Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

Hospitali ya KCMC Moshi! limebaki jina tu.

Mkuu ebandio! sikuwa na jinsi ya kuchukua hatua wakati ule ili hali mgonjwa wangu alikuwa hoi pale hospitalini..
Hatua yoyote ile kwa pale ingehatarisha uhai wake!
Ilifikia hatua yakutaka kumzaba nesi vibao, baada ya yeye kunijibu kwa kejeli!
Kama system ya uongozi haipo sawa, hakuna hatua ambayo ingeleta mashiko kwa wakati ule!
Ni udhaifu kwa upande wangu..
Na hatua ndogo niliyochukukua yakuacha maoni yangu pale juu ya utendaji kazi wa hosp..
Thanks to dr. Makule of mt.meru hospital he tried alot to serve a life of my beloved grandma..may her soul rest in peace!!
Mkuu ebandio hakika umenikumbusha mbali..hasa kuchukua hatua!

Pole ndugu yangu, ila ni muhimu kuchukua hatua maana kwa hatua yako moja utaokoa roho za wengi. Najua usingeweza kuokoa roho ya Bibi yako lakini hujui ya baadaye maana sisi wote tungeweza kuangukia kwenye mkono wa muuguzi huyo. Kumzaba kibao wala kusingekusaidia maana ungeishia kufunguliwa kesi, na nafikiria kama muuguzi angelikuwa mwanamke.

Hata hivyo bado mimi nasisitiza kuchua hatua ya kutoa taarifa kwa uongozi, maana mara nyingi sisi tuna tabia ya kutotoa taarifa halafu tunafikiri uongozi unajua, mara nyingi hawajui. Mpendwa wetu Ntabaye hawezi kuwa kila sehemu kwa wakati mmoja. Viongozi wa sehemu mara nyingi hufichwa uovu labda kama wanakula sahani moja kwa uovu, jambo hili ni gumu kulieleza kwa mtu asiye kwenye mtandao huo. Naomba nikupe hadithi fupi ya jambo hilo ili uone linalojificha, "mathalani mgonjwa alienda kwa rafiki yake ampeleke kwa Daktari bingwa kwa kuwa aliona mpango wa appointment ni mgumu na mrefu, huyu rafiki akamwambia kwa ubize wa yule daktari leta 200,000/=, yule bwana akajikamua akapata 100,000/=, kufika kwa daktari (kwa kuwa walikuwa wawili) akamuomba amtibie kwa ukamilifu sana (kwa kuwa aliambiwa kwa kutoa nusu unaweza usipate matibabu yenye maana), kwa kuwa pesa iliyobaki ataleta baadaye. Daktari katika kushangaa, na kujiuliza akamwita yule jamaa, kwa kuwa yeye alimwambia kuwa yule ni ndugu yake naye akataka kumsaidia, si mfanyakazi mwenzake, baada ya kuulizwa akabaki mdomo wazi, baadaye Daktari alimtaka yule bwana ampe ile pesa yake, na kumrudishia mgonjwa (hii si hadithi bali ilitokea Muhimbili), kama mgonjwa asingejitetea kwa upungufu wa hela, uovu ule usingejulikana. Uongozi haukujua na hata daktari mwenye we hakuwa na habari. HIVI NDIVYO JINA ZURI LA HUDUMA HUHARIBIKA. Taabu zote tunasababisha sisi tunaoamua kutotoa taarifa ili kukomesha uovu. Naomba nisistize kuwa hujachelewa kumtolea taarifa muuguzi mwovu ili asiue wengine. Mungu akutangulie katika hilo.
 
ila pamoja na yote bado naiamin kuliko mwananyamala na zingnezo hapa dar!i reather go there than m/nyamala lol
 
ila pamoja na yote bado naiamin kuliko mwananyamala na zingnezo hapa dar!i reather go there than m/nyamala lol

dada flora mambo mengine magumu kweli, kcmc ni hospital kubwa zaidi ya hyo mwananyamala
 
