Kwa Wana JF wote mlionipa hongera na watakaonipa hongera mara baada ya kusoma thread hii, wote kwa pamoja nawashukuru sana. Ni kweli mke wangu amejifungua mtoto wa kike kwa njia ya operation, kutokana na mtoto kukaa vibaya. Nashukuru Mungu mke wangu na mtoto wote wanaendelea vizuri, hali kadhalika mimi mwenyewe binafsi maana nilishock baada ya kuambiwa mke wako ni lazima afanyiwe operation ili kunusuru maisha yake na mtoto kwa ujumla.
Zaidi ya yote namshukuru kiongozi wangu PakaJimmy kwa kunifariji kipekee baada ya akili yangu kuamini kulikuwa na namna hadi mke wanhu kupelekea afaanyiwe operation. Hii ilitokana na ukweli mtoto wangu wa kwanza mke wangu alijifungua salama kwa njia ya kawaida. Anyway nilikubaliana na ushauri ule na mpaka sasa nipo Ok kabisa.
Mwisho nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitamshukuru WiseLady kwa kupost thread hii ambayo mpaka sasa umma mzima wa JF wanajua nina mtoto wa kike.
Ninaawaomba radhi kuto log inn immeadetly punde thread ilipokuwa hewani kwa sababu nilikuwa njiani kurudi home nikitokea hospitali.