Hongera Rais Samia kwa kuifungua Kigoma kiuchumi

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
WhatsApp Image 2022-10-19 at 12.28.37 AM.jpeg

Uamuzi wa serikali wa kuweka malengo ya kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa wa kimkakati, kiuwekezaji na kibiashara, unastahili kuungwa mkono na Watanzania wote kwa kuwa umelenga kukuza uchumi.

Rais Samia akiwa kwenye ziara ya siku nne mkoani Kigoma, alifungua barabara ya Kidahwe hadi Kasulu yenye urefu wa kilomita 63, alizindua pia miradi ya afya , maji na elimu ambayo kwa ujumla imeufanya mkoa huo kuwa na mabadiliko makubwa tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani.

Ni ukweli ulio wazi kuwa, Mkoa wa Kigoma, umeandika historia mpya ya kuanza rasmi kutumia umeme wa megawati 900 kutoka gridi ya taifa.

Mafanikio hayo ya mkupuo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya 6, chini ya Rais Samia Suluhu, pamoja na kwamba utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, yanastahili pongezi kubwa kwani dhamira yake ni kuwaletea Watanzania maendeleo.

Imani yangu ni kwamba, kwa kutumia nishati ya umeme wa uhakika, wawekezaji hawatajishauri kufanya uwekezaji mkoani Kigoma, watachangamkia wito wa Rais Samia Suluhu wa kuchangai ukuaji wa uchumi kimkoa.

Mwisho, niwakumbushe wananchi, tushirikiane na serikali ili mipango hiyo iweze kuwa na mafanikio makubwa na kuwaletea maendeleo Kigoma na Tanzania kwa ujumla.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom