Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 16,861
- 25,769
Motel Agip iliyopo Posta jijini Dar es Salaam ilifungwa rasmi tarehe 18 Desemba 1998 kutokana na mgogoro mkubwa wa kimkataba wa upangaji na ukodishaji kati ya uongozi wa hoteli hiyo na mmiliki wa jengo, kampuni ya mafuta ya Agip Tanzania Limited. Hoteli hiyo yenye vyumba 57 ilikuwa kitovu kikuu cha burudani na diplomasia nchini.
Mpaka leo , 16-7-2026 Hotel imekuwa gofu, wanalala mateja na vibaka Posta, haizalishi na imekuwa uchafu katikati ya Jiji.
Kuanzishwa kwa Motel Agip:-
- Mwaka wa Ufunguzi: Hoteli ilikamilika na kuanza huduma rasmi mwaka 1964.
- Waasisi: Ilijengwa na kampuni ya mafuta ya Kiitaliano ya Agip (Azienda Generale Italiana Petroli)kupitia shirika mama la ENI.
- Lengo la Mradi: Ilikuwa sehemu ya mpango mkakati wa Italia uliorubuniwa kama "disegno africano"kupanua soko la nishati na huduma barani Afrika.
- Upekee wake: Ilikuwa kielelezo cha usanifu wa kisasa wa Kiitaliano na ilijumuisha ukumbi wa mazoezi ghorofa ya sita ukiangalia Bahari ya Hindi.
- Umaarufu: Ilikuwa maskani ya wanadiplomasia, wafanyabiashara, na wasafiri. Pia ilitamba sana kutokana na Disco la Mawingu lililokuwa likiongozwa na Ma-DJ nguli kama DJ Bonny Love.
Kufungwa kwa Hoteli (1998)
- Sababu Kuu: Mgogoro wa mkataba wa kodi na upangaji uliokuja juu kati ya uongozi wa uendeshaji (chini ya Mkurugenzi Emmanuel Mantheakis) na wamiliki wa jengo (Agip Tanzania).
- Athari: Zaidi ya wafanyakazi 150 walipoteza kazi ghafla usiku wa tarehe 18 Desemba 1998.
- Uamuzi wa Wanahisa: Waendeshaji waliamua pia kuelekeza nguvu zao kwenye hoteli mpya ya Sheraton Dar es Salaam iliyofunguliwa mwaka 1995.
Kwanini Haifunguliwi Hadi Sasa?
Pamoja na kupita kwa miongo kadhaa, jengo hilo limeendelea kusimama bila kufanya kazi kwa sababu zifuatazo:
- Mivutano ya Umiliki na Wawekezaji: Mwaka 2011, kampuni ya Wellworth Group of Companiesilitangaza kununua hoteli hiyo pamoja na Embassy Hotel kwa lengo la kuzikarabati. Hata hivyo, miradi hiyo ilisuasua kutokana na urasimu wa kisheria na mabadiliko ya mipango ya uwekezaji.
- Migogoro ya Kisheria na Kifedha: Majengo mengi ya zamani ya Posta (ikiwemo Embassy iliyo jirani) yalikumbwa na kesi za madai ya wafanyakazi na migogoro ya umiliki wa hisa za serikali na sekta binafsi, hali iliyofanya mali hizo kubaki "frizoni" kisheria.
- Uchumi wa Matengenezo: Miundombinu ya jengo hilo imechakaa sana baada ya kukaa miaka mingi bila matengenezo. Wawekezaji wengi huona gharama ya kubomoa au kukarabati majengo ya kizamani katikati ya jiji kuwa kubwa mno ikilinganishwa na kujenga mapya.
Wameua Hoteli zimelala pale to date hatujui hatma.