Hongera Patrobas, ila umenielewa vibaya

Hongera Patrobas, ila umenielewa vibaya

8 O'clock, sijapata meseji yako, na ikiwa kweli nimealikwa nitahudhuria. Nitaomba kuuliza na kuchangia pia, hope mtatoa nafasi ya vijana kufunguka as kwa definition ya Kongamano..? is it..?

Na zile tabia zako naamini utakuwa umeacha, kitu cha Black pen...! We mtu mbaya sana.
Shhhh.......Don't be so personal...
 
HONGERA PATROBAS, ila umenielewa Vibaya.

Katika sehemu kubwa ya maandiko yangu hapa jukwaani yamekuwa yakijikita kuainisha udhaifu wa Upinzani na hasa CHADEMA, na katika kuizungumza CHADEMA naitaja sana BAVICHA, sihitaji kurudia tena kusema sababu ya kufanya hivyo kwani nimeiweka bayana mara kadhaa..!!

Tofauti na siku zilizopita, leo naandika kutoa pongezi, kusifia na kuonyesha kuridhika kwangu namna ambavyo PATROBAS PASCHAL, Mwenyekiti BAVICHA alivyopokea maoni yangu na kuyafanyia kazi.

Ni kweli kuwa umekuwa ukipata upinzani na changamoto za kipekee sana katika kazi yako ngumu ya kuongoza Vijana wasioamini katika itikadi, hawana muongozo. I have been there, najua unaongoza watu wa namna gani. Pole na hongera..

Ni kweli pia, sikuwa nikikufahamu wakati wa uongozi wangu, hivyo mimi ni kama wengine wasiokujua na wanaoshangaa ulipotokea, sina historia sahihi ya mapambano, uwezo na maarifa yako katika kuongoza na kuyasimamia maslahi ya Vijana kwenye Chama na kwa Taifa kwa ujumla. Ila ninalojua ni kuwa ulipingwa na unapingwa sana hata sasa, ushahidi wa hayo ni kauli hizi za Die Hard Members wa BAVICHA dhidi yako baada tu ya kuteuliwa, Yericko Nyerere alisema hivi;
View attachment 377898

Nae Ben Saanane aliyehenguliwa kwa figisu za Umri alisema hivi;
View attachment 377899

Baada ya hapo wakaibuka wabezaji na wapingaji online…IBILISI alisema haya; John Heche okoa jahazi, BAVICHA imemshinda Katambi, Inakufaa, na Pisto Lero aliandika; Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA, na hata SHIEKA akamaliza Mwenyekiti BAVICHA Patrobass Katambi Naanza Kupoteza Imani Kwako!, hao ni baadhi tu, ukiacha wale ambao walikuwa wafuasi wa Msigwa. Kwa ujumla wake ni kuwa unapigwa, wenzako hawaamini katika wewe, hawaamii uwezo wako na hawajui mwelekeo wako. Hawako tayari kufuata njia na maelekezo yako.

Mimi nilisema siku za nyuma kuwa BAVICHA imepooza, nikimaanisha kuwa imepoteza taswira ya “TAASISI YA VIJANA” baada ya maneno hayo nikaona umeanza kufanya Press Conference kila asubuhi na jioni, lakini kama utakuwa tayari kuungana na mimi katika tathmini ya Press hizo ni sawa na ‘vumbi lenye kupeperuka” hazina substance kabisa kwa sababu nyingi ni za kuunga mkono, maamuzi ya aidha Mwenyekiti, Kamati Kuu au Baraza Kuu, sawa ni jambo jema lakini hivi ni kweli vijana hawana “HOJA” za msingi za kusemewa na BAVICHA isipokuwa kuunga mkono tu..??

Maana mimi najua, pale akina Nusrat Hanje walipokatwa Ubunge wa Viti Maalum na kupewa total strangers BAVICHA ilikuwa kimya, Mwenyekiti alipomleta Mgombea wake “FISADI” Bavicha ilikuwa Kimya, MGOMBEA FISADI anapojitangaza kuwa yeye ni MGOMBEA WA KUDUMU wa CHADEMA 2020, 2025 kinyume na Kanuni na Taratibu BAVICHA iko kimya..? Sawa labda ya Chama makubwa sana na mazito kuyagusa, maana hata MASHINJI mwenyewe hayazungumzii basi tulitegemea mtetee Vijana ngazi ya Taifa lakini nako ni Zero, Mikopo vyuoni hamna mko kimya, Ajira bado mko kimya, ****** wanadahiliwa vyuoni mko kimya,,,ehee Basi anzisheni hata kampeni ya kuhimiza Vijana kujiajiri na kushiriki kilimo, mtengeneze banda la mfano kwenye nane nane, maana hata Meya wa Kinondoni akiwa anazunguka kwenye makundi ya Vijana kuhamasisha kujiajiri na kuunda vikundi wapewe mikopo ya Serikali hampo na wala hamshiriki wala kuunga mkono…!!

Labda ulinielewa Vibaya nilipotaka uanze kuwa active, nilimaanisha uwasemee Vijana ndani ya Chama na ndani ya Taifa.

