Hongera Serikali yetu, kuwatosa Acacia kwa kutowatambua huu ndio uanaume!. acacia kula jeuri yake, faces hostile take over, soon itakuwa kwishney!.

Nimeona katika release yao kuwa offer ya barrick in ndogo kuliko tasimi ya wahasibu na auditors wao ni $1.3 billion na siyo 857 iliyoleta gawio LA acacia $300. Wakigoma kwa hilo kuuza share zao itakuwaje?
Mkuu Ruby, hii ni hostile take over, hivyo kwanza mauziano ni kitu kinachoitwa share to share, na not necessarily money changingi hands, bali wametoa offer kwa shares zote za Acacia ambazo hazimilikiwi na Barrick kuhamishiwa Barrick kwa
The consideration to own new common shares in Barrick, kwa kila share ya Acacia kununuliwa na Barrick kwa 0.153 hivyo wanahisa wote wa Acacia wanageuka wanahisa wa Barrick, this is an offer no one can resist, ni kama ulikuwa unamiliki Toyota Starlet, halafu jamaa akakupa Range Rover Sport mbadilishane, thamani ya Acacia mbele ya Barrick ni kama mti wa mbuyu na mbegu ya mchicha. No one can say no.
P.​
 
Safi Sana mkuu, angalao wewe umeona hii kitu kwa jicho la pili.

Tunakoelekea mbeleni resources za Dunia umilikaji wake unafanyiwa overhaul
Mfano kwenye Diamond, huwezi fanya biashara ya Diamond ukamruka De beers.

Hii sasa inakuja kwenye Gold, tunakoelekea transactions zake itakuwa Kama Diamond sababu wazalishaji wakubwa wa Gold kama Randgold na Newmont tayari washameshajiunga na Sasa Ni kampuni moja ya Barrick Group.

Tukirudi kwenye oil & Gas huku nako Ni yale yale yanaendelea. Baada ya Anadarko kupata reserve kubwa pale Mozambique kaibuka Mmarekani mwingine Occidental Oil, keshafanya takeover kwa Anadarko baada ya kumpiku Chevron.
Major kubwa ambayo inakuja kutikisa Dunia itakuwa kati ya Equinox na Chevron au Equinox na Occidental Oil. Aramco naye anajitahidi kujitanua sababu anaona future yake Ni ndogo kwenye Oil,kule Angola kuna Vita kali sana ya take over inaendelea chini kwa chini.

Kwenye Iron and other Industrial Minerals wamemuachia Rio Tinto na BHP. Soon tutashuhudia super merger kati ya BHP, Rio Tinto na Vale. Ikikamilika hii Basi natural resources zote zitakuwa chini ya beberu mkuu Mmarekani.

Tunakokwenda kuna giza Sana kuliko tunapotoka.
Mamafia wanaendelea na umafia wao, TISS mnatakiwa muonyeshe umahili wenu hapo.
Barrick na Acacia katika hili wanajua wanachofanya, business complication anazoface ACACIA Tanzania huku Barrick Gold PLC akiwa trusted kama mwenye mbwa kwenye viunga vya Dar es salaam.. Anachofanya Barrick hapa nikumtoa dogo mbele na kumrudisha nyuma gizani maisha yakiendelea kama kawa kule Canada.. ACACIA = BARRICK, TISS kuwa makini hapo.. ACACIA ilianzishwa kwa ajili ya wizi Tanzania lakini ACACIA ni BARRICK na BARRICK ni ACACIA.. Wapi ACACIA anamiliki Migodi mingine zaidi ya Tanzania? mbona pale Lumwana - Zambia bado anaitwa Barrick miaka nenda rudi?, kwanini placer dome, east africa gold mine, Pangea, leo Acacia mbona huko kote mpaka leo BARRICK alikuwa nyuma nyuma??

USHAURI:: Serikali msikubali BARRICK anunue hizo hisa, baadala yake tushikilie kwenye deni letu la ACACIA kifupi tunamdai ACACIA hawezi kulipa aondoke na hizo 40% shares ziwe za Tanzania.. Tukomae kwenye umiliki wa 40% za hisa za ACACIA halafu ndio tukae chini kwenye yale makubaliano lakini iwe kwenye ile 60% maana tayari 40% ni zetu baada yakumtaifisha mwizi ACACIA na kwenye deni letu MWISHO WA SIKU TUNATAKIWA KUWA MAJORITY SHARE HOLDER WITH AROUND 60-70% shares..

