Ukiiangalia clip ya tukio utangundua yafuatayo.
1:Mwanausalama/askari alitakiwa atekeleze agizo lake kwa haraka ili kupunguza madhara endapo wananchi wajekaribia eneo hilo(mob psychology), alipomkuta mh Nape aliongea nae kwa sekunde kadhaa, sekunde hizo zinatosha kujitambulisha na kumuomba arudi kwenye gari(mh hakutii), angalia anamgusa begani bado mh hakutii ndio akatoa bastola.
2: Ili kuonesha tukio ni la halali mlinzi wa Mh(japo sijui kuwa ni wa serikali au binafsi) alisaidia kumuingiza mh kwenye gari japo mh aligoma na kushikilia mlango.
3:Tuje kwa maulid, kitendo cha kuingilia kazi ambayo haimuhusu,tena kukiwa na wana usalama wenye bastola viunoni ni cha kukemewa na wapenda amani wote, yeye si mwanausalama wala security detail ya Nape (tunamfahamu kama mwanahabari). jiulize anavomshukuma mwanausalama na huyo mwanausalama akataka kujihami kwa kutumia silaha ingekuwaje, je mwanausalama akajikwaa risasi ikajifatua nani wa kumlaumu, je wananchi wanaomjua kitenge wangeingilia kati hilo sakata nini kingetokea.
4:Mwanausalama baada ya kuona wananchi wamejikusanya akaamua aondoke kuepusha shari zaidi lakini kabla alimsihi kitenge asiingilie,,,,kuna maneno kama bro sikiliza...
5:Angalie matendo aliyofanya jamaa mwingine mwenye fulana nyeusi(nahisi nae ni mwanausalama), kwa heshima alimfungulia mh mlango na kumuonesha aingie ndani ya gari alipoonesha kusita alimshika mkono kumvuta, Pale palikuwa na watu wanne tu nape angeingia kwenye gari kwa nini alikaidi, kitendo kilitakiwa kiwe kimya kmya ila mh ndie alifanya kazi ikawa ngumu kwa kukaidi. Mwenye fulana nyeusi alipoona kitenge anakuja alimsisitiza mlinzi wa mh afanye juhudi mh aingie ndani..kuna maneno yanasikika unasubiri nini. Alipoona kitenge kaingilia kati aliinama kidogo akafanya kitu wakasukumana na kujitawanya.
Kwa mtazamo wangu; Wana usalama walifanya kazi yao kwa ustadi mkubwa bila kuhatarisha usalama. Mh Nape alikosea kukaidi amri/ushauri wa kuingia kwenye gari. Kitenge alihatarisha usalama wa raia kwa kuingilia kaza za wana usalaama.
Rai yangu:
1: Wanahabari kwenye sakata kama hilo jiwekeni mbali muwaache wana usalama wafanye kazi yao.
2: Wana usalama kwenye mikusanyiko ya watu tukiacha wale wanaolinda VIP jitahidini kuhifadhi silaha zenu vizuri.
3: Wanasiasa na watu mashuhuri jitahidini kutii sheria/amri bila shuruti.
NI KWA MTAZAMO WANGU TU