Hongereni STRABAG! Dar Rapid Transit imefana mno!

Hongereni STRABAG! Dar Rapid Transit imefana mno!

Ngoja tuone na ile ya mchina banana to chamazi
 
Designers ndio wakulaumiwa kwa ufinyu wa barabara
 
Barabara ni nyembamba sana. Haifai kabisa. Kupigana pasi hapo kawaida.
 
Naomba kujuzwa, barabara za DART zitakuwa na hizi daladala za kawaida tena?
Nauliza hivi coz nilikuwa na argument na rafiki yangu, tulipita njia hiyo lakini sikuona bus stops za kawaida, aside zile za mabasi ya mwendo kasi, ndio maana nauliza, daladala za "kimara-k.koo, kimara-posta, kimara-mwenge'' zitatumia njia hiyo?

Itakapokamilika, njia hiyo haitakuwa na daladala, ni mabasi ya mradi tu.
 
Foleni itakuwa pale pale kwani naona barabara bado ni finyu mno. Anyways kujuwa ubora wake ngoja tusubiri mvua zetu hizi tuone kama ni lami kweli au ni disel imepakwa kwenye moram. Bongo hii kwa usanii nafikiri tunaongoza duniani tukifuatiwa na wachina.
 
Kweli mkuu barabara zimepunguzwa upana sana kiasi kwamba malori mawili kwenda sambamba kama ilivyokuwa zamani ni shida. Zamani ilikuwa magari makubwa na madogo yanaweza kwenda sambamba na kisha nafsi kubaki hata ya mwendesha baiskeli,pikipiki mtembea kwa miguu kupita lakini sasa ni shida. Labda kuwe na mpango wa kupunguza upana wa magari makubwa kama malori na mabasi

wakuu Bulldog na Tulimumu, ukweli hiyo barabara ni finyu mno. Inabidi uwe dereva mzuri kulipita roli kwani unaona kabisa limemaliza sehemu kubwa ya barabara. Sijui nani alidesign barabara ya hivi.

Tiba
 
Foleni itakuwa pale pale kwani naona barabara bado ni finyu mno. Anyways kujuwa ubora wake ngoja tusubiri mvua zetu hizi tuone kama ni lami kweli au ni disel imepakwa kwenye moram. Bongo hii kwa usanii nafikiri tunaongoza duniani tukifuatiwa na wachina.

Miradi mingi inayo fanywa na serikali ya ccm ni ya kukurupukia haina ubunifu wowote hovyo kabisa hawa watu.
 
Hii barabara ni rafiki kwa mabasi ya mwendo kasi tu lakini kwa watumiaji wengine ni shida! Ajali nje nje kwa wanaovuka popote isipokuwa vituoni tu, na kupigana pasi za hapa na pale.
 
Hii barabara ni rafiki kwa mabasi ya mwendo kasi tu lakini kwa watumiaji wengine ni shida! Ajali nje nje kwa wanaovuka popote isipokuwa vituoni tu, na kupigana pasi za hapa na pale.
Wamepunguza sana upana wa barabara kama kiasi kwamba tutapigana pasi sana na tukijitahidi kukwepana tutakuwa tunazitandika zile nguzo za taa barabarani na si dhani kama zitasalimika zile. Boda boda wajiandae kwa kiama zaidi hasa inapotokea wanakatiza katikati ya magari kwani nafasi haitoshi hivyo wataishia mivunguni mwa magari kwa haraka zao maana wao wanataka kupita sehemu yoyote na wakati wowote. Hata hizo barabara za katikati za mabasi ni finyu sana kama dereva ni mtu wa kupepesa macho pembeni atajikuta ameparamia pavement blocks na kuhamia upande wa barabara za raia ambako nako ni kufinyu. Solution ni kuamua kuwa barabara hizi zitumike na vigari vidogo tu mwisho size ya coaster na canter. Milori na mibasi iishie nje ya mji kwani kwa ukubwa wao moja tu linatosha barabara yote na usiombe liwe na trailer ndio balaa! Na likiharibika barabarani ndio shida kubwa!
 
Mimi kinachoniuma ni kitendo cha sisi wenyewe kutokuwa wastaarabu afu tunasingizia ubora si mzuri. Jamani watu wanatupa taka hovyo magari yanavyo overtake ni shida yaani mtu hatumiii hata akili ya kawaida tu kwamba hii barabara imekuwa nyembamba kwa hiyo hata uendeshaji inabidi uwe makini ili usiharibu miundo mbinu na chombo chako niko against na serikali kwa mambo mengi lakini kuna mengine tunawaonea tu. nimekuwa nikifatilia hata stand ya hapa mbezi asubuhi huwa inafagiwa ukipita hadi unafurahia subiri baada ya masaa 3. Na vyombo vya kuhifadhia taka pale vipo kabisa lakini utakuta uchafu hadi inasikitisha. Kuna mambo tuache kulalamika kabisa mtu akikutengenezea kitu wewe ukaki haribu kwa matumizi ya hovyo hata kingekuwa kitu imara au chenye ubora wa vipi kitaharibika tu kabla ya wakati wake tunapaswa kubadilika

Tatizo ustaarabu kwetu zero. Mbona kwa wenzetu wanaweza? Mimi nimekaa miezi kadhaa kwenye mji mmoja US bila kuona takataka barabarani wala kwenye viunga. Supermarket zinagawa mifuko ya plastic (rambo, marlboro) kama njugu kwa wale wanaonunua bidhaa ili wabebee, lakini hauikuti barabarani kama ilivyozagaa kwetu. Kwa sasa pembeni ya barabara labda utakuta yamejaa majani makavu tu yanayodondoka toka mitini kwa sababu ya majira (fall) lakini si uchafu unaotupwa na watu. Tunatakiwa kubadilika, tuyapendezeshe mazingira yetu ili hatimaye tuyapende.
 
Barabara ni nyembamba sana. Haifai kabisa. Kupigana pasi hapo kawaida.

Huo wembamba ni tatizo, na ndio hapo inatakiwa madereva wabadilike vichwani mwao. Tumezoea kuendesha kibabe sana ndiyo maana hata kabla watu kupigana pasi ilikuwa kawaida. Madereva wakiwa wastaarabu ninao uhakika kabisa hakuna atakayepiga wala kupigwa pasi. Wasiwasi wangu ni je, huo ustaarabu utapatikana kweli? Maana kila mtu ni mjanja, lazima aendeshe kwa kasi, mbwembwe na maringo ili aonekane anafahamu. Katikati ya mji unataka kuendesha kama uko highway. Kwenye zebra crossing unapita tu bila kupunguza hata mwendo uangalie kama kuna watu wanataka kuvuka, kwanza ndio unapiga honi kubwa hadi wenye matatizo ya moyo wanataka kuanguka wakati pale ni haki yao kuvuka, kama wapo inatakiwa uwasubiri.

Mimi naona hapa tusilaumu sana wembamba wa barabara, ni sisi wenyewe madereva aidha kwa sababu ya haraka zetu zisizokuwa na sababu ya msingi, au kwa kuwa wengine hata kuendesha kwenyewe hatujui. Kifupi matatizo zaidi yatatokana na kukosa ustaarabu kuliko wembamba/ufinyu wa barabara kwa vile tu tutataka kuendesha kama tunaenda Mbeya!

Tujipange kubadilika.
 
Kweli kabisa mdau, barabara hii inapita katikati ya mji lakini madereva wengine wanaendesha kwa spidi nakibabe kama vile ni high way iliyo nje ya mji. Labda tukisha pigana pasi za kutosha na kuuwana sana ndo tutabadilika na kuwa wastaarabu lakini nadhani hii itachukua muda
 
Kwahili naipongeza serekali kwa kujitahidi. Mimi kero yangu kubwa na ni viongozi wetu kukosa kiburi cha kujaribu. Inawezakana kabisa huu mradi usikidhi mahitaji yote ya wana-Dar es Salaam lakini angalau serekali imejaribu na kwa kiasi chake imefanikisha. Kazi imebaki kwetu sisi kuwa mabalozi wazuri wa huo mradi. Kama wadau waliotangualia kusema hapo juu, kuna vitu vingine tunalaumu serekali bure. Ili kusonga mbele wananchi na serekali tunatakiwa sote tutumie juhudi sawa. Barabara kuwa nyembamba sio shida tena inawezekana kabisa imetengenezwa hivyo kusaidia kupunguza uendeshaji hatari tunaouoona mjini kila siku. Tuambiane ukweli hizo lanes zingekuwa kubwa mno watu ndo wangefanya Formula 1 practice track. Hiyo barabara iko mjini na nenda miji yote mikubwa duniani barabara za mijini haziko designed ili watu waendeshe kasi tunazoendesha sisi, unless kama iko designed for highspeeds. Kiukweli sisi wananchi pia tunatakiwa tubadilike kwenye matumizi yetu ya barabara.

Afu naona hilo neno "Rapid" kwenye jina la mradi lina-mislead watu. Kwa uelewa wangu sio kwamba mabasi yatakuwa yanaenda kasi kama neno linavyosuggest, ni kwamba mabasi yatasafiri kwa haraka zaidi kwa sababu hayata kuwa na haja ya kuminyana na magari mengine. Au nimekosea?

Afu hamna kitu kinanikera kama kuona mtu anaruka msingi barabarani. No road was designed so you can drive over the curb!! It's there to keep the cars on the road. Kama ni hivyo tungejenga vizuizi vitupu. Watu wanaruka misingi na mabasi, malori, piki piki, mikokoteni, etc, Barabara ikikongoreka wakwanza kulalamikia kiwango cha barabara. Pita Manzese pale uone capstone zimeshaanza kungo'ka mradi bado hata haujakamilika hafu tunalalamika viwango wakati wahalifu wa kwanza ni sisi wenyewe.

Big up to the government for daring, kazi kwetu.
 
Back
Top Bottom