Tatizo la Wanawake Kupata Maumivu Wakati na Baada ya Kujamiiana: Fahamu Sababu na Suluhisho la Tatizo

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
1564438198982.jpg


WADAU WANAOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU MATATIZO HAYA
Habari zenu wana JF.

Nina mpenzi wangu toka nikutane nae analalamika maumivu makali wakati wa tendo na hata baada ya tendo maumivu yanadumu kwa takribani cku mbili mpaka tatu. Hata nimuandae vp lakini tukianza tendo tu basi hali inakuwa sio nzui kwake. Sasa nimejaribu kufikiria nikaona yawezekana tatizo likawa ukavu sehemu zake za uke hivyo naomba msaada juu ya kutatua tatizo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nisaidieni kuhusu hili: inakuaje mwanamke anadai anahisi maumivu wakati wa tendo la ndoa, ni kwamba uume mkubwa au namna ya kufanya nae, ila tatizo style zote anadai maumivu anayasikia.
Habari ya mapumziko waungwana!

Nina mpenzi wangu wa kike anatatizo hili . Wakati wa tendo la ndoa huwa anasikia maumivu makali sana, hainjoi sex kabisa, ana lalamika muda wote.

Kabla ya tendo maandalizi yanakuwepo ya muda mrefu kama kawaida, hata wakati wa sex hawi mkavu kwamba ndo isababishe maumivu, lakini ndo hivyo anaumia sana. Dushelele langu ni la wastani inchi 6 za kawaida.

Wakati wa kusex anatokwa damu, lakini damu hiyo siyo nyekundu ni damu ile kama yupo kwenye Mp period.

Naomba msaada, hatuna ugonjwa wowote wa zinaa, kwamba ndo iwe sababu. Hamu ya tendo anayo ila ndo hivyo tukianza tu maumivu makali anapata.

NB: Tangu nimtoe bikra hii ni mara ya nne kukutana bado anaona yale maumivu na hiyo damu kutoka

Wana JF,

Mke wangu yupo mbali kikazi na kwa sasa ni mjamzito. Tumekuwa tukikaa hata miezi2 bila kuonana. Nikifika na 2kianza sex analalamika kuumia sana na vagina huwa imejirudi sana hata kupenetrate inakuwa kwashida.

Baada ya siku3 au 4 ndipo huanza kuingia kiurahisi. Pia anasema hasikii hamu yakusex tangu apate ujauzito. Wataalamu hebu fungukeni hapa sababu ya maumivu, vagina kujirudi na yeye kutosikia hamu ya sex.
Mpenzi wangu ni mwanafunzi wa chuo hivyo huwa tunakutana wakati wa likizo tu, nimedumu nae kwa muda sasa na mimi ndio nilikuwa mwanaume wake wa kwanza lakini awamu hii alivyokuja mambo yamekuwq tofauti kwanza tulikubalina nae twende kwa dr. Akachome sindano kwajili ya kuzuia ujauzito na tulipoanza kufanya mapenzi mpenzi wangu alilalamika sana anaumia na kesho yake maumivu yalikuwa makali sana akawa analia mpaka tukashindwa malizia mechi kwa ufupi nilishangaa sana ile hali kwani hata kipindi nadate nae kwa mara ya kwanza hakulalamika kiasi kile.Wakuu naombeni ushauri kwani tunashndwa kuelewa tatizo yeye mwenyewe anabaki analia haelewi anafanyaje
Sent using Jamii Forums mobile app
Habari zenu wakuu.
Kupata maumvu ya tumbo au kitovu pia pindi mwanamke anapofanya tendo la ndoa au sex je tatizo ni nini kwa mtu huyo.
Na je nini hafanye ili aweze kujiondoa katika tatizo hili.
Hivi karibuni tulikutana kimwili na mpenzi wangu mpya kwa mara ya kwanza. Sasa kiukweli nilifurahia sana tendo na kufika kilele mara kadhaa lakini baada ya tendo hilo nikajikuta nimepata maumivu makali sana kwa dakika kadhaa (dk 15) kwenye tumbo la chini kama nataka kuanza siku zangu lakini siku zangu ni bado sana kama wiki mbili mbele na sina ujauzito. Na hii hali haijawahi kunitokea hata siku moja huko nyuma. Inaniogopesha nina tatizo gani?, naombeni msaada... nimepima magonjwa ya zinaa nimewambiwa nipo safi.
Asanteni sana.
Hapo vipi,
Juzi kuna msichana nimelala nae then baada ya tendo la ndoa akaniambia anasikia maumivu chini ya kitovu, dah! Mimi nikawa nampa pole nikamuuliza inaweza ikawa inasasabishwa na nini akatulia na kupotezea.
Sasa leo nimemueleza rafiki yangu mmoja, eti akaniambia ndio mimba imenasa.
Je, nini ukweli wake wadau?


