni ya ccm, walewale wanaojali matumbo yao! hawana mpango na hospital tz kwani wao na familia zao wanaenda kutibiwa nje
 
Halafu nasikia kuna doctor mmoja mfupi sana mwembamba ndo mtaalam wa surgery. Kichekesho ni kwamba huwa ni mlevi kupindukia na mara kibao huwa anawachana wagonjwa akiwa mitungi nashindwa kuelewa how come KCMC wamtegee mlevi? Kwa mwenye taarifa hivi anaitwa nani vile yule doctor?
 
kwa hiyo na serikali inahusika? bad government if they are concerned...

Inahusika sana, 2jiulize kwanin kabla palikuwa vzr kuliko sasa. Ni bas 2 kanisa haliwez kuifukuza serikali, mana wao hawakushndwa kuiongoza Hosp.
 
Imebaki jina kwa kuwa uongozi uliopo hauwajali watumishi hasa hao manesi, kwani stahili zao hazilipwi kwa wakati. Je hapo unategemea nini?
 
Ukiangalia kijuu-juu unaweza dhani tatizo hapo ni manesi...lakini ukiangalia kwa upeo mkubwa zaidi utagundua tatizo ni system. Sitegemei nesi anayelipwa hela ya kutosha kukimu maisha yake na familia yake atafanya biashara ICU badala ya kuconcentrate na wagonjwa.

Penda usipende...wahudumu wa afya mahospitalini (wakiwemo madaktari na manesi) ni binadamu, wana mahitaji kama binadamu wengine. Na hayo mahitaji yasipotimizwa, ni dhahiri ufanisi wa hao wahudumu hautakuwa wa kiwango cha kuridhisha...and this is true for every other sectors, wafanyakazi hawako makini na kazi zao wala hawajitumi wasipopata kipato cha kuweza kukimu mahitaji yao. Na wengine wataengage kwenye vibiashara mbali mbali ili kufill hiyo gap inayomiss..sababu watoto lazima waende shule, nyumbani paliwe, kodi ya nyumba ilipwe, watu wavae, akiba kwa huduma mbali mbali kama afya, na nauli ya kwenda kazini.....natimizaje hayo yote kama mshahara wangu haunitoshi hata kwa wiki 1?!

You expect 100% from people....pay them accordingly, in short of that...expect less!

Another issue ni vifaa vya kufanyia kazi (kugundua magonjwa, kutolea tiba na ufuatiliaji wa matibabu) as well as vya kujikinga na maambuki kwani kila siku unadeal na wagonjwa wengi tu na kuna risk kubwa ya kuambukizwa magonjwa mbali mbali...and funny thing is...you dont even afford hizo huduma za afya ambazo wewe mwenyewe unazitoa. Tuliwahi kumchangia hela daktari mwenzetu kununua dawa za kansa ya damu (chemotherapy) kwa mwanae aliyekuwa akiugua kansa ya damu...wakati mwenyewe anatibia watoto wa watu wenye tatizo hilo..can you imagine!?

Usikurupuke tu na kubebesha lawama zote wahudumu wa afya wakati mfumo wenyewe wa utoaji huduma hizo ni mbovu umekufa kwisha kabisa, hasa katika hospitali za level ya chini kama dispensaries, health centres and district hospitals. Bajeti ya wizara ya afya haikidhi hata for service delievery tu, sahau prevention part...tunategemea kuomba omba kwa wafadhili...unategemea manesi wasiuze sabuni? unataka wauze nini....wawe dada poa usiku?!
dr Riwa umejibu vyema sana lkn nina swali moja dogo sana ninalotaka kuuliza hivi hospitali ya mkoa ya iringa, madaktari wake hawana ugumu ambao huko kcmc na kwingine wana upata? je manesi wake nao wanalipwa tofauti na huko kcmc kiasi kwamba hawa wanaweza kuuza bidhaa wodini??

nionavyo mm hata kama hali ni ngumu basi wanapaswa kuwajibika huku wakidai haki zao za msingi na sio kuwaonea wagonjwa nasema hivyo kwasababu niliwah kulazwa hosp ya mkoa wa iringa mwezi mzima kiukweli hii ni hospitali ambayo najivunia kuwa nayo. huduma zao ni nzuri, wodi ni safi hadi wana hire cleaning companies kwaajili ya usafi. nurse station ina madesi 24/7 plus dr in charge wa word. yaani hata dr akitaka kutoka anawaaga kabaisa wagonjwa na mnaridhika kwa ile caring tu nilipata faraja na kupona milele. but nimeuguza mtu hapo kcmc mpaka wa leo yuko wodini tabu tunayoipata mungu hataki. nurse station hakuna wauguzi, hao madaktari wanafunzi na wenyewe wamesha jifunza uvivu hadi wanashindwa na hosp ya taifa ya muhimbili, CT scan haifanyi kazi huko x-ray na kwingine usiseme na wachaga walivyokuwa wababe ndo hata mdomo hufungui, sasa je tusenmeje juu ya hili??
 
Last edited by a moderator:
sio KCMC pekee,, kwani huyo aliyedai rushwa huko muhimbili hamkusikia, vituko vya manesi tanzania nzima hamvisikii, kutokufanya kazi kwa madakitari wengi kwani haionekani,,, swala ni kwamba waligoma halali,, hawakusikilizwa zikabaki kuwa hadithi za kwenye magazeti tu, mara Dr Ulimboka, mara waziri,, wakapotezea,,
HAKIKA NAWAAMBIA KAMA ILIVO KWA WAALIMU KUUZA ICE CREAM, KARANGA, NA BAGIA,, WAKATI WA VIPINDI MADARASANI,, KUTOKUINGIA KWA VIPINDI NDIVYO ITAKAVYOKUA KWA MADAKITARE,, uzuri ni kwamba kama alivosema ****** mwalimu akigoma hakuna shida kwani muda ukifika ataanza pale alipoishia ila kwa madakitari akuna alipoishia,, ukitaka kujua angalia idadi ya vifo katika hospitali bahati mbaya huwezi pata taarifa muhimu kama hizi,, lakini idadi ya vifo imeongezeka kwa kiwango cha juu,, huo ndo mgomo baridi wa madakitare,, ole wenu wenye amuwezi kwenda private kutoa hela za halali,, ole wenu hamna bima za afya za kueleweka, ole wenu wenye hamuwezi kwenda clinic kama mh Lowasa anavyohudhuria clinic ya macho nche ya nchi,, ,,
poleni saaana,, kilio chenu kimesikika, lakini kilio cha samaki akimnyimi mtu kula ugali
 
ujue kuna baadhi ya mapungufu pale tatizo, mtu huwezi kuyasemea moja kwa moja pale kwa usalama wa mgonjwa wako, nilijaribu kufuatilia baadhi ya mambo na madhara yake niliyaona, kama kupiga x-ray mara mbili mbili cjui hizo picha huwa wanazificha wapi.
 
Back
Top Bottom