Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

my Mom died there...... sawa siku zake labda ndio zilifika ila maybe there was the doctors Fault : wahudumu wengi wa afya wanafanya kazi kwa mazoea..... yani unaweza kuwaona wahudumu wanapiga story wakiwa wanamhudumia mgonjwa aliepo serious mbaya..... au mtu akifa wakiwa wanambeba wanaweza pigiana story zenye kuchekesha mpaka wanamwachia maiti anaanguka chini ......mphuuu.
 
Kwakweli Hali ya hospitali hii ni ya kusikitisha mnoo.
Kwanza uchafu uliokithiri,ni aibu Sub ICU kuwa na Mende wengi kama jalalani.Ni aibu na fedheha Ma nurse wengi ni wakenya na wana lugha mbovu kwa wagonjwa.Ni aibu na fedheha Nurses wengi wa night hawafanyi kazi na wanalala ifikapo saa tatu.usiombe ukawa na drip watakacho fanya ni kutundika na kuifungulia hadi mwisho ndani ya dk 5 imeisha na hawajali umri.Dr aliyepo ni mwanafunzi ambaye hata prescription shida kuandika hadi amsubiri intern ambaye naye amsubiri resident.sasa mgonjwa atakuwa anasubiri tu?nimeyashuhudia kwa macho yangu bibi mmoja anamatatizo ya kupumua na kawekewa respiratory aid. oxygen imeisha na Nurse anasema amechoka atabadilisha asubuhi.naambiwa alijafariki!its so shame kuiita hospitali ya msamaria mwema!Malasusa amka toka usingizini!
 
Kwa wale mliofika siku za karibuni hapa kcmc mtakubaliana na mimi, hospital hii kubwa na maarufu haitoi tena huduma za kueleweka, wanaofanya kazi sasa kama madaktari ni wanafunzi..Hili ni tatizo kwani linazorotesha sana huduma..tabu tupu

Dah mkuu shukrani kwa kuleta hii mada hapa,ni kweli kabisa KCMC ni kwishine mie nilimpeleka mgonjwa wangu hapo yaani hamna kitu ni wanafunzi wanazunguka tu huko ndani huduma ni mbovu kupindukia,afadhali hospitali ya Mawenzi,kuna wagonjwa watatu ambao ninawafahamu walishawahi kuletwa pale kwa siku tofauti kwa kweli walifariki wote na ujue ukimlaza mgonjwa wako hapo kama anaugojwa complicated kidogo ujue umekwenda na maji na mgonjwa haudumiwi mpaka utoe hela
 
Kweli usilolijua litakusumbua.
Una maana gani unaposema hakuna madaktari,au madaktari wanafunzi? Unafahamu ranking ktk kada hii,au basi tu umeamua kupost?

Kule kuna madaktari wanafunzi wa degree ya kwanza(hawa bado hawajawa madaktari kamili). Wako kwenye masomo,na ili uwe daktari kuna wakati unafundishwa ukiwa darasani na kuna wakati unafundishwa ukiwa hospitali mbele ya wagonjwa.Hawa hawaruhusiwi kutoa matibabu kwa mgojwa.

Kuna madaktari wanaosomea ngazi ya udaktari bingwa kama vile wa watoto,wa akina mama,upasuaji nk.Hawa tayari ni madaktari kamili na walishafanya kazi miaka kadhaa.Hawa ndio tunaokutana nao ktk hospitali za mikoa na mara chache ktk za wilaya. Mbona hulalamiki ukiwakuta huku mikoani? Kwa mfano KCMC hawa wanasoma miaka minne,kwingine wanasoma miaka mitatu tu. Wanafanya kazi kama madaktari wengine unaowajua wewe. Ni vema ukatambua tu kwamba,hawa ni wanafunzi tu wanapokuwa darasani na mwalimu wao,ila wanapokuwa eneo la kazi wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za kikazi nchini.Na kwa taarifa yako,popote utakapoenda hawa ndio wanaofanya kazi za dk.bingwa sio KCMC. Kwa ukubwa wa hospitali ile sio rahisi kujitosheleza kila sehemu kwa na madaktari bingwa.Hata muhimbili ukienda utakuta wanaofanya kazi za madk.bingwa ni hawa unaowaita hapa wanafunzi.

