Hongera sana na asante kwenu The Islamic Foundation!!

Hongera sana na asante kwenu The Islamic Foundation!!

KAUMZA,

..kujenga shule 7 na misikiti 700, kwa kweli hapo maji yamezidi unga.

..baadaye watu hao hao wanaanzisha kituo cha redio[redio imaan] na kulalamika kwamba wananyimwa elimu.

.......

Mie ningeona watu wa maana mno kama wangekuwa wanamiliki SHULE 700 na kujenga MISIKITI 7 mpaka sasa. Vinginevo pana kitu mbeleni tusichokijua hapa.
 
Hata hizo shule saba ni kitu cha kupongezwa sana!!! Maana ni hatua saba mbele ktk hatua mia saba, visima vya maji navyo ni vya kupongezwa.....!
Wanastahili pongezi....kuhusu Radi imaan na TV imaan kwa kuwa sijawahi kuzitazama wala kusikia sina la kuchangia japo kwa maoni ya wengi kidoogo kuna mushkel!!!
Siku Waislamu wakigundua kuwa adui yao mkubwa ni shetani akisaidiwa na Umaskini, ujinga na Maradhi watapiga hatua 700 mbele!!!
 
Michango inayotolewa hapa kwa wingi ndio hali halisi ya jamiiforums, wale wanaosema mtandao huu hauna UDINI (Haundeshwi kwa Mfumo Kristo) kwa kupitia nyuzi kama hizi ndipo pa kujifunza!
 
Kuna magaidi wengi wamekaribishwa na bado wengine wanakuja kama utitiri. Wameshapewa ardhi kuwekeza nchini, Foundations nyingi tutazisikia, viwanda na NGO's kibao...(kuna sababu maalum) Fuatilia jipe majibu.
 
ulistahili reputation hapa. Maxence Melo, please remind me again; why dont we have reputation button kwenye applications tukufu za jf?
Siku Waislamu wakigundua kuwa adui yao mkubwa ni shetani akisaidiwa na Umaskini, ujinga na Maradhi watapiga hatua 700 mbele!!!
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama kuna kitu cha kujivunia hapa! Labda ungesema kwamba Misikiti hiyo inatumika kwaajili ya kusomesha watoto wa kiislam shule za awali ambazo ni Madrasa ambapo elimu hiyo inafanana na na shule za nursery school...japo haitakuwa kweli...
 
Duh KAUMZA shule 7 na misikiti 700 nimeishiwa nguvu kabisa haya endelee ila msilalamike mfumo kristo.

Naipongeza sana Taasisi hii ya The Islamic Foundation kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya hapa nchini kwetu Tanzania.

Pia naupongeza sana uongozi wa Manispaa ya Morogoro chini ya Meya wake Mhe Nondo na Mkurugenzi Bw Jorvis kwa kutambua mchango wake hadi kuitunuku Taasisi hii Cheti cha shukrani "Certificate of appreciation" katika kuleta maendeleo ya watu bila kuzingatia dini ama itikadi ya mtu.

Katika kipindi kifupi, The Islamic Foundation imefanikiwa kuchimba visima virefu na vifupi vyenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 300 katika kata mbalimbali za manispaa ya Morogoro. Kata ya Mji mkuu imebahatika kupata visima viwili (2) na pia inajengewa ofisi ya kata ya kisasa kabisa.

Katika kata ya Kilakala kwa mujibu wa diwani wa kata hiyo Bw Ribon Mkali, The Islamic Foundation imewekeza katika ujenzi wa vyumba vinne (4) madarasa vinavyojengwa kwa matofali ya block yaliyolazwa. katika ujenzi huo wananchi wa kata hiyo walichangia kiasi cha Tsh 200,000/ na Islamic Foundation imechangia zaidi ya Tsh milioni 40.

Katika kata ya Mji mpya, kwa mujibu wa Diwani wa kata hiyo Bw Wenceslaus, Taasisi ya The Islamic Foundation imechangia kiasi cha Tsh milioni moja kwa ajili ya kufanya ukarabati wa mfumo wa maji katika zahanati katani humo.

Samweli Msuya wa kata ya Mbuyuni anaielezea The Islamic Foundation kama Mkombozi wa kweli kwa jamii ya wana Morogoro na Tanzania kwa ujumla. Ameelezea kuwa viongozi wake ni wasikivu, wenye huruma na wenye imani.

Kwa kila kisima kirefu kilichochimbwa wamefunga jenereta kwa ajili ya kuvuta maji (kwa maeneo yasiyo na umeme)na wameweka Tank lenye ujazo wa lita 5,000.

Pia kwa kujali elimu na kuizingatia, The Islamic Foundation wanamiliki shule saba (7) na wameweza kujenga misikiti 700 nchi nzima. Pia wanatoa ufadhili kwa watoto wanaoshindwa kulipia gharama za masomo katika shule za msingi na sekondari na wanategemea kuanzisha bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Zaidi katika kuisaidia serikali kupambana na umasikini wameweza kutoa mitaji kwa wajane na vijana na pia wameanzisha kitengo maalumu kwa ajili ya councelling kwa vijana waathirika wa madawa ya kulevya.