Tatizo la KCMC ni moja 2 ni baada ya serikali kuingilia kati katika uongoz na uendeshaji coz pale kuna wafanyakaz wanalipwa na serikal na wengine wanalipwa na GOOD SAMARITIAN FOUNDASION(Yaan Kkkt wenye hospital) sasa kutokana na uzembe wa serikal ndo maana Kcmc inakufa taratiibu.
 
tatizo la kcmc ni moja 2 ni baada ya serikali kuingilia kati katika uongoz na uendeshaji coz pale kuna wafanyakaz wanalipwa na serikal na wengine wanalipwa na good samaritian foundasion(yaan kkkt wenye hospital) sasa kutokana na uzembe wa serikal ndo maana kcmc inakufa taratiibu.

mungu anyoshe mkono wake..
 
Nasikia wiki iliyopita manesi waligoma na ikaleta shida kubwa.
Walifanikiwa kuuzima mgomo haraka na watoto ambao wanasoma chuo cha unesi wali take cover kwa muda manesi walikuwa wanadai kutopandishwa ngazi za mshahara tokea waajiriwe.
Kweli RIP kcmc.
Zamani haikuwa hivi
 
Nasikia wiki iliyopita manesi waligoma na ikaleta shida kubwa.
Walifanikiwa kuuzima mgomo haraka na watoto ambao wanasoma chuo cha unesi wali take cover kwa muda manesi walikuwa wanadai kutopandishwa ngazi za mshahara tokea waajiriwe.
Kweli RIP kcmc.
Zamani haikuwa hivi

Our government should do a thing to save this hospital from dyng!
 
haitoi tena huduma za kueleweka
Bodi ianzishe account ambayo tutachangia kwa pesa za mtandao. Hosp hii ilishaokoa ndugu zetu wengi Enzi zake. Na ni tegemeo mikoa ya kaskaz. Hima fanyeni hivo. Madaktari waache malumbano, UKABILA na wafute jesi mahakamani. MaDr Bingwa wamekimbia, wengine anzisha Hosp zao. Maabara nimeona zimechakaa hata Analyzers /equipment, reagents kwisha. Sakafu hazina tiles. Shame on this Country, and its corrupt leadership and Institutions, and un-ethical/ undedicated Drs. Life should come First.!
 
Kwa hiyo hata majengo hayapo? limebaki jina tu! duuh poleni sana!
 
Mimi nina kajukuu kangu kanatakiwa kafanyiwe oprtn wamekalaza week ya 2 sasa wanakapiga tarehe kana 1 yr nimejaribu kuwa mzalendo kuwasikiliza madaktari sasa baada ya kusoma uzi huu nimegundua njia za panya zinahitajika kunusuru uhai wake
 
Mimi nina kajukuu kangu kanatakiwa kafanyiwe oprtn wamekalaza week ya 2 sasa wanakapiga tarehe kana 1 yr nimejaribu kuwa mzalendo kuwasikiliza madaktari sasa baada ya kusoma uzi huu nimegundua njia za panya zinahitajika kunusuru uhai wake

Pole sana ndugu yangu!!
 
Point iseee kama jajaelewa basi ni tatizo.
Kweli usilolijua litakusumbua.
Una maana gani unaposema hakuna madaktari,au madaktari wanafunzi? Unafahamu ranking ktk kada hii,au basi tu umeamua kupost?

Kule kuna madaktari wanafunzi wa degree ya kwanza(hawa bado hawajawa madaktari kamili). Wako kwenye masomo,na ili uwe daktari kuna wakati unafundishwa ukiwa darasani na kuna wakati unafundishwa ukiwa hospitali mbele ya wagonjwa.Hawa hawaruhusiwi kutoa matibabu kwa mgojwa.