Nitarudi baadaye..
 
Mkuu Ruby, hii ni hostile take over, hivyo kwanza mauziano ni kitu kinachoitwa share to share, na not necessarily money changingi hands, bali wametoa offer kwa shares zote za Acacia ambazo hazimilikiwi na Barrick kuhamishiwa Barrick kwa
The consideration to own new common shares in Barrick, kwa kila share ya Acacia kununuliwa na Barrick kwa 0.153 hivyo wanahisa wote wa Acacia wanageuka wanahisa wa Barrick, this is an offer no one can resist, ni kama ulikuwa unamiliki Toyota Starlet, halafu jamaa akakupa Range Rover Sport mbadilishane, thamani ya Acacia mbele ya Barrick ni kama mti wa mbuyu na mbegu ya mchicha. No one can say no.
P.​
Hahahahhaaaha.
When an Asset became a Liability.
Baba nimefungua kampuni, nikaona nimpe mwanangu ila nikiwa bado nimemuweka kwapani kwa kisingizio cha mwanahisa mwenye hisa nyingi. Baadaye dogo anazingua , natumia ukubwa wangu kumtuliza dogo atulie nyumbani. Halafu me baba ake nasonga mbele kivingine na ile ile kampuni kwa muundo wa awali.

Hapa panahitaji umakini Sana aiseee. Tuvumilie muda ndo utaaamua.
 
Wanabodi,

Kati ya vifo vyote vya biashara, kifo kibaya kabisa ninaitwa "hostile take over", ambapo biashara inakabwa koo kwa kunyongwa hadi kufa bila kutaka kwa kuuzwa juu kwa juu. Kifo hiki ndicho kinakwenda kuikuta kampuni ya Acacia, Hongera sana kwa Serikali Yetu, Kuwatosa rasmi Acacia Kwa kuandika barua rasmi za kutowatambua, kutakakopelekea kifo rasmi cha Acacia, Huu Ndio Uanaume!. Haiwezekani madini yetu, Tanzania inazungumza na Baba Mtu, Barrick, halafu wewe mtoto tuu, Acacia kila siku ni kuleta nyodo. Sasa Acacia Itakula Jeuri Yake, it Faces a Hostile Take Over from Barrick, and Soon Itakuwa Kwishney!. A thing of the past, a history!.

Tangu kutokea mgogoro wa makinikia ya Acacia, kwanza tulipongeza hatua ya rais Magufuli kuuzuia mchanga wa makinikia Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...

Baada ya kuzuiliwa kwa mchanga, Rais Magufuli akaunda Tume zake mbili, zikamletea ripoti zake mbili, baada ya kushuhudia live presentation ya tume ya pili, nilitoa opinion yangu Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni ...

Ripoti za tume hizo zikaosnyesha kuwa siku zote, tumekuwa tukiibiwa, TRA wakaja na bili ya ajabu ya deni ya Dola Bilioni 190 US $ sawa na TZS 424 trilioni kwa fedha za madafu, kuhusu deni hili, sisi wachumi wa Sultani Mangungo wa Msovero ya JF, tukamweleza rais wetu kuwa anadanganywa na kumsihi asidanganyike.
Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye ...

Baada ya deni hilo kuwekwa wazi, Acacia wakatugomea kuwa hawadaiwi na hawalipi. Baba wa Acacia, Barrick akaingilia kati kwa Mwenyekiti wao kuja nchini kuonana na rais Magufuli na kukubali kuwa watalipa, hivyo mazungumzo yakaanza.

Maungumzo yakaisha rasmi na tukatangaziwa makubaliano, kikiwemo sisi kulipwa dola milioni 300 za kuonyeshea nia njema ya kulipa. Katika makubaliano hayo Barrick alionyesha kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa baada ya kukubali na Acacia.

Acacia kwanza akatoa taarifa kuwa hayatambui makubaliano hayo kwa vile hakushirikishwa, Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto ...lakini siku chache baadae akatoa taarifa ya kukubali kila kitu.
Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa ...