Kama siasa ngumu unaweza kuchagua kuwa Mkulima, mimi nimechagua kufanya yote mawili. Kauli mbiu ya Wakulima wenzangu mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”
 
Hapo kwenye RED ndio huwa unakoseaga..utanirudisha kwenye ufafanuzi wa nani mzushi na mwenye siasa za mtaroni, nani aliyekula hela za Chama akiwa frontliner wa mapambano ya mitandaoni, ilitoka shilingi ngapi na wenzio uliwapa shilingi ngapi..?

Nitaenda mbele niulize kuhusu KAS yaani Konrad Adeneur Stiftung, na yale makubaliano kuhusu website ya CHADEMA. Wakati mwingine tukianza vizuri acha tumalize vizuri, si vyema kila wakati tukashambuliana na kunyoosheana vidole. kulikuwa hakuna sababu ya kuniita Mzushi na kuniambia nina siasa za mtaroni, kama vile ambavyo mimi sijakuita Mzushi kwenye maandiko yangu wala sijakutaja kuwa una siasa za mtaroni.

Nikisema kila ninalolijua, na kila mpango ulioushiriki unadhani utabaki salama..??? Kuwa mtu mzima now..acha haya mambo.

Naona Ben amekanyaga live wire...ila nilifikiri Ben ana hoja kwa sababu jinsi ulivyomnukuu katika uzi wako, alikanusha na wewe hukujibu kitu. huwezi jua ilivyom-pain. halafu inaonekana Ben na Juliana mlianza kitu ambacho hamkukimaliza, if you know what I mean. hayo mengine siwezi kuyaongelea maana sina facts. but you sound like an angry woman
 
Bvicha wamekuwa watu wakuunga mkono tuu matamko ya Lowasa na Mbowe.

Leo hii Bavicha wanashindwa kumdhibiti Lowasa kujitangaza mgombea kabla ya 2020.

Mimi ndio maana huwaita Nyumbu.
UVCCM kuna ambaye ameisha thubutu kupinga "matamko/tamko" ya "Pombe" au "Mzee Alfani".
 
Ben how are U doing..? It has been long haujachangia kwenye thread zangu lakini pia ni kama ulipotea JF baada ya yaliyokutokea Rombo. Nice to have U back...njoo tupige maneno ndio silaha yetu wanasiasa.
Bado unaimani "maneno" ndio silaha ya mwanasiasa na sio uthubutu na vitendo? Kweli kama ndivyo basi tusitegemee jipya hata kwenye "Tanzania ya viwanda"
 
Naweza kuelewa matatizo yako. kama ulikuwa kweli mpambanaji huko BAVICHA, siyo rahisi ukahama mzima mzima kwenda CCM na ukawa unapiga kama ulivyokuwa unapiga huku. Namkumbuka Dr. Masumbuko Lamwai. Huyo enzi zake alikuwa moto wa kuotea mbali, mithili ya Tundu Lissu, ingawa Lissu naona yuko vizuri zaidi. tangu amehamia CCM, sijaona tena yale makeke yake. Mkapa alimsifia kama bingwa wa kujenga na kubomoa hoja, alipomkabidhi kadi ya CCM. lakini ameshindwa kabisa kufanya huko CCM alichokuwa anakifanya alipokuwa NCCR enzi hizo, wakati NCCR ikiwa ndio chama kikuu cha upinzani. namwona pia Mzee Mwanakijiji alivyodorora baada ya ku-cross over. Ndio maana hata wewe unajikuta kila mara lazima uongelee BAVICHA, kwa kisingizio kwamba ndio unaowafahamu zaidi. lakini kusema kweli moyo wako uliuacha huko huko BAVICHA...

Kuhusu hao uliosema kwamba wanang'ara, yaani Makonda na Hapi, ni kwa sababu tu katika CCM kuna vyeo kada anaweza akapewa. katika Upinzani hakuna vyeo vya kiserikali, wala marupurupu. Kwa hiyo ukitaka kupima mafanikio ya kiongozi wa upinzani, itabidi utafute vigezo tofauti. Binafsi nadhani ni mapema mno kusema Makonda kaimudu Dar. Namshauri atumie zaidi hekima na apunguze spidi. angalau atafanikisha machache. Jiji kubwa hili.
Nadhani kwa namna ulivyoeleza, sidhani kama ulimaanisha kuwa ni matatizo...labda ikiwa neno matatizo limepatiwa tafsiri mpya.

Kimsingi nikianza na hoja yako ya kwanza, kuhusu kuchuja ama kupanda ni lazima kujua unazungumza katika muktadha gani. Kuhusu LAMWAI naweza nisiwe na maelezo mazuri hivyo sitosema lolote ila kuhusu TUNDU LISSU ninayo ya kusema tena mengi,
1. Kama kipimo chako cha ubora wa mtu ni kumlinganisha na TUNDU LISSU naomba mimi nikubali kuwa mtu wa hovyo. Sijawahi, na sitaki kwa namna yeyote kufanana na mtu kama Tundu Lissu, kwa tabia, akili, maarifa, uwezo na hata kitaaluma. Sitaki kufanana nae. Nadhani nimesema yoooote kuhusu Lissu kwenye thread hii Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu, lakini jambo lingine muhimu kulijua ni namna ya kufanya hiyo comparison analysis, CHADEMA ni kikundi cha wanaharakati, BAVICHA ni sehemu katika CHADEMA, ili uwe mwenzao ni lazima uwe kinara wa harakati., hakuna mwanasiasa chadema wala mwelekeo wa kuwaandaa Vijana wanasiasa ama kuandaa viongozi...hakuna Kijana Chadema anaandaliwa kuja kuwa Kiongozi, si tu wa CHADEMA bali wa TAIFA..hakuna hiyo program.

