Wamweru
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 582
- 434
Moja ya kitu kinachonifanya nipende maandiko yako ni ukweli na ufatiliaji wa taarifa wewe mwenyewe ongera kijanaWanabodi,
Kati ya vifo vyote vya biashara, kifo kibaya kabisa ninaitwa "hostile take over", ambapo biashara inakabwa koo kwa kunyongwa hadi kufa bila kutaka kwa kuuzwa juu kwa juu. Kifo hiki ndicho kinakwenda kuikuta kampuni ya Acacia, Hongera sana kwa Serikali Yetu, Kuwatosa rasmi Acacia Kwa kuandika barua rasmi za kutowatambua, kutakakopelekea kifo rasmi cha Acacia, Huu Ndio Uanaume!. Haiwezekani madini yetu, Tanzania inazungumza na Baba Mtu, Barrick, halafu wewe mtoto tuu, Acacia kila siku ni kuleta nyodo. Sasa Acacia Itakula Jeuri Yake, it Faces a Hostile Take Over from Barrick, and Soon Itakuwa Kwishney!. A thing of the past, a history!.
Tangu kutokea mgogoro wa makinikia ya Acacia, kwanza tulipongeza hatua ya rais Magufuli kuuzuia mchanga wa makinikia Kuzuia Mchanga wa Dhahabu, Magufuli Anastahili Pongezi. Tusiishie ...
Baada ya kuzuiliwa kwa mchanga, Rais Magufuli akaunda Tume zake mbili, zikamletea ripoti zake mbili, baada ya kushuhudia live presentation ya tume ya pili, nilitoa opinion yangu Sensationalism kwenye Professional Presentations inakubalika? Ni ...
Ripoti za tume hizo zikaosnyesha kuwa siku zote, tumekuwa tukiibiwa, TRA wakaja na bili ya ajabu ya deni ya Dola Bilioni 190 US $ sawa na TZS 424 trilioni kwa fedha za madafu, kuhusu deni hili, sisi wachumi wa Sultani Mangungo wa Msovero ya JF, tukamweleza rais wetu kuwa anadanganywa na kumsihi asidanganyike.
Maendeleo ya kweli TZ Yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye ...
Baada ya deni hilo kuwekwa wazi, Acacia wakatugomea kuwa hawadaiwi na hawalipi. Baba wa Acacia, Barrick akaingilia kati kwa Mwenyekiti wao kuja nchini kuonana na rais Magufuli na kukubali kuwa watalipa, hivyo mazungumzo yakaanza.
Maungumzo yakaisha rasmi na tukatangaziwa makubaliano, kikiwemo sisi kulipwa dola milioni 300 za kuonyeshea nia njema ya kulipa. Katika makubaliano hayo Barrick alionyesha kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa baada ya kukubali na Acacia.
Acacia kwanza akatoa taarifa kuwa hayatambui makubaliano hayo kwa vile hakushirikishwa, Hivi Hawa Acacia Wana Adabu Kweli?, Baba Akiishasema Kitu, Mtoto ...lakini siku chache baadae akatoa taarifa ya kukubali kila kitu.
Habari Njema Kutoka Acacia: Wakubali Kila Kitu Ikiwemo Kulipa ...
Sisi wahojaji tukaendelea kuhoji sio tuu uwezo wa Acacia kulipa deni letu la dola bilioni 190, bali hata uwezo Acacia kulipa tuu hata hizo dola milioni 300 za goodwill. Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia ...
Pia tukahoji, kama Acacia ndio determinant wa kutulipa, kwa nini hakushirikishwa kwenye mazungumzo?. Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye ...
Mapendekezo ya makubaliano ya mwisho yalitolewa na Barrick kuwa sasa Acacia watalipa ile dola milioni 300 tuu na deni lote la dola bilioni 190, tukasamehe, Acacia akaibuka na kuikana Barick kuwa wao hawajui chochote kwa vile hawakushirikishwa, hivyo wanasubiri taarifa rami ya Barrick ndipo watangaze uamuzi. Acacia Yaikana Barrick Mchana Kweupe!. Yatoa Press Release na ...
Acacia wakaibuka kuwa bado hawajapewa makubaliano. Kwanini Mapendekezo ya Makubaliano yetu na Barrick bado hayajafika ...
Siku ya Jumapili, tarehe 19th May 2019, serikali yetu ikafunga kazi!, licha ya kuwa ni Jumapili, sio siku ya kazi, huwezi kuandika barua za kiserikali siku ya Jumapili, lakini kwa serikali ya Magufuli ya Hapa Kazi Tuu, hakuna cha Jumapili wala sikukuu, ni kazi tuu, ikitokea kazi ya urgency kama hizi barua za kutoitambua Acacia, serikali yetu inaingia kazini, Jumapili ya juzi, serikali imeingia kazini, imeziandikia barua migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, kuwaeleza kuwa hawaitambui Acacia, hali iliyoilazimu Barrick kutoa offer ya hostile take over kwa Acacia kuzinunua hisa zote za Acacia, ambazo hazimilikiwa na Barrick, itake isitake, hivyo kuimeza rasmi Acacia kuwa sehemu ya Barrick. na wana hisa wote wa Acacia wamepewa offer ya kuwa wanahisa wa Barrick. Kwa Tanzania Hostile take over iliwahi kutokea kwa kiwanda cha Bia cha Kibo kule Moshi. Tofauti ya hostile take over ile na hii, migodi ya Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, itaendelea kuwepo, hakuna atakayepoteza kazi na uzalishaji unaendelea, kitakachokufa ni Avavia tuu, nafasi yake inavhukuliwa na Barrick, everything else stays the same.
Kitendo hiki kilichofanywa na serikali yetu kui disown Acacia ni kitendo cha kishujaa sana na huu ndio uanamme. Haiwezekani madini yetu, mtu anayetambulika nchini kama ni mmiliki ni Barrick kupitia Bulyanhulu Gold Mine Limited, North Mara Gold Mine Limited na Pangea Minerals Limited, huyu Acacia ni mtu wa kuja tuu, hatambuliwi halafu analeta nyodo kibao.
Barua hizo za serikali, zimepelekea leo Acacia na Barrick kutoa press release hizi
.Barrick Gold Corporation - Acacia Mining
www.barrick.com
Japo Acacia ni mtoto wa Barrick, huyu ni mwana mkaidi, kama kawaida ya mwana mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi, hivyo siku ya Iddi ya Acacia imewadia. Funzo tunalolipata hapa ni siku zote
kiburi sii maungwana. Acacia alikuwa jeuri, sasa anakula jeuri yake, soon Acacia itabaki kuwa ni historia, kwishney.
Jumatano Njema.
Paskali