Sisi wahojaji tukaendelea kuhoji sio tuu uwezo wa Acacia kulipa deni letu la dola bilioni 190, bali hata uwezo Acacia kulipa tuu hata hizo dola milioni 300 za goodwill. Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia ...
Pia tukahoji, kama Acacia ndio determinant wa kutulipa, kwa nini hakushirikishwa kwenye mazungumzo?. Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye ...

Mapendekezo ya makubaliano ya mwisho yalitolewa na Barrick kuwa sasa Acacia watalipa ile dola milioni 300 tuu na deni lote la dola bilioni 190, tukasamehe, Acacia akaibuka na kuikana Barick kuwa wao hawajui chochote kwa vile hawakushirikishwa, hivyo wanasubiri taarifa rami ya Barrick ndipo watangaze uamuzi. Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na ...

Acacia wakaibuka kuwa bado hawajapewa makubaliano. Kwanini Mapendekezo ya Makubaliano yetu na Barrick bado hayajafika ...

Siku ya Jumapili, tarehe 19th May 2019, serikali yetu ikafunga kazi!, licha ya kuwa ni Jumapili, sio siku ya kazi, huwezi kuandika barua za kiserikali siku ya Jumapili, lakini kwa serikali ya Magufuli ya Hapa Kazi Tuu, hakuna cha Jumapili wala sikukuu, ni kazi tuu, ikitokea kazi ya urgency kama hizi barua za kutoitambua Acacia, serikali yetu inaingia kazini, Jumapili ya juzi, serikali imeingia kazini, imeziandikia barua migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, kuwaeleza kuwa hawaitambui Acacia, hali iliyoilazimu Barrick kutoa offer ya hostile take over kwa Acacia kuzinunua hisa zote za Acacia, ambazo hazimilikiwa na Barrick, itake isitake, hivyo kuimeza rasmi Acacia kuwa sehemu ya Barrick. na wana hisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa wa Barrick. Kwa Tanzania Hostile take over iliwahi kutokea kwa kiwanda cha Bia cha Kibo kule Moshi. Tofauti ya hostile take over ile na hii, migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, itaendelea kuwepo, hakuna atakayepoteza kazi na uzalishaji unaendelea, kitakachokufa ni Avavia tuu, nafasi yake inavhukuliwa na Barrick, everything else stays the same.

Kitendo hiki kilichofanywa na serikali yetu kui disown Acacia ni kitendo cha kishujaa sana na huu ndio uanamme. Haiwezekani madini yetu, mtu anayetambulika nchini kama ni mmiliki ni Barrick kupitia Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, huyu Acacia ni mtu wa kuja tuu, hatambuliwi halafu analeta nyodo kibao.
Barua hizo za serikali, zimepelekea leo Acacia na Barrick kutoa press release hizi
.

Japo Acacia ni mtoto wa Barrick, huyu ni mwana mkaidi, kama kawaida ya mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi, hivyo siku ya Iddi ya Acacia imewadia. Funzo tunalolipata hapa ni siku zote
kiburi sii maungwana. Acacia alikuwa jeuri, sasa anakula jeuri yake, soon Acacia itabaki kuwa ni historia, kwishney.

Jumatano Njema.
Paskali
Pascal Mayalla kwa kuweka hilo tangazo la Barrick umevunja sheria. Rudi kulisoma upya
 
Acacia wakaibuka kuwa bado hawajapewa makubaliano. Kwanini Mapendekezo ya Makubaliano yetu na Barrick bado hayajafika ...

Siku ya Jumapili, tarehe 19th May 2019, serikali yetu ikafunga kazi!, licha ya kuwa ni Jumapili, sio siku ya kazi, huwezi kuandika barua za kiserikali siku ya Jumapili, lakini kwa serikali ya Magufuli ya Hapa Kazi Tuu, hakuna cha Jumapili wala sikukuu, ni kazi tuu, ikitokea kazi ya urgency kama hizi barua za kutoitambua Acacia, serikali yetu inaingia kazini, Jumapili ya juzi, serikali imeingia kazini, imeziandikia barua migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, kuwaeleza kuwa hawaitambui Acacia, hali iliyoilazimu Barrick kutoa offer ya hostile take over kwa Acacia kuzinunua hisa zote za Acacia, ambazo hazimilikiwa na Barrick, itake isitake, hivyo kuimeza rasmi Acacia kuwa sehemu ya Barrick. na wana hisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa wa Barrick. Kwa Tanzania Hostile take over iliwahi kutokea kwa kiwanda cha Bia cha Kibo kule Moshi. Tofauti ya hostile take over ile na hii, migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, itaendelea kuwepo, hakuna atakayepoteza kazi na uzalishaji unaendelea, kitakachokufa ni Avavia tuu, nafasi yake inavhukuliwa na Barrick, everything else stays the same.

Je bado goodwill ipo ?
Je tutapata kodi kwenye hayo Mauzo??

Au kwa vile hatuwajui Accacia hayo mauzo yatakuwa feki hivyo hayana kodi?.
CC Zitto
 
Mkuu sikupingi maoni yako lakini mimi nahisi kuna siri kubwa nyuma ya pazia na hapa tunajaribu kubet tu
Mkuu Uzalendo, hapa ndipo ilipo tofauti ya Wazungu na sisi Waafrika, wenzetu wako very open na transparent, kila anachofanya Barrick kuihusu Acacia, anatoa press release, na ikitokea tuu press release ya Barrick, press release ya Acacia inafuatia.

Tofauti ya pili ni independence ya mtoto, Acacia ni mtoto wa Barrick, kiaAfrika baba akiishasema kitu, mtoto unanyamaza, wazungu Baba anasema kitu kwa press release, mtoto anabisha kwa counter release, niliwahi kusema Acacia hana adabu kabisa.

Haya majibizano ya baba na mwana kwenye press release ndio yanapelekea watu kudhani wanajuana, ila ni kweli pia kuna mambo ya chini kwa chini yalitokea hatukuambia, ila kwa kinachoendelea sasa, kinaashiria Acacia waliyagomea mapendekezo ya serikali na Baarick, kwa vile hawakushirikishwa, hivyo serikali yetu ndio ikawa ya kwanza kuiandikia barua ile migodi mitatu ya Acacia kuwa sasa serikali yetu haiitambui Acacia, Barrick anakuwa hana jinsi bali kuitake over Acacia kwa lazima. Kwa vile Acacia ni listed company kwenye London Stock Exchange na Dar es Salaam Stock Exchange, DSE, lazima utoe offer na wanahisa wanaokubali wanauza hisa zao zote za Acacia, na hapo hapo kununua hisa mpya za Barrick, kukitokea watu wakagoma, then wanauza hisa zao na kupewa Fedha yao wana sepa.

P.
 
Mkuu, lao moja hawa. msimamo wa Acacia ndiyo haswa msimamo wa Barrick.
wameshagundua wakolomije wanachopenda kukisikia na ndicho Barrick wanachokitamka publicly lakini subplots zao behind the curtains si za kitoto.
kama ni kuliwa tushaliwa - "thanks" to my beloved CCM!
Mkuu M-mbabe, possibility ya kuchezewa game ipo na tangu mwanzo nimeizungumza hapa
Barrick ndio the majority shareholder wa Acacia, na maamuzi ya makampuni yanafanywa kwenye boardroom, Baarick ndio controller wa boardroom ya Acacia, sasa hawa Acacia wanawezaje kupinga msimamo wa Barrick?.
Kanisome hapa
P
 
Swali langu ni kuwa ikiwa kama Serikali ilisaini Mkataba na Barrick wa umiliki wa hio migodi Acacia aliingiaje katika Uendeshaji wake?
Na kama point ni kwamba eti na Pacha wa Barrick sasa alitoa wapi nguvu ya kukataa madai yaliyoelekezwa kwa Mkubwa wake ambaye ni Barrick?
Mimi nahisi huenda kuna mambo flani hayakukaa sawa ki mkataba wkt wanasaini na ndio mana Acacia anapata nguvu ya kugomea maamuzi ya serikali
Tz tumekuwa mabingwa wa kukiuka sheria za mikataba na mwisho wa siku tunaishia kuburuzwa mahakama za juu na kulipa mabilioni ya faini.

