All TRUTH
JF-Expert Member
- Nov 20, 2011
- 5,453
- 2,564
Sawa nimekuelewa Chief
Endelea kuwa MKWELI DAIMA
Endelea kuwa MKWELI DAIMA
Mkuu All Truth, ni kweli hivyo ndivyo mimi nilivyo, na kama jina lako lilivyo all truth, mimi ni msema kweli daima, na ukiwa mkweli sana, unaweza kuonekana an enemy of the people.
Mimi ni mkweli na wakweli wenzangu kama mimi, wananielewa.
Serikali ikifanya mazuri, tunaipongeza, ikifanya mabaya tunaikosoa. Kuna watu humu kazi yao ni kukosoa tuu, hata serikali ifanya jema vipi, wao watalikosoa na kulipondea. Ukiwa ni mtu mkweli daima siku zote utausema ukweli, haiwezekani mtu uwe unaona mabaya tuu siku zote, mazuri hujawahi kuyaona,
Kwenye hili mimi nimesimama na rais Magufuli alipouzuia mchanga wa dhahabu wa Acacia na nikampongeza na kushauri
Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?
yaani umeng'ata na kupuliza! HUYO ndiyo mzee wa kungata na kupuliza mzee paskali! Ovawww.jamiiforums.com
Alipounda zile tume zake mbili na matokeo yake, nilikosoa kwa sababu rais wetu amedanganywa mchana kweupe.
Mazungumzo yalipoanza pia nilikosoa uendeshaji wa usiri kwenye rasilimali za taifa, usiri wa nini kwenye rasilimali za Taifa, hizi ni mali za Watanzania, rais wa Tanzania ni mdhamini tuu, aliyepewa dhamana lakini mali ni zetu, hivyo hapa nilikosoa.
Matokeo ya mazungumzo yalipotangazwa, pia nilikosoa rais wetu kushangilia goodwill money na kuipangia bajeti, hata neno kishika uchumba, nililitunga mimi, kama nilivyotunga neno dhaifu.
Nyodo za Acacia zilinichefua sana, hivyo kitendo cha serikali yetu kutowatambua ni kitendo cha kishujaa kinachohitaji pongezi za dhati.
Pamoja na pongezi hizi lakini ikitokea tukaumaliza mgogoro huu bila kuuchenjua ule mchanga tukajua kilichomo, kiukweli kabisa sisi tutakuwa ni watu wa ajabu kuwahi kutokea.
P.