Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa.

Kwa masaa 24 nimekuwa nikierejea Hotuba ya Mh Mbowe ya jana pale Mwanza na nimekuwa nikisikiliza mapokeo ya watu nje na ndani ya Chama katika mitazamo tofautitofauti, Wengi tumeelewa na tulitarajia hotuba kama hii, lakini wapo ambao hawajang'amua hasa wale ambao kwa muda mrefu hawakubaliani na maridhiano, wanaamini Mbowe kakosea vile walivyotarajia iwe pale jukwaani. Walitaraji waone hotuba ya kimapambano ya kimnyukano nk.

Naomba nichukue fursa hii kusema Hotuba ya jana ilikuwa ni kete ya mwisho na ya hatari katika game la kisiasa Chadema vs CCM+Serikali katika mechi iliyoanza tangu Mbowe atoke jela 4 March 2022. Mbowe ameshinda!

Tangu tarehe 4 March 2022, Chadema ilianza game ya kisiasa mezani na ccm na serikali, Mbowe akiwa ameongoza upinzani akiwa na mambo kadhaa mkononi, Moja watu wetu (wanachadema) wote waliokuwa na kesi mahakamani waachiwe huru. Pili waliokuwa jela waachiwe bila masharti. Tatu haki kwa wanachama na watanzania wote waliodhuriwa na kuathiriwa katika utawala uliopita wapewa haki zao. Nne Watu wetu/wanachama walioko uhamishoni wahakikishiwe usalama warudi nchini. Tano mikutano ya hadhara iruhusiwe kwakuondolewa lile katazo haramu. Sita Katiba Mpya na Tume huru, Saba sheria mbovu za vyama vya siasa zirekebishwe/zifutwe. Nane sheria ya vyombo vya habari na sheria za mitandao zirekebishwe (uhuru wa habari). Tisa Usalama wa viongozi wa kisiasa, na Kumi ni kuondolewa Bungeni wabunge haramu (COVID19).

Sasa turudi katika hoja kwanini Mbowe jana kashinda mchezo wa kisiasa? Kwanza ifahamike maridhiano bado yanaendelea na yako katika sehemu muhimu sana sana na yatahadhari, hivyo pande zote mbili Chadema na CCM kila mtu anapokuwa jukwaani au popote anazungumza kwa tahadhari kubwa ili kutovuruga mazungumzo yanayoendelea. Katika Mazungumzo yanayoendelea, Mbowe tayari mambo muhimu 7 katika ya 10 amefanikiwa kushinda katika meza ya mazungumzo, Wanachadema wameachiwa magerezani, Haki za Lissu zimepatikani (matibabu na Usalama wake), Mikutano ya kisiasa imerejeshwa, Wanachadema waliokuwa magerezani wameachiwa, nk. Huu ni ushindi mkubwa kwa Mbowe, Lakini isingempa room ya kurejea kwenye siasa ngumu za mapambano wakati bado mambo makubwa ya kinchi hajashinda, Katiba Mpya na Tume Huru bado yako katika mazungumzo na Rais ameshaonyesha utayari wa kuanza mchakato. Hivyo tamko lololete la kimapambano jana lingevuruga maridhiano yote.

Mchezo wa jana ulikuwa ni defragmenting kwa wale wahafidhina kwanza, na kumfanya mkuu wa nchi awe confirmable na meza ya mazungumzo, katika hilo Mbowe ameshinda, Upande wa ccm wasiopenda maridhiano walitamani sana Mbowe aipige ampige kwelikweli Rais hali ambayo kwao ingekuwa ahueni na mwanya wao kisiasa kuelekea 2025, Hilo limewauma maana Mbowe amewakwepa, Upande wa Chadema wale wasiokubaliana na Maridhiano walitaraji Mbowe aipige sana serikali wakiamini uasili wa Chadema, imekuwa tofauti, Chadema iko kwenye mazungumzo kauli yoyote ya kiongozi wa Maridhiano yenye kuuumiza upande wa maridhiano ingevuruga, Hatutaki tuishie kupata mikutano ya hadhara tu, tunataka kupata Katiba Mpya na Tume huru, hilo ndio lengo mahsusi la Chadema. Diplomatic language imeshinda jana.

Kwavyovyote vile Hata keshokutwa Hotuba ya Lissu akirejea Tanzania itakuwa ya kidiplomasia yenye kupalilia mazungumzo yanayoendelea, tofauti na wahafidhina wanaojaribu kupandikiza chuki ili kuvuruga maridhiano haya. Ni Wazi, Mbowe karata zake katika meza ya maridhiano zimechangwa vizuri na ameokota kete muhimu. Kitu muhimu tunachotakiwa kukielewa Watanzania wote hasa Wanachadema na Wanaccm, Matokeo ya Maridhiano hubadili sura na aina ya siasa. Baada ya maridhiano Chadema na CCM hatutafanya siasa kama za miaka 10 nyuma, tutakuwa na aina mpya ya siasa. Na haya ndio mapokeo sahihi.

