Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,578
- 7,281
Nilivyoelewa (mnaweza kunisahihisha) Barrick ndiye majority shareholder katika Acacia hivyo yote yanayotendwa na Acacia Barrick wamo. Sasa kama wanahisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa Barrick na Acacia kumezwa na Barrick kwangu naona ni sawa na kugeuza baadhi ya viti badala ya kuangalia upande huu vina angalia upande ule. Yaani watu kwa ujumla ni wale wale hata kama management itabadilika. ACACIA ISINGEKUWA SEHEMU YA BARRICK SIONI BARRICK WANGEPATA WAPI JEURI YA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SERIKALI YA TANZANIA BILA KUHUSIKA KWA ACACIA. Kuna mchezo hapa umesha chezwa. Kikubwa wanaume hawa wameshusha madai toka $190B hadi $300M potelea mbali kama katika kufanya hivyo ACACIA itapotea kinamna na sasa BARRICK kwa jina lingine lolote lile wataendelea na shughuli zao Tanzania. Sisi tunaendelea kuwalani ACACIA lakini ukweli ni kwamba BARRICK wametunyonga kiaina. Sio mtaalam wa biashara au sheria lakini hii "take-over" nasita kuuita hostile labda uiite FRIENDLY or FAMILY takeover (Baba amabaye ndiye shareholder mkubwa (majority) anammeza mwanawe wakati huo huo yeye mwenyewe akiwa ndani ya mwanawe huyo). Paskali hapa nani anakula jeuri yake? Je hii ndiyo win win situation?hali iliyoilazimu Barrick kutoa offer ya hostile take over kwa Acacia kuzinunua hisa zote za Acacia, ambazo hazimilikiwa na Barrick, itake isitake, hivyo kuimeza rasmi Acacia kuwa sehemu ya Barrick. na wana hisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa wa Barrick.