Kuna madaktari wanaofanya kazi chini ya uangalizi wa madaktari bingwa(interns),hawa tayari wana degree ya kwanza lkn kwa mujibu wa taratibu zilizopo,ni sharti kwanza wafanye kazi kwa mwaka mmoja chini ya uangalizi wa mabingwa kabla hawajapewa kibali cha kufanya kazi katika hospitali zetu. Hawa ndio waliogoma mwaka jana. Unakumbuka huduma zilivyozorota? Tulikuwa tunawaitaje,wanafunzi?? Kazi yao inaonekana na ndio maana ktk mgomo kilitokea kile ulichokiona.

Kwa hiyo basi ungetwambia ni madaktari wa type gani ambao wewe ukiwaona ndio roho yako inaridhika.Lkn vile vile,ungesema ikiwa hapo kabla hawa unaowaita wanafunzi walikuwa hawatoi huduma hapo hospitali.Pia ungesema mapungufu yaliyopo hapo hospitali kwa kukosekana hao madak.unaowataka.

Napenda pia kukukumbusha kuwa,ufanyaji kazi wa kitabibu hopitali unafuata protocal. Mganga wa kwanza kumwona mgojwa anaposhindwa kutambua/kutibu anamrefer mgonjwa kwa dk.ambaye yuko juu yake kitaalam,naye huyu anaposhindwa anamsogeza mbele kwa mwingine wa juu yake,nk...nk...nk. Labda utuambie huko KCMC utaratibu huo haupo? Kama upo,ni lazima hao unaoita wanafunzi wanauzingatia,na hapo point yako inakuwa imekosa mashiko.

Ni vema watu wakajua kwamba huduma mbaya sio tu kukosa madk.peke yake.Madaktari wanaweza kuwapo na bado ukakosa huduma nzuri vile vile. Kama ndugu yangu umekosa huduma zuri hapo hospitalini sio kwa sababu umehudumiwa na hao unaoita wanafunzi. Hospitali ile imekuwa ikijiendesha hivyo kwa kipindi kirefu sana tu,na imekuwa ikivutia wagonjwa wengi sana kutoka maeneo mbali mbali kutokana na huduma inayotolewa pale(na hao wanafunzi).

Ushauri: Kisheria mgonjwa ana haki ya kuchagua dk.anayehitaji amtibu. Kama unadhani hao wanafunzi hawakidhi vigezo vya kukuhudumia una haki ya kuomba kuonana na daktari unayemwamini,atakusaidia.Hakuna haja ya kuja hapa kulalamika,kwa sababu kuna hospitali nyingi sana wagonjwa wanapoteza maisha kwa kukosa hapo unaoita wanafunzi.

Binafsi ningekuunga mkono ikiwa ungesema labda umeombwa rushwa,au umekataliwa kutibiwa,au labda mgonjwa wako amechelewa kupata matibabu bila sababu ya msingi,au pengine wamekosea dawa nk...nk...nk. Kwa kweli pale KCMC wanajitahidi sana,na kusema limebaki jina tu,mimi nakukatalia kabisa. Binafsi hospitli ile naijua sana tu,na mara kwa mara nakwendaga pale. Kiukweli uwepo wa wanafunzi pale hospitali unarahisisha sana utoaji wa huduma kwa wagonjwa.Huwezi kutambua urahisi wa huduma za pale ni hadi utakapopata bahati ya kutembelea hospitali zingine kubwa ndio utakapopata jibu.Na pengine utarudi hapa kuwaomba radhi jamaa!

Acha kutetea ujinga wewe..
 
Dah mkuu shukrani kwa kuleta hii mada hapa,ni kweli kabisa KCMC ni kwishine mie nilimpeleka mgonjwa wangu hapo yaani hamna kitu ni wanafunzi wanazunguka tu huko ndani huduma ni mbovu kupindukia,afadhali hospitali ya Mawenzi,kuna wagonjwa watatu ambao ninawafahamu walishawahi kuletwa pale kwa siku tofauti kwa kweli walifariki wote na ujue ukimlaza mgonjwa wako hapo kama anaugojwa complicated kidogo ujue umekwenda na maji na mgonjwa haudumiwi mpaka utoe hela

Ni kweli mkuu, nadhani umeona watu wanavyotoa maoni yao juu ya hili,
Pale KCMC, sasa hakuna kazi zinazofanyika..ule mwezi wa kumi na mbili kidogo nimzabe nesi mmoja vibao,
Ilibakia kidogo tuu, sema nilihofia sana usalama wa mgonjwa wangu pale, japokuwa alishafariki (R.I.P). my beloved grandma..
Ni jambo baya sana na linaoondoa uhai wa watu wengi, na linasababishwa na watu wachache.
Mungu awabadilishe watu hawa ili wawe na ethics za kazi...
Inauma sana hasa pale tunapowapoteza wale Tunaowapenda...
 
Kwakweli Hali ya hospitali hii ni ya kusikitisha mnoo.
Kwanza uchafu uliokithiri,ni aibu Sub ICU kuwa na Mende wengi kama jalalani.Ni aibu na fedheha Ma nurse wengi ni wakenya na wana lugha mbovu kwa wagonjwa.Ni aibu na fedheha Nurses wengi wa night hawafanyi kazi na wanalala ifikapo saa tatu.usiombe ukawa na drip watakacho fanya ni kutundika na kuifungulia hadi mwisho ndani ya dk 5 imeisha na hawajali umri.Dr aliyepo ni mwanafunzi ambaye hata prescription shida kuandika hadi amsubiri intern ambaye naye amsubiri resident.sasa mgonjwa atakuwa anasubiri tu?nimeyashuhudia kwa macho yangu bibi mmoja anamatatizo ya kupumua na kawekewa respiratory aid. oxygen imeisha na Nurse anasema amechoka atabadilisha asubuhi.naambiwa alijafariki!its so shame kuiita hospitali ya msamaria mwema!Malasusa amka toka usingizini!

Very Sad kwa kweli na hii kitu inaumiza sana sana...
Can u imagine Nesi anasema amechoka na hawezi kumbadilishia mgonjwa Oxygen?
Where are we going?
 
my Mom died there...... sawa siku zake labda ndio zilifika ila maybe there was the doctors Fault : wahudumu wengi wa afya wanafanya kazi kwa mazoea..... yani unaweza kuwaona wahudumu wanapiga story wakiwa wanamhudumia mgonjwa aliepo serious mbaya..... au mtu akifa wakiwa wanambeba wanaweza pigiana story zenye kuchekesha mpaka wanamwachia maiti anaanguka chini ......mphuuu.

Matukio ni mengi sana..KCMC miaka ya nyuma ilikuwa the best..
but now haikimbiliki...
 
Nakubaliana na wewe kabisa. Kweli limebaki jina tu. Wakati alipokuwepo Prof. Shao mambo yalikuwa mazuri ukilinganisha na mkurugenzi wa Sasa Dr. Ntabaye. Hospital hii haiwajali wafanyakazi wake hata kidogo na watu wanafanya kazi ila mradi siku ipite jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo. Kuna kipindi nilikua na mgonjwa hapo nilisikitika sana hata huduma za maabara ni mbovu kabisa achilia madaktari wenyewe. Maabara haina wafanyakazi kabisa wameondoka karibu wote waliobaki wamebaki wababaishaji tu chini ya uongozi wa Mr. Nyombi. Juhudi za ziada zinahitaji kurudisha hadhi ya hospital hii.
 
