Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,489
Reaction score
18,379
Kwa wale mliofika siku za karibuni hapa kcmc mtakubaliana na mimi, hospital hii kubwa na maarufu haitoi tena huduma za kueleweka, wanaofanya kazi sasa kama madaktari ni wanafunzi..Hili ni tatizo kwani linazorotesha sana huduma..tabu tupu
 
Eti madaktari utawapata grade 1. wapi tunakwenda? mbona siku za nyuma hii hospitali ilikuwa vizuri kwa huduma nzuri?
 
Kwa wale mliofika siku za karibuni hapa kcmc mtakubaliana na mimi, hospital hii kubwa na maarufu haitoi tena huduma za kueleweka, wanaofanya kazi sasa kama madaktari ni wanafunzi..Hili ni tatizo kwani linazorotesha sana huduma..tabu tupu

kwani pesa MUM hazifiki huko?
 
Mimi nilimwuguza mgonjwa ICU pale na nilitishwa sana. Manesi walikuwa busy na biashara zao za kuuza tauli na sabuni. Jikoni chakula kinatengenzwa kwa gharama ya walipa kodi, lakini utakifuata kantini.

Nikajiuliza kama mtu aliye mahututi anaengojea kufa anauziwa tauli ya kunawa, bezeni, chakula n.k. Wale wenye nafuu wauziwa nini? Tanzania tumekosa maadili hadi mwisho. Madaktari ndiyo tena usiseme. Kila mtu anaiba na sasa tunaibia hadi maiti.

Cha kusikitisha mno ni kuwa tuna watoto na ndiyo hayo tunayowafundisha. Je wao watakitendea nini kizazi chao na watoto wao? KCMC kwa sasa hata jina limeshaondoka kutokana na niliyoyaona kwa macho yangu pale ICU.

Pumzika kwa amani kaka niliyekuuguza pale wiki nzima.
 
Nashukuru mkuu Bahati kwa kuliweka hili vizuri zaidi, siyo siri inauma sana kuona mtu anapoteza uhai wake kwa sababu ya uzembe wa daktari, niliingia kitengo cha x-ray mgonjwa anachofanyiwa unatamani umzabe vibao yule jamaa. kcmc sasa wanakera sana..
 
Kweli usilolijua litakusumbua.
Una maana gani unaposema hakuna madaktari,au madaktari wanafunzi? Unafahamu ranking ktk kada hii,au basi tu umeamua kupost?

Kule kuna madaktari wanafunzi wa degree ya kwanza(hawa bado hawajawa madaktari kamili). Wako kwenye masomo,na ili uwe daktari kuna wakati unafundishwa ukiwa darasani na kuna wakati unafundishwa ukiwa hospitali mbele ya wagonjwa.Hawa hawaruhusiwi kutoa matibabu kwa mgojwa.

Kuna madaktari wanaosomea ngazi ya udaktari bingwa kama vile wa watoto,wa akina mama,upasuaji nk.Hawa tayari ni madaktari kamili na walishafanya kazi miaka kadhaa.Hawa ndio tunaokutana nao ktk hospitali za mikoa na mara chache ktk za wilaya. Mbona hulalamiki ukiwakuta huku mikoani? Kwa mfano KCMC hawa wanasoma miaka minne,kwingine wanasoma miaka mitatu tu. Wanafanya kazi kama madaktari wengine unaowajua wewe. Ni vema ukatambua tu kwamba,hawa ni wanafunzi tu wanapokuwa darasani na mwalimu wao,ila wanapokuwa eneo la kazi wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za kikazi nchini.Na kwa taarifa yako,popote utakapoenda hawa ndio wanaofanya kazi za dk.bingwa sio KCMC. Kwa ukubwa wa hospitali ile sio rahisi kujitosheleza kila sehemu kwa na madaktari bingwa.Hata muhimbili ukienda utakuta wanaofanya kazi za madk.bingwa ni hawa unaowaita hapa wanafunzi.

Kuna madaktari wanaofanya kazi chini ya uangalizi wa madaktari bingwa(interns),hawa tayari wana degree ya kwanza lkn kwa mujibu wa taratibu zilizopo,ni sharti kwanza wafanye kazi kwa mwaka mmoja chini ya uangalizi wa mabingwa kabla hawajapewa kibali cha kufanya kazi katika hospitali zetu. Hawa ndio waliogoma mwaka jana. Unakumbuka huduma zilivyozorota? Tulikuwa tunawaitaje,wanafunzi?? Kazi yao inaonekana na ndio maana ktk mgomo kilitokea kile ulichokiona.

Kwa hiyo basi ungetwambia ni madaktari wa type gani ambao wewe ukiwaona ndio roho yako inaridhika.Lkn vile vile,ungesema ikiwa hapo kabla hawa unaowaita wanafunzi walikuwa hawatoi huduma hapo hospitali.Pia ungesema mapungufu yaliyopo hapo hospitali kwa kukosekana hao madak.unaowataka.