Mimi ni zao la HARAKATI za CHADEMA, wakati fulani nilipelekwa nchini UGANDA nikiongozana na Ndugu yangu JOHN MALLYA (ambae kwa sasa ni mwanasheria wa CHADEMA) kulikuwa na mafunzo ya uongozi yaliyoandaliwa na taasisi ya Kiswidishi (KIC) ambayo iliitwa Program for Young Politicians in Africa - PYPA, ambapo vijana kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika wamekuwa wakikusanyika ili kupigwa msasa na kuandaliwa kuwa Viongozi bora wa baadae..Kwa bahati mbaya sana, maandalizi tuliyofanyiwa ili tukashiriki yalikuwa ya ajabu sana, maana tulichapishiwa lundo la Picha za matukio ya mauaji yaliyotokana na maandamano kule Arusha, Morogoro na zile za Mwangosi, Picha za Mama Mushumbusi akivuja damu na zinginezo kuwa tukawaonyeshe wale Wazungu ili Serikali ya Tanzania iadhibiwe kwa kunyimwa mikopo, kwa bahati mbaya sana wakati ule nilikubali kufanya jambo lile ovu kwa nchi yangu...najutia hata sasa kwa kuwa mmoja wa watu walioshiriki kuharibu image ya nchi yangu kwa UJINGA tu..!

Lakini hivyo ndivyo vijana wanavyoandaliwa CHADEMA kuwa hawana cha kujivunia kwenye nchi hii, wanaandaliwa kuikwamisha Serikali, kuharibu IMAGE ya nchi kimataifa. Wanafundishwa kuwa wanaharakati wasiofiriki.

Hali hii sikuikuta UVCCM, kabisa. Niliwakuta Vijana wakiwa watulivu, wanaochangia hoja kwa heshima na nidhamu, waliojaa uzalendo kwa Chama na Nchi yao, wanafunzwa kuitetea popote wawapo duniani, wanatetea Viongozi wao na Serikali yao. Wanafundishwa kujivunia nchi yao na Viongozi wao, wanafanywa wazalendo. Hawa wanakuwa wanasiasa Viongozi. Nilivyojiunga CCM nikapelekwa IHEMI nikawekwa kwa miezi miwili nikifunzwa kuwa Kijana wa CCM, baada ya hapo nikaanza kuchukuliwa kwenye majukwaa ya siasa ya CCM na kushiriki Vikao. Nikaajiriwa makao makuu ya UVCCM na nikatakiwa kujiendeleza kielimu kwa kulipiwa na Jumuiya.. hayo hayafanyiki BAVICHA katu..!

Kuifanyia Comparison UVCCM na BAVICHA ni kufanya makosa ya mfanano, maana utakuwa unafananisha visivyofanana. BAVICHA wanaharakati na UVCCM wanasiasa, wapi na wapi.!!

Hata hiyo HOJA yako kuwa akina MAKONDA watafeli, ni hoja iliyojengwa katika misingi ya Choyo, waswahili wanaita Dua la Kuku. Dar imetulia, hakuna mgambo wa jiji kusumbua akina Mama Ntilie, hakuna mitaro michafu, mji unasimamia usafi akina Makonda wakiwa wahamasishaji wakuu..mji wetu unaingia mikataba mikubwa na miji mikubwa Duniani ya China na Japan...bado unasema hawezi kufanikiwa.,ama kweli BAVICHA mentality ya kuto appreciate kitu imewakolea..Dah.
 
Umeshapata ulaji,lazima uwatetee kwa hali yoyote!Ukitaka kudeal na mwafrika msumbufu,mpe pesa!Hapo kila kitu kitabadilika!Sasa unafikiria kwa kutumia tumbo,una ambition kweli!Labda baadaye magu takufikiria unaibu waziri!
Naamini kesho CCM wakitoka madarakani na chama kingine kikapuka nafasi basi utaanza kuwasema ccm kwa mabaya!Ndio wengi wa waafrica walivyo,tumbo mbele kwanza!
Huna uwezo na kamwe huwezi kuwa na fikra na uelewa kama Lissu,sio kwa uchangiaji ule wa kipuuzi bungeni!Sio kwa nyuzi zako unazoandika JF,nyingi zikiwa zimejaa vioja badala ya hoja!Don't fool yourself,siku ikitokea Lissu akakujadili wewe utajisikia sana!Wewe kila siku,mara Mbowe,mara Lissu unawatolea maneno ya dharau na kebehi lakini one thing for sure uko so cheap kwao kukujadili!
Shame on you
 
Kwa kweli kujua kama UVCCM wako bora ama laa kunategemea zaidi unafananisha na UVCCM ya kipindi gani..?

Na kwa sababu sijaiishi UVCCM kama nilivyoiishi BAVICHA ukweli utabaki kuwa naijua zaidi bavicha kuliko Uvccm...tena naijua ndani nje.