Kuhusu haki ya kupata habari, wamewezesha kusimama imara kwa Radio Imaan na Tv Imaan.

Tunashukuru: "Mmeahidi, mkatimiza. Na ALLAH ni Shahidi"

Mwenye macho haambiwi Tazama
 
Last edited by a moderator:
Shule 7 misikiti 700, wanapongezwa? kama trend itakuwa hivyo siku shule zikiwa 700 manaake misikiti 70,000! nitawapongeza pale itakapokuwa misikiti 700 shule 700

Great. waige mfano wa wakristo kule Moshi na Arusha. kila penye kanisa kuna shule ya sekondari na zahanati. pia shule na zahanati hizo zinahudumia watu wote bila ubaguzi. si ajabu ukakuta wagonjwa wengi ktk hospitali hizo ni waislamu, au watu wengine wasio na imani ya kikristo.
 
Shule 7 misikiti 700, wanapongezwa? kama trend itakuwa hivyo siku shule zikiwa 700 manaake misikiti 70,000! nitawapongeza pale itakapokuwa misikiti 700 shule 700

Great. waige mfano wa wakristo kule Moshi na Arusha. kila penye kanisa kuna shule ya sekondari na zahanati. pia shule na zahanati hizo zinahudumia watu wote bila ubaguzi. si ajabu ukakuta wagonjwa wengi ktk hospitali hizo ni waislamu, au watu wengine wasio na imani ya kikristo.
 
Mie ningeona watu wa maana mno kama wangekuwa wanamiliki SHULE 700 na kujenga MISIKITI 7 mpaka sasa. Vinginevo pana kitu mbeleni tusichokijua hapa.
NDUGU WAISLAMU NAOMBA NIWAPE USHAURI KWA YALE NILIYOYAONA KWENYE MAKANISA:
  1. kwao wakristu mambo muhimu matatu ambayo 1. Imani(elimu ya kiroho), 2.Elimu duunia(chekechea, msingi,sekondari, vyuo vya ufundi stadi), na 3. Afya za waamini(zahanati,mahospitali) vyote hivi vinapikwa katika chungu kimoja.
  2. Kama waislamu tutachukua formular hiyo hiyo na kuamua kutumia viwanja 700 tulivyojengea misikiti katika manispaa ya morogoro peke yake tutaweza kuwa na mafanikio yafuatayo katika manispaa ya morogoro bila kununua viwanja vingine vipya:-
    1. shule za chekechea - 1 x700 = 700
    2. shule za msingi - 1x 700 = 700
    3. shule za sekondari - 1 x 700 =700
    4. vyuo vya ufundi stadi 1 x 700 = 700
    5. zahanati 1 x 700 = 700
    6. mahospitali 1 x 700 = 700
  3. kwa ujumla mtakuwa mmeongeza tija katika huduma zenu za kijamii kwa kujenga vituo vya kuwapatia mafunzo na huduma mbali mbali vipatavyo 700X 6 = 4200 Katika manispaa ya morogoro na vituo hivi vitawafanya bize kujifunza, kufundishana, na kutoa huduma badala ya kushinda katika maeneo ya wazi yaliyotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto mkitoa mihadhara au misikitini mkijifunza judo kwa ajili ya kujihami na makafiri ambao kwa sasa wanatumia zana za electronic na mionzi kujilinda.
  4. my take : kulia lia hakutatusaidia kitu tuchukue hatua endelevu bila kuomba msaada kwa serikali wala wafadhili wa nje. vinginevyo tutaendelea kuzalisha vibarua wasiokubalika katika sekta binafsi wala serikalini matokeo tutabaki tukilalamikia MFUMO jambo ambalo halitakaa litusaidie mpaka siku ya kiama.
 
Hongera ziwaendee Manispaa ya Morogoro chini ya Meya wake Mhe Nondo na Mkurugenzi Bw Jorvis kwa kuruhusu haya yafanyike bila nyinyi kutumia werevu na kuheshimu dini za watanzania hayo yaliofanyika katika manispaa yane yasingelifanyika

Hongera sana The Islami Foundation kwa kutimiza moja katika nguzo tano za kiislam yaani "Dhaka na Sadaka" Mungu akupeni kila la kheri mzidi kuutangaza uislam kwa njia nzuri

Mcheza kwao hutumzwa
 
Shule 7 na misikiti 700 ? Bado mnalalamikia mfumo kristo
 
Mtawalaumu bakwata bure, hivi hawa bakwata ndio wanaowafanyia mitihani? Mbona darasani wengi wenu vilaza sana? Hata wengi wa wanafunzi wanakimbilia Morogoro muslim kwenye mteremko maana hapo nikuendeleza madrasa culture ndio maana nilikuwa naongea na mkuu wa shule mmoja hapo morogoro manispaa akasema wanafunzi wa ordinary level wanawakataa wanafunzi wa morogoro university kisa uwezo wao darasani.

Kibaya zaidi ni kuwa wanapopelekwa kwa ajili ya fieldwork huripoti nakuondoka na hurejea siku mhadhiri wao anapoenda kwa ajili ya assessment basi.

Wewe kereng'ende kaa kimya hujui kitu, unajua ni mali kiasi gani zinazomilikiwa na waislamu tangu kuvunjwa kwa EAMWS sasa hivi zipo chini ya bakwata hazijaendelezwa au zinawanufaisha wao, unajua kuwa hicho kiwanja kilichomuweka Ponda gerezani ilitakiwa kiwe chuo kikuu cha kiislamu lakini mpaka sasa wamebaki na propaganda tu hao bakwata wako> Umeuliza swali zuri kuwa je bakwata ndiyo wanaofanya mtihani sasa ngoja nikujibu Angalia shule zinazomilikiwa na bakwata kama Kinondoni muslim then ufananishe na zinazomilikiwa na taasisi nyingine za kiislamu kama Mudio islamic seminary, Nyasaka na Ubungo islamic then upate conclusion ya swali lako.

Wahenga wanasema ukiona mwenzako anasifiwa na adui yako basi kaa chonjo! Kwanini wewe ambaye uislamu haukuhusu unataka kuipigia chapuo hiyo bakwata?
 
Duh Mnyamwezi wa Urambo

Umetiririka vizuri kweli,hicho kiwanja cha Chang'ombe hakijauzwa bali kimebadilishwa na kiwanja kingine kikubwa zaidi ambacho kingefaa kujengwa chuo kikuu.BAKWATA wamefanya jambo la maana sana mpira unabaki kwenu waIslam kuchangia ujenzi wa hicho chuo kikuu si kulalama.

Ponda ameponzwa na umbulula badala ya kufundisha vijana dini anawafundisha kareti,ukorofi na maandamano yasiyo na tija ndiyo maana sasa hivi yuko ndani.Ifahamike Ponda ana taasisi yake jiulize amejenga shule ngapi ?.Taasisi yake imeshindwa hata kujenga misikiti inachofanya ni kuvamia misikiti inayomilikiwa na BAKWATA.

Wewe kereng'ende kaa kimya hujui kitu, unajua ni mali kiasi gani zinazomilikiwa na waislamu tangu kuvunjwa kwa EAMWS sasa hivi zipo chini ya bakwata hazijaendelezwa au zinawanufaisha wao, unajua kuwa hicho kiwanja kilichomuweka Ponda gerezani ilitakiwa kiwe chuo kikuu cha kiislamu lakini mpaka sasa wamebaki na propaganda tu hao bakwata wako> Umeuliza swali zuri kuwa je bakwata ndiyo wanaofanya mtihani sasa ngoja nikujibu Angalia shule zinazomilikiwa na bakwata kama Kinondoni muslim then ufananishe na zinazomilikiwa na taasisi nyingine za kiislamu kama Mudio islamic seminary, Nyasaka na Ubungo islamic then upate conclusion ya swali lako.

Wahenga wanasema ukiona mwenzako anasifiwa na adui yako basi kaa chonjo! Kwanini wewe ambaye uislamu haukuhusu unataka kuipigia chapuo hiyo bakwata?
 
Last edited by a moderator:
Wewe kereng'ende kaa kimya hujui kitu, unajua ni mali kiasi gani zinazomilikiwa na waislamu tangu kuvunjwa kwa EAMWS sasa hivi zipo chini ya bakwata hazijaendelezwa au zinawanufaisha wao, unajua kuwa hicho kiwanja kilichomuweka Ponda gerezani ilitakiwa kiwe chuo kikuu cha kiislamu lakini mpaka sasa wamebaki na propaganda tu hao bakwata wako> Umeuliza swali zuri kuwa je bakwata ndiyo wanaofanya mtihani sasa ngoja nikujibu Angalia shule zinazomilikiwa na bakwata kama Kinondoni muslim then ufananishe na zinazomilikiwa na taasisi nyingine za kiislamu kama Mudio islamic seminary, Nyasaka na Ubungo islamic then upate conclusion ya swali lako.

Wahenga wanasema ukiona mwenzako anasifiwa na adui yako basi kaa chonjo! Kwanini wewe ambaye uislamu haukuhusu unataka kuipigia chapuo hiyo bakwata?

Usimlaumu sana...unajua mie ni mkristo ila huwa naamini hakuna binadamu wengi wakawa wajinga wote....Kuona waislamu hawaipendi BAKWATA kuna kitu..Umenifungua leo.
Thanx...
 
Back
Top Bottom