Hongera Patrobas, ila umenielewa vibaya

Hongera Patrobas, ila umenielewa vibaya

Shikamoo Mwehishimiwa Hatimae Salama Imeokotwa Na Sasa Inatumika Tena
 
HONGERA PATROBAS, ila umenielewa Vibaya.

Katika sehemu kubwa ya maandiko yangu hapa jukwaani yamekuwa yakijikita kuainisha udhaifu wa Upinzani na hasa CHADEMA, na katika kuizungumza CHADEMA naitaja sana BAVICHA, sihitaji kurudia tena kusema sababu ya kufanya hivyo kwani nimeiweka bayana mara kadhaa..!!

Tofauti na siku zilizopita, leo naandika kutoa pongezi, kusifia na kuonyesha kuridhika kwangu namna ambavyo PATROBAS PASCHAL, Mwenyekiti BAVICHA alivyopokea maoni yangu na kuyafanyia kazi.

Ni kweli kuwa umekuwa ukipata upinzani na changamoto za kipekee sana katika kazi yako ngumu ya kuongoza Vijana wasioamini katika itikadi, hawana muongozo. I have been there, najua unaongoza watu wa namna gani. Pole na hongera..

Ni kweli pia, sikuwa nikikufahamu wakati wa uongozi wangu, hivyo mimi ni kama wengine wasiokujua na wanaoshangaa ulipotokea, sina historia sahihi ya mapambano, uwezo na maarifa yako katika kuongoza na kuyasimamia maslahi ya Vijana kwenye Chama na kwa Taifa kwa ujumla. Ila ninalojua ni kuwa ulipingwa na unapingwa sana hata sasa, ushahidi wa hayo ni kauli hizi za Die Hard Members wa BAVICHA dhidi yako baada tu ya kuteuliwa, Yericko Nyerere alisema hivi;
View attachment 377898

Nae Ben Saanane aliyehenguliwa kwa figisu za Umri alisema hivi;
View attachment 377899

Baada ya hapo wakaibuka wabezaji na wapingaji online…IBILISI alisema haya; John Heche okoa jahazi, BAVICHA imemshinda Katambi, Inakufaa, na Pisto Lero aliandika; Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA, na hata SHIEKA akamaliza Mwenyekiti BAVICHA Patrobass Katambi Naanza Kupoteza Imani Kwako!, hao ni baadhi tu, ukiacha wale ambao walikuwa wafuasi wa Msigwa. Kwa ujumla wake ni kuwa unapigwa, wenzako hawaamini katika wewe, hawaamii uwezo wako na hawajui mwelekeo wako. Hawako tayari kufuata njia na maelekezo yako.

Mimi nilisema siku za nyuma kuwa BAVICHA imepooza, nikimaanisha kuwa imepoteza taswira ya “TAASISI YA VIJANA” baada ya maneno hayo nikaona umeanza kufanya Press Conference kila asubuhi na jioni, lakini kama utakuwa tayari kuungana na mimi katika tathmini ya Press hizo ni sawa na ‘vumbi lenye kupeperuka” hazina substance kabisa kwa sababu nyingi ni za kuunga mkono, maamuzi ya aidha Mwenyekiti, Kamati Kuu au Baraza Kuu, sawa ni jambo jema lakini hivi ni kweli vijana hawana “HOJA” za msingi za kusemewa na BAVICHA isipokuwa kuunga mkono tu..??