Kuna madaktari wanaosomea ngazi ya udaktari bingwa kama vile wa watoto,wa akina mama,upasuaji nk.Hawa tayari ni madaktari kamili na walishafanya kazi miaka kadhaa.Hawa ndio tunaokutana nao ktk hospitali za mikoa na mara chache ktk za wilaya. Mbona hulalamiki ukiwakuta huku mikoani? Kwa mfano KCMC hawa wanasoma miaka minne,kwingine wanasoma miaka mitatu tu. Wanafanya kazi kama madaktari wengine unaowajua wewe. Ni vema ukatambua tu kwamba,hawa ni wanafunzi tu wanapokuwa darasani na mwalimu wao,ila wanapokuwa eneo la kazi wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu za kikazi nchini.Na kwa taarifa yako,popote utakapoenda hawa ndio wanaofanya kazi za dk.bingwa sio KCMC. Kwa ukubwa wa hospitali ile sio rahisi kujitosheleza kila sehemu kwa na madaktari bingwa.Hata muhimbili ukienda utakuta wanaofanya kazi za madk.bingwa ni hawa unaowaita hapa wanafunzi.

Kuna madaktari wanaofanya kazi chini ya uangalizi wa madaktari bingwa(interns),hawa tayari wana degree ya kwanza lkn kwa mujibu wa taratibu zilizopo,ni sharti kwanza wafanye kazi kwa mwaka mmoja chini ya uangalizi wa mabingwa kabla hawajapewa kibali cha kufanya kazi katika hospitali zetu. Hawa ndio waliogoma mwaka jana. Unakumbuka huduma zilivyozorota? Tulikuwa tunawaitaje,wanafunzi?? Kazi yao inaonekana na ndio maana ktk mgomo kilitokea kile ulichokiona.

Kwa hiyo basi ungetwambia ni madaktari wa type gani ambao wewe ukiwaona ndio roho yako inaridhika.Lkn vile vile,ungesema ikiwa hapo kabla hawa unaowaita wanafunzi walikuwa hawatoi huduma hapo hospitali.Pia ungesema mapungufu yaliyopo hapo hospitali kwa kukosekana hao madak.unaowataka.

Napenda pia kukukumbusha kuwa,ufanyaji kazi wa kitabibu hopitali unafuata protocal. Mganga wa kwanza kumwona mgojwa anaposhindwa kutambua/kutibu anamrefer mgonjwa kwa dk.ambaye yuko juu yake kitaalam,naye huyu anaposhindwa anamsogeza mbele kwa mwingine wa juu yake,nk...nk...nk. Labda utuambie huko KCMC utaratibu huo haupo? Kama upo,ni lazima hao unaoita wanafunzi wanauzingatia,na hapo point yako inakuwa imekosa mashiko.

Ni vema watu wakajua kwamba huduma mbaya sio tu kukosa madk.peke yake.Madaktari wanaweza kuwapo na bado ukakosa huduma nzuri vile vile. Kama ndugu yangu umekosa huduma zuri hapo hospitalini sio kwa sababu umehudumiwa na hao unaoita wanafunzi. Hospitali ile imekuwa ikijiendesha hivyo kwa kipindi kirefu sana tu,na imekuwa ikivutia wagonjwa wengi sana kutoka maeneo mbali mbali kutokana na huduma inayotolewa pale(na hao wanafunzi).

Ushauri: Kisheria mgonjwa ana haki ya kuchagua dk.anayehitaji amtibu. Kama unadhani hao wanafunzi hawakidhi vigezo vya kukuhudumia una haki ya kuomba kuonana na daktari unayemwamini,atakusaidia.Hakuna haja ya kuja hapa kulalamika,kwa sababu kuna hospitali nyingi sana wagonjwa wanapoteza maisha kwa kukosa hapo unaoita wanafunzi.

Binafsi ningekuunga mkono ikiwa ungesema labda umeombwa rushwa,au umekataliwa kutibiwa,au labda mgonjwa wako amechelewa kupata matibabu bila sababu ya msingi,au pengine wamekosea dawa nk...nk...nk. Kwa kweli pale KCMC wanajitahidi sana,na kusema limebaki jina tu,mimi nakukatalia kabisa. Binafsi hospitli ile naijua sana tu,na mara kwa mara nakwendaga pale. Kiukweli uwepo wa wanafunzi pale hospitali unarahisisha sana utoaji wa huduma kwa wagonjwa.Huwezi kutambua urahisi wa huduma za pale ni hadi utakapopata bahati ya kutembelea hospitali zingine kubwa ndio utakapopata jibu.Na pengine utarudi hapa kuwaomba radhi jamaa!
 
Back
Top Bottom