Hongereni Chadema

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kama ni kupewa nyota tano basi Chadema wapo katika mstari wa kuweza kutunukiwa Nyota hizo tano na kuwa 5Star political party katika Taifa hili la Tanzania.

Hii ni kutokana na kufanikiwa kwa kiasi fulani kuweza kuikeep bize CCM na serikali yake na kuwafanya watawala tulionao kubabaika na kutojua pa kushika ,silaha hii ya Chadema ndiyo silaha haswa inayotakiwa kutumika katika kuisambaratisha CCM na utawala wake.

Katika muhula huu wa lala salama kwa CCM na wadhamini wake (aka mafisadi) ,tokea ulipomaliza uchaguzi mkuu Chadema awamefanikiwa kumkurupusha Kikwete na Chama chake kutokana na matokeo ya uchaguzi hili halijamalizika tayari wamekurupusha kwenye mambo ya Umeya wakati mapambano yakiendelea kwenye umeya ,Chadema wamepalilia na kulimia kwenye mambo ya kudai Katiba Mpya ,halikadhalika kwenye mdundo wa malipo ya Dowans huko nako kunafuka moshi,nategemea kuitishwa maandamano ya nchi nzima kupinga hatua iliyochukuliwa ya kulipa deni hewa la dowans.

Chadema ni lazima waendelee na safari hii isiwe mwendo mdundo maana jamaa watakuja kupinda kushoto ,iwawache Chadema wakiongoza njia tu,kumbe watu weshakula kona.

Mbinu hii ya kuikeep busy CCM na serikali yake ndio itakayowachanganya CCM na wadhamini wao wachanganyikiwe kila mmoja awe hamjui mwenziwe na kila mmoja ajione mzigo wake ni mzito hakuna nafasi ya kusaidiana.maombi ya maandamano na mikutano yaenee nchi nzima kusiwe na kulala tena.
 
mkuu unanipa mashaka kwa haya mapya niyasomayo toka kwako?

tokea lini ukawa mwema kwa chadema? au CUF wamekufukuza unataka kudandia mkuki kwa mbele
 
Mwiba umenifurahisha, Kama leo umeamua kusema haya kutoka moyoni, basi Tanzania itabadilika. Karibu kwenye mwanga wa asili kuelekea ukombozi wa Tanganyika
 
Dah Mwiba unataka kutuingiza nyavuni na utuvue kiulaini?.Naona hujapata thanks siku nyingi ukaamua kubadili upepo,na watu wameendelea kukuchunia tu. :teeth:
 
in order to overcome we must dare and keep daring forever,,,,,
if you can walk,,walk,,,if you can run run,,,until it is understood.........................
 
mkuu unanipa mashaka kwa haya mapya niyasomayo toka kwako?

tokea lini ukawa mwema kwa chadema? au CUF wamekufukuza unataka kudandia mkuki kwa mbele

Chadema wanastahili hongera kwani jinsi wanavyoiendesha CCM na serikali yake yaani ,kwa habari za yule kigogo anasema kuwa Chadema wanawaendesha mchakamchaka CCM ,na ni mambu yapo wazi kabisa hakutaki utoe mijicho kuona kinachoendelea,kama utapeleleza wakuu wa CCM wote kimya hakuna cha kingunge wala katani ,wote ukiwaona utafikiri wanatafuta vitu sokoni ,Chadema wanatumia mbinu za kivita kabisa ikiwa unaelewa mambo ya kivita,tulipokwenda Uganda kupigana ,Jeshi la Amini lilikuwa likirusha mizinga na kwa kweli walikuwa wakituona na wakitupata ,sasa mkuu wetu akasema ni lazima tujibu mapigo tokea pande tofauti na kwa wakati mmoja ,hivyo tulijigawa au tuligawanywa katika makundi matano na kila kundi likatokomea upande wake na kuanzisha mapigo kwenye saa 9 za usiku ,tulipiga tokea pande tano na kumchanganya Amini na majeshi yake,siku iliyofuata tulianza kupata nafuu na mashambulizi ya kushambuliwa yalipungua tukiamini kuwa adui yetu hajui apige upande gani na tokea hapo tuliendeleza mapambano na kuiteka Uganda nzima.

Na kwa ninavyoona Chadema wameamua kushambulia sehemu zote kwa wakati mmoja.
 
Dah Mwiba unataka kutuingiza nyavuni na utuvue kiulaini?.Naona hujapata thanks siku nyingi ukaamua kubadili upepo,na watu wameendelea kukuchunia tu. :teeth:

ALoo nipo hapa tokea na kabla ya 2007 na ni mwanachama nambari kumi kujiunga na Jambo forum aka Jamii ( ila nilifukuzwa na kurudi tena 2007) ndio nimetulia. Sasa kama unakuja na kuvizia nani kapewa thanks utapata tabu na shida.Nakupa pole sana.
 
Ok bana,nimeshangaa kuwa leo uko upande wa CHADEMA lol! na nilivyokufahamu kwenye post zako nyingi umekuwa Mwiba mchungu kwa wana CHADEMA...Ha haha ha ahaha punguza jazba
 
ALoo nipo hapa tokea na kabla ya 2007 na ni mwanachama nambari kumi kujiunga na Jambo forum aka Jamii ( ila nilifukuzwa na kurudi tena 2007) ndio nimetulia. Sasa kama unakuja na kuvizia nani kapewa thanks utapata tabu na shida.Nakupa pole sana.
tulisha zoea kukuona upande ule wa mafisadi lkn kwa mshituko wa wengi uko upande wa pili....
 