Maana mimi najua, pale akina Nusrat Hanje walipokatwa Ubunge wa Viti Maalum na kupewa total strangers BAVICHA ilikuwa kimya, Mwenyekiti alipomleta Mgombea wake “FISADI” Bavicha ilikuwa Kimya, MGOMBEA FISADI anapojitangaza kuwa yeye ni MGOMBEA WA KUDUMU wa CHADEMA 2020, 2025 kinyume na Kanuni na Taratibu BAVICHA iko kimya..? Sawa labda ya Chama makubwa sana na mazito kuyagusa, maana hata MASHINJI mwenyewe hayazungumzii basi tulitegemea mtetee Vijana ngazi ya Taifa lakini nako ni Zero, Mikopo vyuoni hamna mko kimya, Ajira bado mko kimya, ****** wanadahiliwa vyuoni mko kimya,,,ehee Basi anzisheni hata kampeni ya kuhimiza Vijana kujiajiri na kushiriki kilimo, mtengeneze banda la mfano kwenye nane nane, maana hata Meya wa Kinondoni akiwa anazunguka kwenye makundi ya Vijana kuhamasisha kujiajiri na kuunda vikundi wapewe mikopo ya Serikali hampo na wala hamshiriki wala kuunga mkono…!!

Labda ulinielewa Vibaya nilipotaka uanze kuwa active, nilimaanisha uwasemee Vijana ndani ya Chama na ndani ya Taifa.

Kama siasa ngumu unaweza kuchagua kuwa Mkulima, mimi nimechagua kufanya yote mawili. Kauli mbiu ya Wakulima wenzangu mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”


Mi nafikir wewe kama Mheshimiwa sasa hivi una mambo mengi ya kufanya achana na BAVICHA its non of your business
 
Kaka huo ni upungufu wa kibinadamu, mtu kutokupata mtoto si kujitakia lkn ni mipango ya Mungu maana yeye ndiye anatoa na yy ndiye mwenye uwezo wa kukunyang'anya ata ww ambaye mayai yako hukulia chips, pia kuwa na upungufu wa kibinadamu siyo sababu ya kumzuia yeye kusema. Toa hoja za msingi maswala ya ndoa yake siyo ya kuanika hapa jukwaani maana kila ndoa Ina changamoto zake.
wakati mwingine ni kujitakia! Huu Mfano haumuhusu Juliana,,je,kama mtu akitoa mimba sana ujanani mwake,je haiwezi athiri Uwezo wake Wa kuconcieve tena? Inawezekana,
 
Kwa kweli kujua kama UVCCM wako bora ama laa kunategemea zaidi unafananisha na UVCCM ya kipindi gani..?
UVCCM iliyokuwa inaongozwa na Azimio la Arusha, hiyo ndiyo UVCCM ambayo niliijua mimi na niliiheshimu.
 
bavicha hawana tofauti na ya kwetu uvccm ya wakina mwampamba kusifia baadhi ya viongozi ama kurubuniwa ili wawapambe kwenye media.............
vijana wote sio ccm sio ukawa,wamepoteza hadhi ya kuitwa viongozi wa kesho,ukiangalia kwa makini na kutathimini nani leo anaungalau wa kukigusa hata kiti cha uenyekiti hakuna wote ni wale wale kauli ya mwenyekiti ndio mwisho wa kila kitu kazi yetu ni kuikuza na kuipamba...................
Kula tano mkuu
 
Nadhani kwa namna ulivyoeleza, sidhani kama ulimaanisha kuwa ni matatizo...labda ikiwa neno matatizo limepatiwa tafsiri mpya.

Kimsingi nikianza na hoja yako ya kwanza, kuhusu kuchuja ama kupanda ni lazima kujua unazungumza katika muktadha gani. Kuhusu LAMWAI naweza nisiwe na maelezo mazuri hivyo sitosema lolote ila kuhusu TUNDU LISSU ninayo ya kusema tena mengi,
1. Kama kipimo chako cha ubora wa mtu ni kumlinganisha na TUNDU LISSU naomba mimi nikubali kuwa mtu wa hovyo. Sijawahi, na sitaki kwa namna yeyote kufanana na mtu kama Tundu Lissu, kwa tabia, akili, maarifa, uwezo na hata kitaaluma. Sitaki kufanana nae. Nadhani nimesema yoooote kuhusu Lissu kwenye thread hii Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu, lakini jambo lingine muhimu kulijua ni namna ya kufanya hiyo comparison analysis, CHADEMA ni kikundi cha wanaharakati, BAVICHA ni sehemu katika CHADEMA, ili uwe mwenzao ni lazima uwe kinara wa harakati., hakuna mwanasiasa chadema wala mwelekeo wa kuwaandaa Vijana wanasiasa ama kuandaa viongozi...hakuna Kijana Chadema anaandaliwa kuja kuwa Kiongozi, si tu wa CHADEMA bali wa TAIFA..hakuna hiyo program.