FAHAMU TATIZO LA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA KWA MWANAMKE (DYSPAREUNIA)

Maumivu wakati wa tendo la ndoa au kuumia wakati mnafanya tendo la ndoa kwa mwanamke hujulikana kama Dyspareunia.

Neno Dyspareunia tamka (dis-pa-roon-ia) linatokana na neno la kigiriki lenye maana ya shida katika kuingiliana wakati wa kufanya tendo la ndoa (difficulty mating au badly mated).

Utafiti unaonesha kwamba kati ya wanawake watatu, wawili wamewahi au hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Imefika kwamba baadhi ya ndoa, mwanamke anapata maumivu kiasi cha kutokuwa na hamu tena ya tendo la ndoa na matokeo yake wamekuwa na wakati mgumu linapokuja suala la kufanya mapenzi na pia kila wakirudia kufanya tendo la ndoa, mambo ni yamekuwa ni yaleyale kwa mwanamke kuumia zaidi kuliko mara ya kwanza.

Kawaida huwa haifurahishi kabisa na haina hata ladha kufanya tendo la ndoa huku mmoja kati yenu akiwa anapata maumivu makali au shida hiyo husababisha kutojishughulisha katika kuleta raha ya kweli na hatimaye kuridhishana kimapenzi wakati wa tendo la ndoa.

Tendo la ndoa halikuwekwa ili kukupa shida au maumivu bali kukupa raha, furaha na kuridhishwa.
Moja ya kanuni muhimu sana katika tendo la ndoa ni:

Kama unapata maumivu usifanye
Badala yake tafuta nini kimesababisha na tafuta jibu sahihi la kuondoa hiyo hali au muone daktari akusaidie.
Na baada ya kupata tiba na kupona ndiyo unaruhusiwa kuendelea kufanya tendo la ndoa kwa kufurahia na kukupa raha zaidi, vinginevyo itakuwa ni kuleta maangamizi.

Ni kweli kwamba kama moja wapo ya mahitaji ya msingi ya kihisia (emotions) kama hili la tendo la ndoa halipatikani katika ndoa linaweza kusababisha mmoja ya wanandoa kutokuwa mwaminifu kwa mwenzake na kutoka nje kwenda kutafuta mtu wa kumridhisha zaidi, hata hivyo kwa mwanamke kufanya tendo la ndoa huku anapata maumivu au kuumia kwa kuogopa kwamba asipompa Mume wake haki yake basi anaweza kutoka nje na kutokuwa mwaminifu hilo si sahihi kwani ni kutojiamini na kutojali si afya yako tu bali haki yako ya msingi ya kufanya tyendo la ndoa kwa kupata raha.

Mnahitaji kujulishana na kuelezana ukweli ili muweze kupata dawa na hatimaye kurudi kwenye raha upya badala ya kuumizana.

Kuna mambo mengi yanayosababisha mwanamke au hata mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa na inaweza kuwa ni wakati mwanaume anapoingia (penetrate) au wakati wa kitendo chenyewe au baada ya kitendo chenyewe.

Inaweza kuwa ni maumivu makali sana au inaweza kuwa ni kuwashwa au inaweza kuwa ni maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida au inaweza kuwa ni maumivu ambayo unasikia kama moto unawaka vile ndani yako wakati wa tendo la ndoa.

Naamini kufika mwisho wa hili soma utakuwa umefahamu si nini kinasababisha bali utafahamu jibu la hili Tatizo.


Kichwani (brain & mind) ndiyo kiungo kikubwa cha tendo la ndoa, jinsi unavyojiweka kwenye akili zako inaweza kusababisha raha au maumivu ya tendo la ndoa.

Kwa nini ujisikie maumivu

Maumivu wakati wa tendo la ndoa husababishwa au hutokana na sababu za kihisia na za pia (physical and emotional)
Ili kujua kwa nini maumivu kutokea ni vizuri kujua nini hutokea kwa mwili wa mwanamke wakati wa tendo la ndoa (sex)
Mwili wa mwanamke hupitia hatua nne (4) muhimu kukamilisha tendo la ndoa.

HAMU (dedire)
Hapa mwanamke hujisikia anataka kufanya tendo la ndoa

KUSISIMKA (arousal)
Hapa mwili husisimka kwa sehemu zake za siri (vagina) hutanuka urefu na upana pia hutoa majimaji yanayorahisisha mwanaume kuingia (penis penetration), kisimi hudinda na kuongezeka ukubwa, chuchu husimama na kusisimka, uterus hupanda juu nk

KUFIKA KILELENI (orgasm)
Hapa ni kilele cha mwitikio wa tendo la ndoa, misuli hujikusanya (contradict) na kumpa hisia kubwa za raha na utamu wa tendo lenyewe.

SULUHISHO (resolution)
Viungo vyote vinavyohusika na tendo la ndoa hurudi kwenye hali ya kawaida

Aina za maumivu na sehemu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke zinaweza kutokea kwenye katika sehemu zifuatazoSehemu ya nje ya vagina, yaani vulva na huumia wakati inaguswa au kuwasha hata unapotumia baadhi ya sabuni na wakati mwingine kusababisha makovu au utando unaonesha kuna cheese.sehemu ya tundu la kuingia kwenye vagina na sehemu ya ndani ya Vagina unayoungan na uterus.

