Nafasi ya kazi: Mkoani Dar es salaam

Nafasi ya kazi: Mkoani Dar es salaam

Joined
Jun 2, 2026
Posts
9
Reaction score
5
Ninawasalimu wote, hongereni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa letu zuri sana la Tanzania.

Ninatangaza mtafutaji wa kazi ambaye ni mimi mwenyewe, ninaishi Gongo la mboto mkoani Dar es salaam Elimu yangu ni kidato cha sita. Kazi ikiwa maeneo ya Chanika, Kisarawe, Pugu, Gongo la mboto, Mbagala Temeke itapendeza.

Ninaweza kufanya kazi zifuatazo kuanzia saa 11:00 jioni, muda wa usiku mpaka saa 12:00 asubuhi:

1. Kazi za kutumia kompyuta,
2. Kuhudumia wateja 'supermarket',
3. Ulinzi,
4. Kuuza duka,
5. Kufundisha wanafunzi wa shule ya msingi (English medium schools) darasa la tano mpaka darasa la saba, kidato cha kwanza mpaka cha nne masomo ya sayansi na hisabati
6. Kuhudumia wateja stationery n.k

Ninajisomesha chuo, ninahitaji sana kupata kazi ili posho nitakayopata kama malipo yangu ya kazi inisaidie kulipa ada chuoni, kununua chakula, kulipa kodi n.k.

Hii itaniwezesha kuendelea na masomo asubuhi, mchana mpaka jioni, ili nikijaaliwa kuhitimu nipate fani ya kutumia kupambana na maisha mtaani.

Ninaahidi kufanya kazi kwa unyenyekevu mkubwa, utiifu na uaminifu maana nitakuwa ninategemea sana hiyo kazi inisaidie na sitaichezea kamwe ! Ninaombeni kusaidiwa katika hili suala ndugu. Namba yangu ni 0696343634, asanteni na karibuni.​
 
Ila uandishi wa kichwa cha mada na mada yenyewe 🙌
 
Back
Top Bottom