Mimi ni zao la HARAKATI za CHADEMA, wakati fulani nilipelekwa nchini UGANDA nikiongozana na Ndugu yangu JOHN MALLYA (ambae kwa sasa ni mwanasheria wa CHADEMA) kulikuwa na mafunzo ya uongozi yaliyoandaliwa na taasisi ya Kiswidishi (KIC) ambayo iliitwa Program for Young Politicians in Africa - PYPA, ambapo vijana kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika wamekuwa wakikusanyika ili kupigwa msasa na kuandaliwa kuwa Viongozi bora wa baadae..Kwa bahati mbaya sana, maandalizi tuliyofanyiwa ili tukashiriki yalikuwa ya ajabu sana, maana tulichapishiwa lundo la Picha za matukio ya mauaji yaliyotokana na maandamano kule Arusha, Morogoro na zile za Mwangosi, Picha za Mama Mushumbusi akivuja damu na zinginezo kuwa tukawaonyeshe wale Wazungu ili Serikali ya Tanzania iadhibiwe kwa kunyimwa mikopo, kwa bahati mbaya sana wakati ule nilikubali kufanya jambo lile ovu kwa nchi yangu...najutia hata sasa kwa kuwa mmoja wa watu walioshiriki kuharibu image ya nchi yangu kwa UJINGA tu..!

Lakini hivyo ndivyo vijana wanavyoandaliwa CHADEMA kuwa hawana cha kujivunia kwenye nchi hii, wanaandaliwa kuikwamisha Serikali, kuharibu IMAGE ya nchi kimataifa. Wanafundishwa kuwa wanaharakati wasiofiriki.

Hali hii sikuikuta UVCCM, kabisa. Niliwakuta Vijana wakiwa watulivu, wanaochangia hoja kwa heshima na nidhamu, waliojaa uzalendo kwa Chama na Nchi yao, wanafunzwa kuitetea popote wawapo duniani, wanatetea Viongozi wao na Serikali yao. Wanafundishwa kujivunia nchi yao na Viongozi wao, wanafanywa wazalendo. Hawa wanakuwa wanasiasa Viongozi. Nilivyojiunga CCM nikapelekwa IHEMI nikawekwa kwa miezi miwili nikifunzwa kuwa Kijana wa CCM, baada ya hapo nikaanza kuchukuliwa kwenye majukwaa ya siasa ya CCM na kushiriki Vikao. Nikaajiriwa makao makuu ya UVCCM na nikatakiwa kujiendeleza kielimu kwa kulipiwa na Jumuiya.. hayo hayafanyiki BAVICHA katu..!

Kuifanyia Comparison UVCCM na BAVICHA ni kufanya makosa ya mfanano, maana utakuwa unafananisha visivyofanana. BAVICHA wanaharakati na UVCCM wanasiasa, wapi na wapi.!!

Hata hiyo HOJA yako kuwa akina MAKONDA watafeli, ni hoja iliyojengwa katika misingi ya Choyo, waswahili wanaita Dua la Kuku. Dar imetulia, hakuna mgambo wa jiji kusumbua akina Mama Ntilie, hakuna mitaro michafu, mji unasimamia usafi akina Makonda wakiwa wahamasishaji wakuu..mji wetu unaingia mikataba mikubwa na miji mikubwa Duniani ya China na Japan...bado unasema hawezi kufanikiwa.,ama kweli BAVICHA mentality ya kuto appreciate kitu imewakolea..Dah.



