Hongera Patrobas, ila umenielewa vibaya

Juliana Shonza

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
2,009
1,607
HONGERA PATROBAS, ila umenielewa Vibaya.

Katika sehemu kubwa ya maandiko yangu hapa jukwaani yamekuwa yakijikita kuainisha udhaifu wa Upinzani na hasa CHADEMA, na katika kuizungumza CHADEMA naitaja sana BAVICHA, sihitaji kurudia tena kusema sababu ya kufanya hivyo kwani nimeiweka bayana mara kadhaa..!!

Tofauti na siku zilizopita, leo naandika kutoa pongezi, kusifia na kuonyesha kuridhika kwangu namna ambavyo PATROBAS PASCHAL, Mwenyekiti BAVICHA alivyopokea maoni yangu na kuyafanyia kazi.

Ni kweli kuwa umekuwa ukipata upinzani na changamoto za kipekee sana katika kazi yako ngumu ya kuongoza Vijana wasioamini katika itikadi, hawana muongozo. I have been there, najua unaongoza watu wa namna gani. Pole na hongera..

Ni kweli pia, sikuwa nikikufahamu wakati wa uongozi wangu, hivyo mimi ni kama wengine wasiokujua na wanaoshangaa ulipotokea, sina historia sahihi ya mapambano, uwezo na maarifa yako katika kuongoza na kuyasimamia maslahi ya Vijana kwenye Chama na kwa Taifa kwa ujumla. Ila ninalojua ni kuwa ulipingwa na unapingwa sana hata sasa, ushahidi wa hayo ni kauli hizi za Die Hard Members wa BAVICHA dhidi yako baada tu ya kuteuliwa, Yericko Nyerere alisema hivi;
yericko.PNG

Nae Ben Saanane aliyehenguliwa kwa figisu za Umri alisema hivi;
Ben Saanane.PNG

Baada ya hapo wakaibuka wabezaji na wapingaji online…IBILISI alisema haya; John Heche okoa jahazi, BAVICHA imemshinda Katambi, Inakufaa, na Pisto Lero aliandika; Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA, na hata SHIEKA akamaliza Mwenyekiti BAVICHA Patrobass Katambi Naanza Kupoteza Imani Kwako!, hao ni baadhi tu, ukiacha wale ambao walikuwa wafuasi wa Msigwa. Kwa ujumla wake ni kuwa unapigwa, wenzako hawaamini katika wewe, hawaamii uwezo wako na hawajui mwelekeo wako. Hawako tayari kufuata njia na maelekezo yako.

Mimi nilisema siku za nyuma kuwa BAVICHA imepooza, nikimaanisha kuwa imepoteza taswira ya “TAASISI YA VIJANA” baada ya maneno hayo nikaona umeanza kufanya Press Conference kila asubuhi na jioni, lakini kama utakuwa tayari kuungana na mimi katika tathmini ya Press hizo ni sawa na ‘vumbi lenye kupeperuka” hazina substance kabisa kwa sababu nyingi ni za kuunga mkono, maamuzi ya aidha Mwenyekiti, Kamati Kuu au Baraza Kuu, sawa ni jambo jema lakini hivi ni kweli vijana hawana “HOJA” za msingi za kusemewa na BAVICHA isipokuwa kuunga mkono tu..??

Maana mimi najua, pale akina Nusrat Hanje walipokatwa Ubunge wa Viti Maalum na kupewa total strangers BAVICHA ilikuwa kimya, Mwenyekiti alipomleta Mgombea wake “FISADI” Bavicha ilikuwa Kimya, MGOMBEA FISADI anapojitangaza kuwa yeye ni MGOMBEA WA KUDUMU wa CHADEMA 2020, 2025 kinyume na Kanuni na Taratibu BAVICHA iko kimya..? Sawa labda ya Chama makubwa sana na mazito kuyagusa, maana hata MASHINJI mwenyewe hayazungumzii basi tulitegemea mtetee Vijana ngazi ya Taifa lakini nako ni Zero, Mikopo vyuoni hamna mko kimya, Ajira bado mko kimya, Vilaza wanadahiliwa vyuoni mko kimya,,,ehee Basi anzisheni hata kampeni ya kuhimiza Vijana kujiajiri na kushiriki kilimo, mtengeneze banda la mfano kwenye nane nane, maana hata Meya wa Kinondoni akiwa anazunguka kwenye makundi ya Vijana kuhamasisha kujiajiri na kuunda vikundi wapewe mikopo ya Serikali hampo na wala hamshiriki wala kuunga mkono…!!