Hongera Mbowe, Karibu Lissu. Chadema kupitia nyinyi tutapata Katiba Mpya bila kumwaga Damu bali kupitia njia hii nzuri ya Maridhiano.

Na Yericko Nyerere.
 
Hongera Mbowe umeshinda mchezo wa kisiasa.

Kwa masaa 24 nimekuwa nikierejea Hotuba ya Mh Mbowe ya jana pale Mwanza na nimekuwa nikisikiliza mapokeo ya watu nje na ndani ya Chama katika mitazamo tofautitofauti, Wengi tumeelewa na tulitarajia hotuba kama hii, lakini wapo
View attachment 2491265
Kaka,Yericko Nyerere uzi uko mahali pake....
 
Mimi sio mtaalam wa siasa ila akitokea mtu anipe success story ya mtawala kufanya maridhiano na mpinzani na bado mpinzani akabaki na nguvu basi nitaungana na wanaosema Mbowe kafanikiwa.

Mimi nna mfano hai wa juzi tu hapa, Kenyatta na Odinga. Odinga alipoteza mvuto kwa wananchi baada ya maridhiano yao. CCM ndio wanufaika zaidi wa hayo mnayoita maridhiano yanayowa-limit kuikosoa serikali.
 
Ule ulikuwa ni ufunguzi tu, huwezi ukaanza kuhukumu au kuwa na hoja ktk kilichotokea ktk mkutano wa ufunguzi. Mimi ni mpinzani haswa wa ccm lakini sipendi siasa za fujo, siasa za matusi. Napenda kushindana kwa hoja na penye ukweli pasemwe na uongo usemwe bila kuoneana. Naimani chadema ipo vizuri na inakwenda vizuri sana na itafanikiwa sana ktk juhudi zake za kupigania haki na maendeleo ya taifa hili
 
Mimi sio mtaalam wa siasa ila akitokea mtu anipe success story ya mtawala kufanya maridhiano na mpinzani na bado mpinzani akabaki na nguvu basi nitaungana na wanaosema Mbowe kafanikiwa.

Mimi nna mfano hai wa juzi tu hapa, Kenyatta na Odinga. Odinga alipoteza mvuto kwa wananchi baada ya maridhiano yao. CCM ndio wanufaika zaidi wa hayo mnayoita maridhiano yanayowa-limit kuikosoa serikali.
Siasa za Kenya siyo za kulinganisha kabisa na siasa za Tanzania

Tanzania kuna vyama vyenye defined ideology while Kenya kuna magenge ya matajiri yenye wafuasi tu.

Siasa za Kenya zinajengwa kwa misingi wa ukabila while Tanzania sivyo.

Uelewa wawakenya kwenye haki za kisiasa ni mkubwa zaidi kuliko wa watanzania.

Kenya hakuna chama kinachotawala muda mrefu hivyo hakuna aliyechokwa wakati Tanzania bado wananchi wanatafuta namna ya kuiua ccm.

Yawezekana maridhiano yakampubguzia nguvu Mbowe binafsi ila siyo Chadema na Vuguvugu la mabadiliko.

Slaa alikuwa na ushawishi mkubwa sana kwa wanachadema lakini aliondoka na wakasonga mbele.

Miaka 6 iliyopo hamahama ya wanasiasa imewajenga wanachadema kuamini katika njia yao na siyo wanasiasa binafsi.
 
Tunampongeza mbowe kwa mbinu ya maridhiano isipokuwa inabidi achukue tahadhari kubwa katika mazungumzo yake anapompongeza Rais,

Akumbuke kuwa haki haiombwi kwa hiyo awe makini ni nini cha kupongeza

Pili akumbuke pia yule anabaki kuwa mpizani wake na mkit wa chama pinzani
Mwisho atengeneze mazingira ya wazi ya kimaridhiano ambayo hata kama hatakuwepo wenzake watayaelewa
Mwl Nyerere aliwahi kuulizwa unaonaje wakoloni wakikupa uhuru
Akasema mtu anapokunyanganya koti lako then akakurudishia huwezi kumshukuru maana lilikuwa la kwako
Lakini pia tunazidi kumshauri Mbowe azidi kutengeneza mazingira mazuri ya kukabidhi nafasi yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom