Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,321
Kweli mkuu barabara zimepunguzwa upana sana kiasi kwamba malori mawili kwenda sambamba kama ilivyokuwa zamani ni shida. Zamani ilikuwa magari makubwa na madogo yanaweza kwenda sambamba na kisha nafsi kubaki hata ya mwendesha baiskeli,pikipiki mtembea kwa miguu kupita lakini sasa ni shida. Labda kuwe na mpango wa kupunguza upana wa magari makubwa kama malori na mabasi
Shida kama uko maeneo ya kimara baruti unataka kurudi mbezi ni lazima uende hadi ubungo ndio upate njia ya kurudi
Ni uendeshaji mbovu wa madereva,ukiendesha bila kufuata sheria za barabarani,ajali ni lazima ikutokee.Kuna mapungufu kadhaa kwenye design ya Dar es Salaam Rapid Transit network:
(1) Barabara za lami ni nyembamba mno kiasi kwamba nafasi kati ya gari na gari ni ndogo sana (inch 18).
(2) Kuna baadhi ya sehemu njia ya gari za kawaida imeingiliana na njia ya gari za mwendo kasi (kuanzia Kibo hadi Kimara) na hii imesha sababisha ajali na vifoo kadhaa hadi sasa.
(3) Barabara zimewekewa kinga za kuzuia kuingia au kutoka hadi maeneo maalumu ya matoleo na hivyo kukitokea ajali msongamano unaotokea unakuwa ni tabu kuupunguza haraka
(4) Kule mwishoni Kimara njia ina kona balaa mfano wa herufi S na imeshasababisha ajali kadhaa hasa kwa magari makubwa kupitiliza na kuanguka
(5) na kadhalilka na kadhalilka......nitaongezea baadaye!!
Shida kama uko maeneo ya kimara baruti unataka kurudi mbezi ni lazima uende hadi ubungo ndio upate njia ya kurudi
Technically hiyo barabara italeta ajali sana hususani magari kupigana pasi.
Naomba kujuzwa, barabara za DART zitakuwa na hizi daladala za kawaida tena?
Nauliza hivi coz nilikuwa na argument na rafiki yangu, tulipita njia hiyo lakini sikuona bus stops za kawaida, aside zile za mabasi ya mwendo kasi, ndio maana nauliza, daladala za "kimara-k.koo, kimara-posta, kimara-mwenge'' zitatumia njia hiyo?
Na. 1 Nafikiri serikali inampango wa kuzifanya barabara hizo kuwa za magari madogo tu mwisho size ya coater au canter vinginevyo hizi nguzo za taa zitapigwa chini zote kwani nazo zipo karibu sana na barabara ukizidiwa cha kwanza ni kuzitandika hizo nguzo. Mbona ile ya Sam Nu Joma Iko fresh na nguvu za taa mpaka uzifuate zilipo basi wewe unakuwa na lako jambo. Barabara pana na ni ya kujimwaga na ndio maana ni nadra sana kukuta ajali za kupigana pasi au nyingine katika barabara ile labda dereva awe wa viroba na bangiKuna mapungufu kadhaa kwenye design ya Dar es Salaam Rapid Transit network:
(1) Barabara za lami ni nyembamba mno kiasi kwamba nafasi kati ya gari na gari ni ndogo sana (inch 18).
(2) Kuna baadhi ya sehemu njia ya gari za kawaida imeingiliana na njia ya gari za mwendo kasi (kuanzia Kibo hadi Kimara) na hii imesha sababisha ajali na vifoo kadhaa hadi sasa.
(3) Barabara zimewekewa kinga za kuzuia kuingia au kutoka hadi maeneo maalumu ya matoleo na hivyo kukitokea ajali msongamano unaotokea unakuwa ni tabu kuupunguza haraka
(4) Kule mwishoni Kimara njia ina kona balaa mfano wa herufi S na imeshasababisha ajali kadhaa hasa kwa magari makubwa kupitiliza na kuanguka
(5) na kadhalilka na kadhalilka......nitaongezea baadaye!!
Copy and paste Mkuu, yaelekea kule ilimo patikana hii copy barabara haitymiwi na malori, kwa kuwa ni uwazi baadhi ya sehemu masemi trailer inabidi yawe yanasubiriana;mfano mzuri ni eneo kuelekea KIMARA mwisho na kupita daraja la kimara .
Kitu kingine yaonekana ilikochukuliwa copy ya barabara ni ukanda wa Tetemeko la ardhi, hebu angalia reinforcement ya vituuo vya abiria !
Huo mradi na Mkopo uliotumika kufanikisha mtazamo wangu ni uthibitishho tosha kuonyesha uzuzu wa watz ...
Na ukishatoka ubungo mataa, ukashindwa ku-U- turn SHEKILANGO, safari yk inakuhusu MWEMBECHAI!
mkuu unaweza kukatia pale soko la big brother Kuna u turn pale
Ukiacha ufinyu wa barabara! Shida nyingine ni pale watakaposhuka kwenye mabasi na kutaka kuvuka ili waingie pembeni mwa barabara! Magari katika barabara za kawaida yatalazimika kusimama mara kwa mara karibia kila kituo! Hapo ndo watatengeneza foleni za kufa mtu! Magari yatakuwa hayatembei kabisa!Foleni itakuwa pale pale kwani naona barabara bado ni finyu mno. Anyways kujuwa ubora wake ngoja tusubiri mvua zetu hizi tuone kama ni lami kweli au ni disel imepakwa kwenye moram. Bongo hii kwa usanii nafikiri tunaongoza duniani tukifuatiwa na wachina.