Hongera Waziri Simbachawene, lakini kuwa makini na Jeshi la Polisi

Nzelu za bwino

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
376
450
Nakupongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Kumbuka Wizara yako ndio Wizara inyohusika na kusimamia haki za msingi za maisha ya Watanzania ya kila siku. Pia ndio Wizara inayowajibika kusimamia usalama wa Wananchi na Mali zao.

Hivi karibuni kumekuwa na shutuma nyingi dhidi ya Wizara yako kupitia Jeshi la Polisi kuhusika na mambo mbalimbali ikiwemo kukamata watu kiholela, kubambikia watu kesi, kutumika kisiasa kwa kuvuruga mkutano na shughuli za vyama vya upinzani nk.

Ni matumaini ya Watanzania walio wengi kwamba haya mambo yamefika ukomo baada ya Wizara kupata Waziri mwanasheria anayeijua sheria vizuri na umuhimu wake. Hakika Wizara imepata mtu sahihi na kwa wakati.

Naomba kuwasilisha.
 
Bodaboda nasikia wameshaanza kifunguliwa mziki
Kuna uzi humu ndani unaeleza hayo
 
Sana sana, hasa yale ya kuwakamata raia na bila kuwapa haki zao stahili, kuwekwa rumande kwa masaa au siku nyingi bila kupewa haki zao, rushwa, unyanyasaji wa raia, uonevu...
Kazi anayo...
 
Back
Top Bottom