Kama ni kupewa nyota tano basi Chadema wapo katika mstari wa kuweza kutunukiwa Nyota hizo tano na kuwa 5Star political party katika Taifa hili la Tanzania.

Hii ni kutokana na kufanikiwa kwa kiasi fulani kuweza kuikeep bize CCM na serikali yake na kuwafanya watawala tulionao kubabaika na kutojua pa kushika ,silaha hii ya Chadema ndiyo silaha haswa inayotakiwa kutumika katika kuisambaratisha CCM na utawala wake.

Katika muhula huu wa lala salama kwa CCM na wadhamini wake (aka mafisadi) ,tokea ulipomaliza uchaguzi mkuu Chadema awamefanikiwa kumkurupusha Kikwete na Chama chake kutokana na matokeo ya uchaguzi hili halijamalizika tayari wamekurupusha kwenye mambo ya Umeya wakati mapambano yakiendelea kwenye umeya ,Chadema wamepalilia na kulimia kwenye mambo ya kudai Katiba Mpya ,halikadhalika kwenye mdundo wa malipo ya Dowans huko nako kunafuka moshi,nategemea kuitishwa maandamano ya nchi nzima kupinga hatua iliyochukuliwa ya kulipa deni hewa la dowans.

Chadema ni lazima waendelee na safari hii isiwe mwendo mdundo maana jamaa watakuja kupinda kushoto ,iwawache Chadema wakiongoza njia tu,kumbe watu weshakula kona.

Mbinu hii ya kuikeep busy CCM na serikali yake ndio itakayowachanganya CCM na wadhamini wao wachanganyikiwe kila mmoja awe hamjui mwenziwe na kila mmoja ajione mzigo wake ni mzito hakuna nafasi ya kusaidiana.maombi ya maandamano na mikutano yaenee nchi nzima kusiwe na kulala tena.

Mzima weye? Maana siamini kama hichi ninachokisoma kimeandikwa na wewe au labda kuna mtu kishacheza na password yako. Pia inawezekana umezisoma alama za nyakati na kuamua kubadilika. Kama umzima na password yako iko salama salmini basi nategemea mabandiko yako katika jukwaa hili la siasa yatakuwa yanafanana na hili la leo.
 
mkuu unanipa mashaka kwa haya mapya niyasomayo toka kwako?

tokea lini ukawa mwema kwa chadema? au CUF wamekufukuza unataka kudandia mkuki kwa mbele

Anajua pahala pa kuwashika wapenzi wa chadema ili watulie.

Mwiba,
Hongera kwa kuuona mwanga.

Hongera sana mwiba kwa kutambua Nuru ya kweli iko upande gani.

Lini umezinduka ?

tulisha zoea kukuona upande ule wa mafisadi lkn kwa mshituko wa wengi uko upande wa pili....
 
Kwa kuandika haya, sidhani MWIBA kasema kuwa kahamia Chadema.

Labda yeye na kundi lake wamegundua kuwa NDOA na CCM ni kuzidi kuizamisha Zenji itawaliwe.

Sijui ana malengo gani na labda ni kama alivyosema kuwa "Chadema watafikri kuwa Watz wako nao na kumbe wengine wakifika njiani (sijui na yeye yumo?) watasepa na Chadema watajikuta wako peke yao...."

Hata hivyo, inabidi Mwiba tumpe ASANTE maana hatimaye Dr. Slaa akisoma, ataburudika walau kidogo.
 
Sikonge,unaweza kumpa ASANTE leo halafu kesho akawa mwiba mchungu sana kwetu. Muangalie Maggid Mjengwa nae alivyobadilika.Mimi nahisi hawa watu walinunuliwa na chama ili kuidhoofisha CDM na sasa mkataba umekwisha wanaanza kuwa waTZ wa kawaida
 
Unajua unacho kinena?

Kwa nini isiwe CDM mmenunuliwa na mafisadi kudhoofisha CUF au NCCR
 
ALoo nipo hapa tokea na kabla ya 2007 na ni mwanachama nambari kumi kujiunga na Jambo forum aka Jamii ( ila nilifukuzwa na kurudi tena 2007) ndio nimetulia. Sasa kama unakuja na kuvizia nani kapewa thanks utapata tabu na shida.Nakupa pole sana.

ulifukuzwa eeh? sasa umerudi kwa staili mpya siyo?. Km Umerudi kundini unakaribishwa na utulie kweli kutafakari mustakabali wa Taifa letu.
 
Unajua unacho kinena?

Kwa nini isiwe CDM mmenunuliwa na mafisadi kudhoofisha CUF au NCCR

Aisee CDM hawanunuliki na wao ndio wanaowatia tumbo joto mafisadi. CUF walijidhoofisha wenyewe kwa kung'ang'ania kupeleka nguvu zote Zanzibar na kusahau bara pia pale walipokubali kuolewa na CCM kwa ndoa ya mkeka.NCCR walinunuliwa na mafisadi wamtoe Mrema ili kuua upinzani.
 
ALoo nipo hapa tokea na kabla ya 2007 na ni mwanachama nambari kumi kujiunga na Jambo forum aka Jamii ( ila nilifukuzwa na kurudi tena 2007) ndio nimetulia. Sasa kama unakuja na kuvizia nani kapewa thanks utapata tabu na shida.Nakupa pole sana.

Naona umepata thanks za kutosha.Endelea hivi hivi na usiwe upande wa mafisadi
 
Back
Top Bottom