Ukiingia kcmc unanusa harufu ya kifo. Ukiangalia wagonjwa walivyolala koridoni na jinsi wanavyokuwa treated, oh my God! Its very scary. That place smells death.kuna mtu namfahamu alifanyiwa operation mara mbili, ya kwanza alifanyiwa na mwanafunzi alimkosea, ikabidi afanyiwe mara ya pili na daktari mzoefu, eneo lilelile.kama humfahamu mtu pale, umekwisha.
 
Wapendwa tuwe rational, wote tulijua jinsi Prof Shao alivyoondolewa kuepusha shari ya watumishi waliomkataa waziwazi nani asiyejua. KCMC ilifikia wakati ilishindikana kutawalika. Namheshimu sana Prof. Shao, ila siku za mwisho alizidiwa nguvu na vijana. Kumleta Dr. Ntabaye ilikuwa ni possibility iliyoonekana ingeinusuru KCMC. Mpe resources afanye kazi. Tukiacha mawazo ya kibaguzi, Dr. Moshi Ntabaye ni kiongozi mwenye uzoefu katika nyanja za afya na utawala, na ana uzoefu wa kazi yake. Matatizo ya KCMC hayatofautiani na ya Muhimbili, MOI au Ocean Road, na hata kwa kiasi na Bugando. Shida ni resources ndizo kidogo, na kupata own resources ndiyo tunatakiwa kuchangia kikubwa zaidi.

The best ni kuwapa mawazo ya namna ya kupata the needed resources siyo kuwalaumu. Siku hizi mambo ni magumu.
Kama tunaipenda KCMC tuinusuru na uhaba wa resources.
 
viongozi wao hawajali maana wanajua hospital zao ni Millpark jo burg au Apollo Hyderabad... Nimefika Apollo yaani niliumia sana nilivyolinganisha nurse wake na watanzania,, hospital ina nurse station nyingi hazihesabiki, nurse wana mtreat mgonjwa na tabasam na stories hadi mgonjwa ana smile, yaani kama sio wahindi hawa tunaoishi nao Tanzania... Kiukweli kwenye huduma za afya Tanzania bado sana
 
Hivi hii Ndio miongoni mwa hospital zenye kupata ruzuku .za serikali, hali hii ikoje...?
 
ninachoamini mimi ni mfumo au system mbaya ,maana ukiangalia mfano ukitaka kuchukua fail unawahi pale saa kumi na mbili ili ushike namba .unapewa namba mda wa saa moja .saa mbili wakitoka sala wanakutafutia faili unaitwa unaambiwa nenda kwenye malipo .
unaweza kukaa dirisha la malipo kwa muda usiopungua masaa matatu. usiposikia jina lako unawafuata makarani wanakutuma urudi dirishani uklikotoa namba au kadi ,fail unaweza kulipata mda wa saa sita na .mbaya zaidi kama unatumia bima utazunguka hadi uchoke kabla hujamuona daktari na baada ya kumuona daktari,utazunguka hadi uchoke hadi upate hiyo dawa.mimi natamani huu mfumo kwa wagonjwa wa nje urekebishwe
 
KCMC wanapata ruzuku kutoka hazina kulipa wafanyakazi na shughuli za Maendeleo (UNAUDITED) in billions

KCMC wanapata pesa kutoka kwa wagonjwa kwa malipo ya huduma

KCMC wanapata pesa za sadaka kutoka kwa wafadhili na waumini

Kama siyo ufisadi nipeni jina lingine

Ndugu tumeona msimamo wako, ila kumbuka hakuna fedha ya Serikali ambayo huenda un-audited kama unavyodai, aidha sina hakika na kuwa waumini wa Moshi huchangia sadaka kwenda KCMC, ni asilimia ngapi ya sadaka? maana nijuavyo mimi, KCMC iko chini ya Utawala wa KKKT, na KKKT hawajawa na asilimia fulani kwa matibabu, hata hivyo bado ni kidogo kuendesha huduma.
Kunusuru KCMC, basi tukubali kuwa Serikali iwaruhusu watengeneze pesa, na sisi tukubali, mahali ambapo ulikuwa unachangia Shs 10,000/= kama kuchangia huduma (cost-sharing) basi watoze halisi labda bila mishahara maana Serikali itaendelea kulipa, mathalani ulipe kama 30,000/=, usikie malalamiko hayo yatakavyo miminika. Shida ni umaskini. Naona hata kama Mbowe akiwa Rais 2015 kama slogan yako inavyosema, najua mambo yatabadilika kwa gwanda tu hakuna la maana.
Muhimu naomba sana badala ya kulaumu, toa njia mbadala, maana shida ni RESOURCES yaani MMM (Money, manpower and Materials)