Lakini naiona UVCCM, naisikia kwenye vikao vya Chama na naisikia katika hoja na mabaraza ya kitaifa...

Nawaona vijana wengi wanaofanya vizuri na wanaakisi taswira ya Ujana wengi ni zao la UVCCM. Nikimtazama Makonda anavyolimudu jiji Mama la Dar es salaam naiona UVCCM..nikimtazama Hapi akiwa ameimeza Kinondoni na naiona UVCCM...naiona UVCCM leo na katika Tanzania ya kesho...ila siioni BAVICHA popote
Umeendelea kupotea zaidi kwa kutumia mifano hii!
 
Ukipewa wewe unaomba kuheshimiana! Jee wewe unaheshimu wengine? Wale wazee unao wakashifu na kuwatukana huku unajua hawawezi kukujibu mitandaoni unaona ni sawa?
Jifunze kwanza kuwa na adabu kama mke wa mtu na kama Mbunge, hata kama ubunge wako wa kupewa una agenda za siri

Chakaza,

Muache hasira zipoe kwanza. ....!
 
Nadhani kwa namna ulivyoeleza, sidhani kama ulimaanisha kuwa ni matatizo...labda ikiwa neno matatizo limepatiwa tafsiri mpya.

Kimsingi nikianza na hoja yako ya kwanza, kuhusu kuchuja ama kupanda ni lazima kujua unazungumza katika muktadha gani. Kuhusu LAMWAI naweza nisiwe na maelezo mazuri hivyo sitosema lolote ila kuhusu TUNDU LISSU ninayo ya kusema tena mengi,
1. Kama kipimo chako cha ubora wa mtu ni kumlinganisha na TUNDU LISSU naomba mimi nikubali kuwa mtu wa hovyo. Sijawahi, na sitaki kwa namna yeyote kufanana na mtu kama Tundu Lissu, kwa tabia, akili, maarifa, uwezo na hata kitaaluma. Sitaki kufanana nae. Nadhani nimesema yoooote kuhusu Lissu kwenye thread hii Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu, lakini jambo lingine muhimu kulijua ni namna ya kufanya hiyo comparison analysis, CHADEMA ni kikundi cha wanaharakati, BAVICHA ni sehemu katika CHADEMA, ili uwe mwenzao ni lazima uwe kinara wa harakati., hakuna mwanasiasa chadema wala mwelekeo wa kuwaandaa Vijana wanasiasa ama kuandaa viongozi...hakuna Kijana Chadema anaandaliwa kuja kuwa Kiongozi, si tu wa CHADEMA bali wa TAIFA..hakuna hiyo program.

Mimi ni zao la HARAKATI za CHADEMA, wakati fulani nilipelekwa nchini UGANDA nikiongozana na Ndugu yangu JOHN MALLYA (ambae kwa sasa ni mwanasheria wa CHADEMA) kulikuwa na mafunzo ya uongozi yaliyoandaliwa na taasisi ya Kiswidishi (KIC) ambayo iliitwa Program for Young Politicians in Africa - PYPA, ambapo vijana kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika wamekuwa wakikusanyika ili kupigwa msasa na kuandaliwa kuwa Viongozi bora wa baadae..Kwa bahati mbaya sana, maandalizi tuliyofanyiwa ili tukashiriki yalikuwa ya ajabu sana, maana tulichapishiwa lundo la Picha za matukio ya mauaji yaliyotokana na maandamano kule Arusha, Morogoro na zile za Mwangosi, Picha za Mama Mushumbusi akivuja damu na zinginezo kuwa tukawaonyeshe wale Wazungu ili Serikali ya Tanzania iadhibiwe kwa kunyimwa mikopo, kwa bahati mbaya sana wakati ule nilikubali kufanya jambo lile ovu kwa nchi yangu...najutia hata sasa kwa kuwa mmoja wa watu walioshiriki kuharibu image ya nchi yangu kwa UJINGA tu..!

Lakini hivyo ndivyo vijana wanavyoandaliwa CHADEMA kuwa hawana cha kujivunia kwenye nchi hii, wanaandaliwa kuikwamisha Serikali, kuharibu IMAGE ya nchi kimataifa. Wanafundishwa kuwa wanaharakati wasiofiriki.

Hali hii sikuikuta UVCCM, kabisa. Niliwakuta Vijana wakiwa watulivu, wanaochangia hoja kwa heshima na nidhamu, waliojaa uzalendo kwa Chama na Nchi yao, wanafunzwa kuitetea popote wawapo duniani, wanatetea Viongozi wao na Serikali yao. Wanafundishwa kujivunia nchi yao na Viongozi wao, wanafanywa wazalendo. Hawa wanakuwa wanasiasa Viongozi. Nilivyojiunga CCM nikapelekwa IHEMI nikawekwa kwa miezi miwili nikifunzwa kuwa Kijana wa CCM, baada ya hapo nikaanza kuchukuliwa kwenye majukwaa ya siasa ya CCM na kushiriki Vikao. Nikaajiriwa makao makuu ya UVCCM na nikatakiwa kujiendeleza kielimu kwa kulipiwa na Jumuiya.. hayo hayafanyiki BAVICHA katu..!