Je ni kawaida mwanamke kupata maumivu hata kama hajaambukizwa magonjwa ya zinaa?
Kawaida kila mwanamke ana aina ya chachu au hamila (yeast) kwenye sehemu za siri zake za siri, na hii yeast ikiongezeka sana inaweza kusababisha kuwasha au maumivu wakati wa kukojoa mkojo wa kawaida na pia husababisha kutoa majimaji meupe mithili ya maziwa na hii hutokea kama mwanamke anatumia antibiotics au medication inayosababisha kuua bacteria wanaofanya hiyo yeast kutoleta madhala yoyote. Hivyo ni jambo la kawaida kwa mwanamke kujisikia maumivu mara chache wakati wa tendo la ndoa ingawa maumivu yakizidi inabidi uchukue hatua inayotakiwa ili kupata tiba kamili.

Vitu gani vinavyosababisha kuumia wakati wa tendo la ndoa?
Kukaza kwa misuli ya vagina (Vaginismus) (tamka vaj-uh-niz-muh s)Ni kukaza kwa misuli ya vagina bila hiari (involuntary) na kusababisha tendo la ndoa kuwa gumu au kutofanyika kabisa. Mwanamke mwenyewe anaweza asijue kwamba misuli inayozunguka vagina umekaza na kusababisha maumivu wakati mwanaume anaingiza penis.
Hii hali hutokana na hofu na mashaka aliyonayo mwanamke kuhusiana na suala la tendo la ndoa kwamba anaweza kuumia (kisaikolojia).

Pia wanawake wengi wenye vaginismus hawajawahi pata furaha ya tendo la ndoa maishani mwao na wengi ni waoga sana hata kwenda kwa madaktari kuhofia daktari anaweza kuchokonoa vagina zao hivyo kuongeza tatizo zaidi.

Ni nini husababisha hiyo hofu na mashaka?
Malezi aliyofundishwa kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya na dhambia na hata akiolewa anafahamu kwamba tendo la ndoa ni chafu na baya. Malezi aliyolelewa kwa kuambiwa kwamba vagina ni nyembamba sana na hivyo tendo la ndoa husababisha mwanamke kuumia.

Kama amewahi kudhalilishwa kimapenzi kama kubakwa anaweza kuwa na hofu na tendo la ndoa kwa sababu aliumizwa.
Kama amewahi kupata magonjwa ya zinaa yaliyokuwa yanamuumiza sana na kumpa shida pia anaweza kuwa anahisia za kuumia wakati wa tendo la ndoa.

Wanawake wengi wa aina hii hupata raha sana wakati wa foreplay na utamu wa mahaba huwaisha pale tu penetration ikianza. Kitu cha msingi ni kwamba ili tendo la ndoa liwe tamu na zuri hali ya akili na ubongo ni muhimu sana kwani hisia zote za utamu wa tendo hutafsiriwa kwenye ubongo na ubongo ukipata pollution ya mawazo mabaya basi kila kitu kitaenda kombo. Tutaendelea na somo kuangalia vitu vingine vinavyosababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.


MAJIBU NA MICHANGO YA WADAU KUHUSU TATIZO HILO
SABABU ZA KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

Nimekuwa Napata kesi nyingi sana kutoka kwa akina mama hasa wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea wakihitaji msaada kwenye ndoa zao, maana hawafurahii tendo la ndoa kama vile inavotakiwa. Tatizo linazidi kuongezeka kwa kasi na wengi hawafahamu chanzo cha tatizo hili hivo inakuwa vigumu kulitibu. Leo tutaongelea chanzo cha tatizo na jinsi ya kuepuka na kulitibu ili uendelee kufurahia unyumba. Wanawake hawakuumbiwa matatizo ya kiafya.

SABABU ZA KUPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA

1. KUVIMBA kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi (candida Albicans) au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa, vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.

2. Matatizo ya shingo ya kizazi (cervical incompetence) kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.

3. Kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi (Uterus). Uvimbe huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini `fibroid` ni maarufu Zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hu kua kama boga kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadaye huonekana kama ana mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.

4. Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa maji machafu kutokana na kuzaliana sana eneo hilo, tatizo ambalo hujulikana kitaalam kama Hyrosalpinx.

Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa mazito, kitu ambacho husababisha mayai ya uzazi na mbegu za kiume kushindwa kupenya.

Kutoshika mimba kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni kiashiria kikubwa cha tatizo hili.

Kumbuka matatizo ya uzazi unayokutana nayo kama maumivu makali kipindi cha hedhi, ugumba, kukosa hamu ya tendo la ndoa, kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, mpangilio mbaya wa hedhi, uzito mkubwa na kitambi siyo kitu ulichoumbiwa, bali ni matokeo ya Maisha unayoishi .kwa kifupi matatizo yote haya chanzo chake kikubwa ni kuvurugika kwa homoni za kike au hormonal imbalance. Matatizo haya siyo kwamba ni mabadiliko ya vinasaba kutokana na umri, ila ni matokeo ya mpangilio mbovu wa vichocheo ama homoni zako na hasa homoni za uzazi. Hivo utakubaliana nami kwamba wanawake hawajaumbiwa kupata shida hizi zote hata kama umri wako umeenda, unahitaji kuendelea kufurahia tendo la ndoa. Sawazisha mpangilio wako homoni zako na matatizo yote haya utakuwa umeyakimbiza.

DALILI ZIFUATAZO ZINAASHIRIA KUVURUGIKA KWA HOMONI ZAKO

Hivo unatakiwa kutumia dalili hizi kujifanyia uchambuzi wewe mwenyewe bila hata kufanya vipimo hospitali tayari utagundua kuwa una tatizo kwenye vichocheo ama homoni zako.

1. Uzito kupungua ama kuongezeka bila mpangilio

2. Tumbo kujaa gesi na kuhisi umeshiba mda mwingi

3. Maumivu ya kichwa na kujuskia haupo kwenye mood nzuri

4. Kupata msongo wa mawazo mara kwa mara

5. Ugumba ama kutoshika mimba kwa kipindi kirefu

6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama kupata maumivu makali wakati wat endo la ndoa

7. Kuhisi mwili umechoka mara kwa mara

8. Kuota ndevu na nywele kifuani

9. Kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu

10. Kutokwa jasho jingi usiku na

11. Ngozi kukakamaa

12. Kukosa usingizi

13. Uvimbe kwenye mfuko wa mimba

Baada ya kujifanyiaupembuzi juu ya tatizo lako sasa tuangalie nini cha kufanya ili uweze kutibu dalili hizi kuanzia leo ukiwa nyumbani kwako.

ANZIA JIKONI KWAKO (LISHE /CHAKULA NI SEHEMU YA KWANZA YA KUREKEBISHA)

Nataka nikwabie mpenzi msomaji na unayefatilia Makala hizi kwa makini, kwamba vitu tunavyoweka tumboni vianchangia karibu 80% ya kuvurugika kwa mpangilio wa homoni zako. Unatakiwa kuwa mvumilivu maana kusawazisha homoni ni kitu endelevu na kinachukua kuda kutokana na kwamba unajenga tabia mpya kwenye mwili wako. Hivo hatua ya kwanza katika kupangilia lishe na mlo wako

Endelea kusoma zaidi kutia linki hapa chini

Chanzo: Mkumbo Health

Sent using Jamii Forums mobile app
UNDANI WA KUHISI MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA (DYSPAREUNIA)
Kumekuwa na malalamiko mengi sana yanayo wakuta wanandoa ambapo hupelekea kutokuwa na maelewano mazuri kati yao pale tu linapokuja swala la kushiriki tendo la ndoa na kutofurahia ndoa zao kwa ujumla kwa sababu ya tatizo la maumivu anayohisi mmoja kati ya wanandoa hao.

Hivyo basi twende sambamba tukajifunze kwa pamoja juu ya swala hilo kwa undani zaidi.

Maumivu wakati wa tendo la ndoa huweza kutokea kwa mwanamke au mwanaume, hali ya kuwa na tatizo hili huwakumba sana hasa wanawake ukilinganisha na wanaume.

Sababu zinazopelekea kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspareunia) ni kama zifuatazo:

1. Kupungua au kukauka kabisa kwa ute ute ukeni (vaginal mucous) hali hii humpekekea mwanamke kuhisi maumivu kutokana na msuguano wakati wa tendo la ndoa vile vile huweza kumsababishia michubuko ukeni.

2. Maambukizi ya magonjwa katika via vya uzazi vya mwanamke kama vile fangasi sugu wa ukeni (vaginal fungus), mashambulizi ya maambukizi katika ukuta wa nje wa kizazi (endometriosis).

3. Ukomo wa hedhi (menopause),maumivu huwakumba pia wanawake waliofikia ukomo wa hedhi kutokana na kupungua kwa hali ya unyevuvyevu ukeni (vaginal moisture) na kuwa mkavu ukeni.

4. Kushiriki tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua, baada ya kuvifungua misuli na tishu za uke hulegea na huwa zinarudi katika hali yake pole pole, hivyo basi endapo mwanamke atashiriki tendo la ndoa wakati huo humpelekea kuhisi maumivu makali sana.

5. Matatizo ya kisaikologia (psychological factor)kama vile uoga (anxiety). msongo wa mawazo. Hata mwanaume huweza kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa wa wakati wa kutoa mbegu (Ejaculation), maumivu hayo hutokana na maambukizi au vidonda kwenye (gland)ambazo huruhusu mbegu kutoka (prostate gland). Wakati mwingine maumivu kwa wanaume husababishwa na maambukizi kwenye ngozi inayofunika uume.

*Mpendwa rafiki, magonjwa ya zinaa huchangia tatizo hili kwa kiasi kikubwa, hivyo ni vyema kwenda na mwenza wako mkachunguzwe na kutibiwa kwa pamoja mara nyingi tiba hufanyika kutokana na tatizo husika.

Ni namna gani unaweza kujikinga na tatizo hili?

Ni muhimu kuzingatia usafi kwani hupunguza uwezekano wa kupata maambukizi.

Kila mtua anatakiwa kumuandaa mwenza wake kabla ya kushiriki tendo la ndoa ambalo husaidia kuzalishwa kwa maji maji ya kulainisha njia ya uzazi (ukeni).

Kuepuka kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya kujifungua, ni vyema kushiriki tendo la ndoa angalau wiki sita baada ya kujifungua.

Tiba na ushauri

Endapo mwanamke au mwanaume anapokuwa na tatizo la maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, ni vyema akaenda kwenye kituo cha afya na kuonana na mtaalamu wa afya ya uzazi na mtoto kwaajili ya ushauri, vipimo na matibabu.
MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA TENDO

Tatizo hili huwasumbua baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, yaani kuanzia miaka 18 hadi 40. Tatizo huweza kuanza ghafla au taratibu pale mwanamke anapofanya tendo . Maumivu haya hutokana na hali ya mabadiliko ukeni ambapo uke huwa mkavu daima au mwanamke anapata vipindi vya ukavu ukeni na katika mlango wa kizazi pia husababisha tatizo hili .

Maumivu yanaweza kuwa ndani ya kizazi , yaani wakati wa tendo unahisi kuna kitu kinasukumwa na ukahisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kiuno wakati wa tendo . Maumivu pia yanaweza kutokea baada ya tendo la ndoa , mwanamke akafanya tendo la ndoa vizuri lakini anapomaliza tu akijigeuza anahisi maumivu chini ya kitovu na kiuno na wakati mwingine hata kichefuchefu.

Chanzo cha tatizo Tumeona vyanzo vitatu vya maumivu wakati wa tendo ambavyo ni ukavu ukeni. Huu unatokana na maandalizi hafifu kabla ya endapo hakuna maandalizi yoyote basi uke unakuwa mkavu na unashindwa kufanya tendo au linafanyika kwa nguvu . Ukavu unaweza kusababishwa na kutokuwa na hamu ya tendo au kutojisikia kufanya tendo , hili linaweza kusababishwa na matatizo ya kisaikolojia au katika mfumo wa homoni.

Michubuko ukeni na katika mdomo wa kizazi husababishwa na maambukizi , kansa au kufanya tendo la ndoa kwa nguvu bila maandalizi au ubakaji .

Maambukizi ukeni huambatana na kutokwa na uchafu wenye harufu na muwasho . Maambukizi yanaweza kusababishwa na fangasi, bakteria na magonjwa ya zinaa.

Maumivu ya ndani hutokana na maambukizi katika viungo vya uzazi mfano , ndani ya kizazi , mirija na vifuko vya mayai . Maambukizi haya huanzia ukeni na kusambaa hadi ndani ya kizazi , lakini pia yanaweza kuanzia kwa ndani hasa baada ya kuharibika au kutoa mimba . Dalili za tatizo Maumivu wakati wa tendo la ndoa yanaweza kuanza mara tu tendo linapoanza , au tendo linapoendelea. Vilevile maumivu yanaweza kutokea baada ya tendo kumalizika .

Mwanaume pia anaweza kupata maumivu wakati wa tendo au baada ya tendo kutokana na michubuko katika uume , matatizo katika misuli ya uume , maambukizi ndani ya njia ya mkojo na matatizo ya korodani . Maumivu ya kiuno kwa wanaume na wanawake pia ni mojawapo ya tatizo kubwa. Uchunguzi Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa huchunguzwa hospitali ambapo vipimo mbalimbali hufanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.

Vipimo vya kuangalia ukeni, damu , mkojo na Ultrasound hufanyika kutegemea na ukubwa wa tatizo . Ushauri Ni vema uwahi hospitali kwa uchunguzi wa kina na tiba.

Tatizo likiwa sugu yaani kukusumbua mara kwa mara husababisha upotevu wa hamu na raha ya tendo . Kwa mwanaume hata uwezo wa kufanya tendo la ndoa hupotea . Waone madaktari katika hospitali ya mkoa na wilaya kwa uchunguzi na tiba .
UNAUMIA WAKATI WA TENDO LA NDOA? SOMA HAPA!

HII ni hali ambayo mwanamke anakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa lakini anapata ugumu kutokana na maumivu makali anayopata.

Hali hii inatokana na kubana au kukaza kwa misuli ya uke lakini pia inaweza kusababishwa na matatizo ukeni.