Ufafanuzi wa hili jambo tunaomba wataalam wa sheria watusaidie kulielewa kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
 
Mkuu nimekusoma umeeleweka hizi taarifa si njema ufipani
Watanzania wanaojitambua, siku nyingi waliisha wapuuza ufipa, hawana lolote katika kupigania maslahi ya taifa hata ufipa wenyewe wanajijua, ndio maana wale wa ufipa wanaojitambua, wameisha jitimkia zao kwenda maeneo kunakoeleweka, hata mimi almanusura nimeamue kuingia kwenye siasa za 2020, ningeingia, huyu mbunge wa ufipa dada yangu wa mitaa yangu, ningemsukuma pembeni kama kumsukuma mlevi, ili nilivyo dhaifu kwa viumbe hawa, huruma ikaniingia, hivyo siingii kwenye siasa, ila 2020. ufipa karibu wote watapumzishwa akiwemo Mwenyekiti, yule Dogo jirani atamtoa kiulaini kama kumsukuma mlevi.
2020 tunarudisha Tanzania ya Nyerere, Tanzania ya chama kimoja.

P.
 
Mamafia wanaendelea na umafia wao, TISS mnatakiwa muonyeshe umahili wenu hapo.
Barrick na Acacia katika hili wanajua wanachofanya, business complication anazoface ACACIA Tanzania huku Barrick Gold PLC akiwa trusted kama mwenye mbwa kwenye viunga vya Dar es salaam.. Anachofanya Barrick hapa nikumtoa dogo mbele na kumrudisha nyuma gizani maisha yakiendelea kama kawa kule Canada.. ACACIA = BARRICK, TISS kuwa makini hapo.. ACACIA ilianzishwa kwa ajili ya wizi Tanzania lakini ACACIA ni BARRICK na BARRICK ni ACACIA.. Wapi ACACIA anamiliki Migodi mingine zaidi ya Tanzania? mbona pale Lumwana - Zambia bado anaitwa Barrick miaka nenda rudi?, kwanini placer dome, east africa gold mine, Pangea, leo Acacia mbona huko kote mpaka leo BARRICK alikuwa nyuma nyuma??

USHAURI:: Serikali msikubali BARRICK anunue hizo hisa, baadala yake tushikilie kwenye deni letu la ACACIA kifupi tunamdai ACACIA hawezi kulipa aondoke na hizo 40% shares ziwe za Tanzania.. Tukomae kwenye umiliki wa 40% za hisa za ACACIA halafu ndio tukae chini kwenye yale makubaliano lakini iwe kwenye ile 60% maana tayari 40% ni zetu baada yakumtaifisha mwizi ACACIA na kwenye deni letu MWISHO WA SIKU TUNATAKIWA KUWA MAJORITY SHARE HOLDER WITH AROUND 60-70% shares..

Nitarudi baadaye..

Umemaliza kila kitu.

Barrick anamuokoa Acacia kupitia Dirishani maana mambo si mambo na lengo linaonekana kutimia.
 
Swali langu ni kuwa ikiwa kama Serikali ilisaini Mkataba na Barrick wa umiliki wa hio migodi Acacia aliingiaje katika Uendeshaji wake?
Na kama point ni kwamba eti na Pacha wa Barrick sasa alitoa wapi nguvu ya kukataa madai yaliyoelekezwa kwa Mkubwa wake ambaye ni Barrick?
Mimi nahisi huenda kuna mambo flani hayakukaa sawa ki mkataba wkt wanasaini na ndio mana Acacia anapata nguvu ya kugomea maamuzi ya serikali
Tz tumekuwa mabingwa wa kukiuka sheria za mikataba na mwisho wa siku tunaishia kuburuzwa mahakama za juu na kulipa mabilioni ya faini.