Alamsiki
 
Nurse anasema amechoka hawezi kubadili oxygen, wewe unamwangalia unakimbilia kulipua kwenye JF ambapo hata haioni, je ulichukua hatua? si kuna uongozi, uliwaambia nini hao viongozi wake? Je ni haki kumuacha muovu aendelee na uovu wake bila kumwajibisha, natamani kusikia Mzee Kiwatengu umechukua hatua, vinginevyo hatuwezi kuendelea kwa kutumia JF pekee.
 
Ukiingia kcmc unanusa harufu ya kifo. Ukiangalia wagonjwa walivyolala koridoni na jinsi wanavyokuwa treated, oh my God! Its very scary. That place smells death.kuna mtu namfahamu alifanyiwa operation mara mbili, ya kwanza alifanyiwa na mwanafunzi alimkosea, ikabidi afanyiwe mara ya pili na daktari mzoefu, eneo lilelile.kama humfahamu mtu pale, umekwisha.

Hata kama unamfahamu basi uwe na kitu..au awe nduguyo wa karibu
 
Nurse anasema amechoka hawezi kubadili oxygen, wewe unamwangalia unakimbilia kulipua kwenye JF ambapo hata haioni, je ulichukua hatua? si kuna uongozi, uliwaambia nini hao viongozi wake? Je ni haki kumuacha muovu aendelee na uovu wake bila kumwajibisha, natamani kusikia Mzee Kiwatengu umechukua hatua, vinginevyo hatuwezi kuendelea kwa kutumia JF pekee.

Mkuu ebandio! sikuwa na jinsi ya kuchukua hatua wakati ule ili hali mgonjwa wangu alikuwa hoi pale hospitalini..
Hatua yoyote ile kwa pale ingehatarisha uhai wake!
Ilifikia hatua yakutaka kumzaba nesi vibao, baada ya yeye kunijibu kwa kejeli!
Kama system ya uongozi haipo sawa, hakuna hatua ambayo ingeleta mashiko kwa wakati ule!
Ni udhaifu kwa upande wangu..
Na hatua ndogo niliyochukukua yakuacha maoni yangu pale juu ya utendaji kazi wa hosp..
Thanks to dr. Makule of mt.meru hospital he tried alot to serve a life of my beloved grandma..may her soul rest in peace!!
Mkuu ebandio hakika umenikumbusha mbali..hasa kuchukua hatua!
 
Last edited by a moderator:
ninachoamini mimi ni mfumo au system mbaya ,maana ukiangalia mfano ukitaka kuchukua fail unawahi pale saa kumi na mbili ili ushike namba .unapewa namba mda wa saa moja .saa mbili wakitoka sala wanakutafutia faili unaitwa unaambiwa nenda kwenye malipo .
unaweza kukaa dirisha la malipo kwa muda usiopungua masaa matatu. usiposikia jina lako unawafuata makarani wanakutuma urudi dirishani uklikotoa namba au kadi ,fail unaweza kulipata mda wa saa sita na .mbaya zaidi kama unatumia bima utazunguka hadi uchoke kabla hujamuona daktari na baada ya kumuona daktari,utazunguka hadi uchoke hadi upate hiyo dawa.mimi natamani huu mfumo kwa wagonjwa wa nje urekebishwe

Si kwa wagonjwa wa nje tu.! hata wa ndani mkuu..
 
Back
Top Bottom