Mfano endapo kuna michubuko au vidonda au kasoro yoyote ya uke, aidha uke ni mdogo au maumbile ya uke hayana uwiano na uume. Tatizo hili huwapata wanawake wa rika zote ilimradi tayari yupo katika umri wa kuzaa.

TATIZO LINAVYOGAWANYIKA

Tatizo hili la maumivu wakati wa tendo la ndoa limegawanyika katika maeneo makuu mawili. Kwanza ni Primary Dyspareunia .

Hapa mwanamke anakuwa hana historia ya maumivu wala hana historia ya kuwahi kufanya tendo hilo ndiyo, kwanza anaanza. Kitaalamu hali hii ya maumivu huitwa Honey moon Dypareunia au maumivu ya fungate na hutokea mara tu anapoanza kujamiiana kwa mara ya kwanza. Katika hali hii misuli ya uke inaweza kubana kutokana na michubuko au kuchanika ubikira au hata kuchanika upande wa chini wa uke na wakati mwingine michubuko hutokea katika tundu ya mkojo.Hali ya michubuko inaweza kuwa mbaya na ikajitokeza hata kwa kugusa tu upande wa nje wa uke.

Maumivu yakiendelea au yakizidi husababisha mgonjwa apate matatizo ya kisaikolojia kiasi kwamba huanza kuogopa tendo lenyewe na kuhisi endapo atalifanya ataumia. Tatizo hili likileta michubuko kwenye njia ya mkojo husababisha maambukizi sugu ya kibofu cha mkojo kutokana na michubuko ya mara kwa mara ya tundu ya mkojo.

Maumivu ukeni hutokana pia na maandalizi mabovu kabla ya tendo ambapo uke unakuwa haujalainika kwa kutofanya romance ya kutosha, kutofanya tendo hilo kwa ustaarabu, yaani kutumia nguvu au endapo mwanamke atakuwa na maambukizi ukeni mfano fangasi ambayo huambatana na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho, magonjwa ya uke kama kuvimba kwa tezi za uke, kuvimba kwa mashavu ya uke au hali yoyote inayomwondolea amani mwanamke pale ukeni inaweza kumfanya kisaikolojia aathirike na kuhisi maumivu wakati wa tendo.

Michubuko ukeni au kuhisi moto ukeni wakati wa tendo la ndoa kunaweza kusababishwa na matumizi ya vilainishi visivyofaa au kuumwa kutokana na uwepo wa vinyweleo virefu ukeni na endapo havikupunguzwa vitaingia ukeni wakati wa tendo na kukuchubua. Kasoro katika ubikira pia husababisha mwanamke ahisi maumivu wakati wa tendo.

Maumivu haya huwa hayahusiani na yale ya awali ya fungate na wakati mwingine huanza baada ya kipindi kirefu cha miaka mingi tangu uanze tendo la ndoa na wengine huwa na tatizo hili tayari wana watoto. Chanzo cha tatizo hili ni ukavu ukeni, umri mkubwa wa mwanamke na kusinyaa kwa misuli ya uke.

Matatizo haya isipokuwa la umri mkubwa hutokea katika umri wa kati na tayari mwanamke anayo historia ya kuwa katika mahusiano na hata tayari ana watoto. Umri mkubwa tunaouzungumzia ni zaidi ya miaka hamsini. Kubana misuli ya ukeni hutokana na makovu baada ya kushonwa msamba au kuongezewa njia wakati wa kujifungua au upasuaji wa kurekebisha fistula pia husababisha tatizo hili.

Vyanzo vingine vya maumivu haya ya tendo la ndoa ni kushuka kwa kizazi ambapo mwanamke atahisi kitu kama gololi ukeni wakati akijisafi sha au kuhisi kizazi kinasukumwa wakati wa tendo, kugeuka kwa kizazi, matatizo katika tabaka la ndani la kizazi, maambukizi sugu ukeni ambapo uchafu na muwasho ukeni hujirudiarudia, matatizo katika njia ya mkojo na maambukizi katika viungo vya uzazi ’PID’ husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Matitizo ya kisaikolojia husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa pale ambapo misuli ya ukeni itakaza na mwanamke anapochunguzwa huwa hana tatizo au kasoro yoyote ukeni. Matatizo katika mishipa ya fahamu ya ukeni, kuogopa tendo lenyewe kuhisi utapata maumivu au kama kuna historia ya kuingiliwa kwa nguvu na ukaumia, kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu tendo la kujamiiana, yote haya na mengine mengi humharibu mwanamke kisaikolojia na kujikuta anaanza kuhisi maumivu hata kabla ya tendo lenyewe kwa kuingiwa na hofu.

Hali nyingine inayoweza kumfanya mwanamke aathirike kisaikolojia na asiwe tayari kwa tendo na hata akilifanya apate maumivu ni kuogopa kupata ujauzito wakati hayupo tayari kwa hilo, kuogopa kupata maambukizi, kulazimishwa penzi endapo haupo tayari na mwanaume uliye naye na kuhisi kuna tofauti ya maumbile na mume uliyenaye.