Hilo dua la kuku ndo ambalo kila leo unawashambulia nalo wakina lissu na mbowe bado siamini kama upo timamu kiakili na elimu unayoitangaza jamii forum unatuambia makonda kaimudu dar ktk matamko yake ni lipi limekamilika? ukianza mashoga, omba omba na walimu kupanda magar free?


Ukizungumzia suala la picha na kuvuja damu kwa huyo mkee wa slaa ni uongo? unafagaije sebuleni uchafu unapeleka uvunguni? Watu wanapigwa na polisi halafu unasema ni bad image kuongea kwa yale matendo ovu yafanywayo na vyombo vya dora!!! ina maana raia kupigwa na polisi ni sahihi hayo ndo masomo ya siasa mnayofundishwa huko uvccm
 
Kaka huo ni upungufu wa kibinadamu, mtu kutokupata mtoto si kujitakia lkn ni mipango ya Mungu maana yeye ndiye anatoa na yy ndiye mwenye uwezo wa kukunyang'anya ata ww ambaye mayai yako hukulia chips, pia kuwa na upungufu wa kibinadamu siyo sababu ya kumzuia yeye kusema. Toa hoja za msingi maswala ya ndoa yake siyo ya kuanika hapa jukwaani maana kila ndoa Ina changamoto zake.
Wewe ni baba Paroko au Mama Rwakatale
 
Chaah! Sasa Ben Saanane nilifanyaje Jully?

Kwa kumbukumbu,Hayo Maneno uliyoweka hapo niliandika siku nilipotangaza kuwa sitagombea Uenyekiti kwa sababu zile

Siku hiyo Patrobas hakua amechukua fomu na alikuja kuchukua Fomu Jumatatu yake. Hayo maneno niliandika Jumamosi

Nimekua nae tangu kabla hajachukua fomu na hata katika kampeni na baada ya Uchaguzi

Sasa mbona kama vile unataka kuleta uzushi kiaina Benazir?
Uyu dada awez andika kitu bila kukutaja...huenda anakaugonjwa na wewe...wapo wengine awezi kuweka comment au thread humu pila jina Lowassa
 
Kwa kweli kujua kama UVCCM wako bora ama laa kunategemea zaidi unafananisha na UVCCM ya kipindi gani..?

Na kwa sababu sijaiishi UVCCM kama nilivyoiishi BAVICHA ukweli utabaki kuwa naijua zaidi bavicha kuliko Uvccm...tena naijua ndani nje.

Lakini naiona UVCCM, naisikia kwenye vikao vya Chama na naisikia katika hoja na mabaraza ya kitaifa...

Nawaona vijana wengi wanaofanya vizuri na wanaakisi taswira ya Ujana wengi ni zao la UVCCM. Nikimtazama Makonda anavyolimudu jiji Mama la Dar es salaam naiona UVCCM..nikimtazama Hapi akiwa ameimeza Kinondoni na naiona UVCCM...naiona UVCCM leo na katika Tanzania ya kesho...ila siioni BAVICHA popote
Unatupa picha gani ukiwa kiongozi wa zamani wa BAVICHA?
 
HONGERA PATROBAS, ila umenielewa Vibaya.

Katika sehemu kubwa ya maandiko yangu hapa jukwaani yamekuwa yakijikita kuainisha udhaifu wa Upinzani na hasa CHADEMA, na katika kuizungumza CHADEMA naitaja sana BAVICHA, sihitaji kurudia tena kusema sababu ya kufanya hivyo kwani nimeiweka bayana mara kadhaa..!!

Tofauti na siku zilizopita, leo naandika kutoa pongezi, kusifia na kuonyesha kuridhika kwangu namna ambavyo PATROBAS PASCHAL, Mwenyekiti BAVICHA alivyopokea maoni yangu na kuyafanyia kazi.

Ni kweli kuwa umekuwa ukipata upinzani na changamoto za kipekee sana katika kazi yako ngumu ya kuongoza Vijana wasioamini katika itikadi, hawana muongozo. I have been there, najua unaongoza watu wa namna gani. Pole na hongera..