Napenda pia kukukumbusha kuwa,ufanyaji kazi wa kitabibu hopitali unafuata protocal. Mganga wa kwanza kumwona mgojwa anaposhindwa kutambua/kutibu anamrefer mgonjwa kwa dk.ambaye yuko juu yake kitaalam,naye huyu anaposhindwa anamsogeza mbele kwa mwingine wa juu yake,nk...nk...nk. Labda utuambie huko KCMC utaratibu huo haupo? Kama upo,ni lazima hao unaoita wanafunzi wanauzingatia,na hapo point yako inakuwa imekosa mashiko.

Ni vema watu wakajua kwamba huduma mbaya sio tu kukosa madk.peke yake.Madaktari wanaweza kuwapo na bado ukakosa huduma nzuri vile vile. Kama ndugu yangu umekosa huduma zuri hapo hospitalini sio kwa sababu umehudumiwa na hao unaoita wanafunzi. Hospitali ile imekuwa ikijiendesha hivyo kwa kipindi kirefu sana tu,na imekuwa ikivutia wagonjwa wengi sana kutoka maeneo mbali mbali kutokana na huduma inayotolewa pale(na hao wanafunzi).

Ushauri: Kisheria mgonjwa ana haki ya kuchagua dk.anayehitaji amtibu. Kama unadhani hao wanafunzi hawakidhi vigezo vya kukuhudumia una haki ya kuomba kuonana na daktari unayemwamini,atakusaidia.Hakuna haja ya kuja hapa kulalamika,kwa sababu kuna hospitali nyingi sana wagonjwa wanapoteza maisha kwa kukosa hapo unaoita wanafunzi.

Binafsi ningekuunga mkono ikiwa ungesema labda umeombwa rushwa,au umekataliwa kutibiwa,au labda mgonjwa wako amechelewa kupata matibabu bila sababu ya msingi,au pengine wamekosea dawa nk...nk...nk. Kwa kweli pale KCMC wanajitahidi sana,na kusema limebaki jina tu,mimi nakukatalia kabisa. Binafsi hospitli ile naijua sana tu,na mara kwa mara nakwendaga pale. Kiukweli uwepo wa wanafunzi pale hospitali unarahisisha sana utoaji wa huduma kwa wagonjwa.Huwezi kutambua urahisi wa huduma za pale ni hadi utakapopata bahati ya kutembelea hospitali zingine kubwa ndio utakapopata jibu.Na pengine utarudi hapa kuwaomba radhi jamaa!
 
Mimi nilimwuguza mgonjwa ICU pale na nilitishwa sana. Manesi walikuwa busy na biashara zao za kuuza tauli na sabuni. Jikoni chakula kinatengenzwa kwa gharama ya walipa kodi, lakini utakifuata kantini. Nikajiuliza kama mtu aliye mahututi anaengojea kufa anauziwa tauli ya kunawa, bezeni, chakula n.k. Wale wenye nafuu wauziwa nini? Tanzania tumekosa maadili hadi mwisho. Madaktari ndiyo tena usiseme. Kila mtu anaiba na sasa tunaibia hadi maiti. Cha kusikitisha mno ni kuwa tuna watoto na ndiyo hayo tunayowafundisha. Je wao watakitendea nini kizazi chao na watoto wao? KCMC kwa sasa hata jina limeshaondoka kutokana na niliyoyaona kwa macho yangu pale ICU. Pumzika kwa amani kaka niliyekuuguza pale wiki nzima.

Nimegundua kama naelekea kuzama choo cha kike. Nilidhani tuazungumzia jambo kubwa lenye maslahi kwa jamii kwa kutumia facts rational views,kumbe mada yenyewe ina malengo na kitu nisichokijua. Ngoja niendelee na shughuli zangu,tayari mada imekosa mashiko.

Anyway,pole for your loss.
 
Mrimi,

Watu wenye mawazo kama yako ndo wanadidimiza maendeleo ya nchi, umepewa mpaka mfano wa mgonjwa aliyeko ICU na manesi wanafanya biashara ndogondogo, kweli hapo ni mahala pake? Au hujui maana ya ICU nafikiri zile zama za kutetea uovu namambo ya kulindana zimekwisha. Tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye hii sekta ya afya, hali ni mbaya.
 
Nimegundua kama naelekea kuzama choo cha kike. Nilidhani tuazungumzia jambo kubwa lenye maslahi kwa jamii kwa kutumia facts rational views,kumbe mada yenyewe ina malengo na kitu nisichokijua. Ngoja niendelee na shughuli zangu,tayari mada imekosa mashiko.