Endapo mwanaume anakukwaza kutokana na kutokwa na jasho jingi sana wakati wa tendo, kutoa harufu mbaya ya pua, kinywani, makwapani au sehemu zake za siri, huwa na magonjwa ya ngozi au hata mwilini mwake, matatizo haya huweza kumwathiri mwanamke kisaikolojia na asifurahie tendo na kutotoa ushirikiano wakati wa tendo na kupata maumivu.

UCHUNGUZI Tatizo hili ni pana sana, unaweza kuhisi una kasoro au maambukizi kumbe tofauti. Kwa hiyo basi ni vizuri uchunguzwe kwa umakini katika kliniki za madaktari wa akina mama katika hospitali za mikoa ili kujua chanzo halisi cha tatizo.
Chanzo: GBP
USHAURI KWA ANAYEPATA MAUMIVU WAKATI WA TENDO
 1. Jichunguze wewe mume kwanza. Je, huna vimwana wasiojua kuoga na kusafisha nyeti zao kwa maji safi na salama?
 2. Uwe makini sana na utendaji kazi wako. Uzamishaji wa oil stick kwenye Engine sio sawa na urefu wa stick izame yote. Zamisha Stick kwa uangalifu na si lazoma uende mpaka Brake iwe ni Bulb zako.
 3. Uchanganyaji wa sera ya maandalizi ya mwenzi wako si mke tu anaye andaliwa bali hata mume huandaliwa sawa dada zangu. Mume huandaliwa ili ukali na vurugu ukiherehere wa kupanda gari wakati hujatiza maji yapo? oil imeshuka au lah? na je nyaya za betri ziko active?
 4. Dada zangu Ubinafsi wenu ndio unawafanya mnapata hayo maumivu makali maana nyie mnaona haki ni kwenu tu na wenzenu oooooh!!!!!!!
 5. Mwisho kama unayafanya haya yote na bado unasikia maumivu, Jaribu kumuona daktari mkiwa na mwenzi wako ili mpate ushauri kwani Conc. U.T.I inaweza kusababisha hayo muanza dozi wote.
ZINGATIENI SANA HAYO.
 

NG'ADA

Senior Member
Sep 2, 2011
152
15
Somo zuri kaka. Saaana!! Maana hata mimi limenikuta hilo, kijana nahangaika mwisho wa siku ni kusumbuana tu na kukojolea mashavuni mwa "mma"! Mbaya zaidi maandalizi yalikua yanachukua muda wa kutosha, ila ukitaka tu kubisha hodi, kesi. Ila KY inasaidia.
 

Emasaku

Member
Sep 24, 2011
51
6
Kaka hii kitu mpenzi wangu anayo. Wakati wa tendo yeye anasikia maumivu na wakati mwingine pana waka moto, kuna siku tulikutana kimwili na alipata hiyo hali lakin hakumia sana kivile, chakushangaza kesho yake alinipigia cmu nakudai anasikia maumivu makali na kumevimba! Kaka hii hali inatiba? Hebu nisaidie nisije nikapoteza kipenzi changu!
 

Baba Erick

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
483
74
Nimechoka ila niwape kiprofessional kidogo. Maumivu haya kwa wanawake yanatokana na
i) STDs/STIs
ii) FUNGI
iii) Cancer.
 

Emasaku

Member
Sep 24, 2011
51
6
Asante kwa elimu yako mkubwa kwani mpenzi wangu analo hili tatizo, bora nitafute tiba mapema!
 

AshaDii

Platinum Member
Apr 16, 2011
16,219
17,980
Asante kwa Ujumbe Pidy, ila siku nyingine ukitaka kweli members tusome don't put picha inachkua kama more than five minutes kuingalia. lol
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
Baba erick,

Sisemi muongo ila hizo zinachangia maumivu. Binafsi nikiwa na google nimeona mtu akiwa anaumia kweli ingwa katikati anaita tamu huku mwanzoni kaumia na tukapima zote hapo juu -NIL

Tulichofanya nikuamini hayo ndio mapenzi tuliopewa na muumba mppaka akaja kuolewa, ila ukiona mtu anaumia pls nenda pima hayo juu ukikuta akuna kitu basi hilo neno yaani ndio mzigo wako.
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
Kila mwanamke kwenye uke wake kuna kiwango muhimu cha bacteria, fungus, yeast au protozoa na hawa viumbe hawana madhara yoyote katika mwili hadi hapo kiwango chake kikiathirika na mazingira yake kama matumizi ya antibiotics, kuwa na medication au madawa na uzazi wa mpango na ndipo matatizo hutokea na kupata haya matatizo si kuwa unaumwa magonjwa ya zinaa ni hali ya kawaida kitu muhimu lazima uhakikisha unapata dawa.

Leo tumalizie na mambo yanayosababisha kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke.