Ufafanuzi wa hili jambo tunaomba wataalam wa sheria watusaidie kulielewa kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Mkuu Hardbody, katika kufanya biashara, huwa kuna risks za kibiashara ikiwemo biashara kuanguka au kupata hasara na hata kufilisika, hivyo kujikinga na risk za kibiashara, kuna kitu kinafanywa kinachoitwa diversification kwa ku divisivesfy ili ku mitigate the risks, ili biashara fulani ikifilisika, usiathiri biashara nyingine, nakutolea mfano wa Mzee Mengi, biashara zake zote ziko chini ya mwamvuli wa IPP, chini ya mwamvuli huo, kuna IPP Media inayohusika na media, kuna viwanda, kuna makampuni kibao.
Chini ya IPP Media, kuna ITV/Redio One, kuna The Guardian Ltd, kuna EATV, kuna Capital TV
Chini ya ITV kuna Radio One, chini ya EATV kuna EARadio, chini ya Capital TV kuna Capital Radio, Chini ya The Guardian LTD, kuna magazeti ambayo kila moja linajitegemea. Vyote hivi vikibaki chini ya mwamvuli mmoja, chochote kikila hasara, hasara hiyo inasambaa kote, kimoja kikifilisika, vingine vyote lazima viathirike. Uki diversify, kila kimoja kinajitegemea, kikifa kinakufa chenyewe tuu. Mfano saa hizi Mzee Mengi hayupo, ITV is doing fine and will survive, The Guardian ilikuwa inapumulia mashine Mzee mwenyewe anainusuru, sasa hayupo, ikitokea ikapomulia mashine, there will be no rescue, ama wauze au wafilisike.

Barrick ndio mmiliki ya migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, sasa ili kujinginga na risk kwa migodi hii kufilisika na kuiumiza Barrick, wakaiundia kampuni Tanzu iliyoitwa African Barrick Gold, ABG, ili kumanage migodi yake ya Africa, ndipo ABG ikajibadili jina kujiita Acacia as an independent entity ambayo imesajiliwa soko la hisa la London na DSE. Ingebaki Barrick, Acacia ikifilisika ni Barrick imefilisika, lakini ikiwa ikiwa independent entity Acacia ikifilisika ni Acacia tuu na sio Barrick, na hata baada ya hii offer ya kuinunua Acacia ikipita, hapo hapo wataunda kampuni tanzu nyingine this time na serikali ya Tanzania tutapewa shares za bure za 16% na tutakaa kwenye bodi ya kampuni mpya na tutaingia kwenye menejment team ya hiyo kampuni mpya.
P
 
Kampuni inapokuwa public/private limited company kisheria wenye mali sio sehemu ya kampuni (in terms of liability) wala awahusiki na uendeshwaji wa kila siku, wao wanapokea gawio tu.

Kwa ivyo kuna utaratibu kabla ya kusajiliwa lazima upeleke document mbili moja wapo ni 'article of association' hii inatoa maelezo jinsi kampuni itakavyoendeshwa kila siku, namna mchakato wa kupata management utakavyokuwa na nguvu za management katika maamuzi.

Sasa inategemea article inasemaje, Barrick anaweza kuja kuongea na serikari kwa sababu yeye ndio ana maslahi mapana kama serikari ikiamua kumsikiliza lakini hana maamuzi ya kuamuru management ya Accacia ifanye nini kutokana na mamlaka waliyopewa na article of association. Ndio maana management ya Accacia inaweza dai aija shirikishwa kwenye negotiations pengine hayo mamlaka wamekabidhiwa wao ya kuamua strategic directions na sio shareholders.

As a majority shareholder Barrick na wao wanaweza tumia mbinu zingine kubadili management moja wapo kisheria kunapokuwa na mgogoro na management maamuzi ya wengi ushinda iwapo mmoja tu ana 51% hiyo inaitwa control stake na Barrick wana 65% with that there are lot of things they can do including forcing a takeover wao ndio wenye kuamua as a majority shareholders kama kampuni iuzwe.
Maelezo yako kisheria naona yamekaa vizuri lakini in practice kwa Barrick kuwa na hiyo control stake ya 65% ina maana wana influence kubwa ndani ya ACACIA na vigumu kuamini kwamba kabla ya tatizo hili kuzuka hawakuwa sambamba na pamoja na Acacia. Walijua kilichokua kinaendelea na walichokuwa wanavuna kupitia Acacia. Niaminivyo ni kuwa wamechukua a strategic decision kuhakikisha hawapotezi bali wanaendelea kuvuna Tanzania na kupotezea lile dai la $1.9B.
 
Back
Top Bottom