Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,433
Ilikuwa ni hospitali kubwa ya Kanisa la Anglicana enzi za ukoloni. Hospitali ilikuwa Magila ikiunganishwa na chuo cha Uuguzi na Ukunga , kanisa la Msalabani na shule mbili za middle school Saint Martin’s na Saint Mary’s.Nasikia ni hospitali ya kanisa Anglicana na Askofu wake huko Tanga, ndiye Mkuu wa Kanisa Tanzania.
Nimesema hayo kuonesha ni aibu na fedheha sana kwa Kanisa na Mkuu wa Kanisa.
Katika harakati za kupanua hospitali hii na huduma za afya, mwaka 1976 serikali ililipatia kanisa kiwanja. Ujenzi huu wa hospitali ukisimamiwa na Rev. Bartlet ambae mke wake alikuwa daktari.
Ujenzi ulikamika mwaka 1980 na kuiunganisha hospitali ya kanisa na hospitali ya wilaya iliyokuwa Ubwari hapo zamani. Hospitali ilifunguliwa rasmi 1981 na Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere. Ninaikumbuka hii siku tulijipanga kumsubiri Mwalimu Nyerere alilala Amani.
Hospitali inapata ruzuku ya serikali na wafanyakazi ni wajiiriwa wa wizara ya Afya. Kanisa linatoa misa ada ya dawa.
Bodi ya Wauguzi ni bora mngeyafanyia kazi malalamiko haya.
Chuo cha Uuguzi na Ukunga Teule ni moja ya vyumba vikongwr Tanzani.