Kuifanyia Comparison UVCCM na BAVICHA ni kufanya makosa ya mfanano, maana utakuwa unafananisha visivyofanana. BAVICHA wanaharakati na UVCCM wanasiasa, wapi na wapi.!!

Hata hiyo HOJA yako kuwa akina MAKONDA watafeli, ni hoja iliyojengwa katika misingi ya Choyo, waswahili wanaita Dua la Kuku. Dar imetulia, hakuna mgambo wa jiji kusumbua akina Mama Ntilie, hakuna mitaro michafu, mji unasimamia usafi akina Makonda wakiwa wahamasishaji wakuu..mji wetu unaingia mikataba mikubwa na miji mikubwa Duniani ya China na Japan...bado unasema hawezi kufanikiwa.,ama kweli BAVICHA mentality ya kuto appreciate kitu imewakolea..Dah.

Ahsante, inabidi nikushukuru kwa maelezo ya kina uliyotoa, nimejifunza kitu. lakini:
1) Kuhusu Tundu Lissu, nimesoma hilo andiko lako ambalo umesema umeeleza "yoote", na kwa kweli hakuna ulichosema. Tundu Lissu ni mwanasheria first, na anafanya siasa second. inawezekana kaingia katika siasa out of necessity. Nakumbuka alianzia na kikundi au chama cha wanasheria wanaojihusisha na mazingira, na akapambana sana na dhuluma zilizofanywa na makampuni ya madini. ameshiriki kuwatoa gerezani walalahoi wengi sana waliobambikiwa kesi na wawekezaji kwa kuwahonga viongozi (wa ccm). Mimi natambua mchango mkubwa sana wa Tundu Lissu, ambaye inaonekana ni mtu kwa nature yake anachukia unyanyasaji na ukandamizaji. alichosema kuhusu utendaji wa serikali ya awamu ya 5 ni sahihi kabisa. ni kweli, hata mimi naunga mkono mazuri mengi tu ambayo yanafanywa. lakini lazima kutambua kwamba nia nzuri tu haitoshi. huu kama ni utawala wa sheria, lazima sheria zizingatiwe, ili nia nzuri iwe kweli nia nzuri, itekelezwe vizuri na ionekane hivyo. nothing less. labda nikusaidie kitu kimoja. katika nchi ambayo chama kinachotawala limegeuka kuwa chama dola, kimeacha kufanya siasa (Kama alivyowahi kuishauri CCM Rais mstaaf Kikwete, kwamba isitumie Polisi kufanya siasa, katika mkutano mkuu wa CCM, sikumbuki mwaka gani), kinatumia vyombo vya dola kukandamiza wananchi, siyo jambo la kushangaza kwamba wanasheria wanachomoza sana. Tundu Lissu alipojaribu kupambana bungeni alipigwa ban. huko hoja zinazimwa kwa kelele za CCM! CCM!

Tundu Lissu anapojenga hoja zake bungeni, mbunge wa CCM anayejitokeza kumjibu, badala ya kuzijibu zile hoja, anaishia tu kumtukana kwamba alilazwa Milembe. kauli hii pia imewahi kutolewa na Kigwangala, akidai kwamba amewahi kumtibu kichaa Lissu. hizo ni mbinu za kukwepa kujibu hoja. Na hayo maneno angesema mbunge wa upinzani, angepigwa ban na naibu spika. Lakini kwa kuwa ni "wenzetu wa CCM", mambo yanakwenda. lakini Mahakamani kule ni hoja tena za kisheria. hakuna amri ya Rais wala ya Makonda. kwa hiyo Wapinzani wanalazimika kupeleka mapambano yao mahakamani, maana bungeni wanapigwa ban, kwa wananchi wapiga kura wanakatazwa, huoni kwamba mazingira hayo ni magumu sana kwa upinzani? ingawa, ironically, hapo ndipo upinzani unapostawi zaidi. Lakini binafsi nasikitika sana kwamba kuna nafasi nzuri sana alikuwa nayo Rais Magufuli, kufanya kazi na upinzani nchini. pale mwanzoni alikuwa anaungwa mkono na taifa zima, upinzani wakiwemo.
2) Siasa za BAVICHA lazima zitofautiane na za UVCCM, ingawa ningetarajia UVCCM wawe kama ilivyokuwa zamani. mimi mwenyewe nilikuwa Chipukizi wa TANU enzi hizo, na bado nakumbuka Imani za mwana TANU: binadamu wote ni sawa, binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja. Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu kwa faida yangu...CCM imeacha hayo yote, na kilichopo ni kugombea vyeo tu. CCM ya leo haiamini katika Afrika ni moja, ndio maana leo utasikia huyu siyo raia, ni sera za kibaguzi ambazo zinatumiwa hasa mtu anapotofautiana na wengine kimtazamo. siwezi kujivunia chama cha aina hiyo
 
Nadhani kwa namna ulivyoeleza, sidhani kama ulimaanisha kuwa ni matatizo...labda ikiwa neno matatizo limepatiwa tafsiri mpya.

