elimu pia ni duni huenda alikuwa na effection ya bacteria huyo au dalili za malaria, nyingine huanzia tumboni
Hahaha unaweza kuta marehemu alikuwa anaakili na elimu kubwa kuliko wewe kuliko. Ingawa sikubaliani na maelezo ya mleta mada kuhusu majibu ya maabara kuonyesha kuwa mgonjwa alikuwa na vidonda vya Tumbo. Hiyo maabara wanapiga x-ray au walipimaje vidonda vya tumbo? ingawa nafahamu wanaweza kupima uwepo wa H.pylori lakini pia haimaanishi sasa mgonjwa ana vidonda vya tumbo kwa positive H.pylori.
Rushwa ni nzuri ukipokea , lakini inapofika zamu yako kutoa inauma sana.
Kuna jamaa anafanya kazi TRA, ana piga pesandefuu za rushwa , lakini kuna maeneo hana ujanja naye anapokamuliwa , duh analalamika utadhani ndio katoka mbinguni leo, kwamba hajawahi ku experience ya Tanzania hii.
Kwa ufupi, Hospitali na maabara nyingi hazina huwezo uwezo wa kupima kila kitu, majibu mengine tunapewa ni ya uongo tu. Na kuna vipimo vinachukua muda mrefu kuanzia masaa 24 hadi 48 kutoa majibu, lakini hizi hospitali na maabara zao unaweza kufika ndani ya dakika 10 ukapata majibu, huo ni uongo, na madaktari wamekuwa wazembe wana tibu wagonjwa kwa majibu ya uongo.
Kila taaluma ina utaratibu wake lakini wananchi wamechangia taaluma nyingi kuwa za hovyo hovyo. Mtu anaweza ku google kutafuta miziki ya diamond, lakini hawezi ku google kutafuta symptoms alizonazo angalau apate highlights of what might be causing what he feels, na how to diagnose and even treat the condition or disease of interest. Jamani tujielimishe kwenye mambo hata madogo, ya afya zetu, hii inaweza kukufanya ukauliza maswali sahihi kwa mtaalam wa afya, au ikakupa uelewa wa wapi uende kupata tiba sahihi na unaweza ukajieleza kwa ufasaha zaidi.
HOSPITALI HAKUPIGWI RAMLI JAMANI.