Ni kweli pia, sikuwa nikikufahamu wakati wa uongozi wangu, hivyo mimi ni kama wengine wasiokujua na wanaoshangaa ulipotokea, sina historia sahihi ya mapambano, uwezo na maarifa yako katika kuongoza na kuyasimamia maslahi ya Vijana kwenye Chama na kwa Taifa kwa ujumla. Ila ninalojua ni kuwa ulipingwa na unapingwa sana hata sasa, ushahidi wa hayo ni kauli hizi za Die Hard Members wa BAVICHA dhidi yako baada tu ya kuteuliwa, Yericko Nyerere alisema hivi;
View attachment 377898

Nae Ben Saanane aliyehenguliwa kwa figisu za Umri alisema hivi;
View attachment 377899

Baada ya hapo wakaibuka wabezaji na wapingaji online…IBILISI alisema haya; John Heche okoa jahazi, BAVICHA imemshinda Katambi, Inakufaa, na Pisto Lero aliandika; Kuna kitu hakiko sawa BAVICHA, na hata SHIEKA akamaliza Mwenyekiti BAVICHA Patrobass Katambi Naanza Kupoteza Imani Kwako!, hao ni baadhi tu, ukiacha wale ambao walikuwa wafuasi wa Msigwa. Kwa ujumla wake ni kuwa unapigwa, wenzako hawaamini katika wewe, hawaamii uwezo wako na hawajui mwelekeo wako. Hawako tayari kufuata njia na maelekezo yako.

Mimi nilisema siku za nyuma kuwa BAVICHA imepooza, nikimaanisha kuwa imepoteza taswira ya “TAASISI YA VIJANA” baada ya maneno hayo nikaona umeanza kufanya Press Conference kila asubuhi na jioni, lakini kama utakuwa tayari kuungana na mimi katika tathmini ya Press hizo ni sawa na ‘vumbi lenye kupeperuka” hazina substance kabisa kwa sababu nyingi ni za kuunga mkono, maamuzi ya aidha Mwenyekiti, Kamati Kuu au Baraza Kuu, sawa ni jambo jema lakini hivi ni kweli vijana hawana “HOJA” za msingi za kusemewa na BAVICHA isipokuwa kuunga mkono tu..??

Maana mimi najua, pale akina Nusrat Hanje walipokatwa Ubunge wa Viti Maalum na kupewa total strangers BAVICHA ilikuwa kimya, Mwenyekiti alipomleta Mgombea wake “FISADI” Bavicha ilikuwa Kimya, MGOMBEA FISADI anapojitangaza kuwa yeye ni MGOMBEA WA KUDUMU wa CHADEMA 2020, 2025 kinyume na Kanuni na Taratibu BAVICHA iko kimya..? Sawa labda ya Chama makubwa sana na mazito kuyagusa, maana hata MASHINJI mwenyewe hayazungumzii basi tulitegemea mtetee Vijana ngazi ya Taifa lakini nako ni Zero, Mikopo vyuoni hamna mko kimya, Ajira bado mko kimya, Vilaza wanadahiliwa vyuoni mko kimya,,,ehee Basi anzisheni hata kampeni ya kuhimiza Vijana kujiajiri na kushiriki kilimo, mtengeneze banda la mfano kwenye nane nane, maana hata Meya wa Kinondoni akiwa anazunguka kwenye makundi ya Vijana kuhamasisha kujiajiri na kuunda vikundi wapewe mikopo ya Serikali hampo na wala hamshiriki wala kuunga mkono…!!

Labda ulinielewa Vibaya nilipotaka uanze kuwa active, nilimaanisha uwasemee Vijana ndani ya Chama na ndani ya Taifa.

Kama siasa ngumu unaweza kuchagua kuwa Mkulima, mimi nimechagua kufanya yote mawili. Kauli mbiu ya Wakulima wenzangu mwaka huu ni “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”
Kumbe Yericko Nyerere alikuwa sahihi kumtilia mashaka Katambi
 
Back
Top Bottom