Kimsingi nikianza na hoja yako ya kwanza, kuhusu kuchuja ama kupanda ni lazima kujua unazungumza katika muktadha gani. Kuhusu LAMWAI naweza nisiwe na maelezo mazuri hivyo sitosema lolote ila kuhusu TUNDU LISSU ninayo ya kusema tena mengi,
1. Kama kipimo chako cha ubora wa mtu ni kumlinganisha na TUNDU LISSU naomba mimi nikubali kuwa mtu wa hovyo. Sijawahi, na sitaki kwa namna yeyote kufanana na mtu kama Tundu Lissu, kwa tabia, akili, maarifa, uwezo na hata kitaaluma. Sitaki kufanana nae. Nadhani nimesema yoooote kuhusu Lissu kwenye thread hii Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu, lakini jambo lingine muhimu kulijua ni namna ya kufanya hiyo comparison analysis, CHADEMA ni kikundi cha wanaharakati, BAVICHA ni sehemu katika CHADEMA, ili uwe mwenzao ni lazima uwe kinara wa harakati., hakuna mwanasiasa chadema wala mwelekeo wa kuwaandaa Vijana wanasiasa ama kuandaa viongozi...hakuna Kijana Chadema anaandaliwa kuja kuwa Kiongozi, si tu wa CHADEMA bali wa TAIFA..hakuna hiyo program.

Mimi ni zao la HARAKATI za CHADEMA, wakati fulani nilipelekwa nchini UGANDA nikiongozana na Ndugu yangu JOHN MALLYA (ambae kwa sasa ni mwanasheria wa CHADEMA) kulikuwa na mafunzo ya uongozi yaliyoandaliwa na taasisi ya Kiswidishi (KIC) ambayo iliitwa Program for Young Politicians in Africa - PYPA, ambapo vijana kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika wamekuwa wakikusanyika ili kupigwa msasa na kuandaliwa kuwa Viongozi bora wa baadae..Kwa bahati mbaya sana, maandalizi tuliyofanyiwa ili tukashiriki yalikuwa ya ajabu sana, maana tulichapishiwa lundo la Picha za matukio ya mauaji yaliyotokana na maandamano kule Arusha, Morogoro na zile za Mwangosi, Picha za Mama Mushumbusi akivuja damu na zinginezo kuwa tukawaonyeshe wale Wazungu ili Serikali ya Tanzania iadhibiwe kwa kunyimwa mikopo, kwa bahati mbaya sana wakati ule nilikubali kufanya jambo lile ovu kwa nchi yangu...najutia hata sasa kwa kuwa mmoja wa watu walioshiriki kuharibu image ya nchi yangu kwa UJINGA tu..!

Lakini hivyo ndivyo vijana wanavyoandaliwa CHADEMA kuwa hawana cha kujivunia kwenye nchi hii, wanaandaliwa kuikwamisha Serikali, kuharibu IMAGE ya nchi kimataifa. Wanafundishwa kuwa wanaharakati wasiofiriki.

Hali hii sikuikuta UVCCM, kabisa. Niliwakuta Vijana wakiwa watulivu, wanaochangia hoja kwa heshima na nidhamu, waliojaa uzalendo kwa Chama na Nchi yao, wanafunzwa kuitetea popote wawapo duniani, wanatetea Viongozi wao na Serikali yao. Wanafundishwa kujivunia nchi yao na Viongozi wao, wanafanywa wazalendo. Hawa wanakuwa wanasiasa Viongozi. Nilivyojiunga CCM nikapelekwa IHEMI nikawekwa kwa miezi miwili nikifunzwa kuwa Kijana wa CCM, baada ya hapo nikaanza kuchukuliwa kwenye majukwaa ya siasa ya CCM na kushiriki Vikao. Nikaajiriwa makao makuu ya UVCCM na nikatakiwa kujiendeleza kielimu kwa kulipiwa na Jumuiya.. hayo hayafanyiki BAVICHA katu..!

Kuifanyia Comparison UVCCM na BAVICHA ni kufanya makosa ya mfanano, maana utakuwa unafananisha visivyofanana. BAVICHA wanaharakati na UVCCM wanasiasa, wapi na wapi.!!

Hata hiyo HOJA yako kuwa akina MAKONDA watafeli, ni hoja iliyojengwa katika misingi ya Choyo, waswahili wanaita Dua la Kuku. Dar imetulia, hakuna mgambo wa jiji kusumbua akina Mama Ntilie, hakuna mitaro michafu, mji unasimamia usafi akina Makonda wakiwa wahamasishaji wakuu..mji wetu unaingia mikataba mikubwa na miji mikubwa Duniani ya China na Japan...bado unasema hawezi kufanikiwa.,ama kweli BAVICHA mentality ya kuto appreciate kitu imewakolea..Dah.
Umesema ulipokuwa CDM mlipelekwa Uganda na lundo la picha za matukio ya mauaji ambayo kiini chake ni maandamano, na ulipohamia CCM ulipelekwa Ihemi "kufunzwa kuwa kijana wa CCM na baadaye kuanza kuchukuliwa kwenye majukwaa ya siasa za CCM". Umetumia mfano huu kujaribu kujenga hoja kwamba CDM ni chama cha uanaharakati na ambacho siku zote kinaamini katika kuichafua serikali na CCM ni chama cha kizalendo!