Labda ulinielewa Vibaya nilipotaka uanze kuwa active, nilimaanisha uwasemee Vijana ndani ya Chama na ndani ya Taifa.

Kama siasa ngumu unaweza kuchagua kuwa Mkulima, mimi nimechagua kufanya yote mawili. Kauli mbiu ya Wakulima wenzangu mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”
 
Chaah! Sasa Ben Saanane nilifanyaje Jully?

Kwa kumbukumbu,Hayo Maneno uliyoweka hapo niliandika siku nilipotangaza kuwa sitagombea Uenyekiti kwa sababu zile

Siku hiyo Patrobas hakua amechukua fomu na alikuja kuchukua Fomu Jumatatu yake. Hayo maneno niliandika Jumamosi

Nimekua nae tangu kabla hajachukua fomu na hata katika kampeni na baada ya Uchaguzi

Sasa mbona kama vile unataka kuleta uzushi kiaina Benazir?
 
bavicha hawana tofauti na ya kwetu uvccm ya wakina mwampamba kusifia baadhi ya viongozi ama kurubuniwa ili wawapambe kwenye media.............
vijana wote sio ccm sio ukawa,wamepoteza hadhi ya kuitwa viongozi wa kesho,ukiangalia kwa makini na kutathimini nani leo anaungalau wa kukigusa hata kiti cha uenyekiti hakuna wote ni wale wale kauli ya mwenyekiti ndio mwisho wa kila kitu kazi yetu ni kuikuza na kuipamba...................
 
Chaah! Sasa Ben Saanane nilifanyaje Jully?

Kwa kumbukumbu,Hayo Maneno uliyoweka hapo niliandika siku nilipotangaza kuwa sitagombea Uenyekiti kwa sababu zile

Siku hiyo Patrobas hakua amechukua fomu na alikuja kuchukua Fomu Jumatatu yake. Hayo maneno niliandika Jumamosi

Nimekua nae tangu kabla hajachukua fomu na hata katika kampeni na baada ya Uchaguzi

Sasa mbona kama vile unataka kuleta uzushi kiaina Benazir?
Pole sana ulikatwa bila huruma.
 
Bvicha wamekuwa watu wakuunga mkono tuu matamko ya Lowasa na Mbowe.

Leo hii Bavicha wanashindwa kumdhibiti Lowasa kujitangaza mgombea kabla ya 2020.

Mimi ndio maana huwaita Nyumbu.
 
bureeeee kabisa utazimaje moto kwa jirani wakati kwako kunateketea? nani kakutuma,? kweli kimwili uko Lumumba kiroho uko Cdm, dah kumbe kukufukuzwa chamani ilikuuma kiasi hiki? umechuja huna jipya mrudie mungu achana na siasa huziwezi tena utazeeka bure na njaa zilizopo huko huponi

pitia kila comment ujitathimini acha mbwembwe tulia ufanye yanayokuuma moyoni achana na siasa.
 
HONGERA PATROBAS, ila umenielewa Vibaya.

Katika sehemu kubwa ya maandiko yangu hapa jukwaani yamekuwa yakijikita kuainisha udhaifu wa Upinzani na hasa CHADEMA, na katika kuizungumza CHADEMA naitaja sana BAVICHA, sihitaji kurudia tena kusema sababu ya kufanya hivyo kwani nimeiweka bayana mara kadhaa..!!

Tofauti na siku zilizopita, leo naandika kutoa pongezi, kusifia na kuonyesha kuridhika kwangu namna ambavyo PATROBAS PASCHAL, Mwenyekiti BAVICHA alivyopokea maoni yangu na kuyafanyia kazi.