Anyway,pole for your loss.
Hili ni jambo kubwa na sio vema kulifumbia macho. Kiukweli KCMC imekwisha kabisa, mabadiliko makubwa ya kiutendaji yanahitajika.
 
Hili ni jambo kubwa na sio vema kulifumbia macho. Kiukweli KCMC imekwisha kabisa, mabadiliko makubwa ya kiutendaji yanahitajika.

Ni kweli hakuna mwenye akili timamu anayeweza kuchekelea mambo maovu. Lkn pia nimesema hata mimi mara kadhaa nakwenda hospitali pale.Na binafsi naridhika na huduma inayotolewa pale ingawa siwezi kusema kama hakuna jambo baya linaweza kutokea pale.

Tatizo ninaloona mjadala unakoelekea huenda usiwe wa kujenga. Mada inaweza ikahamia kwingine kabisa ambako hakutusaidii,angalia post no.3 & 4,je hata wewe ungependa mada ihamie huko? Naamini hutapenda. Ninachosisitiza tuwe rational ktk kila tunachojadili hapa. Mimi si msemaji wa hospitali,ila kusema hospitali imebaki jina tu,mimi nakataa. Kwa sababu kila mtu akianza kusema ubaya na uzuri wa huduma anayopata pale utakuta watakaosifia(kama mimi) na watakaoponda(kama wewe) na kila mtu anatoa ushahidi wake. Do you think hiyo itakuwa na manufaa kwa wagonjwa?

Kwanza kitendo cha kulalamikia kwapani mimi nakiita ni unafiki. We unatarajia nani akuletee mabadililiko,au ndo tuilaumu serikali kama ilivyo kwaida yetu? Kwanza siamini kama uongozi wa hospitali unaweza kuwaambia watumishi wake kuignore wagonjwa.Wewe una mgonjwa unaona hahudumiwi ipaswavyo,unachukua hatua gani? Je,umetoa taarifa kwenye uongozi halafu haikufanyiwa kazi? Tusiwe walalamishi tuuu kila wakati halafu hata pahala ambapo tunatakiwa kuchukua hatua tunatazama tu.Mabadiliko yanaanza na mimi na wewe.
 
Watu wenye mawazo kama yako ndo wanadidimiza maendeleo ya nchi, umepewa mpaka mfano wa mgonjwa aliyeko ICU na manesi wanafanya biashara ndogondogo, kweli hapo ni mahala pake? Au hujui maana ya ICU nafikiri zile zama za kutetea uovu namambo ya kulindana zimekwisha. Tunahitaji mabadiliko makubwa kwenye hii sekta ya afya, hali ni mbaya.

Ukiangalia kijuu-juu unaweza dhani tatizo hapo ni manesi...lakini ukiangalia kwa upeo mkubwa zaidi utagundua tatizo ni system. Sitegemei nesi anayelipwa hela ya kutosha kukimu maisha yake na familia yake atafanya biashara ICU badala ya kuconcentrate na wagonjwa.

Penda usipende...wahudumu wa afya mahospitalini (wakiwemo madaktari na manesi) ni binadamu, wana mahitaji kama binadamu wengine. Na hayo mahitaji yasipotimizwa, ni dhahiri ufanisi wa hao wahudumu hautakuwa wa kiwango cha kuridhisha...and this is true for every other sectors, wafanyakazi hawako makini na kazi zao wala hawajitumi wasipopata kipato cha kuweza kukimu mahitaji yao. Na wengine wataengage kwenye vibiashara mbali mbali ili kufill hiyo gap inayomiss..sababu watoto lazima waende shule, nyumbani paliwe, kodi ya nyumba ilipwe, watu wavae, akiba kwa huduma mbali mbali kama afya, na nauli ya kwenda kazini.....natimizaje hayo yote kama mshahara wangu haunitoshi hata kwa wiki 1?!

You expect 100% from people....pay them accordingly, in short of that...expect less!

Another issue ni vifaa vya kufanyia kazi (kugundua magonjwa, kutolea tiba na ufuatiliaji wa matibabu) as well as vya kujikinga na maambuki kwani kila siku unadeal na wagonjwa wengi tu na kuna risk kubwa ya kuambukizwa magonjwa mbali mbali...and funny thing is...you dont even afford hizo huduma za afya ambazo wewe mwenyewe unazitoa. Tuliwahi kumchangia hela daktari mwenzetu kununua dawa za kansa ya damu (chemotherapy) kwa mwanae aliyekuwa akiugua kansa ya damu...wakati mwenyewe anatibia watoto wa watu wenye tatizo hilo..can you imagine!?

Usikurupuke tu na kubebesha lawama zote wahudumu wa afya wakati mfumo wenyewe wa utoaji huduma hizo ni mbovu umekufa kwisha kabisa, hasa katika hospitali za level ya chini kama dispensaries, health centres and district hospitals. Bajeti ya wizara ya afya haikidhi hata for service delievery tu, sahau prevention part...tunategemea kuomba omba kwa wafadhili...unategemea manesi wasiuze sabuni? unataka wauze nini....wawe dada poa usiku?!
 
Mrimi! ni huduma gani nzuri uliyoipata pale kcmc? na hao wanafunz unaosema wanakuwa chini ya uangalizi wakati wa mafunzo, ni kwa namna gani? utoaji huduma hapa unadorora siku hadi siku na hospitali hii hakika inapoteza hadhi yake, hili siyo lakuficha
 
Hili ni jambo kubwa na sio vema kulifumbia macho. Kiukwel KCMC imekwisha kabisa, mabadiliko makubwa ya kiutendaj yanahitajika.

Ni kweli kabisa! hospitali kubwa kama hii huduma dhaifu. je? hizo ndogo itakuwaje?
 
Mimi nadhani mfumo mzima wa sekta ya afya nchini ni dhaifu. Unatakiwa usukwe upya. Wagonjwa wananyanyaswa, madaktari na wauguzi wanapata malipo duni. Vifaa hamna, majengo hayatoshi, hizi vurugu ndio zinafanya kila mtu afanye atakavyo.
Halafu, hakuna neno ninalochokia kama kumsikia 'daktari' au 'nesi' akisema usimtishe, ameshazoea kuona vifo! Hapo ni pale mgonjwa anapolalamika halafu mhusika anachukulia pouwa.
Nilishuhudia kwa macho yangu (nahifadhi hospitali) mgonjwa aliletwa na ambulance akiwa hajiwezi akashushwa, wauguzi wanapita wanamwangalia, kuna mdada wa kizungu akahamaki ikabidi aanze kutoa msaada na kuwaambia manesi wamsaidie. Wenzetu 'dharura' ina maana ya 'dharura' na sio kwetu.

Ifike mahali mgonjwa ahudumiwe kama mteja (mfalme) bila kuzingatia yupo kwenye hospitali ya serikali au binafsi.
Na madaktari na wauguzi walipwe malipo wanayostahili.
 
mkuu Tutaweza! ujue madaktari na manesi pamoja na watumishi wengine, pamoja na kulipwa kidogo bado hawana zile ethics za kazi zao!! jamani vitengo vya casuality hospitalin vina umuhimu gan? kama mgonjwa atapelekwa kwa ambulance wahudumu wamtizame tu?
 
Mrimi! ni huduma gani nzuri uliyoipata pale kcmc? na hao wanafunz unaosema wanakuwa chini ya uangalizi wakati wa mafunzo, ni kwa namna gani? utoaji huduma hapa unadorora siku hadi siku na hospitali hii hakika inapoteza hadhi yake, hili siyo lakuficha

Katika maisha yangu huwa sipendi kuchukulia vitu kijumla jumla, and I wish watu wote wangeepuka tabia hiyo. Sijaignore kama umepata huduma ambayo haijakuridhisha,na sijasema kama hakuna lolote baya halijawahi kutendeka hapo hospitali. Mi nachosisitiza tusichukulie mambo kijumla jumla.Wewe inawezekana hujaridika na huduma ya hao wanafunzi basi,mwingine labda wametibuana na nesi,mwingine labda majengo yalivyokaa hayajamridhisha,lakini kuna wengine waliugua wakapatiwa matibabu kwa uzuri tu wakapona na wameondoka wakisifia huduma ya pale.Kwa hiyo usije ukadhani kila mtu atakuwa na mtazamo kama wa kwako.Kwa mfano,unaponiuliza ni huduma gani nzuri nimeipata pale,we unatarajia nikujibu nini wakati wewe huamini kama kuna huduma yoyote ya maana inaweza kutolewa pale?

Mambo mengine nimeyafafanua kwenye post no.8,sina majibu mengine ya tofauti. Lakini na wewe uniambie,je unataka mabadiliko gani na unatarajia nani akuletee mabadiliko hayo? Nakuuliza hivi kwa sababu wewe ni victim wa huduma ya hapo.Je,unapoona hujaridhika na huduma ya hapo,wewe kwa nafasi yako umechukua hatua gani? Ya kulalamika hapa kwenye mtandao?? Umeonana na wahusika ukajaribu kuwaeleza jinsi huduma wanayotoa hapo isivyoridhisha?
 
Mkuu Mrimi! nimeongea na wahusika(wakubwa), zaidi ya mara moja!! lakini wanamajibu rahisi sana..tena ilibidi niwe polite sana ili mgonjwa wangu asipate shida zaidi coz they can do anything all in all no body care..ilibidi tumwamishie another hospital
 
Back
Top Bottom