Ukiweka pembeni unafiki mlionao vijana mnaotumia siasa kama njia za kufanikisha maisha yenu (kupata fedha, mali, heshima; nakadhalika) ninaamini ulipokuwa CDM na hata sasa, unatambua kuwa maandamano ni haki ya kikatiba na hivyo katika mazingira yoyote yale mauaji yanayotokana na kuzuiwa kwa haki hiyo yanapaswa kulaaniwa mbele ya dunia!

Uzalendo ambao unajaribu kuonyesha kwamba UVCCM mnajengewa kwa kupelekwa Ihemi inabidi utupe tafsiri yake kwa kirefu kidogo, vinginevyo haiwezi kuwa rahisi kukuamini kwani wewe mwenyewe ulipotoka Ihemi ulianza kuzunguka kwenye majukwaa ya siasa za CCM kuitukana CDM na sio kueneza huo uzalendo unaodai. Unakumbuka ulitumika sana kwenye eneo la "kutukana" na "kuzua" jambo ambalo kimsingi haliwezi kuwa uzalendo bali sababisho la kuharibu maadili ya taifa kwa kugeuza siasa kuwa uwanja wa matusi! Na katika hili wewe ukiwa miongoni mwa vijana mlio/mnao tumika mnapaswa kujiangalia sana!

Mwisho, kwa kuwa wewe umekuwa ukiweka cv yako hapa mara kwa mara kwamba unasoma phd, jitahidi maandiko yako nayo yawe yanaakisi mtu anayeelekea kutunukiwa phd kwa kutotaka kulazimisha siasa za CDM na CCM zifanane katika mazingira haya ambayo hayarusu, hata kidogo, kuwepo kwa mfanano unaotaka kutuaminisha kuwa unaweza kuwepo!
 
Chaah! Sasa Ben Saanane nilifanyaje Jully?

Kwa kumbukumbu,Hayo Maneno uliyoweka hapo niliandika siku nilipotangaza kuwa sitagombea Uenyekiti kwa sababu zile

Siku hiyo Patrobas hakua amechukua fomu na alikuja kuchukua Fomu Jumatatu yake. Hayo maneno niliandika Jumamosi

Nimekua nae tangu kabla hajachukua fomu na hata katika kampeni na baada ya Uchaguzi

Sasa mbona kama vile unataka kuleta uzushi kiaina Benazir?

mama ya Kipalestina au nimesahahu?
 
HONGERA PATROBAS, ila umenielewa Vibaya.

Katika sehemu kubwa ya maandiko yangu hapa jukwaani yamekuwa yakijikita kuainisha udhaifu wa Upinzani na hasa CHADEMA, na katika kuizungumza CHADEMA naitaja sana BAVICHA, sihitaji kurudia tena kusema sababu ya kufanya hivyo kwani nimeiweka bayana mara kadhaa..!!

Tofauti na siku zilizopita, leo naandika kutoa pongezi, kusifia na kuonyesha kuridhika kwangu namna ambavyo PATROBAS PASCHAL, Mwenyekiti BAVICHA alivyopokea maoni yangu na kuyafanyia kazi.

Ni kweli kuwa umekuwa ukipata upinzani na changamoto za kipekee sana katika kazi yako ngumu ya kuongoza Vijana wasioamini katika itikadi, hawana muongozo. I have been there, najua unaongoza watu wa namna gani. Pole na hongera..

Ni kweli pia, sikuwa nikikufahamu wakati wa uongozi wangu, hivyo mimi ni kama wengine wasiokujua na wanaoshangaa ulipotokea, sina historia sahihi ya mapambano, uwezo na maarifa yako katika kuongoza na kuyasimamia maslahi ya Vijana kwenye Chama na kwa Taifa kwa ujumla. Ila ninalojua ni kuwa ulipingwa na unapingwa sana hata sasa, ushahidi wa hayo ni kauli hizi za Die Hard Members wa BAVICHA dhidi yako baada tu ya kuteuliwa, Yericko Nyerere alisema hivi;
View attachment 377898

Nae Ben Saanane aliyehenguliwa kwa figisu za Umri alisema hivi;
View attachment 377899

Baada ya hapo wakaibuka wabezaji na wapingaji online…IBILISI alisema haya; John Heche okoa jahazi, BAVICHA imemshinda Katambi, Inakufaa, na Pisto Lero aliandika; Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA, na hata SHIEKA akamaliza Mwenyekiti BAVICHA Patrobass Katambi Naanza Kupoteza Imani Kwako!, hao ni baadhi tu, ukiacha wale ambao walikuwa wafuasi wa Msigwa. Kwa ujumla wake ni kuwa unapigwa, wenzako hawaamini katika wewe, hawaamii uwezo wako na hawajui mwelekeo wako. Hawako tayari kufuata njia na maelekezo yako.

Mimi nilisema siku za nyuma kuwa BAVICHA imepooza, nikimaanisha kuwa imepoteza taswira ya “TAASISI YA VIJANA” baada ya maneno hayo nikaona umeanza kufanya Press Conference kila asubuhi na jioni, lakini kama utakuwa tayari kuungana na mimi katika tathmini ya Press hizo ni sawa na ‘vumbi lenye kupeperuka” hazina substance kabisa kwa sababu nyingi ni za kuunga mkono, maamuzi ya aidha Mwenyekiti, Kamati Kuu au Baraza Kuu, sawa ni jambo jema lakini hivi ni kweli vijana hawana “HOJA” za msingi za kusemewa na BAVICHA isipokuwa kuunga mkono tu..??