Ni kweli kuwa umekuwa ukipata upinzani na changamoto za kipekee sana katika kazi yako ngumu ya kuongoza Vijana wasioamini katika itikadi, hawana muongozo. I have been there, najua unaongoza watu wa namna gani. Pole na hongera..

Ni kweli pia, sikuwa nikikufahamu wakati wa uongozi wangu, hivyo mimi ni kama wengine wasiokujua na wanaoshangaa ulipotokea, sina historia sahihi ya mapambano, uwezo na maarifa yako katika kuongoza na kuyasimamia maslahi ya Vijana kwenye Chama na kwa Taifa kwa ujumla. Ila ninalojua ni kuwa ulipingwa na unapingwa sana hata sasa, ushahidi wa hayo ni kauli hizi za Die Hard Members wa BAVICHA dhidi yako baada tu ya kuteuliwa, Yericko Nyerere alisema hivi;
View attachment 377898

Nae Ben Saanane aliyehenguliwa kwa figisu za Umri alisema hivi;
View attachment 377899

Baada ya hapo wakaibuka wabezaji na wapingaji online…IBILISI alisema haya; John Heche okoa jahazi, BAVICHA imemshinda Katambi, Inakufaa, na Pisto Lero aliandika; Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA, na hata SHIEKA akamaliza Mwenyekiti BAVICHA Patrobass Katambi Naanza Kupoteza Imani Kwako!, hao ni baadhi tu, ukiacha wale ambao walikuwa wafuasi wa Msigwa. Kwa ujumla wake ni kuwa unapigwa, wenzako hawaamini katika wewe, hawaamii uwezo wako na hawajui mwelekeo wako. Hawako tayari kufuata njia na maelekezo yako.

Mimi nilisema siku za nyuma kuwa BAVICHA imepooza, nikimaanisha kuwa imepoteza taswira ya “TAASISI YA VIJANA” baada ya maneno hayo nikaona umeanza kufanya Press Conference kila asubuhi na jioni, lakini kama utakuwa tayari kuungana na mimi katika tathmini ya Press hizo ni sawa na ‘vumbi lenye kupeperuka” hazina substance kabisa kwa sababu nyingi ni za kuunga mkono, maamuzi ya aidha Mwenyekiti, Kamati Kuu au Baraza Kuu, sawa ni jambo jema lakini hivi ni kweli vijana hawana “HOJA” za msingi za kusemewa na BAVICHA isipokuwa kuunga mkono tu..??

Maana mimi najua, pale akina Nusrat Hanje walipokatwa Ubunge wa Viti Maalum na kupewa total strangers BAVICHA ilikuwa kimya, Mwenyekiti alipomleta Mgombea wake “FISADI” Bavicha ilikuwa Kimya, MGOMBEA FISADI anapojitangaza kuwa yeye ni MGOMBEA WA KUDUMU wa CHADEMA 2020, 2025 kinyume na Kanuni na Taratibu BAVICHA iko kimya..? Sawa labda ya Chama makubwa sana na mazito kuyagusa, maana hata MASHINJI mwenyewe hayazungumzii basi tulitegemea mtetee Vijana ngazi ya Taifa lakini nako ni Zero, Mikopo vyuoni hamna mko kimya, Ajira bado mko kimya, ****** wanadahiliwa vyuoni mko kimya,,,ehee Basi anzisheni hata kampeni ya kuhimiza Vijana kujiajiri na kushiriki kilimo, mtengeneze banda la mfano kwenye nane nane, maana hata Meya wa Kinondoni akiwa anazunguka kwenye makundi ya Vijana kuhamasisha kujiajiri na kuunda vikundi wapewe mikopo ya Serikali hampo na wala hamshiriki wala kuunga mkono…!!

Labda ulinielewa Vibaya nilipotaka uanze kuwa active, nilimaanisha uwasemee Vijana ndani ya Chama na ndani ya Taifa.

Kama siasa ngumu unaweza kuchagua kuwa Mkulima, mimi nimechagua kufanya yote mawili. Kauli mbiu ya Wakulima wenzangu mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”
Jitahidi hata Shigongo alianza kama wewe
 
Back
Top Bottom