Hongera kocha wa Taifa Stars kwa kuwa mkweli. Taifa stars haijaenda AFCON kushindana

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,410
Ukweli lazima usemwe na ukweli humuweka mtu huru.

Kocha wa taifa stars anajua uwezo wa wachezaji wa taifa stars, hivyo ameamua kusema ukweli...."kwamba kwa kikosi hiki, taifa stars haitoboi. Hivyo tumekuja kutalii na kuwapa changamoto wachezaji kwa manufaa ya baadaye".

Tujifunze kuwa wakweli kama kocha wa taifa stars. Hivi kweli Kuna mtanzania anaamini taifa stars itavuka hata makundi? Kwa wachezaji gani?

Mungu mbariki kocha wa Taifa Stars.
 
Watu mnajiogopa tu,

Stars anadroo hyo game.

Msidhani kwamba ni rahisi tu.
 
Huwa najiuliza wale wachezaji wetu wanaoishi abroad nao hamna kitu!
Huko wanacheza timu za vichochoroni au
Kwani ulishawahi kuwasikia like playing in big European clubs like R. Madrid, Barca, PSG, Arsenal, Juve, Milan, Man City au hata Aston Villa tukiacha mbali zinazoshiriki daraja la pili UK au Bundasliga?🤣🤣🤣🏃🏃
 
Kwani ulishawahi kuwasikia like playing in big European clubs like R. Madrid, Barca, PSG, Arsenal, Juve, Milan, Man City au hata Aston Villa tukiacha mbali zinazoshiriki daraja la pili UK au Bundasliga?🤣🤣🤣🏃🏃
Watanzania sijui ni zao la nani, Tupo vilaza kwenye kila sekta.

Huyo mzee aliyetuzaa sisi, sijui alimkosea wapi Mungu.
 
Na kwanini mpaka Asubuhi hii ( Leo ) Jumatano TFF haijamfuta Kazi? Mnajitambua kweli nyie?

Hivi Serikali ya Tanzania inajua Athari ya Kidiplomasia ya Kauli yake kwa nchi ya Morocco ambayo inaisaidia mambo kadhaa na muhimu Tanzania?

Na hata Wizara ya Mambo ya Nje nanyi Nawalaumu kwani mlipaswa mlichukulie hatua hili haraka sana kwa Maslahi mapana ya Tanzania na Morocco Kimahusiano.

Algeria anakotoka Kocha wa Taifa Stars kwa muda mrefu sasa imekuwa katika Mgogoro na nchi ya Morocco hivyo huyu Mpuuzi na Kocha mbovu wa Taifa Stars anataka Kutuingiza Tanzania katika Ugomvi usiotuhusu na tusiouhitaji.

Tafadhali afukuzwe haraka sana Ok?
 
Ungetuambia huyo kocha katoa kauli ipi ya kichochezi... then tuangalie kama ni kweli au lah.
Kama mpaka leo hujui au hujajua nini amekisema jana Kocha Mkuu wa Taifa Stars wakati Redio na Tv Stations pamoja na Mitandao imetangaza na Kuandika na mpaka Rais wa TFF Wallace Karia nae amemshutumu Kocha Mkuu huyo basi utakuwa ni huna Akili.
 
Back
Top Bottom