Maana mimi najua, pale akina Nusrat Hanje walipokatwa Ubunge wa Viti Maalum na kupewa total strangers BAVICHA ilikuwa kimya, Mwenyekiti alipomleta Mgombea wake “FISADI” Bavicha ilikuwa Kimya, MGOMBEA FISADI anapojitangaza kuwa yeye ni MGOMBEA WA KUDUMU wa CHADEMA 2020, 2025 kinyume na Kanuni na Taratibu BAVICHA iko kimya..? Sawa labda ya Chama makubwa sana na mazito kuyagusa, maana hata MASHINJI mwenyewe hayazungumzii basi tulitegemea mtetee Vijana ngazi ya Taifa lakini nako ni Zero, Mikopo vyuoni hamna mko kimya, Ajira bado mko kimya, ****** wanadahiliwa vyuoni mko kimya,,,ehee Basi anzisheni hata kampeni ya kuhimiza Vijana kujiajiri na kushiriki kilimo, mtengeneze banda la mfano kwenye nane nane, maana hata Meya wa Kinondoni akiwa anazunguka kwenye makundi ya Vijana kuhamasisha kujiajiri na kuunda vikundi wapewe mikopo ya Serikali hampo na wala hamshiriki wala kuunga mkono…!!

Labda ulinielewa Vibaya nilipotaka uanze kuwa active, nilimaanisha uwasemee Vijana ndani ya Chama na ndani ya Taifa.

Kama siasa ngumu unaweza kuchagua kuwa Mkulima, mimi nimechagua kufanya yote mawili. Kauli mbiu ya Wakulima wenzangu mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”
Naomba nikumbushe kwanza mwenyekiti wa UVCCM dada angu, kweli simfaham wala s8jawahi kumsikia
 
..Kwa bahati mbaya sana, maandalizi tuliyofanyiwa ili tukashiriki yalikuwa ya ajabu sana, maana tulichapishiwa lundo la Picha za matukio ya mauaji yaliyotokana na maandamano kule Arusha, Morogoro na zile za Mwangosi, Picha za Mama Mushumbusi akivuja damu na zinginezo kuwa tukawaonyeshe wale Wazungu ili Serikali ya Tanzania iadhibiwe kwa kunyimwa mikopo, kwa bahati mbaya sana wakati ule nilikubali kufanya jambo lile ovu kwa nchi yangu...najutia hata sasa kwa kuwa mmoja wa watu walioshiriki kuharibu image ya nchi yangu kwa UJINGA tu..!

Lakini hivyo ndivyo vijana wanavyoandaliwa CHADEMA kuwa hawana cha kujivunia kwenye nchi hii, wanaandaliwa kuikwamisha Serikali, kuharibu IMAGE ya nchi kimataifa. Wanafundishwa kuwa wanaharakati wasiofiriki.

Kueleza mauaji ya watu waliouawa wakati wanatumia haki yao ya kikatiba na kisheria, unasema ni jambo ovu. wakati mimi na wengine wengi watakubaliana kwamba uovu ni yale mauaji. kuyatangaza ni sehemu ya kuikosoa serikali isifanye hayo mambo maovu. Kwa hiyo wewe sasa hivi baada ya hayo mafunzo ya IHEMI unaamini kwamba kuuwa watu wanaotumia haki yao ya kikatiba na kisheria ni sawa kabisa, ila kutangaza matendo hayo katika vyombo vya habari na nje ya nchi, ni UOVU, aisee, hapo hata sifa za binadamu unakuwa hunazo...
 
BAVICHA Ilikuwa ya John Heche bwana..... Huyo PATROBAS Hakuna kitu dhaifu zaidi ya ujuavyo....wacha wafu wazikane bwana...
 
Chaah! Sasa Ben Saanane nilifanyaje Jully?

Kwa kumbukumbu,Hayo Maneno uliyoweka hapo niliandika siku nilipotangaza kuwa sitagombea Uenyekiti kwa sababu zile

Siku hiyo Patrobas hakua amechukua fomu na alikuja kuchukua Fomu Jumatatu yake. Hayo maneno niliandika Jumamosi

Nimekua nae tangu kabla hajachukua fomu na hata katika kampeni na baada ya Uchaguzi

Sasa mbona kama vile unataka kuleta uzushi kiaina Benazir?
Cha ajabu nini, katika uzushi.. Wewe ulileta uzi kumzushia mwigulu kuhusu email, ulimzushia Zitto kuhusu mgawo wa Fedha, ulimzushia PM MAJALIWA kuhusu kuimba tunaiman na Edo.. Kwa Hiyo stahimili tu
 
Ruttashobolwa,

Sasa kama BAVICHA ni weak na ovyo si ndio mngekaa kimya na kufurahi zaidi?

Poleni sana. Vijana wanajenga Taasisi. And their Chairman Patrobas is doing the right thing at the Right time.
Mbona wewe ujakaa kimya kuhusu JPM.. Juz umeleta uzi mrefu kuleta lawama, si mngekaa kimya msubiri 2020.. Ili mtupige nayo
 
Back
Top Bottom