Maambukizo (vaginal infection)
Mwanamke anaweza kupata maambukizi kutokana na bacteria, fungus, yeast na amoeba. Kawaida kwenye sehemu za siri za mwanamke kuna kiasi kikubwa cha bacteria, fungus, yeast au amoeba ambao hawana madhara yoyote hadi pale uwiano ukiwa tofauti kutokana na sababu mbalimbali kama vile madawa nk. Maambukizi (infections) yanapotokea kawaida kunakuwa na mabadiliko yafuatayo:
 • Kubadilika rangi kwa majimaji yanayotoka sehemu za siri za mwanamke,
 • Pia kutoa harufu mbaya baada ya tendo la ndoa,
 • Kuvimba sehemu za siri,
 • Kusikia maumivu wakati wa haja ndogo,
 • Kuumia wakati wa tendo la ndoa (maumivu ya kama kuchoma na kuwasha).
Menopause
Upo wakati mwanamke anafikia (miaka 48 - 52) muda ambao hawezi kuzalisha tena homoni za estrogen zinazosababisha kuzalishwa kwa yai kila mwezi. Kutokuwepo kwa hii homoni husababisha uke wake kuwa mkavu hata wakati wa tendo la ndoa. Uke kuwa mkavu husababisha kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa na hasa kama hakuandliwa vizuri.

Zipo sababu zingine kama vile hitilafu katika maumbile ya uke kutokana na operation au kubakwa n.k husababisha mwanamke kujisikia maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Je, wanaume nao hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa?
Ni kweli inawezekana kwa mwanaume kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa ikiwa:
 • Amepata maambukizi ya bacteria, fungus au yeast kutoka kwa partner wake
 • Kama ameambukizwa magonjwa ya zinaaa
 • Kama hajatahiriwa na hasa kama ndo anaanza kufanya tendo la ndoa atajisikia maumivu kwa sababu ya gozi (foreskin) kugoma kujivuta nyuma.
 

mselem nation

New Member
Oct 15, 2011
1
0
USHAURI WANGU
 1. Jichunguze wewe mume kwanza. Je, huna vimwana wasiojua kuoga na kusafisha nyeti zao kwa maji safi na salama?
 2. Uwe makini sana na utendaji kazi wako. Uzamishaji wa oil stick kwenye Engine sio sawa na urefu wa stick izame yote. Zamisha Stick kwa uangalifu na si lazoma uende mpaka Brake iwe ni Bulb zako.
 3. Uchanganyaji wa sera ya maandalizi ya mwenzi wako si mke tu anaye andaliwa bali hata mume huandaliwa sawa dada zangu. Mume huandaliwa ili ukali na vurugu ukiherehere wa kupanda gari wakati hujatiza maji yapo? oil imeshuka au lah? na je nyaya za betri ziko active?
 4. Dada zangu Ubinafsi wenu ndio unawafanya mnapata hayo maumivu makali maana nyie mnaona haki ni kwenu tu na wenzenu oooooh!
 5. Mwisho kama unayafanya haya yote na bado unasikia maumivu, Jaribu kumuona daktari mkiwa na mwenzi wako ili mpate ushauri kwani Conc. U.T.I inaweza kusababisha hayo muanza dozi wote.
ZINGATIENI SANA HAYO.
 

Caroline Danzi

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
3,712
1,244
Leo nimefarijika na somo hili. Kesho nitakuja na maswali yangu. Ngoja niandae kwanza. Asanteni sana kwa muda wentu kutuelimisha.

CD
 

AMINATA 9

JF-Expert Member
Aug 6, 2011
2,128
640
Ila hua watu wengi wanaumia sana alafu mi hua nashangaa wanaume hawaumii hata loh! Kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya Firauni, hebu mie napita tu hapa maaaaana.
 

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
575
Thanx kwa somo hii ndo faida ya JF jamani; burudani na somo juu be blessed wajameni.
 

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
109
Wana JF,

Mke wangu yupo mbali kikazi na kwa sasa ni mjamzito. Tumekuwa tukikaa hata miezi2 bila kuonana. Nikifika na 2kianza sex analalamika kuumia sana na vagina huwa imejirudi sana hata kupenetrate inakuwa kwashida.

Baada ya siku3 au 4 ndipo huanza kuingia kiurahisi. Pia anasema hasikii hamu yakusex tangu apate ujauzito. Wataalamu hebu fungukeni hapa sababu ya maumivu, vagina kujirudi na yeye kutosikia hamu ya sex.
 

Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,540
13,439
Wewe unakuwa na hamu, mwenzio ameshapoteza hamu with time. Unatakiwa uende naye taratibu na Mazingira yawe mazuri.

Kuhusu kukosa hamu wakati wa ujauzito, itakuwa mimba imekukataa tu. Mimi pia ilinitokea, nilimchukia baba wa mtoto wangu, nilikuja kumpa mtoto ana miezi minne.

Wengine hupelekea kuwapenda waume zao na kuwataka 24/7.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom